Tuesday, July 3, 2012

TAKUKUTU Kagera Yawafikisha Mahakamani Watumishi Wa serikali

Na Mwandisi Wetu
Bukoba
TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani Kagera (TAKUKURU) inawashililia na kuwafikisha mahakamani watumishi wawili wa ofisi ya mkuu wa mkoa Kagera na watumishi sita wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba kwa tuhuma ya kujihisisha na kufuja fedha kwa njia ya mishahara hewa.

Akizungumza na waandishi wa habari kaimu kamanda wa TAKUKURU mkoani Kagera Samsoni Bishati alisema kuwa watumishi hao wamejihusisha na suala la kupitisha fedha ambazo ni mishahara ya watumishi hewa na kujinufaisha wao wenyewe.

Alisema kuwa katika kupambana na rushwa inayofanywa na baadhi ya watumishi wa serikali ambao sio waaminifu  ofisi ya TAKUKURU mkoa Kagera iewakamata watumishi hao na baadhi kuwapeleka mahakamani kwa kosa la kupitishamishahara hewa.

Aidha aliwataja baadhi ya watumishi ambao wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Bukoba kuwa ni wawili kuroka ofisi ya mkuu wa mkoa ambao ni Shabani Kitimbisi na Sifa Musa ambao wote ni wa idara ya fedha.

Watumisi wengine ambao tayari wamefikishwa mahakamani ni kutoka katika ofisi ya mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba idara ya Afya ni Davidi Buhenyenge na Martini Muganyizi na alisema kuwa watumishi wanne waliobaki bado wanatafutwa na taasisi hiyo na hakuwa tayari kuwataja majina kwakuwa bado wanatafutwa ili kufikishwa mahakamani.

Katika hatua nyingine kaimu kamada huyo Samsoni Bishati ametoa rai kwa umaa kutojihusisha kwa namna yoyote katika vitendo vya rushwa kwani TAKUKURU ipo makini  na ina uwezo wa kuibuwa na hatimaye kuwafikisha mahakamani watumishi wa umma ambao sio waadirifu.

Watumishi ambao wamekamatwa na kufikishwa mahakamani chini ya hakimu wa mahakama hiyo Willibard Mashauri wako nje kwa dhamana hadi kesi itakapotajwa tena ambayo inaendeshwa na mwendesha mashtaka wa TAKUKURU mkoa wa Kagera Fuja Siabo.

Mwisho

No comments:

Post a Comment