Monday, February 18, 2013

WAJERUMANI WATOA MSAADA WA VITABU VINAVYOELEZEA HISTORIA YA TANZANIA

 Mfano wa nyumba ya msonge iliyokutwa kwenye jengo la mambo ya kale inayomilikiwa na kampuni ya utalii ya Kiroyera.
 Meneja uendeshaji wa kampuni ya utalii ya Kiroyera, William Rutta akiangalia vitabu vilivyotolewa na Mrs.Edith Gottschling raia wa Ujerumani ambaye mme wake marehemu Klaus alikuwa mwenyekiti wa kwanza wa urafiki kati ya nchi ya Ujerumani na Tanzania.
 Yusto Mchuruza aliyekabidhi vitabu vilivyotolewa nba mjerumani akitoa ufafanuzi wa vitabu hivyo.
 Mambo ndania ya jumba linalohifadhi mambo ya kale.
 Yusto Mchuruza akimkabidhi vitabu William Rutta.

Saturday, February 16, 2013

SOMO LA DINI NA MAADILI KUFUNDISHWA RASMI SHULENI NA VYUONI TANZANIA NZIMAMIKOA ya Kagera na Kigoma imezindua rasmi mihtasari  ya  somo la Dini na Maadili litakalofundishwa kuanzia shule za awali, msingi sekondari hadi vyuo vikuu.

Mihtasari hiyo imezinduliwa  rasmi na UMAKA (Umoja wa Madhehebu Kagera) wakishirikiana na serikali baada ya mihtasari hiyo kupitishwa rasmi na Kamishina wa Elimu ili isambazwe katika shule zote tayari kwa kutumika kufundishia wanafunzi katika ngazi mbalimbali.

Somo la Dini na Maadili limerasimishwa rasmi kufundishwa shuleni na vyuoni baada ya UMAKA kuona umuhimu wa kuwa na mihtasari ambayo ni rasmi na inayotambuliwa na serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ili itumike kufundishia watoto pia na kutahiniwa kama masomo mengine.

Umoja wa Madhehebu Kagera  (UMAKA) ulianzisha mchakato wa kuandaa mihtasari ya somo la Dini na  Maadili  wakishirikiana na serikali ili somo hilo liwe na mihtasari inayofanana katika kufundishia wanafunzi kuliko hapo awali ambapo somo hilo halikuwa na mihtasari ya kufundishia.

Kupitia somo la Dini na Maadili, wanafunzi  watafunzwa maadili mema ya kupendana na kuwapenda watanzania wenzao, kujenga jamii yenye kuwajibika na kumcha Mwenyezi Mungu bila kujali tofauti za ki-imani kwao, pia kulelewa na kukua katika malezi ya kufuata sheria na utawala bora.

Serikali katika kuboresha utumiaji wa Mihtasri mipya ya somo la Dini na Maadili imeagiza somo hilo likaguliwe na wakaguzi wa serikali pamoja na walimu wakuu wa shule kama masomo mengine na kutahiniwa katika ngazi zote hadi ile ya taifa.

Pia katika kuona umuhimu wa somo la Dini na Maadili kufundishwa shuleni, serikali imeamua mihtasari ya somo hilo itumike Tanzania nzima badala ya Mikoa ya Kagera na Kigoma walioshirikiana na serikali kuandaa mihtasari hiyo  ili wanafunzi wote wa Tanzania wafunzwe dini na maadili ya kitanzania.

UMAKA ilianzishwa miaka ya 1980 ikiwa na lengo la kushirikiana na Serikali na kushauri masuala mbalimbali yahusuyo maadili, amani, usalama na maendeleo ya jamii ya watanzania. UMAKA inajumuisha  Balaza la Maaskofu Tanzania (TEC),  Balaza la Waislam Tanzania (BAKWATA), na Baraza la Wakristo Tanzania (CCT).

MKUTANO WA UZUNDUZI WA SOMO LA DINI NA MAADILI KAGERA

 Baba Askofu Nestory Timanywa Jimbo Katoliki La Bukoba  Ambaye Amestaafu hivi Karibuni Akitoa Mada ya Historia ya Maadili Tanzania Ambapo Alisistiza sana Uwajibikaji wa Wazazi, Walezi na Viongozi Mbalimbali Kuwajibika Kuwalea Watoto katika Maadili Mazuri.
 Wajumbe wa Kikao cha Uzinduzi wa Mihtasari ya  Somo la Dini na Maadili Wakisiliza kwa Makini na Utulivu.
Hawa ni Viongozi wa Dini Mkoani Kagera Waliohudhuria Uzinduzi Mihtasari ya Somo la Dini na Maadili,Katikati Kutoka Kulia Ni Askofu Elisa Buberwa KKKT, Askofu Nestory Timanywa Jimbo Katoliki la Bukoba, Askofu Severine Niwemugizi Jimbo Katoliki la Rulenge, Nyuma Kabisa ni Masista na Mapadre Kutoka Kigoma, na Mstari wa Kwanza ni Viongozi wa BAKWATA Mkao wa Kagera.

No comments:

Post a Comment