Friday, July 20, 2012

Bukoba Jamii Inaungana Katika Kipindi kigum kutokana Na Katika Ajali Ya Meli Ilyotokea Julai 18 Pata Habari Na Picha za Matukio mbalimbali

TAARIFA YA SMZ KUHUSU AJALI YA MELI YA MV. SKAGIT ILIYOTOLEWA JANA USIKU JULAI 18,2012Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetoa taarifa usiku huu ikieleza idadi ya watu waliopatikana wakiwa hai ni 146 na kupata maiti 62.

Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari usiku leo,Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamuhuna alisema taarifa hiyo ndio sahihi na kuwataka wananchi kutoamini taarifa zinazotolewa na watu wengine zaidi ya Serikali.

Waziri Shamuhuna alisema kwamba maiti 62 walipatikana ambao kati ya maiti hizo watoto ni 9 na kuna raia mmoja wa kike wa kigeni ambaye hakuweza kutambulika  Uraia wake,lakini umeonekana picha yake moja ndogo ya hati ya kusafiria.

Waziri Shamuhuna alisema meli hiyo ilibeba jumla ya abiria 290 kati ya hao watu wazima 250, watoto wadogo 31 na mabaharia 9.

Waziri huyo aliwataka wananchi katika sehemu mbalimbali hasa katika vijiji vilivyo kandokando ya bahari watakapoona maiti au mtu akiwa hai ambaye wanadhani ni wa ajali ya Meli ya Skagit.

Aidha, Waziri Shamuhuna alisema kwamba kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam ambao watakuwa na wasiwasi wa kutowaona ndugu na jamaa zao amewataka kufika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya kupata taarifa zaidi au kuripoti  habari za kupotelewa kwa ndugu au jamaa zao.

Kwa upande wa Zanzibar, Waziri huyo aliwataka wananchi kufika kwa Masheha wao kutoa taarifa kama hizo.

Serikali imewashukuru makampuni binafsi za usafiri baharini kwa msaada wao na wasisite kutoa msaada katika kazi inayoendelea ya kutafuta watu au maiti wengine katika eneo la tukio.

Meli ya Mv. Skagit ilizama Julai 18,2012 karibu na Kisiwa cha Chumbe umbali wa maili sita kuelekea Kusini mwa Kisiwa kidogo cha Yasin Zanzibar ikitokea Bandari ya Dar es Salaam ilikoanza safari saa 5:30 asubuhi.

Meli hiyo inamilikiwa na Kampuni ya Sea Guall Sea Transport Ltd, Kampuni ambayo Meli yake nyengine ya Mv. Fatih ilizama ikiwa Bandarini Malindi Zanzibar na kufariki watu sita mwaka 2009.

Mwisho.

IMETOLEWA NA:
IDARA YA HABARI(MAELEZO) ZANZIBAR
ZANZIBAR, TANZANIA 
JULAI 19,2012

SHUGHULI ZA KUTAMBULIWA MAITI ZILIZOOKOLEWA KATIKA AJALI YA MELI ZILIENDELEA ZANZIBAR JANA

Baadhi ya Maiti zilizookolewa kutoka katika Meli ya Skagit iliozama hapo jana zikitambuliwa na Ndugu zao na kuruhusiwa Kuzichukuwa kwa ajili ya Kufanya taratibu za mazishi hapo katika Viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar jana.
Baadhi ya Maiti zilizookolewa kutoka katika Meli ya Skagit iliozama hapo jana zikitambuliwa na Ndugu zao na kuruhusiwa Kuzichukuwa kwa ajili ya Kufanya taratibu za mazishi hapo katika Viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.
 
Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Learnhat Alfonso wakatikati akionekana na huzuni Baada ya kuziona Maiti zilizookolewa katika Meli iliozama hapo jana katika Bahari ya Chumbe Zanzibar.Balozi alifika katika Viwanja vya Maisara ili kuona namna shughuli za kushughulikia maiti  zinavyoendelea.
 
Waziri wa Mamboya ndani wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Emanuel Nchimbi alifikakatika Eneo lililohifadhiwa Maiti wa Ajali ya Meli ya Skagit ili kutambuliwa na Ndugu zao na Kupata maelezo kwa Daktari Kiongozi hayupo pichani  Hapo katika Viwanja Vya Maisara Zanzibar.
Baadhi ya Maiti zilizookolewa kutoka katika Meli iliozama na kukosa watu wake zikipelekwa kuzikwa na Serikali katika Eneo la Kama lililotayarishwa makusudi kwa ajili hio.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete mwenye koti nyeusi akiwa na Makamu wapili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Ali Idi wakihudhuria katika Eneo la Maisara ili kuona namna shughuli za kutambuliwa kwa Mati zilizookolewa katika Meli iliozama ya Skagit zinavyoendelea na kujuwa hatuwa za kuchukuwa.


RAIS KIKWETE ATUA ZANZIBAR KUFARIJI WALIOPATWA NA AJALI YA MELI

Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimpa pole Bi Salome Abeli, mmoja wa walionusurika katika ajali hiyo ya meli. Yeye ni mfanyakazi wa Tanzania Automic Energy Commission akitokea Arusha kwenda Pemba Kikazi leo July 19, 2012.
 
(PICHA NA IKULU)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea Uwanja wa Maisara, Zanzibar, ambako ndiko miili ya marehemu
huletwa kwa utambuzi baada ya kuokolewa kwenye eneo la ajali  leo July 19, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mmoja wa walionusurika katika ajali ya meli jana huko Chumbwe wakati Rais na Mama Salma Kikwete walipowatembelea kuwafariji na kuwapa pole katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja leo July 19, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakiangalia maiti za ajali ya meli leo iliyotokea huko  huko Chumbwe wakati jana kilomita chache kufika Zanzibar
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mmoja wa walionusurika katika ajali ya meli jana huko Chumbwe wakati Rais na Mama Salma Kikwete walipowatembelea kuwafariji na kuwapa pole katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja leo July 19, 2012.

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AWAFARIJI WAFIWA NA WAHANGA WA AJALI YA MELI YA SKIGET ZANZIBAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, wakati alipofika Ikulu mjini Zanzibar leo Julai 19, 2012 kwa ajili ya kumpa pole kuhusu ajali ya Meli ya Skiget mali ya Kampuni ya seagull, iliyotokea jana eneo la Kisiwa cha Chumbe. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Khamis Haji Khamis, jinsi ulivyandaliwa utaratibu wa kuwahifadhi marehemu watakaokosa kutambuliwa na ndugu zao, wakati Makamu alipofika kwenye Viwanja vya Maisara mjini Zanzibar, leo Julai 19, 2012, kuangalia shughuli za uokoaji na utambuzi wa marehemu. Kushoto ni Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano, Samia Suluhu Hassan. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza mmoja kati ya vijana walionusulika katika ajali ya Meli ya Skiget, Kitwana Makame Ali (24) mkazi wa Unguja, wakati alipotembelea katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Unguja, leo Julai 19, 2012 kuwafariji wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo baada ya kuokolewa katika ajali hiyo iliyotokea jana eneo la Kisiwa cha Chumbe. Kulia ni Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano, Samia Suluhu Hassan.Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na mgonjwa aliyenusulika katika ajali ya Meli ya Skiget, Hamisa Akida (45)mkazi wa Ununio mjini Bagamoyo, wakati alipotembelea katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Unguja, leo Julai 19, 2012 kuwafariji wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo baada ya kuokolewa katika ajali hiyo iliyotokea jana eneo la Kisiwa cha Chumbe. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

HOTUBA YA RAIS WA ZANZIBAR KWA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN LEO

STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEAS
 Zanzibar
    19.7.2012

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali
Mohamed Shein amewataka wafanyabiashara kufanya biashara zao kwa
misingi ya kutodhulumiana katika bei, viwango na vipimo hasa katika
mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Dk. Shein aliyasema hayo leo wakati alipokuwa akisoma risala ya

Ramadhani  kwa wananchi kupitia vyombo vya habari kwa mwaka huu wa
1433 Hijriya sawa na mwaka 2012 Miladia.

Katika maelezo yake Alhaj Dk. Shein alisema kuwa Mwezi Mtukufu wa

Ramadhani ni wa neema kibiashara lakini ni vyema kufanya neema hiyo
iwe kwa wauzaji na kwa wanunuzi.

Alieleza kuwa Muuzaji anauza bidhaa zake nyingi  zaidi kwa hivyo

anapaswa kuhakikisha zina ubora na anachuma faida kwa kiasi ya
anachouza.

Aidha, alisema kuwa mnunuzi naye anahitaji kupewa bei iliyo nafuu hasa

kwa bidhaa ambayo Serikali imeipunguza kodi, kwani Serikali kama
kawaida itapunguza ushuru kwa biadhaa muhimu za chakula ili
kuwawezesha wananchi kupata unafuu wa bei.\

“Ni jambo la kusikitisha kuona baadhi ya wafanyabiashara wenye tamaa

wanasafirisha bidhaa kama vile unga, sukari na mchele walizotozwa kodi
ya chini na kuzisafirisha kwa njia ya magendo nje ya Zanzibar ili
wapate faida kubwa’,alisema Alhaj Dk. Shein.

Kutokana na mambo hayo Alhaj Dk. Shein alisema kuwa husababisha

upungufu wa baadhi ya vyakula na kuwasababishia shida wananchi wakati
huu  wa mwezi wa Ramadhani.

Pamoja na hayo, Alhaj Dk. Shein alitoa shukurani kwa wakulima nchini

kwa kujiandaa kuwaopa huduma nzuri wananchi hasa katika upatikanaji wa
chakula kwa ajili  ya futari huku akieleza kuwa serikali imeweka
mazingira mazuri ya biashara hasa katika Mwezi huo wa Ramadhani.

Alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar nayo itajitahidi kufanya

kila linalowezekana ili kuwasaidia wananchi katika kukabiliana na
tatizo la upatikanaji wa maji katika maeneo mbali mbali nchini.

Alhaj Dk. Shein alisema kuwa Serikali imo katika juhudi za kuwaandalia

wananchi wake maisha bora, kwa kupitia mageuzi ya katiba na pia kwa
kuhesabiwa watu, mambo ambayo yamo katika sheria.


Rais wa Zanzibar Azungumza na Wabunge

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na  Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania,wakiongozwa na Waziri wa Ulinzi Mhe,Shamsi Vuai
Nahodha,walipofika Ikulu Mjini Zanzibar kumpa pole Rais kutokana na
ajali ya Meli ya Mv SKAGIT ya Kampuni ya SEAGUL iliyotokea juzi
ikitokea Dar es Salaam kwenda Zanzibar.[Picha na Ramadhan
Othman,Ikulu.]

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania,wakiongozwa na Waziri wa Ulinzi Mhe,Shamsi Vuai
Nahodha,walipofika Ikulu Mjini Zanzibar kumpa pole Rais kutokana na
ajali ya Meli ya Mv SKAGIT ya Kampuni ya SEAGUL iliyotokea juzi
ikitokea Dar es Salaam kwenda Zanzibar.[Picha na Ramadhan

No comments:

Post a Comment