Monday, May 20, 2013


MOTO WATEKETEZA DUKA USWAHILINI BUKOBA USIKU WA JANA NA KUSABABISHA HASARA KUBWA

 Ni mabaki ya vitu vilivyoteketea kwa moto baada ya duka la mfanyabiashara aliejulikana kwa jina la baba sima kuungua maeneo ya uswahilini karibu na maua gest

 duka lililoungua moto lipo uswahilini barabara ya maua gest,inasemekana machinga wengi wa mtaa huo walikuwa wakiweka mizigo yao katika duka hilo wakifunga shughuli zao muda wa jioni
 chanzo cha moto hakijafahamika, ila kwa habari zisizo rasmi inasemekana na tatizo la umeme baadhi ya vitu vilivyookolewa kutaka katika duka  la baba sima

 ilimradi kilikusanywa kila kilichoonekana hakijaungua

 baba sima mwenye duka (kushoto) akifarijiwa
 wayuka baba sima ebintu mbiigwa orwo omoyo gwaunga( ONGERA BABA SIMA VITU UTATAFUTA BORA UZIMA ni maneno ya mama akimfariji


tunakupa pole sana baba sima

Friday, 17 May 2013

MSAFARA WA MAGARI UNAOPITA MIKOA MBALIMBALI KUTOA ELIMU KUHUSU FISTULA WAZINDULIWA BUKOBA

Balozi wa vodacom Mwana FA akimsikiriza mgeni rasmi mkuu wa wilaya bukoba mama zippola pangani muda mfupi kabla ya kumpa funguo za gari ndogo tax itakayo zunguka maeneo yote yaliyopangwa kutoa elimu kuhusa fistula inatibika.


 umati wa watu ukisikiliza elimu kuhusu fistula, ugonjwa unaowapata akina mama wakati wa kujifungua


 Ni shirika lisilo la serikali ambalo linawataalamu wakiwemo madakitari, kampuni ya vodacom imewakabidhi kiasi cha shilingi bilioni nane kusaidia kutibu wakina mama wenye fistula shirika hili hutoa huduma za matibabu bure zikiwemo na gharama usafiri,chakula na malazi,baada ya wataalamu kubaini tatizo lafistula
 katibu tawala wa mkoa wa kagera(kushoto) akikaribishwa eneo la tukio soko kuu bukoba

 meneja mahusiano ya nje vodacom salumu mwalimu akitoa maelezo kwa nini vodacom imeamua kusaidia akina mama katika janga hili la fistula,kikubwa alisema vodacom kile inachokipata inajari sana huduma za jamii,na aliwataka wamama wanapopata vistura wasikate tamaa ya maisha vodacom kazi ni kwako
 Balozi wa vodacom mwana FA akisikiliza kwa makini

 Bi naima ishengoma mkazi wa katoro bukoba vijijini akitoa ushuhuda ,baada ya kupata  fistula mwanaume alimkimbia,lakini kupitia redio karagwe alipata habari na alipelekwa CCBRT na sasa amepona,aliwasisitiza wamama ambao fistula wasikate tamaa unatibika, tena huduma bure
 shuhuda sofia ibrahimu wa kyerwa karagwe,pamoja na ushuhuda mwingi aliotoa alimshukuru mume wake amidu winstoni kwa kumvumilia kipindi chote cha ugonjwa bila kumnyanyapaa,kumtenga,na kumuhudumia mpaka sasa kapona
 katibu tawala mkoa wa kagera akimkaribisha mgeni rasmi azungumze

 mgeni rasmi mkuu wa wilaya bukoba akitoa neno kwenye uzinduzi wa msafara kupita mikoa mbalimbali kutoa elimu kuhusu fistula inatibika
 piga hiyo namba ni bure eleza tatizo lako la fistula utasaidiwa
 ni gari maalumu linotumika katika msafara
 Balozi wa vodacom mwana FA kwa heshima ya wakazi wa bukoba alimwaga mistari


 Dj slay kwa siku hiyo alikuwa mc wa shughuli nzima,hapo yupo na balozi wa vodacom mwana FA

 Ulifika wakati wa mgeni rasmi kukabidhi ufunguo kuashiria uzinduzi wa msafara

 mmiliki wa jamcobk.blogspot.com akiwa na balozi wa vodacom mwana FA


MENEJA MAHUSIANO YA NJE VODACOM AKIONGEA NA VYOMBO VYA HABARI KABLA YA MSAFARA KUONDOKA KUPITIA ,CHATO,GEITA, MWANZA , SHINYANGA,SINGIDA,MOROGORO NA ATIMAE TAREHE 23-5-2013 MSAFARA UTAPOKELEWA NA MH RAIS JAKAYA KIKWETE,PONGEZI VODACOM NA CCBRT KWA KUONYESHA UZALENDO KWA AKINA MAMA

No comments:

Post a Comment