mama kikwete aendelea na ziara lindi

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasalimia watoto na wananchi wa kata ya Msinjahili waliohudhuria mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Kitumbikwela kilichoko katika wilaya ya Lindi Mjini tarehe 17.2.2013
Wanachama
wa Chama Cha Mapinduzi wa Kata ya Msinjahili wakishangilia wakati wa
mkutano wa hadhara ulihutubiwa na Mjumbe wa NEC wa wilaya ya Lindi Mjini
Mama Salma Kikwete katika kijiji cha Kitumbikwela tarehe 17.2.2013.
Wanachama
wapya wa Chama Cha Mapinduzi na jumuia zake wakila kiapo mara baada ya
kukabidhiwa kadi na Mjumbe wa NEC wa Lindi Mjini Mama Salma Kikwete
katika kijiji cha Kitumbikwela tarehe 17.2.2013.
Mjumbe wa NEC wa Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wananchi wa kata ya Msinjahili kwenye kijiji cha Kitumbikwela tarehe 17.2,2013.
PICHA NA JOHN LUKUWI
No comments:
Post a Comment