Thursday, May 23, 2013

WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI TUMAINI MANISPAA YA BUKOBA WAKO HATARINI KUPATA MAGONJWA YA MILIPUKO.

 wanafunzi na walimu wa shule ya msingi Tumaini manispaa ya bukoba wako hatarini kupata magonjwa ya milipuko kutoka na wapita njia kutumia  vyoo vya shule kutokana na ukosefu wa uzio katika shule hiyo,Akiongea kwa masikitiko mwalimu mkuu wa shule hiyo Tegamaisho Deogratias alisema wakazi wengi wanaoishi kashai ukatiza katika maeneo ya shule ,na wengi wao hutumia vyoo vya shule,bwana tegamaisho aliendelea kusema kuwa baadhi ya wazazi wameleta malalamiko kuhusu watoto wao ambao wamekutwa na tatizo la UTI,kingali ni watoto wadogo.
 changamoto nyingine waliyonayo ni uchakavu wa miundo mbinu,mwalimu tegamaisho amesema wakati wakifidia kupisha ujenzi wa uwanja wa ndege walipewa kiasi cha shilingi laki sita kwa ajili ya miti na mazao yaliyokuwa katika eneo hilo, lakini uharibifu wa miundo mbinu na majengo uliotokea katika shule hiyo hawakuwahi kulipwa chochote, kitu ambacho kimesababisha wanafunzi kusoma katika mazingira magumu sana,amesema shule hiyo imeezekwa na mabati ya udongo(vigae) amayo ni ya miaka mingi sana ambayo yameishatoboka na kipindi cha mvua wanafunzi wanalazimika kusogeza madawati  maeneo ambayo hayavuji.



 Wanafunzi wa shule ya msingi Tumaini wakimsikiliza Mwalimu mkuu wao wakati wa mkusanyiko Shuleni hapo PICHA KWA HISANI YA JAMCO

No comments:

Post a Comment