John Magufuli akizungumza na wafanyakazi wa kampuni ya CHICO
Magufuli akikagua barabara inayokarabatiwa na kampuni ya CHICO kutoka nchini China baada ya kujenga chini ya kiwango mwaka 2008
Meneja TANROADS mkoa Singida Yustak Kangole akitoa taarifa ya marudio ya ujenzi wa barabara Sekenke-Shelui, km 33.3, kwa waziri
Singida.
Oktoba09,2012.
Makandarasi.....
WIZARA
ya Ujenzi imewakumbusha Wakandarasi nchini kujenga barabara
zinazolingana na thamani ya fedha, iliyopo kwenye mikataba yao.
Agizo
hilo limetolewa leo mkoani Singida na Waziri John Magufuli, wakati
anakagua marudio ya ujenzi wa barabara, eneo la mlima Sekenke-Shelui,
yenye urefu wa kilomita 33.3.
Amesema
serikali imetumia zaidi ya Sh.Bilioni 35, kugharamia ujenzi huo, lakini
mkandarasi China Henan International Cooparation Group Co Ltd(CHICO),
ilijenga chini ya kiwango.
Aidha ameuagiza
uongozi wa kampuni hiyo kuwapatia wafanyakazi wake vifaa vya kufanyia
kazi, hasa viatu na gloves kwa ajili ya kuvaa mikononi.
Hata
hivyo meneja TANROADS Mkoa Singida, Yustak Kangole amesema barabara
hiyo baada ya kukamilika Januari, 2008, ilichukua miezi miwili kuanza
kubomoka, kutokana na ujenzi hafifu.
Kwa
mujibu wa meneja mradi wa barabara hiyo, mhandisi Stone Chen, marudio
ya ujenzi yanaigharimu kampuni zaidi ya S h.Bilioni kumi.
Na Elisante John
No comments:
Post a Comment