BAYERN MUNICH WAMTAMBULISHA RASMI PEP KATIKA MKUTANO MZITO ALLIANZ ARENA…JUPP HEYNCCKES SAFARI YAIVA!!
Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Mabingwa
wa mataji matatu, Bayern Munich wamemtambulisha kocha wao mpya, Pep
Guardiola leo katika Mkutano na Waandishi wa Habari, The Bavarians
wakijiandaa kuendelea kutamba katika soka ya nyumbani na Ulaya.
Kocha
huyo wa zamani wa Barcelona amesema yuko tayari kukabiliana na
changamoto za kufundisha timu iliyofanya vizuri msimu uliopita chini ya
Jupp Heynckes, ikishinda mataji ya Ligi Kuu ya nyumbani na makombe
mawili, pamoja na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
“Lazima
nikubali mlinganisho,” alisema Guardiola, akiwa katika vazi nadhifu la
suti ya vipande vitatu ya rangi ya kijivu akizungumza Kijerumani kwenye
Mkutano uliofanyika ukumbi wa mikutano wa klabu, Allianz Arena.
“Lazima
niwe tayari kuishi na hiyo. Nipo chini ya shinikizo, wazi, lakini
nafahamu hili na nakubali changamoto hii bila woga na ndiyo maana mimi
ni kocha,”alisema.
Guardiola,
ambaye aliyeshinda mataji 14 katika miaka minne ya kuwa na Barcelona,
usajili wake ni mkubwa Bayern na hasa ikizingatiwa anahamia timu
iliyofanya vyema. Alitumia mwaka wake mzima baada ya kuacha kazi
Hispania mwaka 2012, kwa kupumzika New York, Marekani.
“Kitu
nachofikiria kwa sasa ni zawadi, baraka kuwa hapa na Bayern,”alisema
kocha huyo Mspanyola, aliyesaini Mkataba wa miaka mitatu.
Shinikizo? Pep Guardiola anakuwa kocha wa mabingwa wapya wa Ulaya, Bayern Munich
Kujiamini: Guardiola akizungumza leo
Waliohudhuria mkutano huo wa kutambulishwa Guardiola bosi mpya Bayern
Wanne mashuhuri: Guardiola aliungana na Matthias Sammer, Karl-Heinz Rummenigge na Uli Hoeness
Aisema sababu ya kwanza iliyomfanya akubali ofa ya kuifundisha Bayern ni wachezaji wa klabu hiyo na historia yake.
Karibu, Pep! Kocha tayari anajisikia nyumbani katikati ya watu
Kiroho safi? Guardiola akiwa na kocha anayeondolewa Bayern, Jupp Heynckes.
No comments:
Post a Comment