Friday, April 12, 2013

Kagera Press Club yafanya mkutano Mkuu Wa Mwaka 2013


Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Kagera(KPC) kimefanya Mkutano Mkuu wa mwaka,ambapo pamoja na mambo mengine kimejadili na kupitisha wanachama wapya.

Katika Mkutano huo uliofanyika ukumbi wa St Francis,mjini Bukoba pia wanachama walijadili taarifa mbali mbali zilizowasilishwa na uongozi na kufikia maazimio mbalimbali.


Miongoni mwa maazimio ya Mkutano huo,ni kuendeleleza umoja kwa ajili ya ustawi wa chama,huku waandishi wa habari wakikumbushwa kufanya kazi zao kwa maadili na weredi.


Pia Mkutano huo ulimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe,pamoja na wadau wengine wa Kagera Press Club ambao kwa nyakati tofauti wameunga mkono juhudi za Umoja huo ili kufikia malengo yake.

Baadhi ya waandishi wa habari katika matukio mbalimbali ndani na nje ya ukumbi,Baadhi wakikagua vifaa vya kisasa vya kazi na wengine wakitoa michango yao.

Katibu wa chama cha waandishi wa habari mkoa Ndg Phinias Bashaya na Mwenyekiti John Rwekanika
 Method Kalikila wa Gazeti la Rumuli na Livinus Feruzi wa Gazeti la Majira wakifuatilia mjadala
Ayoub Mpanja(Radio Free Africa)Ashura Jumapili-Tanzania Daima
Mathias Byabato-Channel Ten
Antidius Kalunde Mkuu Wa Bukoba Jamii Akijaribu Mambo
Ashura Jumapili-Tanzania Daima
Mdau Arodia Domonick,Radio Karagwe akimpa mtoto haki yake
Winrida Saimon Mwandishi wa Gazeti la Ijawebonele linalomilikiwa na ELCT/Dayosisi ya Kaskazini Magharibi
Meddy Mulisa-Mhariri Radio Kasbante na mwandishi wa Daily News akinukuu mambo muhimu wakati wa mkutano.
Anaonekana Jonas Mchunguzi-Mwandishi na mtaalamu wa kupiga picha  za habari na matukio akikagua kamera ya kisasa.
 Prudence Kibuka-Nipashe  akiendeleza majadiliano na wenzake wakati wa mapumziko.
 Picha kwa Hisani ya Phinias Bashaya

No comments:

Post a Comment