MMILIKI WA AC MILAN ATUPWA JELA MIAKA SABA KWA KUKUTWA NA HATIA YA KUFANYA NGONO NA KIBINTI CHA MOROCCO
Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
MMILIKI
wa AC Milan, Silvio Berlusconi amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela
na kufungiwa maisha kufanya kazi katika ofisi za umma baada ya kukutwa
na hatia ya kumlipa binti mdogo afanye naye ngono katika moja ya pati
zake za ‘bunga bunga’.
Waziri
huyo Mkuu wa zamani wa Italia, Berlusconi, mwenye umri wa miaka 76,
alimlipa binti mdogo wa Morocco, Karima El Mahroug, anayekwenda kwa jina
la utani, Ruby, kwa ajili ya ngono na baadaye akajaribu kumbambikizia
kesi ya wizi kwa kuwapigia simu Polisi na binti huyo akakamatwa.
Berlusconi na mwanamke huyo wamekanusha kufanya ngono.
Mwendesha
mashitaka alipendekeza afungwe miaka sita kwa kuzini ni binti mdogo na
matumizi ya nguvu, lakini majaji watatu wa kike katika Mahakama ya
Jijini Milan jana walitaka afungwe muda mrefu zaidi, miaka saba.
Mfungwa:
Mmiliki wa AC Milan, Silvio Berlusconi (juu) amekutwa na hatia ya
kumlipa binti mdogo wa Morocco, Karima El Mahroug wafanye naye ngono
San
Siro: Berlusconi ni mmiliki wa AC Milan, hapa akiwa katika picha ya
pamoja na kocha wa zamani wa klabu hiyo, Carlo Ancelotti mwaka 2007
Berlusconi pia amefungiwa maisha kufanya kazi katika ofisi za umma baada ya Waziri huyo Mkuu wa zamani kukutwa na hatia leo.
Lakini mfungwa huyo anaweza kukata rufaa mara mbili kabla hajamaliza kifungo chake, ambayo inaweza kuchukua miezi au miaka.
Maana yake hatatumikia kifungo chake hadi ashindwe rufaa zake.
Klabu
yake ya AC Milan – ambayo amekuwa Rais wake kwa vipindi vitatu tofauti
tangu mwaka 1987 – inayoundwa na nyota kadhaa akiwemo Mario Balotelli –
ilimaliza katika nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu ya Italia, Serie A msimu
uliopita ikizidiwa pointi 15 nyuma ya wapinzani, Juventus.
Kifungo: Rais wa Mahakama, Giulia Turri (katikati) akisoma hukumu
Baada
ya hukumu, Mwanasheria wa Berlusconi, Niccolo Ghedini, mara moja
alitangaza kukata rufaa akisema hukumu hiyo ni kama ilivyotarajiwa,
haikutenda haki.
“Hii
ni kinyume cha uhalisia,” Ghedini aliwaambia Waandishi wa Habari nje ya
Mahakama. “Nimetulia kwa sababu nimekuwa nikisema kwa miaka mitatu
kwamba kesi haiwezi kuendeshwa hapa,” alisema Ghedini.
Kimwana:
Alisema
pati hiyo ya chakula cha usiku ilikuwa kwa ajili ya watu maaum;
Mwendesha mashitaka amesema walifanya ngono na mwanamke huyo aliyelipwa
kuhudhuria.
Hata
kama Berlusconi alikuwa anamjua mwanamke huyo katikati ya kesi hiyo,
Karima el-Mahroug, anafahamika vyema kwa jina lake la utani, Ruby the
Heart Breaker, ametoa ushahidi.
Alikuwa
ana umri wa miaka 17 wakati huo anadaiwa kufanya kitendo hicho, lakini
sasa amefikisha miaka 24. wakati umri wa kufanya ngono Italia ni miaka
14, na ni kinyume cha sheria kumlipa binti aliye chini ya umri wa miaka
18 kwa ajili ya ngono.
El-Mahroug
aliitwa kwa utetezi, lakini akashindwa kutokea kwa sababu
kadhaa,kuchelewesha hukumu. Timu ya Berlusconi mara moja ikamengua
katika orodha ya mashahidi.
Maelezo:
Mwanasheria wa Silvio Berlusconi, Niccolo Ghedini akizungumza na
Waandishi wa Habari nje ya Mahakama jana Jijini Milan, Italia.
No comments:
Post a Comment