Thursday, April 2, 2015

Magazetiiii Leo


Na Awadh Ibrahim

SUMATRA YASEMA LAZIMA NAULI ISHUKE

  • Written by  Bukobajamii
david-Mziray1_b0adf.jpg
Meneja Mawasiliano wa SUMATRA, David Mziray
SIKU chache baada ya Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta kutaka uangaliwe uwezekano wa kushusha nauli za vyombo vya usafiri nchini, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imesema inatekeleza agizo hilo na kwamba nauli za daladala na mabasi ya mikoani zitashuka wakati wowote kuanzia sasa.

Imeongeza kuwa, licha ya bei ya mafuta kupanda kidogo jana, hakutaathiri kushuka kwa nauli, kwani ukokotoaji utafanyika kwa wastani wa bei ya mafuta ilivyoshuka kwani haitapanda kwa kiasi kikubwa kwa mara moja.

Hayo yalisemwa jana na Meneja Mawasiliano wa Mamlaka hiyo, David Mziray aliyesema wanatekeleza agizo la Waziri Sitta aliyetaka nauli zishuke kufikia kesho, lakini wamechelewa kutokana na muda wa kuwasilisha maoni kwa wadau waliopewa siku 14 kufikia ukomo leo.

“Tunawahakikishia wananchi kuwa baada ya kumaliza siku za kupokea maoni ya wadau hususan wamiliki wa mabasi ya daladala waliopewa siku 14, mchakato huu utakwenda haraka na mapema iwezekanavyo tutatangaza nauli hizo mpya,” alisema.

Mziray alisisitiza kuwa hakuna sababu ya kutoshusha nauli, bali wanafuata taratibu na kanuni hivyo kuwataka wananchi kuwa na subira kwa siku chache zijazo.

Wiki hii, Waziri Sitta aliwataka Sumatra kuharakisha mchakato huo wa kushusha nauli ufanyike haraka iwezekanavyo na ifikapo kesho wawe wametangaza nauli hizo mpya, kwani kwa muda mrefu bei za mafuta zimeshuka kutoka zaidi ya sh 2,200 hadi chini ya Sh 1,800.

Wadau wa usafiri walipendekeza kupunguzwa kwa nauli za mabasi yaendayo mikoani kwa viwango vya kati ya asilimia 15 na 25 huku wakitaka nauli za daladala zipungue kutoka Sh 400 hadi Sh 300 kwa njia ya umbali wa kilometa 10.

Walitaka kwa mabasi ya kawaida kwa Moshi na Arusha (Sh 17,000 badala ya Sh 22,700), Mwanza (Sh 32,369 badala ya Sh 42,000), Mbeya (Sh 23,365) badala ya Sh 30,700), Bukoba (Sh 40,756 badala ya Sh 55,000) na Dodoma (Sh 12,678 badala ya Sh 16,700).

Kwa usafiri wa daladala wamesema wanataka iwe Sh 300 kwa kilometa kuwa Sh 31.39 kwa usafiri wa kilometa 10 badala ya Sh 400. 

CHANZO: HABARI LEO (Muro)

Monday, January 20, 2014

Maishaaaa


Magazeti

DSC 0014 2a44b
DSC 0015 e26b5
DSC 0016 efbd8
DSC 0017 293a5
DSC 0018 15111
DSC 0019 7103d
Hudugu
DSC 0020 330c7
DSC 0021 7439c
DSC 0022 3b0e7
DSC 0023 d94a9
DSC 0024 42a54
DSC 0025 a8eda
DSC 0026 df291

Tuma Maoni

Kiapo

Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Adam Malima, kuwa Naibu Waziri wa Fedha, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam

 Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Charles Kitwange, kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam

 Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Jenista  Mhagama, kuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam

  Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Dkt. Pindi Chana, kuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu.



 Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Mwigulu Nchemba, kuwa Naibu Waziri wa Fedha, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Juma Nkamia, kuwa Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam

Wageni wa heshima.

Picha ya pamoja.

WAZIRI MKUU AKIKAGUA MAREKEBISHO YA UKUMBI WA BUNGE

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua marekebisho yanayofanyika katika ukumbi wa Bunge  mjini Dodoma Januari 18, 2013 ikiwa ni maandalizi ya  Bunge la Katiba linalotarajiwa kuanza mwezi ujao. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akikagua kazi ya uwekaji viti vipya  katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Januari 18,2014 ikiwa ni maandalizi ya  Bunge la Katiba linalotarajiwa kuanza mwezi ujao. (Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu)