Thursday, April 11, 2013

MAELEZO YA ZITTO KABWE KUHUSU BARUA ALIYOMUANDIKIA SPIKA MAKINDA

"Nimeandika barua Kwa Spika wa Bunge kutaka Waziri wa Nishati na Madini kutoa maelezo Bungeni kuhusu uamuzi wake wa kuwapa leseni kubwa ya kuchimba #Uranium huko wilayani Namtumbo. Mnamo tarehe 10 Agosti 2012 Waziri alitamka ndani ya Bunge "sisi tunajua zaidi ya anavyojua yeye, Leseni haijatolewa na haitatolewa mpaka Kampuni ya #MantraResources ilipe kodi".

Kodi ya ongezeko la mtaji (capital gains tax) ya $189m kufuatia mauzo ya mradi wa #MkujuRiverProject kutoka kampuni ya Mantra kwenda kampuni ya AMRZ ya Urusi iligomewa kulipwa. #TRA wamepeleka shauri hilo mahakama ya kodi na mpaka sasa maamuzi hayajatolewa. Kwa mujibu wa mabadiliko ya Sheria ya mwaka 2012, kabla ya Waziri mwenye dhamana ya madini kubariki mauzo ya kampuni, anapaswa kupata Kibali Cha kwamba kodi zote stahili zimelipwa. Kibali Kwa kampuni ya mantra kilitolewa bila kujali hitaji la kisheria na sasa kampuni hii imepewa leseni.

Maamuzi haya ya Waziri wa Nishati na Madini yanalikosesha Taifa mapato ya zaidi ya tshs 300bn ambazo zingeweza kumaliza tatizo la nyumba za walimu nchi nzima na kulipia madai yote ya walimu. Fedha hizi zingeweza kujenga barabara ya lami kutoka Manyoni mpaka Itigi. Fedha zingeweza kukarabati reli ya Kati na kuirejesha katika ubora wa unaotakiwa. Kwa mujibu wa kanuni za Bunge nimetaka Waziri atoe maelezo bungeni na wabunge wajadili. Ni dhahiri kwamba serikali inayoongozwa na CCM imeamua kumaliza utajiri wote wa nchi na kuugawa Kwa wageni Kwa bei ya Che. Wananchi Ni lazima kusimama imara kukataa uporaji huu na maamuzi haya ya kiburi Cha kudharau Bunge yaliyoyafanywa na Serikali.

BUNGE LA BAJETI WABUNGE WAPANGUA KANUNI

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akiuliza swali katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa 11 wa Bunge la Bajeti, Dodoma Picha na Edwin Mjwahuzi
 Spika wa Bunge, Anne Makinda akipitia makabrasha yake wakati akiongoza kikao cha kwanza cha Mkutano wa 11 wa Bunge la Bajeti, Dodoma jana

Dodoma. Baada ya siku mbili za mjadala mzito kuhusu mabadiliko ya Kanuni za Bunge, jana Bunge limepitisha azimio la mabadiliko yanayohusu utaratibu wa kutunga sheria kuhusu mambo ya fedha pekee.

Kwa uamuzi huo, mambo mengine ambayo yalikuwa yamependekezwa lakini hayahusiani na sehemu hiyo, yaliachwa baada ya kuibua mjadala mzito na kupingwa na baadhi ya wabunge.
Miongoni mwa mabadiliko yaliyofanyika, muda wa kuchangia hoja kwa wabunge katika Mkutano wa Bajeti unaoendelea umepunguzwa kutoka dakika 15 hadi 10, huku wabunge wakipigwa marufuku kutumia muda wao adhimu kutoa pongezi na pole, bali kuingia moja kwa moja kwenye hoja.

Hayo yaliamualiwa jana bungeni baada ya Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni za Bunge na Naibu Spika, Job Ndugai kuwasilisha azimio la marekebisho ya kanuni za Bunge ambalo lilipitishwa.

Akichangia hoja ya azimio hilo Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu hakutaka muda wa kuzungumza upunguzwe kwa kuwa sehemu hiyo ni sehemu ya mazungumzo na si vinginevyo.

Hata hivyo Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki alikubaliana na pendekezo la kubadili muda kutoka dakika 15 hadi 10 akieleza kuwa litatoa nafasi kwa wabunge wengi kuchangia.

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Anna Abdallah alisema mabadiliko hayo yanalipa Bunge uwezo wa kuisimamia Serikali katika mambo ya fedha.Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid alisema dakika 10 ni nyingi na mtu akijipanga vizuri zinatosha kukamilisha hoja zake.

Suala jingine ambalo limefanyiwa mabadiliko ni kuwekwa uwiano wa kuchangia hoja ambapo wabunge sasa watapangwa kulingana na idadi yao kivyama.

No comments:

Post a Comment