Wednesday, July 4, 2012

Serikali Yakubali Kurekebisha Mipaka Ya mbuga Ya Serous Kuruhusu Uchimbaji Wa Madini Ya Urania


PICHA NA PHILEMON SOLOMON  WA FULLSHANGWE

SERIKALI kwa kushirikiana na kamati ya ulithi wa Dunia ya UNESCO imekubali ombi la kurekebisha mpaka wa pori la akiba la Selous ili kuruhusu uchimbaji wa madini ya Urani.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki alisema kamati hiyo katika kikao chake cha 36 kilichofanyika juni 24 mwaka huu Saint Petersburg nchini Russia imekubali ombi hilo.

Kagasheki  alisema  tayari kamati hiyo imetenga eneo la Km 200 kwa ajili ya uchimbaji wa madini hayo ambayo yataanzwaa kuchimbwa wakati wowote kuanzia sasa.

“Mimi nimerudi kutoka Russia ambapo nilikwenda kuhudhuria mkutano huo kwa niaba ya serikali, na kwa mara ya kwanza ombi hilo lilipelekwa kwa kamati hiyo ya urithi wa Dunia ya UNESCO mwezi julai 2011 ambapo lilijadiliwa katika kikao chake cha 35 na hatimaye limekubaliwa mwaka huu” alisema Kagasheki.

Alisema uamuzi huo ulifanyika ili kuruhusu tathimini ya ardhi mazingira na kukamilisha kwa kutoa muda kwa wataalamu kufika eneo linarohusika ili kuhakiki taarifa ya tathimini hiyo.

Wakati huohuo Tanzania imekuwa mwenyeji wa mkutano wan chi za Kusini mwa Afrika utakaofanyika octoba 15 hadi 19 jijini Arusha mwaka huu ukiwa na lengo la kujadili masuala mbalimbali ya utalii pamoja na uhifadhi katika hifadhi .

Aidha utajadili changamoto pamoja na mafanikio mbalimbali yakiwemo masuala ya ulinzi na usalama wa watalii na tanzania imechaguliwa kutokana na usalama wan chi ulioko hivi sasa na wageni wapatao 300 wanategemea kuhudhuria mkutano huo.

Prof. Ibrahim Lipumba atembelea Sabasaba leo

-Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba(kulia) akipata maelezo kutoka kwa Msimamizi wa Ofisi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Pilly Mpenda (kushoto)  juu ya faida za kujiunga na mfuko huo wakati kiongozi huyo alipotembelea maonyesho ya 36 ya kimataifa ya Dar es alaam jana katika Viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere. Katikati ni Afisa wa NSSF anahusika na mambo ya Itifiki Juma Kintu.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba(kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mauzo na Masoko David Manyanga(kulia) juu ya faida ambazo mkulima anaweza kuzipata baada ya kununua mashine ya kupanda mpunga aina ya SPW 48C wakati kiongozi huyo alipotembelea maonyesho ya 36 ya kimataifa ya Dar es alaam jana katika Viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba(kulia) akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Fao la Matibabu wa  Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Aisha Marine  (kushoto)  jinsi wanachama wa mfuko huo wanavyonufaika na huduma hiyo  wakati kiongozi huyo alipotembelea maonyesho ya 36 ya kimataifa ya Dar es alaam jana katika Viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere. Katikati ni Afisa wa NSSF anahusika na mambo ya Itifiki Juma Kintu.

No comments:

Post a Comment