Tuesday, September 4, 2012

Picha Mbalimbali


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe akimlaki Waziri wa Ulinzi na Veterani wa Jeshi wa Afrika Kusini Bi. Nosiviwe Mapisa-Nqakula.Rais Joseph Kabila akipeana mikono na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Bw. Suleiman Kova wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere akiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete. Rais Kabila alihudhuria mkutano huo kama mgeni mwalikwa.Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi ya Kusini mwa Afrika(SADC TROIKA) Rais Jakaya Kikwete akiongea na wanbahabri mara baada ya kumalizika kikao cha siku moja cha asasi hiyo katika hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Rais wa Masuala ya Biashara za Kimataifa wa Kampuni ya TBEA ya China,Bw. Wang Pinshan kabla ya mazungumzo yao, Ofisini kwake jijini Dar es salaam September 4, 2012. Kulia ni Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo wa Masuala ya Biashara, Bw. Shi Qiwen na wapili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Bw. Andy. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment