Wednesday, October 31, 2012

Kongamano La Afya Ya Uzazi Kwa Vijana

 naibu meya wa manispaa gervas ndaki
mratibu wa maadhimisho meshack mollel
Baadhi ya washiriki
wadau kutoka manispaa mshana mbele na mushi aliyekaa nyuma)
  dr mariam mohamed
Na Denis Mlowe - Iringa
 Maadhimisho ya siku ya afya ya uzazi kwa vijana kwa mwaka 2012 yaliyoandaliwa na wizara ya afya kitengo cha uzazi na mtoto kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la AMREF na wadau wengine yamefanyika mkoani Iringa katika ukumbi wa Highland Hall na kuhudhuriwa na rika za watu mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari. Maadhimisho hayo yaliyokuwa na kauli mbiu ya "Andaa taifa bora kwa kuwekeza katika afya ya uzazi wa vijana" mgeni rasmi alikuwa katibu tawala wa mkoa aliyewakilishwa na msaidizi wake pia yalihudhuriwa na naibu meya wa manispaa Gervas Ndaki, mkuregenzi wa manispaa na mwakilishi wa vijana yalikuwa na lengo la kuongeza ufahamu kwa vijana katika suala zima la afya ya uzazi kwa vijana. Mratibu wa maadhimisho hayo kutoka AMREF, Ndugu Meshack Mollel amesema kwamba wizara ya afya kupitia AMREF na wadau mbalimbali wamewezesha maadhimisho hayo kufanyika kwa mara ya kwanza mkoani hapa na ni kitu cha kujivunia kwa mkoa wa iringa kwa kuwa mwaka jana lilifayika jiji dar es salaam na litakuwa faida kubwa sana kwa vijana wa mkoa huu katika kujadili na kuwa na ufahamu mkubwa sana katika suala zima la afya ya uzazi kwa vijana na kutetea na kujenga afya bora kwa vijana wote. Afya ya uzazi kwa vijana yamekuwa na mafanikio makubwa sana kwa vijana tangu yalipoanzwa kufundishwa kwani yamefanikiwa kushirikiana kwa vijana katika kubadilishana uzoefu na utaalamu juu ya afya ya uzazi kwa vijana, aidha yamewezesha vijana kujenga uwezo wa kutetea hoja mbali mbali za kuimarisha afya ya vijana katika uzazi Aidha afya ya uzazi kwa vijana ina changamoto kubwa kama kuwa na majukumu kwa wadau kutotekelezwa ipasavyo na mabadiliko ya mara kwa mara ya uongozi katika asasi mbalimbali ni changamoto nyingine katika afya ya uzazi kwa vijana na kutokuwa na chombo cha kitaifa kinachounganisha wizara zote. Mratibu wa afya ya uzazi na mtoto katika manispaa ya Iringa Dr. Mariam Mohamed  amesema kwamba kuna vituo 42 ndani ya manispaa vinavyotoa huduma ya afya ya uzazi kwa vijana. "Vituo hivyo vinakumbana na changamoto ya upungufu wa watumishi wa afya ya huduma rafiki kwa vijana, ushiriki mdogo wa wazazi katika kupata elimu ya uzazi kwa vijana aidha mfumo wa ukusanyaji wa taarifa na vituo kutokuwa na alama ya utambulisho ndio changamoto" alisema Dr Mariam Mohamed Aliongeza kwa kusema matarajio ya manispaa ni kuongeza watumishi katikam vituo mbali mbali aidha kushirikiana na jamii katika kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana na kusimamia takwimu na kushirikiana na wadau wa mikoa Njombe, Mbeya katika elimu ya afya ya uzazi.
Reactions::

No comments:

Post a Comment