Monday, April 15, 2013


KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDURAHMAN KINANA AWASILI MAHENGE MOROGORO

1Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana akishuka kutoka kwenye Kivuko cha Mto Kilombero leo akiwa njiani kuelekea Mahenge ambako atakuwa akiongea na wananchi na kuamsha ari ya kushiriki katika shughuli za maendeleo na kukagua uhai wa chama pia kukagua shughuli za maendeleo katika kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi leo jioni atahutubia mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Mahenge  3 4Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana akipata vitumbua baada ya kununua  kutoka kwa mmoja wa akina mama mara baada ya kuvuka mto Kilombero na ujumbe wake 5Katibu wa  NEC Itikidi na Uenezi Nape Nnauye naye alipata Kitumbua kama anavyoonekana pichani 6Ndugu Abdurahman Kinana akiingia kwenye gari tayari kwa kuanza msafara wa kuelekea Mahenge 7Nape Nnauye akijaribu kupanda katika moja ya mitumbwi ya wavuvi wa mto Kilombero. 8Haji Mponda kulia Mbunge wa Ulanga Magaharibi akizungumza na katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana mara baada ya kumpokea katika mto  Kilombero . 9Msafara ukiwa tayari kuelekea Ulanga na Mahenge j 11 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana akitembelea karakana ya mafundi Ushirika wa mafundi seremala wa Ulanga ambao wanatengeneza mizinga ya nyuki. 13Ndugu Abdurahman Kinana akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya CCM Ulanga mara baada ya kuwasili ofisini hapo kwa ajiji ya kupata taarifa za chama 14 katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana akiangalia ngoma za asili kutoka Ulanga mkoani Morogoro 15 katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana akifuarahia ngoma zilizokuwa zikipigwa wakati wa mapokezi yake. 16 katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana wa pili kutoka kulia  akiwa katika mkutano wa ndani wa chama ili kupata taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 17Wajumbe mbalimbali wakiwa katika mkutano huo 18Wajumbe mbalimbali wakiwa katika mkutano huo wakimsikiliza Katibu Mkuu Ndugu Abdurahman Kinana.

No comments:

Post a Comment