Thursday, April 18, 2013

Mamlaka Ya Mawasiliano Na Makampuni Ya Simu Yatoa Tamko

2 9f498
Mkurugenzi wa Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof JOHN NKOMA  mapema leo asubuhi akitoa tamko juu ya usajili wa namba za simu za mkononi.


3 013c6
Mkurugenzi wa Vodacom RENE MEZA akisisitiza umuhumu wa kusajili namba za simu za mkononi.

4 2b0b3
Mkurugenzi wa Airtel SUNIL CALASO akifafanua jambo kwenye mkutano na waandishi wa habari juu ya tamko la usajili wa namba za simu za mkononi.
5 507cd
Mkurugenzi wa Zantel PRATAP GHOSE akizungumzia juu ya tamko la pamoja kuhusu usajili wa simu za mkononi.
Mapema leo asubuhi mkurugenzi wa  mamlaka ya mawasiliano nchini ametoa tamko la pamoja lililo azimiwa kwa kushirikiana na makampuni ya simu kwamba watumiaji wote wa simu za mkononi ambao hawaja sajili namba zao wafanye hivyo mara moja,kwani utaratibu unao fuata hivi sasa ni kufunga namba zote ambazo hazija sajiliwa,
Akifafanua zaidi amesema kwamba ni kosa la jinai kutumia namba ya simu isiyo sajiliwa na adhabu yake ni faini ya shilingi laki tano au kifungo cha miezi mitatu jela.
Mwisho amewataka  wananchi kuhakiki usajili wao kwa kupiga namba nyota 106 alama ya reli kutoka  katika simu zao za mkononi kwa mtandao wowote.
mtumiaji utapata ujumbe wa taarifa zako za usajili,na kama taarifa si sahihi tafadhali wasiliana na kampuni husuka haraka sana.

No comments:

Post a Comment