Monday, July 9, 2012

KAMPUNI YA NDEGE YA ATC YAZINDUA SAFARI ZAKE KATI YA DAR ES SALAAM NA MORONI COMORO JANA

Kaimu Mkurugenzi wa Biashara kampuni ya ndege ya ATC wanamvua Ngucho akihojiwa na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa kiamtaiafa wa Prince Said Ibrahim Ahaya Njini Moroni Comoro mara baada ya ndege ya shirila hilo kuwasili katika uwan ja huo, Shirika la ndege la ATC limeanzisha safari za Dar es salaam Comoro leo, katika picha kulia ni Sitti Mohamed Nourou.mwakilishi wa kampuni ya ATC Nchini Comoro kutoka Shirika la Com Air
Wafanyakazi wa kampuni ya ndege ya ATC wakitoa huduma kwa abiria wakati wa safari ya ndege hiyo kutoka Dar es salaam kwenda Moroni visiwa vya Comoro.
Wadau kutoka kampuni ya Push Mobale tuliambatana nao na ilikuwa burudani kweli.
Mmoja wa wafanyakazi wa ndege ya shirika la ndege la ATC akitoa maelekezo ya vifaa vya usalama kwa abiria wa ndege hiyo
Moja ya eneo la mji wa Moroni visiwa vya Comoro linavyoonekana angani.
Abiria wakishuka kwenye ndege mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Prince Said Ibrahim Ahaya njini Moroni.
Kaimu Mkurugenzi wa Biashara kampuni ya ndege ya ATC wanamvua Nguchu akisalimiana na maafisa usalama wa uwanja wa ndege wa Prince Said Ibrahim Ahaya mjini Moroni mara baada ya ndege hiyo kuwasili nchini humo..
Hili ndilo jengo la kisasa la kupokea abiria na kusafirisha ililopo katika uwanja wa ndege wa Prince Said Ibrahim Ahaya mjini Moroni Comoro
Ndege ya Shirika la ndege la ATC ikiwa katika uwanja wa ndege wa Prince Said Ibrahim mjini Moroni.
Abiria wakielekea katika eneo la kutokea kwenye uwanja huo
Wadau kutoka kampuni ya ndege ya ATC wakijadili jambo katika uwanja wa ndege wa Prince Said Ibrahim Ahaya mjini Moroni.
Ah!, Bi Kidude tulikuwa naye jamani katika safari yetu kama mnavyoona akipozi kwa picha na wafanyakazi wa unwaja wa ndege wa Moroni
Kaimu Mkurugenzi wa Biashara kampuni ya ndege ya ATC wanamvua Nguchuakimsindikiza Bi Kidude mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Prince Said Ibrahim leo mjini Moroni
Kamanda wa Fullshangweblog akipozi kwa picha kwenye uwanja wa ndege wa Prince Said Ibrahim Ahaya mjini Moroni kulia ni Mdau Freddy Mwanjala wa Chanel Ten.
Hapa wadau tukipozi kwa picha kwenye uwanja huo.

No comments:

Post a Comment