Wednesday, February 27, 2013

RAIS KIKWETE ATEMBELEA JKT

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na uongozi wa juu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) jijini Dar es salaam alipotembelea leo February 27, 2013. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange pia walihudhuria.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa juu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) jijini Dar es salaam alipotembelea leo February 27, 2013. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange pia wapo.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya saa toka kwa  Mkuu  wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael Muhuga huku  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange wakishuhudia. Saa hiyo imeandaliwa na makamanda wa JKT kumpongeza Rais Kikwete kwa kurejesha mafunzo ya jeshi la ulinzi kwa mujibu wa sheria kuanzia mwaka huu.

UZINDUZI WA MPANGO GSI

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikata utepe kuashiria uzinduzi  wa Mpango  Mkakati  wa Miaka Mitano  wa Taasisi  ya  GSI Tanzania  kwenye ukumbi wa hoteli ya Blue Pearl  jijini Dar es salaam Februari 27, 2013. Wapili kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dr.Abdallha Kigoda. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Joyce Mapunjo.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama mikoba katika maonyesho yaliyoambatana na Uzinduzi wa  Mpandgo Mkakati wa Miaka  Mitano wa Taasisi  ya GSI Tanzania kwenye ukumbi wa Hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es slaam Februari  27, 2013. Kushoto ni Waziri wa Viwanda,Biashara na Masoko, Abdallah Kigoda na kulia ni  Katibu  Mkuu wa Wizara hiyo, Joyce Mapunjo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Tuesday, February 26, 2013

MANDHALI YA CHAMA CHA MSINGI MWEYANJALE KINACHOUNDA KCU 1990 LTD

 Jengo la chama cha msingi cha Mweyanjale kinachojihusisha na kilimo cha kahawa hai 'organic coffee' kinachounda chama cha ushirika Kagera (KCU 1990 LTD).
 Mwenyekiti wa chama hicho, Leopord Mtalemwa akiwa nje ya jengo la chama hicho.
 Maeneo yanayozunguka chama hicho.
Mtalemwa akiongea na waandishi wa habari.

Monday, February 25, 2013

NDANI YA MANISPAA YA BUKOBA KWAWAKA MOTO

MANISPAA ya Bukoba hapakaliki, hii inafuatia hatua ya madiwani wa manispaa hiyo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kususia kikao chama hicho ambacho hufanyika kabla ya kikao cha baraza la madiwani.


Baadhi ya madiwani wa CCM wamesusia kikao hicho baada ya watu wasiofahamika kusambaza waraka unaowakashfu.


Waraka huo unawakashfu madiwani kumi ambao ni pamoja na madiwani wa CCM 8 na wa vyama vya vya upinzani vinavyowaunga mkono 2.


Mwandishi wa waraka huo anatoa kashfa nzito kwa madiwani waliosaini waraka wa kutaka Mstahiki Meya wa manispaa ya Bukoba Anatory Amani apigiwe kura za kutokuwa na imani naye kufuatia tuhuma mbalimbali zinazomkabili.


Baadhi ya madiwani waliiongea walidai mgogoro ulioko kati ya Meya huyo na madiwani kuwa umeishaigawa CCM, kwa anyakati tofauti walisema kuwa hawana imani na meya huyo na ndio maana wanataka kumng'oa.


Walisema kuwa hata kama nyaraka zikisambazwa na kuwakasfu kamwe hawatarudi nyuma, "tunajua waraka huu aliyeuandaa hivyo hatuna wasiwasi nao, moto wetu uko palepale wa kumuondoa Amani madarakani" walisema bila kutaka majina yao yatakjwe.

Walisema kuwa hawataki kuongozwa na kiongozi yoyote mwenye huruka ya ufisadi ambaye anabuni miradi mingi kwa maslahi yake binafsi," Kiongozi yoyote atakayekuwa na mlengo wa kutaka kuifilisi manispaa tutakula naye sahani moja" walimaliza.


Manispaa ya Bukoba sasa kumewaka moto, pande zote zinazopingana kila mmoja anijiona ni mbabe, pande zinazopingana moja unaundwa na kundi la waziri wa maliasili na utalii, Balozi Khamis Kagasheki na upande nyingine inaongozwa ana Meya wa manispaa ya Bukoba Anatory Amani.

Kambi ya Kagasheki inamtaka Meya wa manispaa ya Bukoba Amani anga'atuke na kambi ya Amani inapinga mapendekezo hayo.



WAZIRI PINDA AKUTANA NA BALOZI WA CANADA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akisalimiana na Balozi wa Canada nchini, Mhe.Alexandre Leveque kabla ya mazungumzo yao, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Februari 25, 2013. (Picha na Ofisi a Waziri Mkuu)

VIONGOZI WASAINI MPANGO WA AMANI WA UMOJA WA MATAIFA

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maal: umu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 24, 2013
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe Ban Ki-moon akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maal: umu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 24, 2013

Monday, February 18, 2013

WAJERUMANI WATOA MSAADA WA VITABU VINAVYOELEZEA HISTORIA YA TANZANIA

 Mfano wa nyumba ya msonge iliyokutwa kwenye jengo la mambo ya kale inayomilikiwa na kampuni ya utalii ya Kiroyera.
 Meneja uendeshaji wa kampuni ya utalii ya Kiroyera, William Rutta akiangalia vitabu vilivyotolewa na Mrs.Edith Gottschling raia wa Ujerumani ambaye mme wake marehemu Klaus alikuwa mwenyekiti wa kwanza wa urafiki kati ya nchi ya Ujerumani na Tanzania.
 Yusto Mchuruza aliyekabidhi vitabu vilivyotolewa nba mjerumani akitoa ufafanuzi wa vitabu hivyo.
 Mambo ndania ya jumba linalohifadhi mambo ya kale.
 Yusto Mchuruza akimkabidhi vitabu William Rutta.

Saturday, February 16, 2013

SOMO LA DINI NA MAADILI KUFUNDISHWA RASMI SHULENI NA VYUONI TANZANIA NZIMA



MIKOA ya Kagera na Kigoma imezindua rasmi mihtasari  ya  somo la Dini na Maadili litakalofundishwa kuanzia shule za awali, msingi sekondari hadi vyuo vikuu.

Mihtasari hiyo imezinduliwa  rasmi na UMAKA (Umoja wa Madhehebu Kagera) wakishirikiana na serikali baada ya mihtasari hiyo kupitishwa rasmi na Kamishina wa Elimu ili isambazwe katika shule zote tayari kwa kutumika kufundishia wanafunzi katika ngazi mbalimbali.

Somo la Dini na Maadili limerasimishwa rasmi kufundishwa shuleni na vyuoni baada ya UMAKA kuona umuhimu wa kuwa na mihtasari ambayo ni rasmi na inayotambuliwa na serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ili itumike kufundishia watoto pia na kutahiniwa kama masomo mengine.

Umoja wa Madhehebu Kagera  (UMAKA) ulianzisha mchakato wa kuandaa mihtasari ya somo la Dini na  Maadili  wakishirikiana na serikali ili somo hilo liwe na mihtasari inayofanana katika kufundishia wanafunzi kuliko hapo awali ambapo somo hilo halikuwa na mihtasari ya kufundishia.

Kupitia somo la Dini na Maadili, wanafunzi  watafunzwa maadili mema ya kupendana na kuwapenda watanzania wenzao, kujenga jamii yenye kuwajibika na kumcha Mwenyezi Mungu bila kujali tofauti za ki-imani kwao, pia kulelewa na kukua katika malezi ya kufuata sheria na utawala bora.

Serikali katika kuboresha utumiaji wa Mihtasri mipya ya somo la Dini na Maadili imeagiza somo hilo likaguliwe na wakaguzi wa serikali pamoja na walimu wakuu wa shule kama masomo mengine na kutahiniwa katika ngazi zote hadi ile ya taifa.

Pia katika kuona umuhimu wa somo la Dini na Maadili kufundishwa shuleni, serikali imeamua mihtasari ya somo hilo itumike Tanzania nzima badala ya Mikoa ya Kagera na Kigoma walioshirikiana na serikali kuandaa mihtasari hiyo  ili wanafunzi wote wa Tanzania wafunzwe dini na maadili ya kitanzania.

UMAKA ilianzishwa miaka ya 1980 ikiwa na lengo la kushirikiana na Serikali na kushauri masuala mbalimbali yahusuyo maadili, amani, usalama na maendeleo ya jamii ya watanzania. UMAKA inajumuisha  Balaza la Maaskofu Tanzania (TEC),  Balaza la Waislam Tanzania (BAKWATA), na Baraza la Wakristo Tanzania (CCT).

MKUTANO WA UZUNDUZI WA SOMO LA DINI NA MAADILI KAGERA

 Baba Askofu Nestory Timanywa Jimbo Katoliki La Bukoba  Ambaye Amestaafu hivi Karibuni Akitoa Mada ya Historia ya Maadili Tanzania Ambapo Alisistiza sana Uwajibikaji wa Wazazi, Walezi na Viongozi Mbalimbali Kuwajibika Kuwalea Watoto katika Maadili Mazuri.
 Wajumbe wa Kikao cha Uzinduzi wa Mihtasari ya  Somo la Dini na Maadili Wakisiliza kwa Makini na Utulivu.
Hawa ni Viongozi wa Dini Mkoani Kagera Waliohudhuria Uzinduzi Mihtasari ya Somo la Dini na Maadili,Katikati Kutoka Kulia Ni Askofu Elisa Buberwa KKKT, Askofu Nestory Timanywa Jimbo Katoliki la Bukoba, Askofu Severine Niwemugizi Jimbo Katoliki la Rulenge, Nyuma Kabisa ni Masista na Mapadre Kutoka Kigoma, na Mstari wa Kwanza ni Viongozi wa BAKWATA Mkao wa Kagera.

mama kikwete aendelea na ziara lindi

IMG_8445
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasalimia watoto na wananchi wa kata ya Msinjahili waliohudhuria mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Kitumbikwela kilichoko katika wilaya ya Lindi Mjini tarehe 17.2.2013


IMG_8485Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wa Kata ya Msinjahili wakishangilia wakati wa mkutano wa hadhara ulihutubiwa na Mjumbe wa NEC wa wilaya ya Lindi Mjini Mama Salma Kikwete katika kijiji cha Kitumbikwela tarehe 17.2.2013.
IMG_8499Wanachama wapya wa Chama Cha Mapinduzi na jumuia zake wakila kiapo mara baada ya kukabidhiwa kadi na Mjumbe wa NEC wa Lindi Mjini Mama Salma Kikwete katika kijiji cha Kitumbikwela tarehe 17.2.2013.
IMG_8525
Mjumbe wa NEC wa Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wananchi wa kata ya  Msinjahili kwenye kijiji cha Kitumbikwela tarehe 17.2,2013.
 PICHA NA JOHN LUKUWI