Thursday, September 13, 2012

Magazeti Magazeti











Vijana Watakiwa Kujishugulisha Na Kazi za Maendeleo Na Kuachana Na Matumizi Ya Dawa Za Kulevya

Na Mwandisi wetu
Bukoba

VIJANA mkoani Kagera wameshauriwa kujishugulisha na kazi mbalimbali za kuwaletea maendeleo na kutakiwa kuachana na matumizi ya dawa za kulevya ili kuweza kuwasaidia kutatua matatizo ambayo yanawakabili kimaisha ili kukabiliana na tatizo kubwa la ajila kwa vijana.

Ushauri huo umetolewa na Godfrey Inocenti ambaye ni mwenyekiti wa shirika la Maejor Allienge education center (MAEC) la mkoani Kagera linalojishugulisha na kupambana na dawa za kulevya hasa kwa vijana wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo ikiwemo utawala bora wa asasi na usimamizi wa fedha kwa wanachama wa shirika hilo.

Alisema kuwa kwa hivi sasa nguvu kazi nyingi ya vijana imepotea kutokana na kujihusisha na madawa ya kulevya ikiwemo uvutaji wa bangi unywaji wa pombe uliokithiri jambo ambalo limepelekea vijana kukumbwa na wimbi la umasikini.

Inocenti aliongeza kuwa shirika hili la MAEC linajitahidi kwa kasi kubwa kuhakikisha linawashawishi vijana kutambua athari za utumiaji wa madawa ya kulevya na kuwataka wapinge utumiaji huo na kujihusisha na shughuliza uzalishaji mali.

Kwa upande wake mratibu wa mafunzo hayo  Edwini Sebastiani alisema kuwa jumla ya wanachama 45 wamenufaika kupata mafunzo ambayo yamefadiliwa na shirika la the foundation for civil society ambao wao ndio watakuwa mabarozi wazuri kwa vijana wengine mkoani Kagera na kuomgeza kuwa mbali na kutoa elimu watapata uongozi bora,usimamizi wa fedha na uandishi bora wa miradi.

Aliongeza kuwa shirika hilo lililo anzishwa mwaka 2007 mkoani Kagera limewanufaisha jumla ya vijana 1250 kwa kuwapa elimu bora na kuwanusuru na utumiaji wa dawa za kulevya na wao kuendelea kuwashauri vijana wengine.




Wednesday, September 12, 2012

Maisha................................

 

CHADEMA V/c CCM





 Godfrey Chikandawali alipokuwa akitambulishwa rasmi baada ya kuvua gamba na kuvaa gwanda
 John Heche Mwenyekiti wa BAVICHA akihutubia mkutano wa wananchi wa Mwenge wilaya ya kinondoni

CHADEMA Imeendelea kuwatesa wapinzani wao CCM kwa kuendeleza kwa kasi kampeni yake ya VUA GAMBA VAA GWANDA,ambapo jana jioni kabisa Mwenyekiti Vijana (BAVICHA) John Heche aliwapokea wanachama wengi wa CCM walioamua kujivua magamba na kujiunga na M4C.Anayeonekana na gwanda jeusi pichani akiwa na mwenyekiti heche ni ndg Godfrey Chikandamwali aliyekuwa mjumbe wa kamati ya utendaji wa CCM wilaya ya Kinondoni,pamoja naye ni ndugu yake Anna Chikandawali mjumbe wa UWT wilaya,na wengine wengi.Heche amepokea wanachama hao Mwenge jijini Dar es Salaam
Picha kwa hisani ya Jackson Makala

Magazeti Magazeti











TCCIA Kagera Yakutana Na Waranya Biashara



Afisa wa mamlaka ya mapato mkoani Kagera, Lufungu Mtafya akitoa elimu kwa wafanyabiashara wa manispaa ya Bukoba wanatumia mashine zinazoisaidia mamlaka hiyo kukusanya ushuru, semina ilifanyika kwenye ukumbi wa chama cha msalaba mwekundu na iliandaliwa na TRA kwa kushirikiana na chama cha wafanyabiashara, wakulima na wenye viwanda nchini (TCCIA).



Meneja wa TRA Kagera Leonard Shija kushoto na meneja wa SUMATRA wakisikiliza kwa makini elimu yaliyokuwa inatolewa kwa walipa bodi wanaotumia mashine kukusanya ushuru wa serikali.




Mkurugenzi wa kampuni ya Bukoba Machinery, Rose Kagilita inayojihusisha na uwakala wa ndege ya precision na mataili alikuwa pia miongoni mwa washiriki wa semina, kulia ni diwani wa kata ya Hamgembe Robert Katunzi maarufu kwa jina la tabu gani mara moja.




Baadhi ya viongozi walioandaa semina ya wafanyabiashara wanaotumia mashine za kukusanya ushuru, kutoka kushoto ni Katibu wa TCCIA Rwiza, Meneja wa TRA mkoani Kagera, Leonard Shija na kulia ni meneja wa SUMATRA, Japhet Ole Roysimaye.



Mhasibu mkuu wa kiwanda cha kusindika kahawa kilichoko mkoani Kagera TANICA Joston Rwiza, alikuwa miongoni mwa walioudhuria semina hiyo.




Mwanasheria wa kujitegemea Bw. Chamani alikuwa miongoni mwa walioudhuria semina hiyo.




Baadhi wa wafanyabiashara walioudhuria semina iliyoandaliwa na TRA kwa kushirikiana na TCCIA.

Tuesday, September 11, 2012

Waandishi Kagera Wataka RPC Iringa Ang'olewe

HOTUBA FUPI YA KUPOKEA MAANDAMANO YA KULAANI KIFO CHA DAUD MWANGOSI NA RAIA WENGINE WALIOUWAWA KATIKA MAZINGIRA YENYE  UTATA NA POLISI
Ndugu waandishi wa habari wa Mkoa wa Kagera leo tumeungana na waandishi wengine kote nchini kulaani  tukio la kuuawa kwa aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha television cha Chanel Ten Daud Mwangosi,pamoja na raia wengine waliopoteza maisha katika mazingira yenye utata.
Kifo cha marehemu Daud Mwangosi sio tu kuwa kiliishitua jamii ya waandishi wa habari hapa nchini,bali pia kifo chake kimekuwa sehemu ya mjadara katika vyombo vya habari vya Kimataifa hasa baada ya mazingira ya kifo chake kuonyesha alifia mikononi mwa Polisi.
Leo tumefanya maandamano ya amani kuonyesha kutoridhishwa kwetu na matumizi makubwa ya nguvu za jeshi la Polisi ambao mara nyingi wamehusishwa na vifo vya raia wasio na hatia yakiwemo mauaji ya Daud Mwangosi ambaye alikuwa akitekeleza majukumu yake ya kazi.
Matukio ya vifo katika maeneo mbalimbali nchini yameliweka jeshi la Polisi katika uhusiano wenye shaka kati yao na waandishi wa habari ambapo wajibu wa msingi wa askali Polsi ni kuwalinda raia na mali zao.
Kwa mujibu wa ushahidi wa picha katika eneo la tukio,mauaji ya Mwangosi yalikuwa ya kikatiri,unyama na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.Ni mauaji yaliyolifedhehesha taifa ambalo tangu mwaka 1961 tumejipatia sifa ya taifa lenye utulivu na linaloheshimu na kulinda haki  ya kuishi kwa raia wake.
Hivyo wakati tukiendelea kuomboleza kifo cha mwenzetu pamoja na raia wengine waliopoteza maisha katika mazingira yenye utata unaohusishwa na nguvu kubwa za jeshi la Polisi sisi waandishi wa habari wa Mkoa wa Kagera tunatoa tamko lifuatalo.
Kwamba tunataka  askali wanaohushwa na tukio la kifo cha Daud Mwangosi wasimamishwe kazi ili kupisha uchunguzi unaoendelea ufanyike kwa uhuru na haki.
Kwamba kwa kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda alikuwepo katika tukio hilo na alikataa kutoa msaada wa kuokoa maisha ya Mwangosi wakati askali wake wakiendelea kumsurubu, tunamtaka awajibike au wajibishwe na nafasi yake apewe RPC atakayekuwa tayari kutekeleza kwa vitendo ulinzi na usalama wa raia.
Kwamba kama tutaona mwenendo wa suala hili hauleti tija na kutoridhishwa na majibu ya tume iliyoundwa tutashirikiana na taasisi nyingine zinazotetea haki za binadamu ili kutafuta njia bora ya kuishitaki Serikali.
MWISHO tunalitaka Jeshi la Polisi kuweka utaratibu utakaowawezesha wanahabari kufanya kazi yao bila dharau na kujengewa hofu inayotokana na  vitisho vya Polisi. Tunataka Serikali iandae utaratibu ambao  wanahabari,wanasiasa na polisi watautumia kufanya kazi hasa katika kipindi hiki ambapo nchi inakua katika demokrasia ya vyama vingi ili kuepusha nchi isitumbukie katika mazingira ya hatari zaidi.

JK Yuko Kenya Kwa Ziara Ya Kiserikali


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Mwai E. Kibaki wa Kenya pamoja na ujumbe wake wakiingia Ikulu ya Nairobi  Jumanne, 11 Septemba , 2012,  alipoanza Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu nchini humo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Mwai E. Kibaki wa Kenya wakipata picha ya kumbukumbu  Ikulu ya Nairobi  Jumanne, 11 Septemba , 2012,  alipoanza Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu nchini humo. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Mhe Bernard Membe na kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Profesa Sam K. Ongeri
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete  pamoja na ujumbe wake na wenyeji wao wakianza  Mazungumzo Rasmi ya Kiserikali kati ya nchi hizo mbili.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete  pamoja na ujumbe wake na wenyeji wakiongea na wanahabari na kisha kupiga picha ya pamoja baada ya  Mazungumzo yao Rasmi ya Kiserikali kati ya nchi hizo mbili.

.
PICHA NA IKULU

 =====================================================================
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili nchini Kenya  Jumanne, 11 Septemba , 2012,  kuanza Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu ikiwa ni ziara yake ya kwanza rasmi nchini humo ingawa ameshawahi kufanya ziara kadhaa za kikazi nchini Kenya.
Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi, Rais Kikwete ambaye amefuatana na mkewe, Mama Salma Kikwete, amepokewa na mwenyeji wake, Rais Mwai E. Kibaki na kwa mbwembwe zote za kiprotokali zinazoambatana na ziara rasmi za kiserikali.
Baadaye mchana, Rais amekwenda Ikulu ya Kenya ambako ametia saini kitabu cha wageni, akafanya mazungumzo ya faragha na Rais Mwai Kibaki kabla ya kufanyika kwa Mazungumzo Rasmi ya Kiserikali kati ya nchi hizo mbili majirani na wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC).
Baada ya mazungumzo hayo, Rais Kikwete na ujumbe wake amekwenda kwenye Chuo Kikuu cha Kenyatta ambako wamepokewa na Waziri wa Elimu ya Juu, Mheshimiwa Margaret Kamar, Mkuu wa Chuo hicho, Jaji Mstaafu Onesmus Mutungi na Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Olive Mugendi.
Kwenye chuo hicho ambacho Desemba 8, mwaka 2008, kilimtunuku Rais Kikwete Shahada ya Uzamivu ya Heshima, amefungua rasmi Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo hicho.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Shule hiyo, Rais Kikwete amesema kuwa utalii ni sekta muhimu sana katika chumi za nchi za Afrika Mashariki na ambayo mchango wake unagusa maisha ya maelfu kwa maelfu ya wananchi wa nchi za ukanda huo.
Rais pia amesema kuwa nchi hizo za Afrika Mashariki sasa zimekuwa ni eneo lenye mvuto mkubwa katika nyanja ya utalii ambao unaweza kuwaingizia wananchi na mataifa ya Afrika Mashariki mapato zaidi kama changamoto zinazoikabili sekta ya utalii kwa sasa zitashughulikiwa ipasavyo na kwa pamoja na nchi hizo.
Miongoni mwa changamoto ambazo Rais Kikwete amezitaja ni ukosefu wa miundombinu ya kutosha kufanikisha kwa namna bora zaidi sekta ya utalii, ukosefu wa juhudi za pamoja kuitangaza Afrika Mashariki kama eneo muhimu la utalii, na umuhimu wa kuboresha kiwango cha usalama wa watalii.
Aidha, Rais Kikwete amezielezea changamoto nyingine kuwa ni pamoja na umuhimu wa kuwepo na viza ya pamoja ya utalii kwa nchi zote za Afrika Mashariki, kuwepo kwa safari za ndege za kutosha kutoka kwenye mataifa makubwa yanayozalisha watalii kwa wingi kuja Afrika Mashariki na umuhimu wa kupungua kwa nauli za ndege za kuja Afrika Mashariki.
Jioni, Rais Kikwete ametembelea Taasisi ya Utatifi wa Kilimo ya Kenya (KARI) ambako anatarajiwa kupokelewa na Waziri wa Kilimo wa Kenya, Mheshimiwa Dr. Sally J. Kosgei na usiku alikuwa mgeni rasmi kwenye Dhifa ya Kitaifa ambayo itaandaliwa na mwenyeji wake, Rais Mwai Kibaki.
Leo Jumatano 11 Septemba, 2012  Rais Kikwete ataweka shada la maua kwenye Kaburi la Mwanzilishi wa Taifa la Kenya, Hayati Jomo Kenyatta, kwenye Viwanja vya Bunge la Kenya na kutembelea Kiwanda cha Maziwa cha Brookside Diary kwenye Barabara ya Thika.
Kwa mujibu wa ratiba ya ziara yake, Rais Kikwete atatembelea Chuo cha Taifa cha Ulinzi cha Kenya (National Defence College) kilichoko Karen, Nairobi, ambako atapokelewa na Waziri wa Nchi wa Ulinzi, Mheshimiwa Yusuf Haji na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Kenya, Jenerali Julius Karangi.
Baadaye, Rais Kikwete atakwenda kutembelea Kituo cha Magonjwa ya Moyo na Kansa kwenye Hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan ambako atapokelewa na Waziri wa Huduma za Matibabu, Mheshimiwa Anyang Nyong’o.
Baadaye jioni, Rais Kikwete, ambaye anaongozana na kundi kubwa la Wafanyabiashara wa Tanzania, atashiriki chakula cha jioni ambacho ameandaliwa na Jumuiya ya Wafanya Biashara ya Kenya.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
11 Septemba, 2012

Taswira Mbalimbali Za Wanahabari Waliondamana Leo Mjini Iringa Kulaani Mauaji Ya Mwangosi



 


           Mmoja wa wanahabari akilia kwa uchungu 
                 
                  Picha Denis Mlowe na Said Ng'amilo

Singida Nao Waandamana

 Askari wa usalama barabarani akiongoza maandamano ya wanahabari wa Singida walioandamana kupinga mauaji ya mwenzao
 Baadhi ya waandishi wa habari mkoa Singida-SINGPRESS wakiwa ofisi za klabu wakimsikiliza Mwenyekiti waoo, Seif Takaza
 Maandamano yakiendelea katika barabara mbalimbali manispaa ya Singida
 Mwenyekiti wa SINGPRESS, Seif Takaza(katikati), mratibu wa klabu hiyo Evarista Lucas(kushoto) na Shabani Msangi
 Wanahabari wa mkoa wa Singida wakiwa kwenye maandamano kwenye moja ya barabara za manispaa Singida kupinga mauaji ya mwandishi

Singida
Septemba 11,2012.

WANAHABARI Mkoani Singida wameungana na wenzao nchini kwa maandamano ya kulaani na kupinga kitendo cha jeshi la polisi kuhusika na mauaji ya mwandishi wa kituo cha Channel Ten mkoani Iringa Daudi Mwangosi, wakati akiwa kazini.

Kupitia umoja wa klabu yao ya habari mkoa Singida(SINGPRESS),  maandamano hayo yakisindikizwa na askari polisi yalianzia eneo la Benki ya NBC na kuendelea barabara ya Kawawa hadi kituo cha mafuta Esso.

Baadaye yaliingia barabara ya Soko kuu, msikitini, Mghandi, Ipembe, Karume, Kinyeto na kumalizikia kwenye ofisi ya klabu, kabla ya kupokelewa na Mwenyekiti wa SINGPRESS, Seif Takaza.

Akizungumza na waandishi 19 wa mkoa Singida walioshiriki maandamano hayo, Takaza alisema kitendo cha polisi kuhusika na mauaji hayo kimedhalilisha chombo hicho, pia ni ukiukwaji wa haki za binadamu, kulingana na mafunzo yao ya kijeshi.

“Mauaji ya mwangosi ni ya makusudi, hasa ikizingatiwa alikuwa chini ya mikono ya polisi, lakini mwisho wa siku akafia mikononi mwao….jambo hili lazima lipingwe kwa nguvu zote na watetesi wa haki za binadamu,”alisema.

Alisema mauaji hayo ni ya uonevu, kikatili na yanalifedhehesha taifa ambalo tangu lipate uhuru mwaka 1961 limejipatia sifa kubwa ya kudumu katika hali ya amani na utulivu kiasi cha kuitwa jina la kisiwa cha amani.

Aidha wanahabari hao wameomba kudumishwa kwa mahusiano ya jeshi la polisi na waandishi wa wa habari ili kuondoa uwezekano wa kutokea mauaji mengine kama hayo.

Hata hivyo wananchi wengi, waliyaunga mkono maandamano hayo na kuwakipunga mikono waandishi huku wakitamka neno la ‘Poleni’, kila ambako wanahabari walipita katika barabara mbalimbali za mjini Singida.
Na Elisante John