Friday, June 15, 2012

Maisha Yanaendelea



Magazeti Magazeti
























Reactions::

Star Yatua Maputo Kuivaa The Mambas





Kocha Kim Paulsen akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Shamim Nyanduga mara baada ya timu hiyo kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Maputo




Kocha Kim Paulsen akiwaongoza wachezaji wake baada ya kushuka kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa maputo jana, nchini Msumbiji. Taifa Stars itakipiga na timu ya Msumbiji The Mambas Jumapili, katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Afrika zitakazofanyika nchini Afrika Kusini mwaka ujao.


Taifa Stars imewasili Maputo saa 5 asubuhi kwa saa hapa tayari kwa mechi dhidi ya Msumbiji (The Mambas) na kupokewa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maputo na Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Balozi Nyandugu.


Stars yenye kikosi cha wachezaji 20 chini ya Kocha Mkuu Kim Poulsen imefikia Hotel 2010 LDA iliyoko karibu na Uwanja wa Taifa Zimpeto ambapo mechi hiyo itachezwa Jumapili kuanzia saa 9 kamili kwa saa za hapa ambapo Tanzania itakuwa saa 10 kamili.


Kwa mujibu wa programu ya Kocha Kim, timu itafanya mazoezi leo na kesho katika muda ule ule wa mechi ya Jumapili ambayo itachezeshwa na waamuzi kutoka Madagascar. Mpaka timu inawasili hapa hakuna mchezaji yeyote mwenye matatizo ambayo yanaweza kusababisha asicheze mechi ya Jumapili.



Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Maputo
+258840669404

Usiku Wa Kuamkia Ijumaa


Rais Mstaafu wa awamu ya Mzee Ali Hassan Mwinyi akimkabidhi Mchezaji bora wa mwaka kutoka timu ya Simba na Taifa Stars Shomari Kapombe tuzo yake ya mwanamichezo bora wa mwaka wa  katika tuzo za  zinazoandaliwa na chama cha waandishi wa habari za michezo TASWA  na kudhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti zilizofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa  Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.

Shomari Kapombe pia amezawadiwa kitita cha shilingi milioni 12 kutoka kwa wadhamini wa tuzo hizo kampuni ya bia ya Serengeti kutokana na ushindi huo wa tuzo ya mwanamichezo bora wa mwaka
Shomari Kapombe mchezji bora wa mwaka akiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa tuzo hizo pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Simba huku akiwa ameshikilia tuzo yake na mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 12 za kitanzania  kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa Serengeti Richard Wells, kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano SBL Teddy Mapunda na wa pili kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Simba Geofrey Nyange Kaburu

Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa zamani wa timu ya taifa iliyofanikiwa kushiriki mashindano ya kombe la mataifa huru ya Afrika mwaka 1980 mara baada ya kuwakabidhi tuzo ya heshima usiku wa kuamkia leo
Mzee Ali Hassan Mwinyi akizungumza na kutoa nasaha zake katika utozji wa tuzo hizo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Kampuni ya bia ya Serengeti SBL Teddy Mapunda akitoa shukurani zake mara baada ya kukamilika kwa utoaji wa tuzo hiyo usiku wa kuamkia leo.
Baba mwenye uzao wa mabondia Mzee Matumla kulia  akikabidhi tuzo ya mwanamchezo bora wa kigeni katika soka Emmanuel Okwi kwa Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Simba Geofrey Nyange aliyepokea tuzo hiyo kwa niaba ya mchezaji huyo,
Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Zanzibar ZBC Omar Said Ameir akikabidhi tuzo ya mchezaji bora wa Tanzania katika soka Agrey Morris katika hafla hiyo.
Mchezaji wa zamani wa timu ya Coast Union ya Tanga na Timu ya taifa Salim Amir akikabidhi tuzo kwa mchezaji Shomari Kapombe
Mpiga picha wa siku nyingi Athmani Hamisi akikabidhi tuzo kwa mchezaji bora wa kiume katika mchezo wa VoliboMbwana Ally huku akisaidiwa na msaidizi wake

Mwenyekiti wa kamati ya Tuzo za TASWA Masoud Saanane akizungumza katika hafla ya utozi wa tuzo hizo usiku huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.
Mkurugenzi wa kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Richard Wells akizungumza katika hafla ya utoaji wa tuzo za

Mkuu Wa Mkoa Wa Kagera Na Usafi Mjini Bukoba


Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe akiendeleza juhudi zake za kuhimiza usafi mkoani Kagera, hapa alikuwa akishiriki kwenye usafi, juhudi zake zimeiwezesha manispaa ya Bukoba kuibuka mshindi wa tatu wa taifa katika masuala ya usafi.




Mkuu wa wilaya ya Bukoba Ziporah Pangani akiwahimiza wananchi washiriki kwenye usafi.




Hali inayodhihiri juhudi zinazofanywa na mkuu wa mkoa wa Kagera za kuimarisha masuala ya usafi, hili ni eneo la wakina mama wanaouza vyakula maaarufu kwa jina la mama Ntilie, liko kwenye machinjio ya zaman



Mkuu wa wilaya ya Bukoba Zeporah Pangani akishiriki kwenye masuala ya usafi




Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Wanachuo wa Chuo cha Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa cha Hombolo, Dodoma kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma, Juni 14, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)




Waziri Mkuu, Mstaafu, Edward lowassa akisalimiana na Mbunge wa Vunjo. Augustine Mrema kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 14,2012. Katikati ni Mbunge wa Simanjiro. ChristopherOle Sendeka. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)




Waziri Mkuu, MizengoPinda akizungumza na Mbunge wa Sengerema., William Ngeleja kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 14, 2012.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Thursday, June 14, 2012

Wenyeviti Wa Upinzani Walia Na Bajeti



Neville Meena na Mussa Juma, Dodoma
WENYEVITI wa vyama vya Chadema, NCCR Mageuzi na CUF wameiponda Bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha 2012/2013 iliyowasilishwa bungeni jana na Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa wakisema imeongeza mzigo kwa walipa kodi kutokana na gharama kubwa za uendeshaji wa Serikali.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya kuwasilishwa kwa bajeti hiyo jana, wenyeviti hao walisema hakuna matumaini kwa Watanzania kupitia Bajeti hiyo kwani fedha nyingi zimerundikwa kuwanufaisha wachache huku umma ukiambulia patupu.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema: “Hakuna mkataba wa makusudi wa kupunguza matumizi ya Serikali, ahadi yake ya kupunguza matumizi kwa kupunguza posho zisizo na tija na matumizi mengine haikutekelezwa.”
Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alisema ameshangazwa na kutokuwapo kwa nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma na badala yake fedha nyingi kurundikwa katika matumizi ya kawaida ya Serikali.

“Mfumo wa kodi kama mlivyosikia ni mbaya kabisa, hakuna kinachoashiria kwamba mkulima wa kawaida atapunguziwa mzigo na badala yake wanaendelea kuwanufaisha wafanyabiashara wa vyakula kwa kuwaruhusu kuagiza vyakula nje bila kodi, hiki naweza kusema ni kichekesho,” alisema Mbowe na kuongeza:

“Hakuna ubunifu kwenye kupanua wigo wa kodi, tungeweza kusikia katika construction (sekta ya ujenzi) ambayo inakua haraka na inachukua asilimia 18 ya Pato la Taifa kwamba tungetoza kodi huko, lakini badala yake ni yaleyale ya siku zote, kodi kwenye sigara, vinywaji na bia.”

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema matatizo makubwa katika bajeti hiyo ni kutengwa kwa fedha kidogo za maendeleo na kwamba kinachoshangaza ni Serikali kushindwa hata kugharimia matumizi ya kawaida.

“Utawala unagharimiwa kwa Sh10 trilioni hali uwezo wa kukusanya mapato ya ndani ni Sh8 trilioni, hii inamaanisha kwamba Serikali yetu pia inatumia fedha za wahisani kugharimia matumizi ya kawaida,” alisema Profesa Lipumba ambaye pia ni mtaalamu wa uchumi.

Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia alisema Serikali lazima ijifunze kubadilika kwani kilichotangazwa jana kwenye Bajeti yake ni marudio ya miaka yote.

“Huwezi kuchukua fedha zote ukaurundikia utawala halafu ukawaacha wananchi bila kitu, hicho ndicho tulichokiona leo, Sh10 trilioni ni kwa ajili ya mishahara na watumishi na matumizi ya kawaida, maendeleo ambako ndiko wananchi waliko kumeachwa tena kutegemea fedha za wafadhili,” alisema Mbatia.

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) Tundu Lissu alisema, Bajeti hiyo haitatekelezeka... “Mwaka jana wamekuja na Bajeti kama hii ya kutegemea fedha za wafadhili, zaidi ya asilimia 40 ya fedha zilizotengwa hazikupatikana na leo wanakuja na bajeti ya aina ileile,” alisema Lissu.

Mbunge wa Ngorongoro (CCM) Saning’o Ole Telele, alisema Bajeti hiyo ni pigo kubwa kwa wafugaji kwani wameshindwa kutengewa fedha kwa ajili ya kuboresha ufugaji hasa wale ambao wanahamahama.
Hoja hiyo ya Telele, iliungwa mkono na Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Rose Kamili ambaye alisema Bajeti ya mwaka huu, badala ya kuongeza fedha kusaidia wafugaji hasa wa asili ambao wanatangatanga, imeendelea kupunguza fedha za wizara hiyo.

Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher Ole Sendeka alisema Bajeti hiyo kama zilivyo nyingine, imeendelea kujikita katika kuongeza kodi katika bidhaa zilezile kila mwaka.
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Ester Bulaya alisema Bajeti hiyo ni nzuri akipongeza mkakati wa ukarabati mkubwa wa Reli ya Kati.

Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Cecilia Paresso alisema, Bajeti ya mwaka 2012/13 kama alivyoisikiliza imeendelea kukosa ubunifu wa vyanzo vipya vya mapato na hivyo kuongeza makusanyo ya ndani.

Wadau wengine
Rais Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba alisema fedha zilizotengwa kwenye Wizara ya Elimu ni ndogo kiasi cha kutoweza kukidhi mahitaji ya walimu na kueleza kuwa hiyo itaendeleza migogoro.
“Kwa kweli ni kiasi kidogo sana, tena imetuvunja nguvu, kwa sababu tulitegemea wafanyakazi tutapewa kipaumbele kwenye Bajeti, lakini kilichotokea ni tofauti kabisa,” alisema Mukoba.
 Chanzo,Mwananchi  http://www.mwananchi.co.tz

WAZAZI WADAI SERIKALI CHANZO CHA MIMBA KWA WANAFUNZI SEKONDARI

JE NINI KIFANYIKE JUU YA MAISHA YA WATOTO HAWA

mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Iwalanje akijisomea katika moja kati ya chumba cha darasa kilichogeuza bweni shuleni hapo
Makamu mkuu wa shule ya sekondari Iwalanje Frank Meck akizungumza na timu ya wanaharakati wa mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP ) waliofika shuleni hapo
mmoja kati ya wanafunzi wa shule ya sekondari Iwalanje Mbeya akitoka gheto kuelekea shule
Maisha ya getho
WAZAZI wanaosomesha watoto wao katika shule ya sekondari ya Iwalanje kata ya Ijombe wilaya ya Mbeya mkoani Mbeya wamedai kuwa chanzo cha watoto wa kike kukatisha Masomo kwa mimba limechangiwa uamuzi wa serikali kuwatoa wanafunzi hao katika bweni na kuwaacha kuishi katika katika vyumba vya kupanga maarufu Kama magheto .

Hali hiyo umepelekea baadhi ya wananchi wa kijiji hicho cha Iwalanje kutumia mwanya huo kuwarubuni watoto hao wa kike kwa kuwapangisha nyumba zao na mwisho wa siku wamekuwa wakiwataka kimapenzi na kuwageuza wanafunzi hao ni nyumba ndogo .

Wakizungumza na wanahabari wanahabakati wa mtandao wa jinsia Tanzania ( TGNP) kijijini hapo Jana wazazi hao walisema kuwa pamoja na shule hiyo kuendelea kuwa na sifa nzuri ya kufaulisha ila bado mimba kwa watoto wa kike zimeendelea kuwa ni tatizo .

Anna mwanjala alisema kuwa wananchi wa kata hiyo ya Ijombe walikuwa wamejitolea kujenga bweni kwa ajili ya watoto wa kike Kama njia ya kupunguza tatizo la Mimba kwa watoto hao ila serikali iliamua kuwatoa wanafunzi hao katika bweni lao na kuwaweka watoto wa kiume ambao wanasoma kidato cha Tano na sita.

Alisema kuwa uamuzi huo wa serikali kuifanya shule hiyo kuwa high school na kuwatoa watoto wa kike katika bweni lao na kuwaweka wanafunzi hao wa kiume kutoka nje ya kata hiyo ,wao Kama wazazi na wananchi wa eneo hilo ambao walijitolea kujenga bweni Hilo hawajapendezwa .

Hivyo alisema ili kuondoa masikitiko kwa wananchi waliojenga bweni hilo kwa ajili ya watoto wao wa kike wanaotoka vijiji vya mbali na shule hiyo ni vema serikali kutimiza ahadi yake ya kuwajengea bweni watoto hao wa kidato cha kwanza hadi cha nne ambao wamekuwa wakipata shida kwa kupanga katika magheto mitaani.

"kweli tunashindwa kujua uamuzi wa serikali yetu kuwapokonya bweni watoto wa kike na kuwaweka watoto wa kiume wakati sisi wananchi tulijenga bweni hilo kwa ajili ya watoto wetu wa kike Kama njia ya kupunguza tatizo la mimba"

John Samweli amasema kuwa mbali ya baadhi ya wamiliki wa nyumba kijijini hapo kuwageuza wanafunzi hao kuwa ni wake zao wadogo bado baadhi ya vijana wamekuwa wakiwarubuni wanafunzi hao kwa kuwapa vizawadi vidogo Kama chakula ,mboga na miwa .

Alisema kuwa kutokana na baadhi ya wanafunzi kuishi mbali kijiji hicho wamekuwa wakishindwa kurudi Kwao mwisho wa wiki kwa ajili ya kufuata mahitaji na kutoa nafasi kwa vijana hao kuwasaidia mahitaji hayo kwa sharti la kupewa mapenzi.

Kwani alisema katika kijiji hicho kumekuwepo na matukio ya wanafunzi kukatisha Masomo kwa mimba na kesi zinapopelekwa ofisi za serikali za vijiji na kata wahusika wamekuwa wakiachiwa ama kubadilishiwa mashtaka na kupewa Yale ambayo yanaunafuu wa kupewa dhamana .

Aidha alisema kuwa tatizo la watoto wa kike kukaa nje ya shule ndilo limekuwa likichangia kuwepo kwa mazingira hatarishi ya wanafunzi hao kujisomea.

Makamu mkuu wa shule hiyo Frank Meck alikiri kuwepo kwa tatizo la mimba katika shule hiyo na kuwa chanzo ni jamii inyozunguka shule hiyo kutokuwa na mwamko wa elimu.

Meck alisema kuwa shule hiyo inajumla ya wanafunzi 681 Kati yao wasichana ni 317 na kuwa wanafunzi Wanafunzi wavulana 68 ambao ni Wa kidato cha tano na sita ndio wanakaa katika mabweni Mawili yaliyo shuleni hapo.

Alisema kuwa wanafunzi hao wanaoishi bweni ni wale wanaotoka maeneo ya mbali na kata hiyo huku wanafunzi wasichana 20 Kati ya 68 waliokuwa wakiishia bweni wamekuwa wakilala katika vyumba viwili vya madarasa vilivyogeuzwa Kama mabweni ya muda kwa wanafunzi hao.

Kuhusu tatizo la mimba alisema kuwa Kati ya mwaka 2011 hadi sasa jumla ya wanafunzi 7 wameshindwa kuendelea na msomo kutokana na mimba .

Alisema mwaka 2011 wanafunzi wanne walipata mimba na mwaka 2012 wanafunzi watatu akiwemo mwanafunzi mmoja wa kidato cha nne na wawili kidato cha tatu.

Meck alisema pamoja na kuwa idadi kubwa ya mimba zimesababishwa na jamii inayoizunguka shule hiyo pamoja na wafanyabiashara mmoja Kati ya wanafunzi hao Saba waliokatisha Masomo kwa mimba alipewa mimba hiyo na mwanafunzi mwenzake ambaye walikuwa wamepanga katika getho moja mtaani.

Afisa Elimu sekondari katika wilaya ya Mbeya mwalimu Magreth Mbwilo mbali ya kuthitibidha ukubwa wa tatizo hilo la mimba katika shule hiyo ya Iwalanje bado alisema kuwa katika Wilaya hiyo changamoto kubwa ni mabweni kwa wanafunzi na kuwa kati ya shule 27 za sekondari katika wilaya hiyo ni shule mbili pekee ndizo zinamabweni japo bado hayatoshi.

Alisema mkakati uliopo ni kuendelea kujenga Hosteli zaidi na tayari ujenzi wa Hosteli 10 unaendelea katika shule mbali mbali huku Kati ya Hosteli hizo tatu zipo katika hatua ya mwisho.

Life Go Is On.......................Maisha ......................







Dk Mwakyembe Awasha Moto TRL





Mussa Juma, Dodoma

BAADA ya kusafiri kwa treni kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amebaini hujuma nzito katika Shirika la Reli Tanzania (TRL) ikiwamo ofisa mmoja kuwaibia abiria kwa kughushi viwango vya nauli na ameagiza afukuzwe kazi.

Licha ya kuagiza kutimuliwa kwa ofisa huyo, pia alitangaza kuandaliwa utaratibu wa kufanya mabadiliko kadhaa katika kuboresha usafiri huo, ikiwamo kuondoa malipo ya nusu nauli kwa watoto wadogo kuanzia miaka mitatu hadi miaka 10 na pia kuondolewa kwa utaratibu wa malipo ya mizigo midogo ya abiria.

Juzi, Dk Mwakyembe ambaye tayari amewang’oa vigogo wanne wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), aliamua kusafiri kwa treni hadi Dodoma akitokea Dar es Salaam ili kujionea utendaji kazi wa shirika hilo.

Mara baada ya kuwasili katika Stesheni ya Dodoma saa 1:30 asubuhi, Waziri Mwakyembe alizungumza na waandishi wa habari na kusema akiwa katika safari hiyo, amepata fursa za kutembelea mabehewa yote na kuzungumza na abiria.

Dk Mwayembe alisema ingawa safari ilikuwa nzuri, kuna mengi ambayo ameyabaini ambayo ni pamoja na abiria kulipa nauli kubwa na kuandikiwa tiketi tofauti jambo ambalo alisema ni wizi na kamwe wizara yake haiwezi kulifumbia macho.

“Unakuta nauli halali ni Sh9,000 lakini, abiria ameandikiwa Sh29,000. Sasa nimeagiza huyu anayehusika afuatiliwe na kujulikana na nipewe taarifa ameondolewa,” aliagiza Dk Mwakyembe.
Alisema pia katika safari hiyo, alibaini uchakavu mkubwa wa mabehewa na hakuna tofauti ya daraja la tatu na la kwanza, upungufu mwingine ni katika utendaji na taratibu jambo ambalo linapaswa kuchukuliwa hatua.

Dk Mwakyembe alisema si vyema mtoto kuanzia miaka mitatu kulipishwa nusu nauli, kwani taratibu zinapaswa kufanywa ili hadi mtoto wa miaka 10 ikiwezekana asilipishwe nauli kwani treni ndiyo usafiri wa umma.

Kuhusu mizigo, alisema kwa sasa mizigo ya abiria inalipiwa kwa kilo kama ilivyo usafiri wa ndege jambo ambalo si sawa kwani mzigo wa abiria kuanzia kilo 20 unalipishwa jambo ambalo linapaswa kuangaliwa.

“Usafiri huu mimi nasema ndiyo wa umma hivyo, tusizuie watu kupeleka hata zawadi nyumbani kwao ni vyema tuwe na utaratibu walau mizigo kidogo ya abiria isilipiwe,” alisema Dk Mwakyembe.