KAMATI
Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) itakutana katika
kikao cha dharura kwa siku mbili mfululizo, kuanzia tarehe 6-7 Julai,
2013, jijini Dar es Salaam.
Katika
muda huo wa siku mbili, kikao hicho kitajadili masuala mbalimbali,
ambapo agenda zitakuwa; Rasimu ya Katiba Mpya, taarifa ya hali ya siasa
nchini, taarifa juu ya mfumo wa uendeshaji wa chama kwa kanda (uzinduzi)
na taarifa juu ya uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 26,
uliofanyika Juni 16, 2013.
Kupitia
agenda za kikao hicho, Kamati Kuu ya CHADEMA, itajadili, kuazimia na
kutoa msimamo wa chama juu ya masuala ya kitaifa na mengine yanayohusu
maeneo mbalimbali, ikiwa ni sehemu ya kufanikisha moja ya malengo ya
chama ambayo ni pamoja na kutoa uongozi bora, sera sahihi, mikakati
makini na oganaizesheni thabiti kwa ajili ya maendeleo endelevu ya jamii
nzima ya Watanzania
Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa Habari.
hdg
No comments:
Post a Comment