Monday, December 16, 2013

TAARIFA YA KUTATUA MGOGORO YAHAIRISHWA

Mkaguzi wa hesabu za serikali ameahirisha kwa muda kutoa taarifa ya juu tuhuma ya matumizi mabaya ya madaraka iliyokuwa imeelekezwa kwa mstahiki Meya wa manispaa ya Bukoba, Khamis Kagasheki iliyoelekezwa kwake na baadhi ya madiwani wanaompinga wanaoongizwa na waziri wa maliasili na utalii, Balozi Khamis Kagasheki.

Mkaguzi huyo wa serikali alikuwa atoe taarifa hiyo desemba 16, mwaka huu, taarifa hiyo ilikuwa itolewe na mkaguzu huyo kwenye ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Kagera.

Taarifa za kuhairishwa kwa utolewaji wa taarifa hiyo zilipatikana siku ya jumapili, kabla ya hapo  madiwani wote walikuwa wameishapatiwa barua za kuhudhuria kikao hicho maalumu kilichokuwa kimeandaliwa na ofisi za mkaguzi huyo.

Taarifa zinadai kuwa mkaguzi huyo ameaahirisha zoezi la kutoa taarifa hiyo kufuatia majukumu yaliyomkabili, hata hiyo uamzi wa kuhairisha kikao hicho umewakatisha tamaa baadgi ya wananchi katika manispaa ya Bukoba, wananchi walikuwa na shauku kubwa ya kusikia mgogoro unahitimishwa ili masuala ya maendeleo yaliyokwama katika manispaa hiyo yaendelee kutekelezwa, ambayo ni pamoja na ujenzi wa soko kuu la Bukoba na standi kuu ya mabasi.

Taarifa ambazo zimepatikana zinadai kuwa mkaguzi huyo ameahidi kutoa taarifa wakati wowote bila kueleza taarifa hiyo itatolewa siku gani.

WANAOCHANGIA KUUENEZA UGONJWA WA UNYANJANO KUKIONA CHA MOTO

 Baadhi ya waandishi wa habari mkoani Kagera wakibadilishana mawazo.
 Ndizi ambayo haijakumbana na ugonjwa wa mnyauko maarufu kwa jina la unyanjano.
 Migomba ambayo haijaathirika.
 Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe, wa pili toka kulia akiwa na baadhi ya watafiti wa kituo cha utafiti wa mazao cha Maruku.

 Mkuu wa mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu Fabian Massawe ameziagiza halmashauri za wilaya na manispaa katika mkoa wa Kagera kutunga sheria ndogo ndogo zitakazowabana wakulima wanaochangia kueneza ugonjwa wa unyanjano.

Ametoa agizo hilo mara baada ya kutembelea shamba la mkulima bora wa ndizi lililopo eneo la mwanzo mgumu katika wilaya ya Misenyi, amesema ugonjwa wa unyanjano unathibitiwa, amewaambia wakulima watumie mbinu bora za kilimo za kuuzuia ugonjwa huo unaoenea kwa kasi katika maeneo mbalimbali mkoani Kagera.

Amewaambia viongozi kuanzia ngazi ya kata hadi mkoa kuwafikisha mahakamani wakulima wote ambao watakuta migomba yao imeathirika, pia ameahidi kuwawajibisha watendaji wote wa serikali ambao watashindwa kusimamia zoezi la kuthibiti uginjwa wa mnyauko.
Baadhi ya watafiti, kulia Bw. Sayi Bulili na kushoto nbi Bw. Leonard Mkandala.

TAHADHALI YA MABADILIKO YA HALI YA HEWA

     JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
                                   WIZARA YA UCHUKUZI
                      MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

Simu: 255 22 2460735/2460706
FAKSI: 255 22 2460735/2460700                                                          S.L.P. 3056
Barua pepe: met@meteo.go.tz                                                   DAR ES SALAAM
Tovuti:  www.meteo.go.tz

Unapojibu tafadhali nakili:
Kumb. Na.: TMA/1622                                                           12 Desemba, 2013

     Taarifa kwa umma: Vipindi vya mvua kubwa vinatarajiwa katika maeneo ya
nyanda za juu kaskazini-mashariki, ukanda wa Ziwa Victoria pamoja na magharibi
                                              mwa nchi.

Taarifa Na.                          201312-02
Muda wa Kutolewa
                                     Saa 10 Jioni
Saa za Afrika Mashariki
Daraja la Taarifa:                   Tahadhari
Kuanzia:
                                     12  Desemba, 2013
Tarehe
Mpaka:
                                     13 Desemba, 2013
Tarehe

                                     Vipindi vya mvua kubwa (zaidi ya mm 50 katika masaa 24
Aina ya Tukio Linalotaraji wa
                                     yajayo) katika maeneo yaliyotajwa hapo chini.

Kiwango cha uhakika:                 Juu (80%)

                                     Baadhi ya maeneo ya nyanda za juu kaskazini-mashariki (Arusha, 

Manyara na Kilimanjaro), ukanda wa Ziwa Victoria (Kagera, Mwanza
                                     na Mara) pamoja na magharibi mwa nchi (Kigoma na Tabora).

                                     Hali hii inatokana na kuimarika kwa mfumo wa mgandamizo mdogo
Maelezo:
                                     wa hewa ikiwa ni muendelezo wa ukanda wa mvua wa ITCZ.

Angalizo:                            Wakazi wa maeneo hatarishi wanashauriwa kuchukua tahadhari.

                                     Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa
Maelezo ya Ziada
                                     mrejeo.

Imetolewa na
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

Taabini ya Rais Jakaya Kikwete kwa Nelson Mandela kijijini Qunu wakati wa mazishi ya Tata Madiba

JK_a472d.jpg
JUMAPILI 15 DISEMBA 2013
Mheshimiwa Jacob Zuma wa Jamhuri ya Afrika Kusini;
Mama Graca Machel,
Mama Winnie Mandela,
Wanafamilia waliondokewa na mpendwa wao,
Mtukufu Mwanamfalme Charles,
Waheshimiwa Wakuu wa Nchi na Serikali,
Waheshimiwa Mawaziri,
Wajumbe wa Mashirika ya Kidiplomasia na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa,
Waombolezaji wenzangu,
Mabibi na Mabwana;
Ninawaleteeni salamu za undugu na mshikamano kutoka kwa kaka zenu na dada zenu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wameniomba niwafikishieni salamu za dhati za rambirambi kwako Rais, Mama Graca Machel, Mama Winnie Mandela, familia nzima ya Madiba na watu wote wa Afrika Kusini kutokana na kifo cha Mheshimiwa Nelson Rolihlahla Mandela, Rais wa zamani wa Afrika Kusini na African National Congress.
Wanapenda mfahamu kuwa hampo peke yenu. Wapo pamoja nanyi katika kipindi hiki kigumu na chenye majonzi. Wanasema huzuni yenu ni huzuni yetu, kuondokewa kwenu ni kuondokewa kwetu. Nelson Mandela alikuwa kiongozi wetu, shujaa wetu na baba yetu kama alivyokuwa kwenu. Watu wa Tanzania wamempoteza rafiki mkubwa na komredi mkubwa katika mapambano.
Rais Mandela amekuwa na uhusiano thabiti wa muda mrefu na Tanzania. Umeanza zamani wakati wa uhuru na mapambano ya ukombozi hapa Afrika Kusini na Tanzania. Vyama vyetu, African National Congress (ANC) na Tanganyika African National Union (TANU) vilikuwa na uhusiano maalum. Haikutokea tu, kuwa, baada ya ANC kuamua kuanzisha kitengo cha jeshi, Umkotho we Sizwe, baada ya njia za amani kushindikana, Dar es Salaam ikawa kituo cha kwanza cha Madiba baada ya kuondoka Afrika Kusini mwaka 1962 akiwa njiani kutafuta msaada kwa ajili ya mapambano ya kijeshi na mahali pa mafunzo kwa ajili ya wapiganaji wa MK.
Makomredi na marafiki;
Kimsingi, ziara yake ilihanikiza mafanikio. Ni ziara hiyo iliyochangia kubadili mwelekeo wa historia ya hili taifa kubwa iliyofanikiwa kuuangusha ubaguzi wa rangi na kuzaliwa kwa Afrika Kusini mpya mwaka 1994. Ingawa Rais wetu wa kwanza na Baba wa Taifa Mheshimiwa Julius Nyerere alisita mwanzoni, baadaye alilikubali ombi la Madiba na kuwapa wapiganaji wa MK ruhusa ya kuishi na kuendesha mafunzo ndani ya Tanzania.
Nina hakika kwa wakongwe wa MK, majina kama Kongwa, Mgagao, Mazimbu na Dakawa yamezoeleka kwao na pengine kuamsha kumbukumbu nzito za maisha waliyoishi Tanzania. Rais Nyerere alikwenda mbali zaidi ya kuwapa mahali pa kuishi na kuendesha mafunzo, akajitolea msaada wa Tanzania na akawa nyenzo katika kuhamasisha msaada wa kimataifa katika kutoa mafunzo na silaha kwa wapambanaji. Kimsingi, msaada huu ulifanywa kwa vyama vyote vya ukombozi Kusini mwa Afrika ambavyo ni MPLA, SWAPO, ZANU, ZAPU na FRELIMO.(P.T)
Makomredi na marafiki;
Ziara hii pia iliyabadili majaliwa ya ANC baada ya kuwa kimepigwa marufuku na utawala wa ubaguzi wa rangi hapa Afrika Kusini. ANC ikapata nyumbani kupya Tanzania ambako iliendesha, kupanga na kuchochea mapambano. Kutoka Tanzania ANC ikaweza kuwafikia makada na wanachama wake waliobaki na kuendesha mapambano kutoka ndani ya Afrika Kusini kwa kupitia mawasiliano ya tahadhari kubwa.
Kutoka Tanzania ANC ilimudu kufikisha ujumbe kwa hadhira kubwa ya watu wa Afrika Kusini kwa dhati kwa kupitia matangazo ya redio. Kama haitoshi, Serikali ya Tanzania ikajenga kituo cha redio kwa ajili ya mapambano ya ukombozi. ANC ikaweza kuifikisha sauti iliyokuwa imezuiliwa na utawala wa ubaguzi wa rangi.
Makomredi na marafiki;
Kuna jambo la kufurahisha kuhusu ziara ya kwanza ya Madiba Tanzania mwaka 1962. Ili kuifanya ziara ya kuwa na usiri mkubwa, asingeweza kukaa mahotelini; aliishi nyumbani kwa Mhazini wa TANU ambaye kwa wakati huo alikuwa Waziri wa Biashara na Viwanda ndugu Nsilo Swai (sasa ni marehemu). Wakati akiondoka kuelekea Accra, Lagos, Addis Ababa na Algiers, aliviacha viatu vyake nyumbani kwa ndugu Swai akiwa na matumaini ya kuvipitia akiwa njiani kurejea. Kwa bahati mbaya, hakupitia Dar es Salaam na muda mfupi tu alipowasili Afrika Kusini, Mandela alikamatwa, kushitakiwa, na kufungwa jela kwa miaka 27. Kwa bahati nzuri, familia ile ilivitunza viatu hivyo na kusubiri.
Madiba alipoachiwa kutoka jela na mwaka 1994 kuwa Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini mpya, jozi ya viatu vya kahawia ilikabidhiwa kwake mwaka 1995. Alikabidhiwa na Mama Vicky Nsilo mjane wa marehemu Nsilo Swai aliyefariki mwaka 1994 ambao Madiba alikuwa Rais. Nilichukua jukumu la kumleta Mama Vicky Nsilo sambamba name aweze kumuaga mgeni wao maalumu na rafiki.
Yeye na marehemu mumewe ni binadamu wa kipekee mno kuvitunza viatu vya mtu mgeni aliyeishi nao kwa siku tatu tu na kutoweka kwa zaidi ya miaka 32. Nilipomwuliza nini kiliwafanya kuvitunza viatu kwa muda mrefu huo, aliniambia kuwa mumewe aliamini kuwa Mandela angetoka jela siku moja na kuvidai. Ili wakiulizwa wawe navyo mkononi. Hata hivyo, hawakusubiri, badala yake akamtafuta Madiba na kumkabidhi kilichokuwa chake. Ni marafiki waaminifu kiasi gani ambao Mandela alikuwa nao.
Makomredi;
Baada ya kutoka kwake jela na baada ya kuitembelea Zambia kwa ajili ya mkutano wa NEC ya ANC alikuja Dar es Salaam. Alikutana na halaiki kubwa ya watu ambao jiji halijawahi kuwashuhudia. Kumbukeni, mvua kubwa ilinyesha siku ile lakini watu walisongamana uwanja wa ndege na kujipanga katika mitaa ya Dar es Salaam wakiivumilia mvua ili kumwona kiongozi wao. Haiba kubwa ya Mandela haikuwa na kifani. Pia alizuru Morogoro na kulala Mgagao kwenye kambi ya mafunzo ya MK.
Makomredi na marafiki;
Nimesimulia hadithi hizi zote na michapo ya matukio ya kweli ili kuwafanya watu wafahamu ni muda mrefu kiasi gani, uhusiano wa sasa uliotukuka baina ya nchi zetu umetoka. Si jambo la kushangaza kuwa Afrika Kusini na Tanzania wanafurahia uhusiano wao uliotukuka baina yao. Tunatazama kwa pamoja mambo mengi ya kikanda na kimataifa. Tunaungana mkono kwenye kila baraza la kikanda na kimataifa.
Sisi ni marafiki na washirika wa karibu kwa sababu ya historia yetu inayofanana inyotuunganisha. Si kingine zaidi ya waasisi wetu Rais Mwalimu Julius Nyerere aliyefariki mwaka 1999 na Rais Nelson Mandela tunayemwombeleza leo waliofanikisha hili. Walijenga misingi imara mno. Ndiyo maana nilisema mwanzoni kuwa Madiba ni kiongozi wetu, shujaa na baba mno kama alivyo kwenu. Hii ndiyo sababu huzuni yenu na simanzi yenu ni yetu pia.
Makomredi na Marafiki;
Tunapoomboleza kifo cha huyu shujaa Nelson Rolihlahal Mandela ni vemu tujikite katika kuyaimarisha mahusiano baina ya Afrika Kusini na Tanzania. (Hii ni alama na urithi wa kipekee aliotuachia ili tuukamilishe). Tufanye kazi kwa ushirikiano katika mabaraza ya kikanda na kimataifa ili kukuza falsafa zake kwa SADC imara, Umoja wa Afrika ulio hai na Umoja wa Mataifa wenye uwezo wa kupigania haki na usawa kwa mataifa yote na watu wote. Na, tunapaswa kuzitimiza ndoto zake kwa kuona nchi zinazoendelea zikishirikiana kwa umoja na mshikamano katika kutafuta haki zao na kujikwamua kutoka katika umasikini kuelekea kwenye ustawi.
Nanyi, kaka zangu na dada zangu wa Afrika Kusini, Madiba ameishi maisha yake vema, mnatakiwa kuhakikisha urithi wake unadumu. Ameliacha taifa lenye demokrasia bora ambapo Waafrika Kusini Weusi na Weupe wanaishi kwa maelewano.
Taifa ambalo weusi pia wanaweza kustawi tofauti na ilivyokuwa hapo nyuma waliposhutumiwa na kuishi katika kudhalilishwa, kupokwa utu wao kama raia wa daraja la pili ama la tatu ndani ya nchi yao wenyewe. Tunafahamu kuwa siyo yote aliyoyasimamia yamefikiwa. Ni kujipotosha kudhani kuwa maovu yote ya mfumo uliopita wa ubaguzi wa rangi yamesahihishwa katika hii miaka 19.
Tafadhali simameni katika hilo na daima mpanie kufanikiwa zaidi. Namna hii, mtamuenzi kiongozi huyu mweledi kwa namna ambayo ingemridhisha kama angekuwa hai. Hii ndiyo namna bora zaidi ya kuuishi urithi wake.
Udumu milele Nelson Mandela!
Mdumu milele watu wa Afrika Kusini!
Ninawashukuruni kwa ukarimu wenu.
Imetafsiriwa katika Kiswahili na Fadhy Mtanga.

Sudan Kusini yatibua jaribio la mapinduzi

59D9A9A4-69A8-4F4C-8E86-9FF0663BC5F3_mw1024_n_s_f229c.jpg
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, anasema vikosi vyake vimefanikiwa kutibua jaribio la mapinduzi, baada ya usiku mzima wa mapigano katika mji mkuu wa nchi hiyo Juba.
Bw. Kiir, anayetoka katika kabila kubwa zaidi la wa Dinka amewatupia lawama wanajeshi wanaomtii aliyekuwa makamu wake Riek Machar, anayetoka katika kabila dogo la Nuer.
Aidha Kiir ametangaza amri ya kutotembea usiku mjini Juba na kusema serikali sasa inaudhibiti mji huo.
Makundi hasimu ya wanajeshi walipigana vikali kwa saa kadhaa na kuna ripoti za kuwepo majeruhi maelfu wakiripotiwa kukimbilia usalama wao.
Milio ya risasi sasa inaripotiwa kupungua. Kumekuwa na hali tete ya kisiasa nchini Sudan Kusini tangu mwezi Julai wakati Rais Kiir alipovunja na kuwafuta kazi mawaziri wote katika baraza lake akiwemo Makamu wa Rais Bw.Machar.(P.T)

OKWI ATUA YANGA SC


KLABU ya Yanga SC ya Dar es Salaam imemsajili mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Emmanuel Arnold Okwi raia wa Uganda kwa Mkataba wa mia miwili na nusu. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya klabu ya Yanga, Abdallah Ahmed Bin Kleb amesema jioni hii mjini Dar es Salaam kwamba wamemsajili Okwi na ataanza kuichezea timu hiyo mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Bara na michuano ya Afrika.
Okwi (katikati) akitia dole gumba kwenye fomu za Yanga.
Ametua Jangwani; Emmanuel Okwi ataitumikia Yanga SC kwa misimu na nusu ijayo. Chini ni Bin Kleb kushoto akiwa na viongozi wenzake wa Yanga SC, Mussa Katabaro na Seif Magari. 

Etoile du Sahel ya Tunisia ilimnunua Okwi kutoka Simba SC Januari mwaka huu kwa dola za Kimarekani 300,000, lakini mchezaji huyo akaamua kuachana na klabu hiyo na kurejea kupumzika kwao Uganda, kwa madai hakulipwa mishahara kwa miezi mitatu.
Wakati huo huo, Etoile hadi sasa haijailipa Simba SC fedha zake za kumnunua mchezaji huyo na sakata lake limefikishwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Baada ya Okwi kukaa bila kucheza kwa miezi sita, Shirikisho la Soka la Uganda (FUFA) lilimpigania aruhusiwe kurejea nyumbani kuichezea SC Villa ya huko ili kunusuru kiwango chake. 
Hata hivyo, baada ya kung’ara na timu ya taifa ya Uganda ‘The Ceanes’ nchini Kenya kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge mwezi huu , Okwi anasajiliwa Yanga SC.
Bin Kleb amesema kwamba walimsajili Okwi tarkiban siku sita zilizopita, lakini Hati yake ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) imepatikana leo na ndiyo maana wameamua kumtangaza.
“Amesaini mkataba kiasi cha siku sita zilizopita, ila taratibu za uhamisho zimekamilika leo. Atakuwa nasi kwa misimu miwili na nusu ijayo,”alisema Bin Kleb.
Alipoulizwa kuhusu utata wa sakata lake ambalo limefika hadi FIFA, Kleb alisema; “Tumefuatilia kote, hadi kwa wanasheria, na tumefanikiwa kupata hadi ITC yake, nawaambia mashabiki wa Yanga wajue viongozi wao wanafanya kazi, hatuna stori nyingi, sisi tunafanya vitendo, tunafanya kazi kwa siri sana,”.
“Na tumepitia sehemu zote, tumeona kabisa tuko sahihi katika kumsajili mchezaji huyu na hakutakuwa na tatizo lolote upande wetu,”alisema. 
Bin Kleb alisema lengo la Yanga SC ni kufanya vizuri katika Ligi ya Mbingwa Afrika mwakani na ndiyo maana wameamua kuimarisha timu kwa kusajili wachezaji wazuri.

KWA HISANI YA BIN ZUBER

Thursday, December 12, 2013

Maisha yana.......................

Pinda,nipo tayari kung’olewa nikibainika ni mzigo...............

pindapx_82928.jpg
Na Daniel Mjema, Mwananchi
Dodoma.Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amevunja ukimya na kusema yuko tayari kuachia ngazi endapo tu Rais Jakaya Kikwete ataamua kumwondoa na kama itatokea hivyo, atamshukuru Rais kwa kumwambia, ahsante.
Pinda aliliambia Bunge mjini Dodoma jana kwamba endapo Rais hatafanya hivyo, bado wabunge wanayo mamlaka ya kikatiba ya kumwondoa kwa njia ya kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye.(E.L)
Ibara ya 53 A(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977, Bunge linaweza kupitisha azimio la kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu endapo itatolewa hoja kupendekeza hivyo.
Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Rukia Kasim Ahmed (CUF) katika utaratibu wa Bunge wa Waziri Mkuu kujibu maswali ya papo kwa hapo kutoka kwa wabunge.
Katika swali lake, Mbunge huyo alisema; Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alikaririwa akiwa jijini Mbeya kuwa wapo mawaziri mzigo katika Baraza la Mawaziri.
Mbunge huyo alisema, katika ziara hiyo, Kinana alifuatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Dk Asha-Rose Migiro.
"Walipokuwa Mbeya wakifuatilia utekelezaji wa Ilani ya CCM, Kinana alisema kuna baadhi ya mawaziri ni mzigo, wewe kama kiongozi mkuu wa shughuli za Serikali unachukuliaje kauli hii?" aliuliza.
Akijibu swali hilo, Pinda alisema hata yeye ameyasikia hayo kwenye vyombo vya habari na kusema, kiutu uzima hawezi kutoa maoni yake kwa kuzingatia yale yanayosemwa kwenye magazeti.
"Sisi tunangoja arudi (Kinana) tukae naye ili tujue alichokuwa anasema hasa ni nini na ninaamini alikuwa na baadhi ya wizara kichwani kwake," alisema Pinda bungeni jana.
Katika swali lake la nyongeza, Rukia alisema wakati wanachangia taarifa ya Kamati ya Bunge ya Serikali za Mitaa, yupo Mbunge wa CCM alisema kuwa Pinda ni mzigo namba moja.
"Kuna mbunge, tena wa CCM, alinukuu kauli ya Katibu Mkuu wa CCM na akasema kama ni mawaziri mzigo basi mzigo nambari moja ni wewe Waziri Mkuu, unawaambiaje Watanzania?" aliuliza Rukia.
Akijibu swali hilo, Pinda alisema yeye anasimamia wizara 20 hivyo kama wapo watakaomhukumu kwa wizara moja ama mbili kwa kutofanya vizuri basi watu hao watakuwa hawamtendei haki
Kauli ya Pinda ameitoa siku moja tu baada Bunge kupitisha azimio la kumtaka Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa Ghasia kupima kama bado anatosha kuiongoza wizara hiyo.
Pia, azimio hilo liliwahusu Naibu Mawaziri wa Tamisemi, Aggrey Mwanri na Kassim Majaliwa kutokana na tuhuma mbalimbali za ufisadi, ubadhirifu na kuwapo mtandao wa kifisadi ndani ya Tamisemi.
Hata hivyo, alipohojiwa jana, Ghasia alisema kuwa hana kinyongo na amelipokea azimio la Bunge. "Sina kinyongo, nimelipokea na ninalitafakari azimio," alisema kwa kifupi.
Naye Mwanri alisema kuwa hakuwa na habari kama suala la Tamisemi linamuhusu na yeye na kwamba atakapothibitika kuwa ni miongoni mwao, ndipo atakuwa kwenye nafasi ya kujibu.
Tangu kuanza kwa mkutano wa 14 wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma, kumekuwapo vuguvugu la kuwang'oa mawaziri waliotajwa na Kinana kuwa ni mzigo katika kutekeleza majukumu yao.
Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM), yeye alienda mbali na kumshauri Rais kumfukuza kazi Pinda kutokana na kuwa mpole mno kiasi kwamba mawaziri wanamdharau na hawamsikilizi.
Pendekezo hilo liliungwa mkono pia na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) na wabunge wengine waliochangia taarifa za Kamati za Bunge walionyesha shaka dhidi ya Pinda.
Ghasia afunguka
Ghasia, ambaye yeye na wasaidizi wake waliundiwa Azimio la Bunge kujipima juzi, amefunguka na kusema analifanyia kazi azimio hilo kabla ya kuchukua uamuzi wa kufanya chochote.
Juzi Bunge lilipitisha azimio la pamoja kuwataka Waziri na Naibu Mawaziri katika Wizara ya Tamisemi kujitathmini wenyewe kabla ya kufikia uamuzi kutokana na kuelezwa kuwa wameshindwa kusimamia majukumu yao.
Azimio la wabunge lilipitishwa na wabunge kwa kura ya 'ndiyo' bila ya kupingwa baada ya kuhojiwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda iwapo wabunge wanaipokea Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (Laac) iliyowasilishwa na Mwenyekiti wake, Rajab Mbarouk.
"Mimi nimepokea Azimio hilo bila shaka siwezi kusema chochote kwa sasa kwani naendelea kulifanyia kazi baada ya hapo nitakuwa na cha kusema, nashukuru kwa kuniuliza," alisema Waziri Ghasia kwa njia ya simu
Kwa upande wake, Mwanri alisema yeye si mlengwa katika jambo hilo hivyo hawezi kusema chochote. Alisema Azimio hilo lilimgusa moja kwa moja Waziri wa Tamisemi ambaye si yeye hivyo kutoa majibu ya jambo hilo si wakati wake.
"Mimi nilivyosikia na nilivyoelewa ni waziri mwenyewe ndiye anayeguswa moja kwa moja na jambo hilo, kwa hiyo unaweza kwenda kwake atakuwa na majibu ya kukupa na bila shaka atakusaidia vizuri," alisisitiza Mwanri.
Kwa upande wake Kassim Majaliwa hakupatikana kuzungumzia jambo hilo kwa madai kuwa yuko nje ya nchi kwa shughuli za kiserikali.

MAGAZETI

DSC 0030 1a82e
DSC 0031 dc2cc
DSC 0032 6ecac
DSC 0033 c0bd3
DSC 0034 1abf9
DSC 0035 94aea
DSC 0036 c61be
DSC 0037 b7a28
DSC 0038 d3f09

TASAF yatoa elimu kwa wanahabari juu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

IMG 8511 1cbbf
Mkurugenzi wa Huduma za jamii kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF) Amadeus Kamagenge akitoa mada leo kwa baadhi ya waandishi wa habari na wahariri kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kwenye warsha ya siku mbili ya kujenga uelewa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini wa awamu ya tatu inayoendelea kwenye hoteli ya Oceanic Bay, Bagamoyo
IMG 8521 f8d6f
Ni Baadhi ya waandishi wa habari na wahariri kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wakiwa katika ya warsha siku mbili leo ya kujenga uelewa wa mpango wa awamu ya tatu wa kunusuru kaya masikini inayoendelea kwenye hoteli ya Oceanic Bay, Bagamoyo iliyoandaliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF)
IMG 8533 ae7d6
Afisa Uhawilishaji fedha kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF), Edith Mackenzie akifafanua jambo leo katika ya warsha siku mbili ya kujenga uelewa wa mpango wa awamu ya tatu wa kunusuru kaya masikini inayoendelea kwenye hoteli ya Oceanic Bay, Bagamoyo.(P.T)

IMG 8584 380d1
Mkurugenzi Mtendaji wa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF), Ladislaus Mwamanga akifafanua jambo leo kwa baadhi ya waandishi wa habari na wahariri kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kwenye warsha siku mbili ya kujenga uelewa wa mpango wa kunusuru kaya masikini wa awamu ya tatu inayoendelea kwenye hoteli ya Oceanic Bay, Bagamoyo.
IMG 8592 fe49c
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka Zanzibar wakiwa katika ya warsha siku mbili leo ya kujenga uelewa wa mpango wa awamu ya tatu wa kunusuru kaya masikini inayoendelea kwenye hoteli ya Oceanic Bay, Bagamoyo iliyoandaliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF).
IMG 8601 - Copy 50034
Msanifu wa gazeti la Uhuru ,Lilian Timbuka akiuliza swali leo kuhusu mpango wa kunusuru kaya masikini kwenye warsha ya siku mbili ya kujenga uelewa wa mpango wa kunusuru kaya masikini wa awamu ya tatu inayoendelea kwenye hoteli ya Oceanic Bay, Bagamoyo.
IMG 8625 1cb20
Baadhi ya waandishi wa habari na wahariri kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF) , wa tatu kutoka kushoto waliokaa ni Mkurugenzi Mtendaji wa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF), Ladislaus Mwamwanga mara baada ya kufunguliwa kwa warsha ya siku mbili leo ya kujenga uelewa wa mpango wa awamu ya tatu wa kunusuru kaya masikini inayoendelea kwenye hoteli ya Oceanic Bay, Bagamoyo.
IMG 8642 48752
Mtaalamu wa Habari na Mawasiliano kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF), Zuhura Mdungi akifafanua jambo leo katika ya warsha siku mbili ya kujenga uelewa wa mpango wa awamu ya tatu wa kunusuru kaya masikini inayoendelea kwenye hoteli ya Oceanic Bay, Bagamoyo.
Picha na Magreth Kinabo

Serikali yatumia zaidi ya shilingi Bilioni 16 kujenga Kampasi mpya ya Makao Makuu ya Chuo cha Taifa cha Utalii.

IMG_0962_83f7f.jpg
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii Bi. Rosada Msoma akieleza kwa waandishi wa Kuhusu mafanikio yaliyofikiwa na Chuo hicho tangu kuanzishwa kwake, wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mkufunzi na Msimamizi wa Usajili wa Chuo hicho Bi. Ishika Perpetua.
IMG_0979_aab9d.jpg
Mkufunzi na Msimamizi wa Usajili wa Chuo cha Taifa cha Utalii Bi. Ishika Perpetua akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu vigezo vinavyotumika kudahili wanafunzi katika chuo hicho.kushoto ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Chuo hicho Bi. Rosada Msoma.
IMG_0993_9433c.jpg
Meneja wa Kampasi ya Temeke ya chuo cha Taifa cha Utalii Bw. Steven Madenge akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu namana ambavyo chuo hicho kinaendelea kujidhatiti katika kuhakikisha wanatoa elimu bora katika sekta ya utalii,wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Chuo hicho Bi. Rosada Msoma.
(Picha na Hassan Silayo)(P.T)
Na Frank Mvungi
Serikali yatumia zaidi ya shilingi Bilioni 16 kujenga Kampasi mpya ya Makao Makuu ya Chuo cha Taifa cha Utalii Jijini Dar es salaam.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Chuo hicho Rosada Msoma wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam.
Rosada aliongeza kuwa kampasi hiyo imejengwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Ufaransa ili kupanua wigo wa utoaji wa huduma bora katika sekta ya utalii.
Akifafanua zaidi alisema kuanzishwa kwa chuo hicho ni matokeo ya Kukua kwa Sekta ya Utalii nchini ambako kumepelekea kuongezeka kwa uhitaji wa watumishi wenye weledi katika fani za Ukarimu na Utalii.
"Tunaishukuru serikali ya Ufaransa kwa kuona umuhimu wa kuchangia kukuza sekta ya utalii nchini kwa kuchangia katika ujenzi wa chuo chetu katika kampasi ya Bustani,ambayo ni makao makuu ya chuo chetu"alisema Rosada.
Aliongeza kuwa kwa mwaka 2012 jumla ya watalii 1,077,058 walitembelea Tanzania ukilinganisha na na wastani wa watalii 501,669 waliotembelea nchi yetu katika kipindi cha mwaka 2000.
Rosada alibainisha kuwa jukumu kuu la Wakala ni kutoa mafunzo bora katika fani za ukarimu na Utalii hapa nchini hali ambayo imechangia kukuza utalii nchini.
Naye Meneja wa Chuo hicho kampasi ya Temeke bw. Steven Madenge alisema kuwa chuo hicho kinaendelea na taratibu za kuhakikisha kuwa wahitimu wanaomaliza katika chuo hicho wanakidhi viwango vya kimataifa.
Chuo cha Taifa cha Utalii ni wakala pekee wa Serikali ulioanzishwa mwaka2003 kwa sheria ya wakala no. 30 ya mwaka 1997 kwa lengo la kutoa mafunzo ya Utalii na Ukarimu hapa nchini.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA MPANGO WA TAIFA HUDUMA ZA FEDHA NCHINI.

unnamed_b8eb0.jpg
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) , Prof. Benno Ndulu, akisaini mfano wa cheti cha Mpango wa Taifa wa Huduma za Fedha wenye lengo la kusimamia na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazozorotesha huduma za fedha nchini. Wanaoshuhudia nyuma (katikati) ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kulia kwake ni Malkia Maxima wa Uholanzi (kushoto) ni Naibu Waziri wa Fedha Sada Mkuya Salumu. Hafla hiyo imefanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
unnamed_1_f8844.jpg
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango wa Taifa wa Huduma za Fedha, wenye lengo la Kusimamia na kutatua ufumbuzi wa changamoto zinazozorotesha huduma za fedha nchini. Hafla hiyo imefanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
unnamed_2_f4dcc.jpg
Malkia Maxima wa Uholanzi, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango wa Taifa wa Huduma za Fedha wenye lengo la Kusimamia na kutatua ufumbuzi wa Changamoto zinazozorotesha huduma za fedha nchini. Hafla hiyo iliyohudhuriwa pia na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dkt. Mohammed Gharib Bilal imefanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMR
unnamed_3_4f844.jpg
Malikia Maxima wa Uholanzi, akibofya kitufe kama ishara ya uzinduzi wa Mpango wa Taifa wa Huduma za Fedha. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMR(P.T)
unnamed_4_fddc4.jpg
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) Malkia Maxima wa Uholanzi na Naibu Waziri wa Fedha, Sada Mkuya Salumu, wakiwa wameshikilia Mpango wa Taifa wa Huduma za Fedha baada ya kuzinduliwa leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania. Picha na OMR
unnamed_5_728f9.jpg
unnamed_6_bf214.jpg
Baadhi ya wadau wa Sekta za Fedha waliohudhuria uzinduzi huo wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, alipokuwa akihutubia, wakati wa uzinduzi.