Thursday, April 18, 2013

SUMATRA Yawataka Abilia Kudai Tiketi Kwenye Mabasi

Na Mwandishi
Bukoba

WASAFIRI wanaotumia usafiri wa magari ya kusafirishia abilia mkoani Kagera wametakiwa kuhakikisha kila wanapopnda vyombo hivyo vya usafiri wanapatiwa tiketi ambazo zimeandikwa nauli halali zilizopitishwa na mamlaka ya usafiri wa majini na nchi kavu(SUMATRA) hivi karibuni.

Hayo yamesemwa na afisa mfawidhi wa mamlaka hiyo mkoani Kagera Kapteni Alex Katama wakati akizungumza na Tanzania daima na kusema kuwa mara nyingi wasafirishaji wa abilia wamekuwa wakipandisha nauli kihorela kutokana na kutotoa tiketi kwa abilia wao.

Alisema kuwa hii inachangia mara nyingi wasafiri kujikuta wanalipa nauli zaidi kutokana na kutodai tiketi hizo ambazo zinakuwa zimekaguliwa na mamlaka ya usafiri wa majini na nchi kavu (SUMATRA).

"SUMATRA inatangaza viwango vya nauli lakini unakuta wasafiri wanalipa nauli tofauti na ambazo zinatangazwa na mamlaka husika hii inatokana na watu kutokuwa na jadi ya kudai tiketi ambazo ni halali jambo hili litaedelea kuleta malalamiko kwa wasafiri na serikali kulaumiwa bila sababu"alisema Katama.

Aidha alisema kuwa kuna baadhi ya abilia wanaona kero kubwa kudai tiketi hizo na kuwa baadhi ya wasafirishaji ambao wanafuata sheria wanapowakatia tiketi abilia wengine wanazikataa kwakuwa wanaona hazina umuhimu.

Katika hatua nyingine
 afisa huyo alisema kuwa tamgu SUMATRA makao makuu itangaze mabadiliko ya nauli mpya hapa nchini katika mkoa wea Kagera viwango vingi vimebaki pale pale na wananchi hawajaleta malalamiko yoyote juu ya upandishaji holera wa nauli tofauti na zilizopitishwa.

Kwa upande wao wasafiri wanaotegemea usafiri kila siku walesema kuwa viwangoi sambavyo vilipitishwa na SUMATRA maeneo mengine vinawanyonga wananchi lakini kwingine viwango ni vyakawaida lakini waiimba serikali kuhakikisha wanafuatilia kwa karibu wasafirishaji ili wasije pandisha nauli kihorera.

Aidha waliimba SUMATRA ihakikishe inakagua magari yote kama yamebandika mabadilko ya nauli ndani ya magari yao ili wasafiri wajue nauli ambazo inawabidi kuzilipa bila kulalamika.

MWISHO

No comments:

Post a Comment