Tuesday, May 21, 2013

Rais obama kuzuru Afrika ikiwemo Tanzania

obama 087f8
Rais wa Marekani, Barack Obama

White House imesema Rais. Obama atakwenda Tanzania, Afrika Kusini na Senegal.
White  House inasema rais wa Marekani Barack Obama atakwenda Afrika  mwishoni mwa mwezi wa sita ambapo atazuru nchi tatu.

Katika taarifa Jumatatu jioni, White House  ilisema rais Obama na mke wake Michelle watakwenda Senegal,  Afrika Kusini na Tanzania mwishoni mwa Juni na mapema mwezi Julai.
Utawala wa rais Obama  unasema rais huyu wa Marekani atakutana na maafisa wa serikali, viongozi wa kibiashara, asasi za kiraia na makundi ya vijana.

Safari ya bw.Obama itaanza Juni 26 mpaka Julai 3 na inalenga kudhihirisha mahusiano ya karibu kati ya Marekani na nchi za Afrika, kusini mwa jangwa la Sahara.

Rais Obama ambaye baba yake alizaliwa Kenya, alizuru Afrika  mara moja  katika muhula wake wa kwanza, alipotembelelea Ghana mwaka 2009.

Mkewe Michelle Obama pia amesafiri kwenda Afrika Kusini na Bostwana. Chanzo: voaswahili

No comments:

Post a Comment