Sunday, July 15, 2012

Madereva wazembe Mkoani Kagera kufutiwa Leseni

Na Mwandishi Wetu
Muleba
JESHI la polisi mkoani kagera limesema kuwafutila leseni za udereva madereva wote ambao wanajihusisha na uvunjifu wa sheria za usalama barabarani ili kuweza kupunguza ajali nyingi ambazo zinatokea kutokana na uzembe wao.

Hayo yalisemwa jana kwa nyakati tofauti  na kamanda wa polisi mkoani Kagera Philip Kalangi wakati wa kuhitimisha mafunza ya udereva katika kata Ijumbi,Kashasha,Kamachumu na Muhutwe wilayani Muleba ambayo yaliendeshwa na chuo cha udareva cha Lake zone driving school cha Mjini Bukoba kwa kushirikiana na jeshi la polisi mkoani Kagera.

Kamanda Kalangi alesema kuwa kwa hivi sasa tatizo la ajali za barabarani bado ni changamoto kwa jeshi la polisi nchini kwani madereva wengi wamekuwa wanasababisha ajali kwa makusudi jambo ambalo bado linaleta tatizo kwa wananchi na mali zao.

"Jeshi la Polisi nchini ili tupambane na hizi ajali lazima tuhakikishe kila dereva anayefanya uzembe kwa maksudi tunapombaini pamoja na kumpatia adhabu lazima leseni yake tuifute ili asiendeshe gari tena jambo hili litatupunguzia ajali za mara kwa mara"alisema Kalangi.

Katika Hatua nyingine Kamanda Kalangi alisema kuwa kwa hivi sasa madereva ambao wananufaika na mafunzo muhimu kwa madereva wahakikishe wanakuwa mabarozi kwa wale ambao bado hawataki kujifunza na wawape elimu ya usarama barabarani.

Aliongeza kuwa jambo hilo litapunguza idadi kubwa ya waendeshaji wa vyombo vya moto ambao hawana uelewa mzuri wa sheria ambazo zinabadilika kila mara hasa za uendeshaji bora na umakini wa barabarani.

Kwa Upande wake Mkufunzi wa mafunzo hayo ambaye pia ni mkurugenzi wa chuo kilichotoa elimu kwa madereva Winstoni Kabantega alisema kuwa jumla ya madereva 218 wamenufaika na mafunzo hayo maalumu kwa muda wa siku saba na wamakumbushwa kuzingatiasheria mpya na kuzifuata ili kupunguza ajali.

Alisema kuwa wapo madereva amabao ni wazoefu na wana muda mrefu wakiendesha magri au pikipiki lakini hawajawahi kujifunza sheria za usarama barabarani na ndio maana kumekuwepo umuhimu wa kupeleka mafunzo katika maeneo ya vijijini ili kuondoa tatizo hilo.

Aliongeza kuwa Madereva wahakikishe wanazingatia kila walichojifunza na wakemee vitendo vya uvunjifu wa sheria za usarama barabarani na watoe taarifa kwa jeshi la Polisi kikosi cha usalama brabarani ili madeeva wanaoendelea kuvunja sheria hizo wakamatwe nakufutiwa leseni zao.

Mwisho

No comments:

Post a Comment