Saturday, April 27, 2013

 

Yanga bingwa 2012/13 baada ya Azam kutoka sare 1-1 na Coastal Union

Yanga f391d
Kikosi cha Yanga

Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salam
Klabu ya Yanga ya Dar es salaam leo imejitangaziwa ubingwa wake wa 24 wa ligi kuu soka Tanzania bara baada ya wapinzani wake wakubwa kwa muda mrefu klabu YA Azam fc kutoa sare ya kufunga bao 1-1 na Wagosi wa kaya Coastal unioni katika dimba la CCM Mkwakwani jijini Tanga.

Matokeo hayo yana maanisha, Azam FC waliokuwa washindani wakuu wa Yanga SC waliojikusanyia pointi 56 kibindoni, hawawezi tena kufikisha pointi hizo ambazo wanazo mabingwa hao wapya, kwani hata wakishinda mechi zao nyingine  mbili zilizobaki, watamaliza na pointi 54. 


Shukurani kubwa kwa  nyota wa Coastal union Danny Lyanga, ambaye aliifungia Coastal bao la kusawazisha dakika ya 72 akipokea pande maridhawa kutoka kwa nyota wa zamani wa Yanga Pius Kisambale. 
Azam ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao katika mchezo wa leo, lililofungwa na beki Aggrey Morris kwa penalti dakika ya 60, baada ya mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC, Gaudence Mwaikimba kuchezewa rafu kwenye eneo la hatari  na beki Yussuf Chuma- na refa Andrew Shamba wa Pwani akaamuru pigo hilo.

Matokeo haya yanakuwa sawa na Coastal kulipa fadhila kwa Yanga, kwani hata wao, ubingwa wao pekee wa Ligi Kuu waliochukua mwaka 1988 ulitokana na ‘msaada’ wa wana Jangwani hao.

Kilichobaki kwa Yanga sasa ni kulinda heshima kutokana na kubakiwa na mechi mbili ambapo watashuka dimbani kuvaana na Coastal union waliowapa ubingwa msimu huu pamoja na mechi ya kufunga dimba dhidi ya Mnyama Simba uwanja wa Taifa Dar es salaam

Lakini licha ya Coastal union kuwapa ubingwa wanajangwani hao, Kocha mkuu wa wagosi Wakaya Hemed Morroco  amesema mchezo wa leo walistahili kushinda na kilichokwamisha ushindi leo ni waamuzi kuchezesha hovyo.

“Unajua Azam walikuwa na Presha kubwa ya kutaka ushindi, lakini tuliwabana na waamuzi wameshindwa kuchezesha vizuri na ndio maana wameambulia sare vinginevyo walikuwa wanafungwa leo”. Alisema Morroco.

Kikosi cha Coastal Union leo kilikuwa; Shaaban Kado, Hamad Khamis, Othman Tamim, Philip Mugenzi, Yussuf Chuma, Abdi Banda, Joseph Mahundi, Razack Khalfan, Pius Kisambale/Mohamed Soud dk85, Suleiman Kassim ‘Selembe’/Danny Lyanga dk71 na Twaha Shekuwe. 
Azam FC; Mwadini Ally, Himid Mao, Erasto Nyoni, David Mwantika, Aggrey Morris, Jabir Aziz/Salum Abubakar ‘Sure Boy Jr.’ dk75, Brian Umony/Seif Abdallah Karihe dk68, Ibrahim Mwaipopo, Gaudence Mwaikimba/Abdi Kassim ‘Babbi’ dk82, Humphrey Mieno na John Bocco ‘Adebayor’.

No comments:

Post a Comment