JK :AFUNGA SEMINA YA UTEKELEZAJI WA MFUMO MPYA WA UTENDAJI SERIKALINI
Rais Jakaya Kikwete akifunga semina kwa mawaziri na makatibu wakuu walioketi na kupanga mikakati ya utekelezaji wa mfumo mpya wa kusimamia utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya maendeleo katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma. Mfumo huo unaanza kutekelezwa kwa kutumia uzoefu wa Performance Management and Delivery Unit (PEMANDU) ya Malaysia. Mfumo huu utajumuisha uanzishwaji wa taasisi ya President’s Delivery Bureau (PDB) ambayo itafanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Katika mfumo huu, uchambuzi wa kina wa kimaabara (labs) utafanyika ili kuandaa programu za utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Awamu ya kwanza ya labs ilizinduliwa rasmi na Rais Kikwete tarehe 22 Februari, 2013 na kukamilika Aprili, 2013. Maeneo ya awamu ya kwanza ya labs yanahusisha elimu, kilimo, nishati, mapato, maji na miundombinu ya uchukuzi.
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali na Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue wakiwa na mawaziri na makatibu wakuu wakimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Performance Management and Delivery Unit (PEMANDU) ya Malaysia Dkt Idris Jala wakti wa kuujadili mfumo mpya wa kusimamia utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya maendeleo uliokabidhiwa kwa wizara hizo sita katika semina elekezi kwa mawaziri na makatibu wakuu iliyofanyika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma. Mfumo huo unaanza kutekelezwa kwa kutumia uzoefu wa PEMANDU, ambapo utajumuisha uanzishwaji wa taasisi ya President’s Delivery Bureau (PDB) ambayo itafanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Katika mfumo huu, uchambuzi wa kina wa kimaabara (labs) utafanyika ili kuandaa programu za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilali na Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue wakiweka saini kama wadhamini wa waraka wa kujifunga katika utekelezaji wa mfumo mpya wa kusimamia utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya maendeleo uliokabidhiwa kwa wizara hizo sita katika semina elekezi kwa mawaziri na makatibu wakuu iliyofanyika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma. Mfumo huo unaanza kutekelezwa kwa kutumia uzoefu wa Performance Management and Delivery Unit (PEMANDU) ya Malaysia. Mfumo huu utajumuisha uanzishwaji wa taasisi ya President’s Delivery Bureau (PDB) ambayo itafanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Katika mfumo huu, uchambuzi wa kina wa kimaabara (labs) utafanyika ili kuandaa programu za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Rais Jakaya Kikwete akiongea wakati wa semina kwa mawaziri na makatibu wakuu kujadili mikakati ya utekelezaji wa mfumo mpya wa kusimamia utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya maendeleo katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma. Mfumo huo unaanza kutekelezwa kwa kutumia uzoefu wa Performance Management and Delivery Unit (PEMANDU) ya Malaysia. Mfumo huu utajumuisha uanzishwaji wa taasisi ya President’s Delivery Bureau (PDB) ambayo itafanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Katika mfumo huu, uchambuzi wa kina wa kimaabara (labs) utafanyika ili kuandaa programu za utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Awamu ya kwanza ya labs ilizinduliwa rasmi na Rais Kikwete tarehe 22 Februari, 2013 na kukamilika Aprili, 2013. Maeneo ya awamu ya kwanza ya labs yanahusisha elimu, kilimo, nishati, mapato, maji na miundombinu ya uchukuzi (Picha zote na Muhidin Michuzi).
No comments:
Post a Comment