Thursday, July 5, 2012

Kahawa Ya Magendo Yanaswa Bukoba

Na Mwandishi Wa Bukobajamii Blog
Bukoba


HALMASHAURI ya wilaya Bukoba mkoani Kagera,imeendelea na operaisheni ya kupambana na wasafirishaji wa kahawa kuipeleka nje ya nchi kwa njia ya magendo ili kunusuru uchumi wa halmashauri na nchi kwa ujumla.

Opereisheni hiyo inayoendeshwa na wakuu wa idara wote katika halmashauri hiyo kwa kushirikiana na jeshi la Polisi,imeonyesha mafanikio kwa kuzuia kahawa zilizokuwa zikisafirishwa kwa njia ya magendo kwendanchi jirani ya Uganda ikiwa ni takribani mwezi mmoja na nusu tangu msimu wa kahawa ufunguliwe.


Akiongea na Nipahe mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Beatrice Dominick,alisema kuwa utaratibu huo ni wa kawaida ili kuweza kuzuia biashara ya magendo ya kahawa inayofanywa na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu kwa uchumi wa nchi yao.


Beatrice alitaja tukio la Alhamis Juni 28, majira ya saa nne asubuhi gari namba T 413 BMJ (Saloon)mali ya Abdallah Mwaga Kichwabuta,ilikamatwa likiendeshwa na dereva aliyejitambulisha kwa jina hilo la Abdallah Kichwabuta katika barabara ya Kyaka likiwa tayari kwa safari ya kuelekea nchi Uganda.


Alisema kuwa mtuhumiwa alikuwa amepakia ndani ya gari husika kiasi cha kilo 998 za kahawa safi(iliyokobolewa)ambapo mafanikio ya kukamata yametokana kwa ushirikiano mkubwa na maafisa kutoka bodi ya kahawa waliotilia mashaka gari hilo.


Beatrice alisema kuwa kutokana na kukamatwa kwa mtuhumiwa kukiri kuwa alikuwa anasafirisha kahawa,halmashauri imetaifisha kahawa kama sheria zinavyoelekeza na tayari zimeuzwa na kuingizia halmashauri kiasi cha shilingi 1,835,400/=kutokana na kubinika kilo 200 zilikuwa zimeshapoteza ubora,huku gari liliendelea kushikiliwa na halmashauri ili mtuhumiwa aweze kulipa faini.


Ameongeza kuwa tayari halmashauri imekusanya kiasi cha milioni 5.2 kutokana na faini zinazotozwa kwa baadhi ya wafanyabiashara wanaofanyabiashara ya ununuzi wa kahawa kinyume na utaratibu.


Kwa upande wake mwanasheria wa halmashari hiyo Jane Sandi,anasema halashauri inatakiwa kuchukua sheria katika kudhibiti uaramia huu,kwani sheria inaeleza wazi kuwa kama mtu atafanya

No comments:

Post a Comment