Tuesday, October 9, 2012

Matukio Mbalimbali

 Dr Diodorus Kamala balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji akiwa katika picha ya pamoja na Watanzania na Watanzania waliomkaribisha nchini humo.
 Mke wa Balozi Kamala kulia akiwa na baadhi ya Watanzania waliomkaribisha nchini Ubelgiji.
Watoto wa Balozi Kamala waliovaa nguo za zambarau walikuwa miongoni mwa walioudhuria sherehe ya kumkaribisha na Dr. Kamala nchini Ubelgiji  iliyoandaliwa na Watanzania waishio nchini humo.

UONGOZI WA YANGA WAKANUSHA HABARI ZA UZUSHI

 Mchezaji wa yanga Osca Joshua akiwa ndani ya chumba chake.
 Wachezaji wa timu ya YangaOmega na Frank wakiwa wamejipumzisha ndani ya vyumba vyao.
 Meneja wa hoteli ya Smart ambayo wachezaji wa timu ya yanga walikuwa wamefikia.



Na Mwandishi wetu maalumu
VIONGOZI, wachezaji wa timu ya Yanga African na uongozi wa hoteli ya Smart ambayo hiyo ilikuwa imefikia ilipokuwa mkoani Kagera kucheza ligi kuu ya vodacom na timu ya Kagera sugar wamepinga vikali  taarifa zilizochapishwa kwenye moja ya  chombo vya habari.
Kwa nyakati tofauti wakati wakiongea na vyombo mbalimbali vya habari vilivyoko mkoani Kager wamesema sio kweli kwamb wachezaji wa timu hiyo uongozi uliwalaza mzungu wa  nne yaani chumba kimoja kwa wachezaji wa nne.
Walisema taarifa hizo sio sahihi kuwa zinalenga kuugawa uongozi wa timu hiyo na washabiki wake pamoja na wanachama, kiongozi  wa msafara wa timu hiyo Tito Osollo aliwaambia waandishi wa habari kuwa chumba kimoja kilikuwa kinatumiwa na wachezaji wawili tu.
“Walioandika habari hizi wanatumiwa haiwezekani mwandishi akaandika habari kuwa sababu za timu ya Yanga kufungwa na Timu ya Kagera Sugar kwamba zimechangiwa na wachezaji wane kulala chumba kimoja” alisema.
“Mwandishi aliyeandika habari hizi hafai kabisa ni mwongo na ninawaomba wanachama na mapenzi ya timu ya Yanga kumpuuza , hayuko makini na kazi yake hivyo anafanya kazi kwa matakwa ya wanaomtumia” alisema Osollo kwa hasira.
Alisema Club ya yanga kamwe haitawavumulia waandishi wanaotaka kuchonganisha wachezaji, wapenzi, wanachama na viongozi wa timu hiyo, “ Tumefungwa, unaposhindana tegemea mambo mengi kushinda, kushindwa na kutoka sare” alimaliza.
Kutokana sakata hilo meneja  wa hoteli ya Smart ameahidi kumfikisha mwandishi wa habari aliyeandika habari za upotoshaji kuwa wachezaji wa nne wa timu ya Yanga walikuwa wanalala ndani ya chumba kimoja.
“Nimeishawasiliana na mwanasheria wetu tunaandaa hati ya madai, mwandishi huyu nitamdai fidia ya shilingi bilioni 2 , ameidhalilisha hoteli yangu, sasa namshughulikia ipasavyo, nitamshtaki kama yeye sio chombo, chomo hakikumtuma aandike habari za uongo” alisema kwa msisitizo.
Nao wachezaji wa yanga walioongea kwa nyakati tofauti walikanusha taarifa hizo kwa kusema kuwa uongozi wa klabu ya Yanga haukuwalaza wachezaji wane kwenye chumba kimoja.

PROFESA LIPUMBA AWASILI KAGERA

Msafara ulienda kumpokea mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba.
Profesa Lipumba akiwa kwenye gari la wazi akiwapungia wananchi mara baada ya kuwasili mkoani Kagera ambapo atafanya mkutano wa hadhara katika kata ya Bakoba.

Monday, October 8, 2012

ZIARA YA MKUU WA MKOA KAGERA WILAYANI MULEBA

 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Massawe Akiwa Katika Picha ya Pamoja na Uongozi wa Shule ya Sekondari ya Katoke Lweru.
Mkuu wa Mkoa Akiongea na Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza Katika Shule ya Sekondari Katoke Lweru.

PINDA AKIWEKA SHADA LA MAUA KWENYE KABULI LA KARDINARI RUGAMBWA

VIJANA WAMUENZI PROTACE ISHENGOMA

jumuia ya umoja wa vijana ya CCM ikipatia hati maalumu kamanda wa UVCCM wa wilaya ya Misenyi, Protace Ishengoma

UCHAGUZI WA JUMUIA YA VIJANA CCM MKOANI KAGERA

 Vijana wakishangilia kabla ya uchaguzi
 Mmoja wa wagombea wa nafasi ya uenyekiti wa VCCM mkoani Kagera.
 Mjumbe wa NEC wa wilaya ya Karagwe Amri Karim alikuwa miongoni mwa walioudhuria mkutano wa uchaguzi wa UVCCM wa mkoa wa Kagera.

Makada wa CCM mkoani Kagera.

Sunday, October 7, 2012

MANDHARI YA MKOA WA KAGERA

 sehemu ya mji wa Bukoba.
 Mitaa ya mji wa Bukoba.
 Sehemu ya mto Kagera.
 Mto Ruvuvu ulioko wilayani Ngara.
Uwanja wa ndege wa Bukoba.

UGONJWA WA MNYAUKO WAENDELEA KUHATARISHA USALAMA WA NDIZI KAGERA

UGONJWA unaoshambulia migomba wa mnyauko bacteria umeanza kuathiri upatikanaji wa ndizi kwenye maeneo mbalimbali yaliyoko mkoani Kagera.

Ugonjwa huo unasambaa kwa kasi hasa kwenye maeneo ya wilaya za Muleba na Karagwe ambayo uzalisha  ndizi nyingi mkoani Kagera na maeneo mengine ya wilaya za Bukoba na Misenyi.

Hali ya ugonjwa huo unaoshambulia migomba wa mnyauko bacteria imechangbia kupunguza uzalishaji wa ndizi mkoani Kagera jambo ambalo limechangia kupanda kwa bei ya ndizi zinapopelekwa kwenye masoko.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kwamba kwenye soko kuu la Bukoba ndizi kubwa inauzwa kwa wastani wa kati shilingi 15,000 hadi 20,000 ambapo miaka iliyopita ndizi kubwa zilikuwa zinauzwa kwa wastani wa kati ya shilingi 6,000 hadi 8,000.

Kupanda kwa bei ya ndizi iliyochangiwa na ugonjwa wa mnyauko bacteria wa migomba kumewalazimisha baadhi ya wakazi wa mkoa wa Kagera ambao hutegemea ndizi kama chakula chao kikuu kubadilika ambapo sasa wanalazimika kula ugali na wali.

Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Kagera wamelazimika kubadili fikira zao za kudhani kuwa ndizi ndicho chakula kikuu baada ya kushindwa kumudu gharama za kununua ndizi kwenye masoko ambazo bei yake ni kubwa.

Baadhi ya wakulima bora wa migomba mkoani Kagera ambao mashamba yao yameathirika kutokana na ugonjwa wa mnyauko bacteria wa mogomba ni pamoja kamishina mstaafu wa jeshi la polisi Alfred Tibaigana.

Kamishina Tibaigana shamba lake liko katika kijiji cha Buganguzi wilayani Muleba limeathirika sana, Mkulima huyu kabla ya ugonjwa huu alikuwa na uwezo wa kuzalisha wastani tani 40 za ndizi kwa wiki ambapo sasa anazalisha wastani wa tani zisizozidi 10 kwa wiki.

Aidha, baadhi ya wakulima mkoani Kagera wameitahadharisha serikali kuchukua hatua za haraka za kuthibiti ugonjwa huu unaosambaa kwa kasi ili zao la ndizi mkoani Kagera lisibaki kwenye vitabu vya historia.

Saturday, October 6, 2012

WAZIRI MKUU PINDA AWASILI KAGERA

 Waziri mkuu Mizengo Pinda  akisalimiana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya usalama ya mkoa wa Kagera mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba kuhudhuria uzinduzi wa kanisa kuu la jimbo katoriki la Bukoba.
 Mkuu wa mkoa wa Kagera kanali mstaafu Fabian Massawe akimpokea Pinda.
Massawe akiongea jambo na waziri wa mali asili na utalii Balozi Khamis sued Kagasheki wakati wakisubili ujio wa waziri mkuu, Pinda kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba, kushoto ni katibu tawala wa mkoa wa Kagera Nassor Mnambila na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Kagera.

RAIS KIKWETE AFUNGUA MKUTANO WA DIASPORA JIJINI EDMONTON, CANADA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na ujumbe wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) katika ukumbi wa mikutano wa Fantasy Land jijini Edmonton, Canada, baada ya kufungua mkutano wa Watanzania waishio nchini humo (Tanzania Diaspora Conference) Ijumaa Oktoba 5, 2012

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua vifaa vya kukamu asali baada ya kufungua maonyesyesho ya mazo ya asali kwenye uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dae sa salaam Oktoba 5, 2012 kulia kwake ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdallh Kigoda. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MATAGE MKUU WA UPELELEZI WA JESHI LA POLISI KAGERA AAGWA

Baadhi ya askari walioudhuria sherehe za kumuaga Peter Matage anayehamia makao makuu ya jeshi la polisi.
Viongozi walioudhuria sherehe ya kumuaga Matage.
 Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Philip Kalangi, akiwatambulisha viongozi wa serikali walioudhuria sherehe za kumuaga Matage.
 Baadhi ya maofisa wa jeshi la polisi.
 Baadhi ya askari wa kikosi cha usalama barabarani walioudhuria sherehe hiyo.
 Baadhi ya askari wakigonganisha glasi na viongozi waliodhuria sherehe hiyo.
 Matage (kushoto) anayehamia makao makuu ya jeshi la polisi akiwa kwenye picha mkuu mpya wa upelelezi wa mkoa wa Kagera aliyetokea Zanzibar.
 Mtaalamu China, alikuwa miongoni mwa walioudhuria sherehe ya kumuaga Matage.
Matage akiwa ameshika tuzo aliyoipokea toka kwa mwakilishi wa mkoa wa Kagera, Fikir Kisimba, ilitolewa na askari wa kikosi cha upelelezi.

Thursday, October 4, 2012

RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE KATIKA ZIARA RASMI OTTAW, CANADA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na  ujumbe wake katika mazungumzo na  Gavana Jenerali wa Canada Mhe. David Johnson na mkewe Mama Sharon Johnson na viongozi wa serikali ya nchi hiyo katika  jumba la Rideau jijini Ottawa, Canada, katika hatua yake ya kwanza ya  ziara rasmi ya siku mbili jijini humo Jumatano Oktoba 4, 2012

ZITTO KABWE ACHANGIA BIMA YA AFYA KWA MJANE WA MWANGOSI NA MWANAWE KUPITIA NSSF

KATIKA siku ya mwisho ya harambee ya kumchangia mjane wa marehemu Daud Mwangosi, Ndugu Zitto Kabwe amejitolea kumchangia mjane wa marehemu kwa kumlipia ada ya uanachama wa Mfuko wa Hifadhi ya Kijamii (NSSF) kwa kila mwezi na kwa miaka mitatu mfululizo.

" Nimeona nami niunge mkono harambee hii.Pamoja na michango ya fedha iliyotolewa kumsaidia mjane kuanzisha mradi wa kujikimu, mimi naona ni muhimu pia mjane akawa na hakika ya huduma ya afya yake na watoto wake wanne. Hivyo, mchango wangu utakuwa ni kwenye eneo hilo Bima ya Afya na kwa miaka mitatu." Anasema Zitto Kabwe alipoongea na Mjengwablog.com, mtandao wa Kijamii ulioratibu harambee ya mjane wa Daud Mwangosi.


Hii ni mara ya pili kwa Ndugu Zitto Kabwe kuchangia kwenye masuala ya kijamii kupitia mtandao wa kijamii wa Mjengwablog.com, mara ya kwanza ni alitoa mchango wake pale Mtandao wa Mjengwablog.com ulipoendesha harambee ya kuwachangia watoto wa Somalia waliokuwa katika hatari ya kufa kwa njaa.


Katika harambee iliyomalizika Jumapili ya Septemba 30 mwaka huu na iliyochukua kipindi cha mwezi mmoja,zaidi ya shilingi milioni tano na nusu zimekusanywa.


Mchango huo wa Ndugu Zitto Kabwe una maana mjane wa marehemu ataweza kuwa na hakika ya yeye na watoto wake wanne kupata huduma za afya bila kufikiria malipo kwa kipindi cha miaka mitatu. Baada ya hapo,michango ya mjane huyo ya kila mwezi kwa mfuko huo wa hifadhi ya kijamii ( NSSF) ambayo atakuwa akilipiwa na Ndugu Zitto Kabwe itakuwa ni malimbikizo ya akiba yake ambayo mjane atakuwa na uwezo wa kuichukua kama akipenda. Kwa sasa mjane wa Daud Mwangosi hayuko kwenye utaratibu wowote wa Bima ya Afya, kwake yeye na wanawe.


Harambee ya mjane wa Daud Mwangosi iliyoendeshwa kwa uwazi kwa njia ya MPESA, TigoPesa, Airtel Money, NMB Mobile na Western Union ilimwezesha mchangiaji kuliona jina lake na mchango wake kwenye orodha ya wachangiaji iliyokuwa ikiwekwa mtandaoni kila siku. Michango ilikuwa ni hiyari, hakuna aliyeombwa kutoa na utaratibu haukuruhusu ahadi za kuchangia, bali, mwenye nacho alitoa na hapo hapo kuorodheshwa kama mchangiaji. Utaratibu haukuruhusu pia michango iliyofungamana na siasa za vyama.


Hatua hiyo ya uwazi na kutanguliza ubinadamu na si itikadi kwenye uchangiaji imechangia kupelekea Watanzania wengi wa kada zote, kwa namna moja au nyingine kushiriki kwenye kuchangia. Kuna waliochangia shilingi elfu moja na kuna waliochangia mpaka shilingi milioni moja.


Ari hii ya Watanzania kujitolea kusaidiana kwenye hali kama iliyomkuta mjane wa Daud Mwangosi imedhihirisha umoja na upendo tulionao kama Watanzania, na pia imeonyesha jinsi tunavyoijali amani yetu na hivyo jamii, kupitia michango hii, imeonyesha pia kwa vitendo, dhamira ya kulaani kwao vitendo vya maovu na vinavyotokana na matumizi ya nguvu yasiyo ya lazima kama kile kilichomtokea mwandishi Daud Mwangosi.


Baadhi ya watu maarufu katika jamii waliojitokeza kwa hiyari yao kumchangia mjane wa Daud Mwangosi kupitia mtandao wa kijamii wa Mjengwablog.com ni pamoja na Shy- Rose Bhanji, Ananilea Nkya, John Bukuku ( Mmiliki wa Fullshangwe.blog) na Ndugu Mobhare Matinyi aliyepata kuwa mhariri wa gazeti la Majira.


Michango kwa mjane wa Daud Mwangosi itaingizwa kwenye akaunti ya mjane ya CRDB, Iringa leo alhamisi, Oktoba 4, 2012. Vielelezo vya kibenki vitawekwa kwenye mtandao wa Mjengwablog.com kwa kila mmoja kuona jumla iliyowasilishwa kwa mjane na orodha ya majina ya wachangiaji.

No comments:

Post a Comment