Saturday, July 6, 2013

Mwaka Huu Wetu


ARSENAL WAANZA MAANDALIZI YA MSIMU MPYA

gana edbdc
Theo Walcott akifanya mazoezi (HM)
gana2 0be6b
gana3 fe806
gana4 b7d25
NYOTA wa uzito wa juu wa Arsenal wamerejea mazoezini jana asubuhi huku kikosi cha Arsene Wenger kikianza maandalizi ya msimu mpya.
The Gunners wakielekea kwenye kampeni ya kushinda taji la kwanza kwa zaidi ya miaka nane, wachezaji walifanya mazoezi mepesi ya kukimbia na kunyanyua vitu vizito katika Uwanja wao wa mazoezi wa Colney, London. 

Mashabiki wa Arsenal watamuona Jack Wilshere akifanya mazoezi kikosini, na wengi wakiamini uimara wa nyota huyo wa England ni dalili nzuri kwa kikosi cha Wenger kuelekea msimu mpya. Chanzo: sportmail


No comments:

Post a Comment