Wednesday, July 4, 2012

WABUNGE WATAKIWA KUACHA MZAHA WAKATI WAKICHANGIA HOJA BUNGENI

BAADHI ya watu maarufu nchini wamewataka wabunge kuacha mzaha katika kujadili mambo mazito yanayogusa maslahi ya nchi.
 Kauli ya wananchi hao imekuja siku chache baada ya kubaini kuwepo na ushabiki wa baadhi ya vyama ndani ya vikao vya bunge vinavyoendelea na kulisababishia kukosa hadhi ya bunge.
 Wakizungumza kwa nyakati tofauti na FULLSHANGWEBLOG jijini Dar es Salaam jana, watu hao walisema kuna ulazima kwa viongozi wa vyama vyote kutoa elimu kwa wabunge wao ili kuepuka vurugu zinazotokea bungeni hivi sasa.
 Miongoni mwa watu hao, ni Mhadhiri Msaidizi Chuo Kikuu cha Dar es Slaam Bashiru Alli alisema bunge hilo limetawaliwa na mzaha mwingi.
 Alisema mambo mengi yanayohitaji kupatiwa ufumbuzi kupitia mijadala hiyo yamekuwa hayajadiliwi kwa kiwango cha kina kitendo kinachosababisha wananchi kukosa majibu ya kuridhisha katika kero zao.
 Alli alisema kutokana na vitendo hivyo pengine kuna ulazima wa kupatikana mfumo mwingine wa utakao weza kuliendesha bunge kwa heshima na maslahi ya wananchi na si vinginevyo.
 Vile vile anasikitishwa na mahudhurio ya wabunge katika vikao hivyo muhimu vinavyojadili matatizo ya wananchi kwa madai kuwa wengine wako safarini.
Aidha, hapendezwi na vitendo vya Kamati za Bunge Kuendelea wakati huu muhimu wa kujadili bajeti kwani kikao hicho cha bunge kinauzito hivyo kila mbunge anapaswa kuwa bungeni.
Katibu Mkuu wa Chama cha (NCCR) Mageuzi, Sam Ruhuza alisema anashangazwa na mfumo wa bunge la sasa unavyoendelea kwa sababu haukidhi mahitaji ya wananchi badala yake unaangalia ushabiki wa chama.
 Aliongeza kuwa kutokana na wabunge hao, kushindwa kuzungumzia hoja au changamoto zilizopo katika majimbo yao na kuzitafutia ufumbuzi,kuna haja ya kupatiwa semina ya kuwakumbusha wajibu wao wakati wakiwa bungeni.
 Naye Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT)Usharika wa Matumbi, Christophile Kalata, alieleza kuwa watanzania walipofika sasa wanahitaji kiongozi shupavu anayeweza kusimamia rasilimali au maendeleo ya nchi kwa maslahi yao.
 “Nchi zilizoendelea zinapenda kuona au kushuhudia Tanzania ikikumbwa na misukosuko, hivyo zinaweza kutumia mwanya huo kwa kuwatumia viongozi waliopo kulumbana ili kazi za maendeleo ya nchi zisimame au zizorote” alisema Kalata.
 Naye Hashim Rungwe ambaye ni Mwanasheria aliwataka wabunge kutekeleza wajibu wao waliotumwa na wananchi kuliko kutaka kujijengea umaarufu usiokuwa namsigi.
Alisema wabunge hawako pale kwa lengo la kuonyeshana kuwa nani bingwa wa kusema japo anachosema hakina maslahi na nchi.

Maisha..............................

Tumaini La Taifa La Kesho


Ni Bukoba vijijini.

RAIS KIKWETE AREJEA TOKA RWANDA NA BURUNDI

  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jana jioni 
wakitokea Burundi na Rwanda walikohuidhuria sherehe za miaka 50 wa uhuru wa nchi hizo. Anayeongozana nao ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Mecky Sadik.
  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Inspekta Jenerali wa Polisi Afande Saidi Mwema na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jana jioni wakitokea Burundi na Rwanda walikohuidhuria sherehe za miaka 50 wa uhuru wa nchi hizo

PICHA NA IKULU

Tuesday, July 3, 2012

Maisha..............................

Mama na watoto wake wawili mbele na mmoja mgongoni, wakiwa wametoka kuokota kuni wakipita dararajani Ruaha,Kalenga
                                     
       
                                   

Figo Za Dk Ulimboka Zaanza Kufanya Kazi



AFYA ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Steven Ulimboka imeendelea kuimarika baada ya kupata matibabu nchini Afrika Kusini na sasa figo zake zimeanza kufanya kazi.Dk Ulimboka alipelekwa nchini huko mwishoni mwa wiki baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana kiasi cha kusababisha figo zake kushindwa kufanya kazi.Katibu wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Rodrick Kabangila alisema Dar es Salaam jana kwamba, hali ya Dk Ulimboka imeimarika na kuwaomba Watanzania wamuombee apone haraka.“Taarifa tulizozipata kutoka Afrika Kusini zinasema kwamba, hali ya Dk Ulimboka imezidi kuimarika tofauti na alivyokwenda, figo zimeanza kufanya kazi ingawa kwa polepole na amefanyiwa vipimo vingine,” alisema Dk Kabangila na kuongeza:

“Pia ameanza kuzungumza, anawatambua watu vizuri na zaidi amewaomba Watanzania wamuombee apone haraka.”
Awali, chanzo kimoja cha habari kilidokeza kwamba hali ya Dk Ulimboka imeimarika kutokana na kupatiwa huduma za matibabu kwa haraka kwa kufanyiwa pamoja na vipimo vingine, kile cha usafishaji damu na figo (Dalysis), mara kwa mara. Kabla ya kuondoka nchini, Dk Ulimboka alifanyiwa usafishaji huo mara mbili.

Madaktari walisema kuwa, kipimo hicho kililenga kupunguza kiwango cha sumu iliyoonekana kwenye damu, ambayo haikutambulika mara moja kama ilitengenezwa ndani ya mwili au vinginevyo kwa kuwa hakuna kipimo cha kubaini tatizo hilo nchini.

Migomo hospitalini
Licha ya huduma kurejea taratibu katika baadhi ya hospitali nchini, mgomo wa madaktari bingwa umeendelea chini kwa chini.Pia jana, Serikali imewataka madaktari wote walio katika mafunzo ya vitendo kuripoti Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ifikapo Ijumaa.

Jana, wizara hiyo ilitoa taarifa ikitaka madaktari wote nchini wanaofanya mafunzo kwa vitendo (interns) ambao walipewa barua za kurudishwa wizarani, kuripoti Dar es Salaam Julai 6, mwaka huu.

Mgomo wa madaktari bingwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), umekuwa na utata baada ya kuwapo taarifa mbili zinazokinzana.

Uongozi wa (MNH) kupitia kwa Msemaji wake, Aminiel Aliegaeshi umetoa taarifa kwa umma kupitia vyombo vya habari jana ukisema huduma za matibabu zinaendelea kama kawaida, lakini kwa kiwango cha kati.

“Huduma hapa hospitalini zinaendelea kutolewa kwa kiwango cha kati, wagonjwa ni wachache wanaokuja kutibiwa. Madaktari Bingwa wote wameingia na kufanya kazi na Interns kumi na moja wamefanya kazi,” alisema.

Jana waandishi wetu walishuhudia baadhi ya huduma zikiendelea kutolewa kama kawaida katika hospitali hiyo zikiwemo x-ray katika Taasisi ya Mifupa (Moi) na hospitali hiyo kuu.

Awali, huduma hiyo na nyingine zilisimama baada ya tukio la kutekwa na kupigwa kwa Dk Ulimboka.

Lakini, wakati Aliegesha akitoa taarifa hiyo, madaktari bingwa wamesisitiza kuwa wako kwenye mgomo huku msemaji wao, Dk Cathrine Mng’ong’o akitaka waandishi wa habari kulinganisha maneno hayo ya uongozi na hali halisi hospitalini hapo.

“Mimi siwezi kujibu swali hilo (kama wako kwenye mgomo au wamerudi), sababu sipo katika eneo la hospitali leo, niko nyumbani. Wewe angalia kwa macho yako uone kisha linganisha maneno hayo na hali halisi,” alisema Dk Mng’ong’o.Alipoulizwa kuwa kama jana alikuwa zamu alijibu kwa kifupi kuwa madaktari bingwa hawana zamu na hufanya kazi saa 24.

Madaktari hao juzi walitangaza mgomo wakitaka Serikali kuwarudisha kazini madaktari wote waliofukuzwa.

Uongozi wa MNH ulisema, idara ambazo madaktari walikuwapo ni ya huduma za dharura na katika vitengo vingine ilidaiwa kuwa walifika kwa kiwango kikubwa.

Katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru, hali imezidi kuwa tete baada ya wagonjwa kuhamishiwa hospitali za binafsi kutokana na kuzorota kwa huduma.Mkazi wa Sakina aliyejitambulisha kwa jina moja la Manka, ambaye mtoto wake alikuwa amelazwa hospitalini hapo akisubiri upasuaji alisema, amelazimika kumhamisha mtoto wake kutokana na kukosa huduma.

Hata hivyo, Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Eliringia Mlay alikanusha madai ya kuwapo kwa mgomo hospitalini hapo na kusema kuwa, ulikuwapo awali lakini kwa sasa umekwisha na madaktari wanaendelea na kazi kama kawaida. Hospitali binafsi

Hospitali ya TMJ imeanza kutoa huduma ya tiba kwa baadhi ya wagonjwa waliokuwa Muhimbili baada ya kuingia mkataba na Serikali ili kutoa huduma ya matibabu katika kipindi ambacho madaktari wa Serikali wapo katika mgomo.

Msemaji wa Hospitali hiyo, Huzaifa Seif alisema jana kuwa wagonjwa wanaotibiwa katika hospitali hiyo ni wale wenye kadi za Bima ya Afya na wagonjwa walioandikiwa rufaa kutoka MNH.
Hata hivyo, mmoja wa wagonjwa, Anaeli Mbasha alisema ingawa Serikali imeingia mkataba na hospitali hiyo, wagonjwa wengine wenye kipato kidogo wanashindwa kuhimili malipo.

Hospitali ya Regency imekuwa na ongezeko la wagonjwa ikiaminika kuwa ni kutokana na mgomo huo wa madaktari. Mmoja wa madaktari hospitalini hapo, Dk Emmanuel Jonathan alisema wagonjwa ni wengi hasa kutoka Muhimbili.

Katika Hospitali ya Aga Khan, baada ya wiki iliyopita kuwa na ongezeko la wagonjwa kwa asilimia 15, idadi hiyo imepungua kati ya jana na juzi.Mkurugenzi wa Tiba wa Aga Khan, Dk Jaffer Dharsee alisema: “Ongezeko kubwa lilikuwa katika vipimo ambavyo vinapatikana katika Hospitali ya Muhimbili na hapa (Aga Khan), peke yake kwa mfano MRI (Magnetic Resonance Imaging).”

Geofrey Nyang'oro, Victoria Mhagama, Halima Shebuge, Zakhia Abdallah, Sam Jacob (SJMC), Pamela Chilongola na Sam Jacob, Moses Mashalla, Arusha.

Chanzo:  http://www.mwananchi.co.tz/habari

Wananchi Wafaidika Na Huduma Za Vodacom-Sabasaba.

Wafanyakazi wa Kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania wakimpa maelekezo mteja alienunua simu aina ya ZTE 502 inayouzwa kwa shilingi elfu 13 katika maonesho ya Biashara ya kimataifa Sabasaba jijini Dar es Salaam,leo.


Wateja waliojitokeza katika maonesho ya biashara ya Kimaifa Dar Es salaam (sabasaba) wakipewa maelekezo na wafanyakazi wa kampuni ya simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania,namna ya kutumia simu ya ZTE 502 inayouzwa kwa shilingi elfu 13 katika maonyesho hayo.

Wakala wa Vodacom M PESA akitoa huduma ya M- PESA kwa mteja alietembelea maonesho ya sabasaba jijini Dar-es-salaam. Kampuni ya Vodacom Inashiriki katika maonesho hayo kama mdhamini rasmi wa mawasiliano.

Maisha Yanaendelea

                           
     

TAKUKUTU Kagera Yawafikisha Mahakamani Watumishi Wa serikali

Na Mwandisi Wetu
Bukoba
TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani Kagera (TAKUKURU) inawashililia na kuwafikisha mahakamani watumishi wawili wa ofisi ya mkuu wa mkoa Kagera na watumishi sita wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba kwa tuhuma ya kujihisisha na kufuja fedha kwa njia ya mishahara hewa.

Akizungumza na waandishi wa habari kaimu kamanda wa TAKUKURU mkoani Kagera Samsoni Bishati alisema kuwa watumishi hao wamejihusisha na suala la kupitisha fedha ambazo ni mishahara ya watumishi hewa na kujinufaisha wao wenyewe.

Alisema kuwa katika kupambana na rushwa inayofanywa na baadhi ya watumishi wa serikali ambao sio waaminifu  ofisi ya TAKUKURU mkoa Kagera iewakamata watumishi hao na baadhi kuwapeleka mahakamani kwa kosa la kupitishamishahara hewa.

Aidha aliwataja baadhi ya watumishi ambao wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Bukoba kuwa ni wawili kuroka ofisi ya mkuu wa mkoa ambao ni Shabani Kitimbisi na Sifa Musa ambao wote ni wa idara ya fedha.

Watumisi wengine ambao tayari wamefikishwa mahakamani ni kutoka katika ofisi ya mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba idara ya Afya ni Davidi Buhenyenge na Martini Muganyizi na alisema kuwa watumishi wanne waliobaki bado wanatafutwa na taasisi hiyo na hakuwa tayari kuwataja majina kwakuwa bado wanatafutwa ili kufikishwa mahakamani.

Katika hatua nyingine kaimu kamada huyo Samsoni Bishati ametoa rai kwa umaa kutojihusisha kwa namna yoyote katika vitendo vya rushwa kwani TAKUKURU ipo makini  na ina uwezo wa kuibuwa na hatimaye kuwafikisha mahakamani watumishi wa umma ambao sio waadirifu.

Watumishi ambao wamekamatwa na kufikishwa mahakamani chini ya hakimu wa mahakama hiyo Willibard Mashauri wako nje kwa dhamana hadi kesi itakapotajwa tena ambayo inaendeshwa na mwendesha mashtaka wa TAKUKURU mkoa wa Kagera Fuja Siabo.

Mwisho

Rais kikwete ahudhuri maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Burundi mjni Bujumbura

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakiwa pamoja na viongozi wengi ne waliohudhuria maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Burundi mjini Bujumbura leo asubuhi.kutoka kishoto ni Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rais Teodoro Nguema wa Equatorial Guinea,Mwenyeji Rais Pierre nkurunzinza wa Burundi na mkewe na, Rais Mwai  Kibaki wa Kenya. picha na freddy Maro)
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakifurahia jambo wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Burundi yaliyofanyika mjini  Bujumbura leo asubuhi.Kulia ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.

Warsha ya watu wenye ulemavu kuhusu hali ya utekelezaji wa mkataba wa Kimataifa


Mkurugenzi mtendaji wa Mfuko wa Asasi za Kiraia Foundation for Civil Society. Bw. John Ulanga akiongea na washiriki wa mkutano huo juu ya ushiriki wa walemavu katika mchakato wa katiba nchini Mkutano uliandaliwa na Asasi za kiraia za  watu wenye ulemavu nchini chini ya ufadhili wa The Foundation for Civil Society.uliofanyika katika Hotel ya Umbungo Plaza leo jijini Dar es salaam.
PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE
Mkurugenzi wa Haki za Bianadamu kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora nchini, Bw;Francis Nzuki akiongea na washiriki juu ya kazi za tume na wajibu wake kwa jamii ya watu wenye ulemavu nchini.

Mmoja wa washiriki kutoka chama cha walemavu wa ngozi nchini akizungumzia changamoto wanazokabiliana nazo katika washa hiyo.
Mwanasheria na mmoja wa waliofanya utafiti kuhusu hali ya utekelezaji wa mkataba wa kimataifa wa fursa na haki kwa watu wenye ulamvau na sheria zilizopo nchini Bw;Crarence Kipobotoca akiwasilisha utafiti kwa washiriki hao.

Baadhi ya washiriki walioudhuria  mkutano huo wa siku tatu unaoendelea Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam

Maisha..............................

       

Mgomo Wa Madaktari: JK Akoleza Moto


Waandishi Wetu
SIKU moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kusema daktari anayeona kuwa hawezi kufanya kazi serikalini bila ya kulipwa mshahara wa Sh3.5 milioni aache kazi, viongozi wa dini, wanasiasa, wabunge na wasomi wamemtaka apunguze jazba.Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana walisema mgogoro wa madaktari na Serikali bado unajadilika huku Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika akienda mbali zaidi na kusema Serikali iache kisingizio cha Mahakama kulizuia Bunge kujadili mgogoro baina yake na madaktari, wakati yenyewe inajadili na kutoa maelezo.

Juzi, katika hotuba yake ya kila mwisho wa mwezi, Rais Kikwete alisema Serikali haiwezi kuahidi kuwa inao uwezo wa kuwalipa madaktari mshahara huo na posho zote kwani ikifanya hivyo malipo ya daktari anayeanza kazi yatakuwa Sh7.7 milioni kwa mwezi kitu ambacho hakiwezekani.

Jana, wakizungumza kwa nyakati tofauti, wadau hao walisema mgogoro huo kati ya Serikali na madaktari bado unajadilika na kusisitiza kuwa hotuba ya Rais Kikwete haijajibu madai ya madaktari.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Bashiru Ally alisema ingekuwa jambo jema kama kungekuwa na uwezekano wa mazungumzo kuendelea.

Alisema kauli ya Rais ni upande wa Serikali hivyo, ingekuwa vyema kama madaktari nao wangepata nafasi ya kujieleza.

Wanasiasa
Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi), Moses Machali alimtaka Rais apunguze hasira na kuitaka Serikali ikubali kurudi katika meza ya mazungumzo hata kama ndiyo iliyokuwa ya kwanza kuwapeleka mahakamani madaktari waliogoma.

Alisema kama Serikali haiwezi kulipa kiwango cha mshahara kilichopendekezwa na madaktari, irudi katika meza ya mazungumzo ili kutafuta suluhu ya mgomo huo unaowaumiza zaidi wananchi.

“Warudi kwenye meza ya majadiliano siyo kila mmoja kusema la kwake na kuacha mgomo kuendelea huku, watu wakiteseka hospitalini bila msaada wowote,’’ alisema Machali.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro alisema Serikali haipaswi kuwafukuza madaktari kwa kuwa imetumia gharama kubwa kuwasomesha.

“Ikiwafukuza madaktari italazimika kuwaleta walio nje ya nchi ambao ni gharama kubwa… Serikali itatue mgogoro huu,” alisema.

Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika alisema Serikali iache kutumia kisingizio cha Mahakama kulizuia Bunge kujadili mgogoro wa madaktari wakati yenyewe ikitoa ufafanuzi.

“Uamuzi wa Serikali kutoa kauli kupitia hotuba ya Rais una mwelekeo wa kukwepa wabunge kujadili hotuba husika ambayo awali, ilielezwa kuwa ingetolewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda bungeni. Inawanyima haki wabunge wasitimize wajibu wa kikatiba wa Ibara 63 (2) wa kuisimamia Serikali kwa niaba ya wananchi,” alisema Mnyika.

Mnyika alisema, kwa kuwa Bunge litajadili mapitio ya utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Rais kwa mwaka wa fedha 2011/2012 na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2012/2013 kuanzia leo, ni muhimu wabunge wakajadili pia masuala ambayo Rais ameyaeleza kwa taifa na kutimiza wajibu wa kikatiba.

“Hotuba ya Rais imeendeleza kauli za upande mmoja ambazo zimekuwa zikitolewa na Serikali kuhusu mgogoro huo bila taifa kupewa fursa ya kupata maelezo na vielelezo vya upande wa pili, hivyo Serikali imetoa kauli yake hadharani badala ya bungeni au mahakamani.

Viongozi wa dini

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo Kibangu, Anthony Lusekelo alisema madaktari hao wanatakiwa kurudi kazini kwa kuwa tayari Serikali imeshasema kuwa haina fedha za kuwalipa na kuongeza kuwa hata kama wana madai yao, wadai wakiwa kazini.

“Asilimia kubwa ya madaktari wamesomeshwa na Serikali… Serikali hiyohiyo inawaeleza kuwa haina fedha za kuwalipa kama wanavyotaka, binafsi nawaomba tu warudi kazini kwa kuwa mgomo wao unawaathiri zaidi wananchi kuliko hata hao viongozi wa Serikali.

“Tunajua tulikotoka ila hatujui tunakokwenda, kama ni kuboreshwa kwa sekta nzima ya afya, Serikali imesema itatekeleza hilo, haiwezi kuyatekeleza kwa siku moja, haya mambo yanajadilika.

Alisema kama Serikali itakuwa na makosa yake, itayajibu mbele za Mungu... “Madaktari watekeleze wajibu wa kazi yao kwa uwezo wa Serikali iliyopo madarakani.”

Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Kagera, Dk Methodius Kilaini alisema kanisa hilo haliwezi kuunga mkono mgomo huo.

Alisema pamoja na kuwa madaktari wana madai yao, jukumu lao kubwa ni kufuata maadili ya kazi yao ambayo hayawaruhusu kugoma.

Katibu Mkuu wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania, Askofu David Mwasota alisema madaktari wanatakiwa kutenganisha siasa na maadili ya kazi yao.

“Hata kama Serikali ina makosa yake lakini, wao kuendelea kugoma si jambo zuri kwa jamii na hata mbele za Mungu, watumie njia nyingine kudai madai yao, lakini waendelee kutoa huduma. Madaktari ni watu muhimu, kurudisha viungo vya binadamu katika hali ya kawaida si kazi ndogo, warudi kazini kuokoa mamia ya Watanzania maskini.”

Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (Bakwata), Mkoa wa Arusha Abdulkarim Jonjo alisema ipo haja kwa Serikali kukaa meza moja na madaktari hao.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mjini Kati, Thomas Laizer alisema mgogoro wa madaktari umalizwe kwa mazungumzo.

Alisema Serikali inapaswa kuwa wazi inapozungumza na madaktari kwa kueleza ni mambo gani yanawezekana na kwa muda gani ili, kuondoa migogoro.

Akizungumza juzi katika ibada maalumu katika kanisa la KKKT Kimandolu, alisema ili kuondoa hisia kuwa Serikali inahusika na tukio la kutekwa Dk Ulimboka ni lazima iundwe tume huru.

“Nadhani ili kuondoa haya maneno ambayo si jambo dogo, Serikali inapaswa kuunda tume huru kuchunguza tukio hili, kwani inawezekana waliohusika ni watu wengine tu wenye nia mbaya na Serikali lakini ili ukweli ujulikane ni muhimu kuwepo tume huru,” alisema Askofu Laizer.

Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Mussa Salum aliwataka madaktari kutii agizo lililotolewa na Mahakama kwa kurudi kazini.

“Rais ameshaeleza wazi kwamba Serikali haina fedha za kuwalipa kama wanavyotaka, warudi tu kazini na kuweka masilahi ya Watanzania mbele na kuacha kutanguliza masilahi binafsi,” alisema Sheikh Salum.

Wanaharakati

Mkurungezi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Hellen Kijo-Bisimba alisema hotuba hiyo ya Rais haina jipya zaidi ya kurudia maelezo yake ya awali alipokutana na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam.

“Nilitarajia kuwa hotuba itakuwa tofauti lakini sivyo. Amerudia maelezo yaleyale aliyoyasema Machi 12 (mwaka huu) alipokutana na wazee katika Ukumbi wa Diamond Jubilee,” alisema Bisimba.

Wakili Peter Jonathan alisema kama kweli Serikali inataka kurudisha imani kwa Watanzania kuhusu tukio la Dk Ulimboka ni lazima ijisafishe kwa kuunda tume huru nje ya Serikali.

“Watafute hata Jaji mstaafu, si lazima atoke Tanzania kuongoza tume huru ikibidi tuchukue hata nje ya nchi ili wakitoa taarifa iweze kuaminiwa na jamii na hiyo ndiyo dhana sahihi ya utawala bora,” alisema.

Mjumbe wa Chama cha Watabibu wa Tiba Asili (ATME), Boniventure Mwalongo ameitaka Serikali kuacha kutumia nguvu kushughulikia madai ya madaktari badala yake ipanue wigo wa majadiliano ili kutatua tatizo hilo.

“Nimesikiliza hotuba ya Rais lakini, haijaonyesha kama kuna jawabu la mgomo hivyo wapanue wigo wa majadiliano ili kumaliza mgogoro huu,” alisema Mwalongo.

Habari hii imeandikwa na Fidelis Butahe,
Nora Damian, Bakari Kiango, Freddy Azzah, Daniel Mwingira, Dar; Daniel Mjema, Moshi; Mussa Juma, Arusha na Frederick Katulanda, Mwanza.

DR:Shein Afanya Uteuzi Zanzibar


Na Ali Issa Maelezo Zanzíbar
RAIS wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DKT. Ali Mohammed Shen kwa uwezo alio pewa chini ya kifungu 9 (1) ((a) cha sheria ya mafunzo ya Amali Zanzíbar namba 8 ya mwaka 2006 amemteuwa DKT. Mohammed Hafidh khalifan kuwa mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzíbar .

Kwamujibu wa barua ya tarehe 2 /7/2012 ilio tiwa saini Katibu wa Baraza la Mapinduzi na katibu mkuu kiongozi zanzibabr DKT Abdull Hamid Yahaya Mzee uteuzi huo umeaza tangu tarehe 30/6/2012 mwaka huu.

Monday, July 2, 2012

Sakata La Mgomo Wa Madaktari

Madaktari Hospitali Ya Taifa Muhimbili Jana Warejea Kazini

JULAI 2, 2012
Huduma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili zimerejea katika hali ya kawaida baada ya Madaktari kurejea kazini Jumatatu ya leo Julai 2, 2012.

Tathimini iliyofanyika kuanzia asubuhi saa mbili hadi saa 11 jioni inaonyesha kuwa katika Idara ya Tiba, Madaktari Bingwa 19 kati ya 21 wamefika kazini ambapo watatu wako likizo. Aidha Registrars wote 12 walikuja kazini. Kliniki zote za tiba zimefanyika kama kawaida.

Katika Idara ya watoto, yenye Madakatari Bingwa 16, kati yao 14 walikuja kazini wengine wawili wako likizo na Registrar watatu kati ya sita walikuja kazini ambapo watatu wako likizo.

Upande wa OPD yenye Registrars saba, sita kati yao walikuja kazini na mmoja yuko likizo. Aidha Madaktari Bingwa wote walikuja kazini.

Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili yenye Madakatri Bingwa 10, tisa walikuja kazini na mmoja wao yuko masomoni.

Upande wa Emergency Medicine, Registrars wote 10 walikuja kazini.

Kuhusu huduma za upasuaji, wagonjwa wote waliolazwa wodini wameonwa, na baadhi ya kliniki za huduma ya upasuaji zilifanyika. Hata hivyo, upasuaji haukufanyika kwani hakukuwa na orodha ya wagonjwa waliopangwa kufanyiwa upasuaji..
KWA UJUMLA, MADAKTARI WAMEREJEA KAZINI.
Imetolewa na;
Aminiel Buberwa Aligaesha
Afisa Uhusiano Mwandamizi

Maisha Yanaendelea