Tuesday, September 11, 2012

Picha Mbali Mbali


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi Chuo cha UIinzi (National Defence College) leo Septemba 10, 2012 Kunduchi jijini Dar es salaam. Kulia kwake ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange na kushoto kwake ni Mkuu wa Chuo hicho, Meja Jenerali Charles Makalala na kushoto kabisa ni aBalozi wa China nchini Tanzania Mhe. Lu Younqing.



Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi makubaliano yaliyofikiwa na Wakuu wenzake wa Nchi na Serikali za Ukanda wa Maziwa Makuu baada ya mkutano wao uliofanyika Septemba 8, 2012 katika Hoteli ya Speke Resort Munyonyo mjini Kampala, Uganda. Picha na Ikulu




Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wazee wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Halmashauri ya wilaya mjini Kahama Septemba 8,2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)




Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (kulia) akisalimiana na Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Buzwagi wilayani Kahama kwa ziara ya siku moja wilayani huomo, Septemba 8, 2012. Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum, Azza Hilal na watatu kulia ni mbunge wa Kahama, James Lembeli




Wasanii wa Khama wakicheza ngoma ya Waswezi wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Buzwagi, Kahama kwa ziara ya siku moja Septemba 8, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)




Hii ndio hifadhi iliyoko katika kisiwa cha Rubondo, angalia tembo wanaopatikana ndani ya kisiwa hiki.




Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda katika hoteli ya Speke Resort Munyonyo jijini Kampala leo Septemba 7, 2012. Rais Kikwete amewasili nchini Uganda leo kuhudhuria mkutano wa viongozi wa nchi za maziwa makuu.




Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani ya mkoa wa Kagera Winston Kabantega akiongea na waendesha pikipiki zinazofanya kazi ya kusafirisha abiria, Kabantega ni mdau mkubwa wa jeshi la polisi, amejitoa muanga hasa katika zoezi zima la kuwahamasisha waendesha pikipiki wahudhurie mafunzo ya udereva.




Baadhi ya waendesha pikipiki wengine wakisiliza kwa makini maelekezo yaliyokuwa yakitolewa na viongozi.




Baadhi ya waendesha pikipiki wakimsikiliza Mkonda.




Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, William Mkonda akiongea na waendesha pikipiki zinazofanya kazi ya kubeba abiria katika halmashauri ya manispaa ya Bukoba.




Baadhi ya pikipiki zinazofanya biashara mkoani Kagera.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange salamu za rambirambi kuomboleza kifo cha Luteni Kanali (mst) Adam Hussein Mwandu Makwaia (kwenye picha juu), aliyekuwa Mpambe wa Rais wa kwanza wa Tanzania, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Rais Ali Hassan Mwinyi.

Katika salamu zake, Rais Kikwete amemwambia Jenerali Mwamunyange: “Nimepokea kwa majonzi na masikitiko taarifa za kifo cha Luteni Kanali Makwaia ambaye nimejulishwa kuwa alipoteza maisha Jumanne, Septemba 4, mwaka huu, 2012, katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo mjini Dar es Salaam.” “Katika miaka yote ya utumishi wa Jeshi na utumishi wa umma, Luteni Kanali Makwaia alikuwa mwadilifu na mwaminifu kwa nchi yake, alikuwa na weledi wa kiwango cha juu katika taaluma yake ya kijeshi na alikuwa mtiifu kwa viongozi wake.

Nakutumia wewe Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi salamu zangu za rambirambi kufuatia kifo hiki,” amesema Rais Kikwete na kuongeza: “Aidha, kupitia kwako natuma salamu za pole nyingi kwa familia ya marehemu Makwaia ambao wamempoteza baba na mhimili wa familia. Pia, kupitia kwako, natuma salamu za rambirambi kwa maofisa na wapiganaji wote wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambao wamempoteza ofisa na mpiganaji mwenzao.”

Luteni Kanali (mst) Makwaia alijiunga na Jeshi Machi 24, mwaka 1974, na alilitumikia kwa miaka 23 na miezi tisa kabla ya kustaafu. Alikuwa Msaidizi wa Mpambe wa Rais kati ya mwaka 1978 na 1981 na kuwa Mpambe wa Rais kwa miaka sita hadi 1987. Amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 62.
Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu. Dar es Salaam.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo leo Keko, jijini Dar es salaam, kufuatia kifo cha Luteni Kanali (mst) Adam Hussein Mwandu Makwaia, aliyekuwa Mpambe wa Rais wa kwanza wa Tanzania, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Rais Ali Hassan Mwinyi. Marehemu amezikwa leo Septemba 6, 2012 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.




Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhiwa Tuzo ya Uongozi Bora wa sera ya Kilimo na Chakula toka kwa Bw. Ajay VAshee, Makamu Mwenyekiti wa asasi isiyo ya kiserikali inayohusika na sera za kilimo na chakula na Maliasili n ijulikanayo kama Food, Agriculture and Natural Resources Policy (FANRPAN) katika hoteli ya White Sands jana Septemba 5, 2012. Anayeshuhudia kulia ni Katibu Mtendaji wa FANRPAN) Dkt Lindiwe Sibanda. Tuzo hiyo, ambayo hutolewa kwa kiongozi aliyefanya juhudi kuhakikisha kuwepo kwa sera bora za kilimo na chakula nchini kwake, ilichukuliwa na Malkia Ntombi Indlovukazi wa Swaziland mwaka jana, wakati Rais Hifikepunye Pohamba alitunukiwa mwaka 2010, Rais Armando Emilio Gwebuza mwaka 2009 na Rais wa Malawi, Hayati Bingu Wa Mutharika, aliipokea mwaka 2008.




Waombolezaji wakiuweka kaburini mwili wa aliyekuwa Katibu wa Chama cha Wanajeshi Wastaafu (RAMETEA),Luteni Kanali Mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, `Adam Hussein Makwaiya katika mazishsi yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kisutu jijiniDar es salaam Agust 6, 2012 na serikali iliwakilishwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)




Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Naibu Waziri Mkuu wa China, Mhe. Hui Liangyu wakati alipompokea kwenye wuwanja wa ndege wa Dar es salaam Septemba 5, 2012. Mhe. Hui yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)




Nyumba ya asili ya Wahaya aina ya msonge ambayo huwavutia watalii wengi watembeleao mkoa wa Kagera, msonge huu unapatikana maeneo ya camp site yaliyoko kwenye ufukwe wa ziwa Victoria, msonge huu unatumika kwa malazi na mapumziko ya muda, mtu akiwa ndani hawezi kusikia joto.
Kiroyera Tours www.kiroyeratours.com www.kagera.org www.budap.org http://www.facebook.com/pages/Kiroyera-Tours-and-Consulting/171058592931255 http://www.twitter.com/kiroyeratours http://www.youtube.com/user/kiroyeratours P.O. BOX 485 BUKOBA, KAGERA, TANZANIA Tel: +255 28 2220203 Tel: +255-713-526649 or +255-784-568276 FAX: +255 28-2220009 Wasiliana na uongozi wa Kampuni ya utalii ya Kiroyera kwa maelezo zaidi kupitia kwa mawasiliano yafuatayo-




William Rutta, meneja uendeshaji wa kampuni ya utalii ya Kiroyera iliyoko mkoani Kagera akiwa ndani ya hema maalumu ambalo hutumiwa na watalii mbalimbali kwa ajili ya mapumziko, hema hili linapatikana eneo la Camp site lililoko kwenye ufukwe wa ziwa victoria.




Meneja uendeshaji wa kampuni ya utalii mkoani Kagera ya Kiroyera akiwa ndani ya nyumba asili ya wahaya aina ya msonge iliyoko kwenye eneo la Camp site ambayo ni kivutio kikubwa cha watalii, camp site iko kwenye ufukwe wa ziwa Victoria.




Baadhi ya wageni mbalimbali wakiwa wamekipumzisha kwenye ufukwe wa ziwa Victoria lililopo eneo la Camp site linalotaribiwa na kampuni ya utalii ya Kiroyera iliyoko mkoani Kagera.




Mandhari ya ndani ya nyumba za asili ya wahaya aina ya msonge, zinapatikana kwenye aneo la camp site, nyumba hizi huwavutia sana watalii wa ndani na nje ya nchi.




Mandhari ya camp site iliyoko ufukweni mwa ziwa Victoria inayomilikiwa na kampuni ya utalii ya Kiroyera ambayo watalii huitumia kwa ajili ya mapumziko.




Sehemu nyingine ya mandhari ya camp site.




Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Dr Diodorus Kamala akishikana mkono na mfalme Albert wa II wa falme ya ubelgiji baada ya kuwasilisha hati ya utambulisho. (picha kwa hisani ya ubalozi wa Tanzania nchini Ubelgiji)

Tuesday, September 4, 2012

Picha Mbalimbali


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe akimlaki Waziri wa Ulinzi na Veterani wa Jeshi wa Afrika Kusini Bi. Nosiviwe Mapisa-Nqakula.



Rais Joseph Kabila akipeana mikono na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Bw. Suleiman Kova wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere akiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete. Rais Kabila alihudhuria mkutano huo kama mgeni mwalikwa.



Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi ya Kusini mwa Afrika(SADC TROIKA) Rais Jakaya Kikwete akiongea na wanbahabri mara baada ya kumalizika kikao cha siku moja cha asasi hiyo katika hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency jijini Dar es salaam.




Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Rais wa Masuala ya Biashara za Kimataifa wa Kampuni ya TBEA ya China,Bw. Wang Pinshan kabla ya mazungumzo yao, Ofisini kwake jijini Dar es salaam September 4, 2012. Kulia ni Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo wa Masuala ya Biashara, Bw. Shi Qiwen na wapili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Bw. Andy. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Magazeti Magazeti











Wanahabari Walipomzika Mwanahabari Mwenzao



Pichani kushoto ni Rais wa Vilabu Vya Wanahabari Tanzania Bw. Ken Simbaya na kulia ni mwanahabari mkongwe Chris Nyanyembe. Ni kwenye mazishi ya Mwandishi Daud Mwangosi kijijini kwao Rungwe, Mbeya hii leo. Picha na Said Ng'amilo wa Mjengwablog.
Reactions::

Profesa Mwandosya Leo Ameshiriki Mazishi Ya Mwandishi Daud Mwangosi

Kijijini kwao, Mbeya. Picha: Said Ng'amilo wa Mjengwablog.
Reactions::

Mwandishi Daud Mwangosi Azikwa Kijijni Kwao

Mke wa marehemu akiaga

Mh. Mark Mwandosya akiweka Taji la maua pamoja na mke wake 
Picha zote kwa hisani ya http://mbeyayetu.blogspot.com
Reactions::

Tamko Rasmi La MISA Tanzania Kuhusiana Na Kifo Cha Mwandishi Daudi Mwangosi.

P.O. Box 78172, Phone: 2137547/8, Fax: 2137548, E-Mail: info@misatan.org, Dar es Salaam, Tanzania.
TAARIFA KWA UMMA/VYOMBO VYA HABARI
KUHUSU KUUAWA KWA MWANDISHI WA HABARI WA CHANNEL TEN NA MWENYEKITI WA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA IRINGA (IPC) DAUDI MWANGOSI
Tasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Nchi za Kusini mwa Afrika (MISA Tan) imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha mwandishi na kiongozi mahiri wa waandishi hapa nchini.
Aidha tunaungana na waandishi na wafanyakazi katika tasnia ya habari nchini, Jumuiya ya Klabu za Waandishi nchini (UTPC) pamoja na familia ya marehemu Mwangosi katika kipindi hiki kigumu ambacho tasnia yetu ya habari imelazimika kuingia matatani kutokana na matumizi ya mabavu ya Jeshi la Polisi.
Tunalaani kwa nguvu zote matumizi ya mabavu ya polisi ambayo yamesababisha kifo cha mwandishi wa habari akiwa kazini na pia akiwa chini ya ulinzi wa Polisi. Tunatambua uhasama kati ya Polisi wa mkoa wa Iringa dhidi ya waandishi wa habari uliodumu kwa muda mrefu.
Uhasama huu kiini chake ni kutokana na matumizi ya nguvu kupita kiasi yanayotekelezwa mkoani Iringa na hivyo kila mara waandishi wanaporipoti habari wanaingia katika mlolongo wa uhasama na vituko vya mara kwa mara. Hatimaye polisi kwa makusudi wameamua kuua mwandishi. Hili ni doa ambalo litaichukua Tanzania kujisafisha machoni pa jumuiya ya kimataifa.
Huu ni mwendelezo wa matumizi ya nguvu kupita kiasi yanayofanywa na polisi kwa raia wa nchi hii. Ni lini polisi watasimamia ulinzi wa raia na mali zao badala ya kugeuka kuwa jeshi la mauaji kila wananchi wanapokusanyika kwa minajili ya kutimiza ndoto zao?
Kifo cha Mwangosi kimegubikwa na sintofahamu hasa ukijua kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Bwana Michael Kamuhanda alikuwa anamtambua kama kiongozi wa waandishi wa habari mkoa na alikuwepo kwenye tukio wakati Mwangosi akiwa mikononi mwa polisi, na kuuliwa mbele yake.
Lakini ikumbukwe kuwa siku zote hata katika vita waandishi wanafanya kazi bega kwa bega na askari ili kuwajuza wananchi nini kinachotokea kwenye uwanja wa mapambano. Kwa jeshi la polisi hapa nchini limedhihirisha kuwa baada visa na mikasa kuwatokea raia wa kawaida sasa wamewageukia waandishi wa habari na kukatisha maisha yao kikatili.
Sasa Polisi wamevunja daraja lililokuwa linawanganisha wananchi na serikali yao. Hii itazidisha chuki ya wananchi dhidi ya serikali yao kuliko kipindi kinginecho chote.
Ikumbukwe pia kuwa wakati mauaji haya yanatokea kuna mkutano mkuu wa UTPC unaoanza wiki hii huku wawakilishi wa vyama vya waandishi wa mbalimbali wa kimataifa wakitegemea kushiriki katika mkutano huo wa mwaka. Na hii itatoa taswira halisi ya jinsi Jeshi la Polisi linavyofanya kazi hapa nchini.
Jumuiya ya kimataifa itaweza kujionea hali halisi jinsi waandishi wa habari hapa nchini wanavyofanya kazi katika mazingira hatarishi na kwamba sasa Tanzania inawezekana isiwe mahali salama pa kuishi kama walivyokuwa wakisikia kwenye vyombo vya habari vya kwao. Mfano halisi ni mhanga Daudi Mwangosi ambaye ataingia katika vitabu vya kumbukumbu duniani kwa mwaka 2012.
Tunaiomba serikali ichukue maamuzi makini ya kukaa pamoja na vyama vya siasa ili kutafuta njia muafaka ya kutuliza mikusanyiko ya wananchi kwa njia za amani na sio kutumia mabavu katika kuwatawanya.
Ni imani yetu kuwa historia imeonyesha kuwa nguvu kupita kiasi kwa wananchi inaongeza chuki dhidi ya serikali yao ya wakati huo na kamwe hainyamazishi dukuduku zilizoko mioyoni mwa wananchi. Kokote kule duniani matumizi ya polisi yalipovuka mipaka yakaamsha hasira za wananchi na kuzifanya nchi hizo zisikalike.
Matumizi ya mabavu, nguvu kupita kiasi kuzima vuguvugu za wananchi kwa kile wanachokiamini pamoja na mauaji na hasa kwa wanahabari na raia wasio na silaha hayajawahi kufanikiwa kokote kule duniani.
Tunaamini kuwa serikali yetu ni sikivu na itachukua hatua stahiki. Pamoja na kwamba uchunguzi huru sio utamaduni wa serikali yetu lakini katika hili la mwandishi akiwa na kalamu na kamera yake afie mikononi mwa polisi tunahitaji uchunguzi huru na wa kina.
Taasisi yetu imetoa ubani wa shilingi laki tano (500,000/-) kwa familia ya marehemu Mwangosi. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi. Amen!

Tumaini Mwailenge
Mkurugenzi,
MISA Tanzania

Monday, September 3, 2012

Picha Mbalimbali


Kanisa la jimbo kuu la Bukoba ambalo mwli wa marehemu Kardinari Laulean Rugambwa utapumzishwa milele 0ct0oba 6, mwaka huu, mwili huo ulikuwa umepumsishwa kwa muda kwenye maeneo ya maziko ya parokia ya Kashozi.



Hali ya kanisa katoriki la jimbo la Bukoba ambalo sasa linafanyiwa ukarabati



Wafanyabiashara hasa wenye magari makubwa yakusafirisha mizigo na abiria mjihadhari sana, kuna matairi feki ya Michelin ambayo sasa yanauzwa, matairi haya yanadaiwa kuuzwa na matapeli walioko jijini Mwanza, haya ni matairi ambayo mmiliki wa magari yanayosafirisha abiria aliuziwa, matairi haya hayawezi kusafiri hata kwa umbali wa zaidi ya kilomita 1 yanapasuka hovyo hata wakati wa kupachikwa kwenye Rim zake, matairi feki hayo ndigu zangu mkiyanunua ndugu zangu wasafirishaji watakuwa mnahatarisha maisha ya watu.




Matairi feki ya Michelin.