Thursday, August 23, 2012

Taasisi Za Kidini Zakanusha Uamsho


Na:  Idara ya Habari,MAELEZO
Taasisi mbalimbali za kidini hapa nchini zilizopata usajili rasmi kwa Mrajis Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zimekanusha kuhusika na tamko lililotolewa na Amiri Mkuu wa Jumuiya ya Uamsho, Sheikh Mselem Ali la Waislamu wa Zanzibar wagomee kushiriki katika Sensa ya Watu na Makaazi Kitaifa inayotarajiwa kufanyika Jumapili ijayo.

Wakizungumza na Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhil Soraga Wawakilishi wa Taasisi hizo wamelaani tabia ya Uamsho ya kujipa Mamlaka ya kuzisemea Taasisi hizo.

Aidha,wameitaka Jumuiya ya Uamsho kuthibitisha ni kikao gani kilichokaa na kuzungumza na Taasisi za Kidini na kuamua kwa pamoja kutowa tamko hilo la kupinga kushiriki kwa Waislamu katika Sensa.

Aidha, wameihakikishia Afisi ya Mufti na Serikali kuwa watashiriki katika Sensa ili kusaidia maendeleo ya Zanzibar na kutatua baadhi ya migogoro ya kijamii na sio kujiingiza katika siasa na kupingana na Serikali kama ambavyo imekuwa ikifanya Jumuiya ya Uamsho.

Taasisi zimewataka Waislamu kushirikiana na Serikali na kuachana upotoshaji unaofanywa na Uamsho.

Aidha, wameitaka Jumuiya ya Uamsho kuachana mara moja kutumia kivuli cha umoja wa Taasisi za kidini Zanzibar wanapoamua mambo yao kwani Jumuiya hizo nyingi hazikubaliani na Sera yao ya fujo na vurugu.

Mwisho.
Imetolewa na:
Idara ya Habari(MAELEZO) Zanzibar
23/08/2012

Mkuu Wa mkoa Wa Kilimanjaro Awapa Siku Moja Wenyeviti Wa Vitongoji Hai Kufafanua Wanataka Kufanya Kazi Za Serikali Ama La




Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akizungumza na wanahabari (pichani chini ) kuhusiana na maandalizi ya Sensa katika mkoa huo.

Na Dixon Busagaga Hai.
WENYEVITI wa vitongoji 116 katika wilaya ya Hai,wametishia kutoshiriki zoezi la sensa ya watu na makazi inayotarajia kufanyika usiku wa kuamkia Agosti 26 nchini kote kwa madai wanaidai halmashauri hiyo kiasi cha Sh Mil 280.8 ikiwa ni fedha zao za posho kuanzia mwaka 2009 hadi sasa.

Mkuu wa mkoa huo,Leonidas Gama, aliyasema hayo katika mkutano wake na wanahabari akizungumzia maandalizi ya zoezi hilo ambalo alisema limekamilika kwa asilimia kubwa .

Pamoja na kuwepo kwa tishio hilo,mkuu wa mkoa alisema wenyeviti hao wamepewa muda wa siku moja kufafanua msimamo wao iwapo wanataka kuendelea kufanya kazi za serikali ama la kutokana na kwamba madai yaohayahusiani na shughuli ya sensa.

“Kwa sasa tunachangamoto mbili kubwa, hii ya kikundi cha waislamu na hawa wenyeviti wa vitongoji wilayani Hai….nimeongea na viongozi wa wilaya yao nikawataka kama msimamo wao ni kutoshiriki zoezi hili, basiwaandike barua ya kujiondoa katika nafasi zao za uenyekiti”alisema Gama..

Aidha Gama amesema kwa mujibu uongozi wa halmashauri ya wilaya, madai ya wenyeviti hao hayakulipwa mapema kutokana na kukosekana kwa fedha katika bajeti lakini kwa mwaka huu ni miongoni mwa madai yatakayopewakipaumbele katika malipo.

Kuhusu kikundi cha waislamu wanaopinga zoezi hilo kilichopo katika wilaya za Same,Mwanga,Moshi mjini na Hai ,Gama alisema tayari jitihada zimefanyika kuwashirikisha viongozi wa madhehebu ya dini ili kuwaelimisha waumini wao kushiriki zoezi hilo.

Alisema mkoa una makarani wa sensa 4937 ambao wamegawanyika katika makundi mawili moja likiwa na makarani 2156 kwa ajili ya kujaza dodoso refu na 2279 kwa ajili ya Dodoso fupi huku makarani wa akiba wakiwa 153 na wasimamizi 349.

Akizungumzia vituo kwa ajili ya zoezi hilo alisema kuna vituo 3357 vilivyogawanywa katika makundi mawili ya Dodoso fupi vilivyopo 2279 na dodoso refu vipo 1078 na kwamba Agosti 23 imetengwa kwa ajili ya kutambua maeneo ya kazi ambapo wataongozwa na wenyeji wao ambao ni wenyeviti wa vitongoji,vijiji na mitaa.

Mkuu wa mkoa aliwataka wananchi kutunza kumbukumbu za taarifa za watu watakaolala katika nyumba zao kwa usiku wa kuamkia Agosti 26 na kwamba zoezi hilo litafanywa kwa siku saba na wasihofu iwapo makaranihawatafika tarehe 26 bali wasubiri hadi watakapofika kwa takribani siku saba

Magazeti














Wednesday, August 22, 2012

Sheriagua Walemavu Yadaiwa Kuwabagua Walemavu Wa akili

Mtetezi wa Haki za Watu wenye Ulemavu na Rais wa Shirika la Kutetea Haki za Binadamu(POTA)Idrisa Masalu akitoa mada katika semina ya kutetea haki za walemavu wa akili iliyofanyika mjini Bukoba
Ofisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Kagera Rebeca Gwambasa akifungua semina
Washiriki wa semina
Picha ya pamoja na mgeni Rasmi
Mtaalamu wa kitengo cha watoto wenye ulemavu wa akili kutoka Bunazi Wilayani Missenye Mwl Gervase Anatory akitoa mchango wake wakati wa semina
Phinias Bashaya,Bukoba
SHERIA ya watu wenye ulemavu imetajwa kuwabagua watu wenye ulemavu wa akili baada ya haki zao kutofikiwa kwa urahisi tofauti na walemavu wengine huku sheria ikishindwa kulitaja moja kwa moja kundi hilo.
Hayo yamebainishwa katika semina iliyoandaliwa na Chama kwa Ajili ya Watu wenye Ulemavu wa Akili(TAMH)na kuwakutanisha wataalamu wa watu wenye ulemavu wa akili kutoka wilaya mbalimbali za Mkoa wa Kagera.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa chama hicho Anacret Rugaihuruza watu wenye ulemavu wa akili wana mahitaji makubwa zaidi ya wenzao na sheria ilitakiwa kufafanua haki zao bila kujumuishwa moja kwa moja katika sheria ya jumla ya haki za walemavu.
Alisema chama hicho pamoja na jukumu la kuwasemea walemavu wa akili ni muhimu jamii kutambua kuwa hata walemavu wa kundi hilo wana haki ya kupata mahitaji mengine kama kuoa na kuwa na familia.
Katika semina hiyo iliyofadhiliwa na Shirika la The Foundation for Civil Society,Ofisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Kagera Rebeca Gwambasa alikiri sheria ya walemavu kuwa na mapungufu  yanayolitenga kundi la walemavu wa akili.
“Katika haki za walemavu kundi la walemavu wa akili halifikiwi na haki hizo inaonekana wakati sheria inatungwa makundi yote hayakushirikishwa hata hivyo Serikali iko tayari kupokea ushauri”alisema Gwambasa
Miongoni mwa washiriki wa semina hiyo Gervase Anatory ambaye ni mtaalamu wa
kwa hisani ya bukoba pamoja blog

JK: Amteua Winfrida Korosso Kuwa Katibu Wa Tume Ya Kurekebisha Sheria Nchini.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bibi Winfrida Beatrice Korosso kuwa Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria nchini.

Taarifa iliyotolewa leo, Jumatano, Agosti 22, 2012 mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inasema kuwa uteuzi huo ulianza Agosti 14, mwaka huu, 2012.

Kabla ya uteuzi wake, Bibi Korosso alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Mkurugenzi wa Mashtaka katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dar es Salaam.

Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.  Dar es Salaam.
22 Agosti, 2012
Reactions::

Mitaala Shule Za Msingi Inawachanganya Wanafunzi – Walimu

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kitopeni ya Mjini Korogwe, akizungumza na mtandao wa Thehabari.hivi karibuni.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Kitopeni kutoka Wilaya ya Korogwe.

“Mabadiliko ya mitaala na mchanganyiko wa vitabu bila utaratibu mahususi ni tatizo, kwa sasa hivi kila shule ina kitabu chake katika somo fulani…hata hivyo licha ya mabadiliko ya mara kwa mara hakuna maandalizi, mimi tangu nimalize chuo 1979 sijaenda semina yoyote wala mafunzo kujiandaa na mabadiliko ya mitaala hii. Hili linachangia pia,” alisema mwalimu Mtui.

Akifafanua zaidi Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Muungano, ya wilayani Moshi, Ashati Elihaki alisema mbali na mchanganyiko juu ya suala la vitabu vya masomo mabadiliko ya mitaala yamegeuza baadhi ya masomo kubaki kama ‘kiini macho’ jambo ambalo ni tatizo kwa walimu.

“…angalia kwa mfano somo kama la Tehama linaloanza kufundishwa darasa la tatu hadi la saba somo hili lipo kinadharia zaidi, hakuna walimu ambao wameandaliwa kufundisha somo hili lakini linatakiwa kufundishwa eti kwa kutumia mwongozo wa mwalimu kimsingi hii si sawa,” alisema Elihaki.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kitopeni ya Mjini Korogwe, Theodolph Karigita alisema tofauti na ilivyokuwa hapo awali mitaala ya sasa imevurugwa kiasi kikubwa jambo ambalo linawachanganya walimu na hata wanafunzi hivyo kushindwa kufanya vizuri.

“…Mitaala imevurugwa sana, kunamchanganyiko wa masomo nadhani unakumbuka kuna kipindi baadhi ya masomo yaliunganishwa kama Jiografia, Historia na Uraia wakaita maarifa ya jamii…kipindi hiki wanafunzi walifanya vibaya sana hivyo ikabadilishwa sasa watoto wanafanya vizuri tofauti na awali,” alisema Karigita.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Lwengera Darajani, Youze Mbwambo alisema idadi kubwa ya masomo kwa wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la tatu ni chanzo kingine cha wanafunzi hao kufanya vibaya kwani wamekuwa wakibebeshwa mzigo pasipo sababu za msingi.

Akizungumzia hoja hizo zilizotolewa na baadhi ya walimu, Ofisa Elimu Taaluma, Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Elius Mkwizu alisema mabadiliko yanayofanywa na wataalamu hufanywa kwa malengo mazuri licha ya kuwepo na changamoto kadhaa maeneo tofauti.

Habari hii imeandaliwa na Mtandao wa Thehabari.com (www.thehabari.com) kwa kushirikiana na Taasisi ya HakiElimu.

Tuesday, August 21, 2012

Matukio Mbalimbali


Katibu tawala wa mkoa wa Kagera, Nassor Mnambila akifungua kikao cha kuhamasisha masuala ya sensa na makazi kilichoandaliwa na halmashauri ya manispaa ya Bukoba kwa kushirikiana na wilaya ya Bukoba kilichowashirikisha viongozi wa madhehebu ya dini, viongozi wa vyama vya siasa na waandishi wa habari kilichofanyika kwenye ukumbi wa manispaa ya Bukoba, alikuwa akisema kuwa serikali haitawavumulia wale wote watakaokataa kuhesabiwa.




Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya manispaa ya Bukoba Robert Kwela Kushoto na katibu tawala wa wilaya ya Bukoba Clement Ndyamkama kulia wakiwasikiliza kwa makini viongozi waliokuwa wanahamasisha masuala ya sensa na makazi.




Mkuu wa wilaya ya Bukoba akiwaeleza viongozi wa dini, waandishi wa habari na viongozi wa vyama vya siasa wawahamasishe wananchi washiriki kikamilifu kwenye zoezi la sensa wa watu na makazi.



Katibu wa Chama Cha Mapinduzi akiongea na wajumbe wa kikao cha kuhamasisha masuala ya sensa.




Baadhi ya waandishi walioudhuria mafunzo ya habari ya uchokonozi wakimskiliza Phil Karashani.




Baadhi ya waandishi wakijadili mambo kwenye makundi.



Baadhi ya waandishi walioudhuria mafunzo ya kuandika habari za uchokonozi wakijadili mambo kwenye makundi.




Phil Karashani akitoa elimu kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Kagera juu ya habari cha uchokonozi.

Taifa Kubwa


Maisha Yanaendelea


Magazeti Magazeti











Mahakama Yatengua Ubunge Jimbo La Igunga

Mahakama Kuu Kanda ya Tabora imetoa hukumu ya kesi ya ubunge iliyokuwa ikimkabili mshindi wa ubunge jimbo la Igunga Dk Peter Kafumu (CCM).Hukumu hiyo ya kupinga matokeo yaliyompatia ushindi Dk Kafumu imetolewa leo ambapo imemuengua mbunge huyo katika nafasi yake ya ubunge

Shauri hilo lilifunguliwa na mlalamikaji Joseph Kashindye dhidi ya Dk Kafumu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na msimamizi wa uchaguzi

Picha Mbalimbali


Baadhi ya wakati wa manispaa ya Bukoba wakiadhimisha sikukuu ya Idd El Fitri kwenye hoteli ya kimataifa ya Bukoba Coop Hoteli inayomilikiwa na chama cha ushirika Kagera (KCU) iliyoko kwenye ufukwe wa ziwa Victoria.




Baadhi ya wakazi wa manispaa ya Bukoba wakila vitu ndani ya hoteli ya Paradise wakati wa sikukuu ya Idd El Fitri.




Vijana wakibembea kwenye mabebea ya manispaa ya Bukoba yaliyojengwa kwa hisani ya Rotary club ya Bukoba.




Mambo hayo! hii sio foleni ya jambo lolote bali ni baadhi ya vijana wakijimwaga kwenye ukumbi wa disco wa stone hoteli ulioko kwenye ufukwe wa ziwa victoria.




Baadhi ya wakazi wa manispaa ya Bukoba wakijivinjali kwenye ufukwe wa hoteli ya kimataifa ya Spice wakati wa sikukuu ya Idd.




Viburudisho mbalimbali vilivyokutwa kwenye ufukwe wa hoteli ya spice wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya Idd el Fitri.




Na hawa walikutwa wakivinjali kwenye ufukwe wa hoteli ya Spice.




Mmoja wa wamiliki wa tovuti hii Margareth Mwesiga akijadili masuala ya arusi ya Edius Njunwa na Dr. Buberwa na mkewe kulia kwenye viwanja vya Bukoba Club vilivyoko katika manispaa ya Bukoba.




Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Askofu Mstaafu wa Jimbo la Dodoma Mhashamu Mathias Isuja katika sherehe za kuadhimisha miaka 10 ya Kijiji cha Matumaini cha Dodoma kinacholea watoto yatima, Agust 18, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)




Jengo la hospitali ya mkoa wa Kagera litakalotumiwa kutoa huduma ya tiba ya daraja la kwanza, linatoa matibabu kwa waginjwa wa nje na wanaolazwa, lina vyumba vya kulaza wagonjwa vyenye huduma zote vikiwemo viyoyozi, gharama ya chumba ni kati ya shilingi 30,000 hadi 75,000 kwa siku.




Mandhari ya jengo la hospitali huu ya mkoa linalotumika kutoa huduma ya tiba ya daraja la kwanza.




Mabasi haya hufanya safari zake kati ya mikoa mingine na mkoa wa kagera yalikuwa maeneo ya kituo kikuu cha polisi inadaiwa yalikiuka kanuni za sheria za usalama barabarani.




Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua kampeni ya uhamasishaji wa sensa ya watu na makazi kwenye viwanja vya mnazimmoja jijini Dar es salaam Agust 17,2012.Watatu kushoto ni Makamu wa Pili wa rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd na kulia kwake ni Kamishina wa Sensa, Hajati Amina Mrisho(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika swala ya Magharibi kabla ya kushiriki katika futari aliyoandaliwa na wananchi wa Tanga jana Agosti 15, 2012 jijini Tanga



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea hati za utambulisho toka kwa balozi mpya wa Spain hapa nchini Mhe Luis Manuel Cuesta Civis leo Agosti 16, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam




Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na balozi mpya wa India hapa nchini Mhe Debnath Shaw baada ya kupokea hati zake za utambulisho leo Agosti 16, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam.




Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali mstaafu Fabian Massawe akiongea na waumini wa dhehebu la kiisilamu aliowaandalia futari kwenye viwanja vya Ikulu ndogo iliyoko katika manispaa ya Bukoba, alikwa akiwaeleza waapuuze waislamu wachache wanaotaka kukwamisha zoezi la sensa ya watu na makazi, alikuwa akiwaambia kuwa mungu ni mmoja.




Mmiliki wa Cable inayosambaza mawasiliano katika manispaa ya Bukoba, Mohamed akiagana na mkuu wa mkoa baada ya kula futari.




Askofu Buberwa wa kanisa la kiinjiri la kirutheri diosisi ya kaskazini Magharibi alikuwa ni miongoni wmwa wageni walioalikwa kushiriki kwenye futari iliyoandaliwa na mkuu wa mkoa, kulia kwake ni sheikh Haruna Kichwabuta.




Baadhi ya viongozi walioungana na mkuu wa mkoa kula futari aliyoiandaa kwa ajili ya waumini wa dini ya kiislamu.




Massawe katikati, kulia kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Philip Kalangi na kushoto afisa wa ofosi ya mkuu wa mkoa, Mrisho.




Waumini wa dini ya Kiislamu na wageni waalikwa wakila futari iliyoandaliwa na Massawe kwenye viwanja vya Ikulu ndogo ya Bukoba.




Baadhi ya wageni walialikwa kula futari.




Baadhi ya wageni waalikwa wakila Futari, kulia ni anajulikana kwa jina maarufu la China na anayefuata anajulikana kwa jina la Cheyo.



Mjumbe wa sekretarieti ya mkoa wa Kagera Fikir Kisimba (kulia) akiwa na wakuu wa wilaya nje ya viwanja vya ukulu ndogo ya Bukoba.