Tuesday, June 12, 2012

Baraza La Madiwani Manispaa Ya Bukoba Lafanyika


Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya manispaa ya Bukoba Khamis Kaputa akiongea wakati wa kikao cha baraza la madiwani wa pili toka kushoto ni meya wa manispaa hiyo Anatory Amani, kulia mkuu wa wilaya ya Bukoba Ziporah Pangani na anayefuata makamu meya Ngalinda.




Ofisa wa UTT, Kamugisha akiwaelezea madiwani wa halmashauri ya manispaa ya Bukoba maendeleo ya mradi wa upimaji wa viwanja katika manispaa hiyo.




Madiwani wengine wa manispaa ya Bukoba wakiwa kwenye kikao chao cha kawaida.



Baadhi ya madiwani wengine wa halmashauri ya wilaya ya Bukoba.




Baadhi ya watendaji wa manispaa ya Bukoba walioudhuria kikao cha baraza la madiwani.




Watendaji wengine wa manispaa ya Bukoba.

RPC Kagera Akionyesha Nguo Za JWTZ Walizokamata Wakati Wa Mapambano Kati Ya Polisi Na Majambazi


Huyu ndiye kamanda mpya wa jeshi la polisi mkoani Kagera aliyemrithi Henry Salewi aliyestaafu, anaonekana ameshika bunduki sare za jeshi la wananchi ambazo majambazi yalikuwa yakizitumia kufanya uharifu.




Mkuu wa upelelezi mkoani Kagera Peter Matagi akionyesha dola feki 1,000 ambazo jeshi la polisi lilizinasa kufutia msako mkali unaofanywa na jeshi hilo mkoani humo wa kuthibiti uharifu.




Baadhi ya silaha ambazo jeshi la polisi lilizikamata zilizokuwa zikitumiwa na majmbazi kufanya uharifu mkoani Kagera



 
NARUDIA TENA HII STORI
 
JESHI la polisi limefanikiwa kuliua jambazi sugu lililokuwa linamiliki silaha tatu za kivita zilizokuwa zinatumika kutekeleza vitendo vya uharifu kwenye maeneo mbalimbali yaliyoko mkoani Kagera vikiwemo vya utekaji wa magari na wizi na unyanganyi.

Jambazi hilo ambalo jina lake halikuwe kutambuliwa limeuwawa jana majira ya saa 4.30 halfajiri na kikosi maalumu cha upelelezi kilichooongozwa na mkuu wa upelelezi wa mkoa wa Kagera Peter Matagi.


Kwa mijibu wa kamanda wa jeshi la polsi mkoani Kagera Philip Kalangi ni kwamba jeshi hilo lilifanikiwa kulinasa jambazi hilo na hatimaye kuliua wakati lilipokuwa liko kwenye harakati za kuvamia mgodi unamilikiwa na kampuni ya barrick wa Tulawaka uliko wilayani Biharamulo.


Kalangi ambaye ni kamanda mpya wa jeshi la polisi mkoani Kagera aliwaambia waandishi wa habari kuwa jeshi la polisi kabla ya kukabiliana na jambazi hilo lilipata taarifa za siri toka kwa wasiri wake jambo lililolisaidia jeshi hilo kuweka mtego ulionasa jambazi hilo.


Alisema jambazi hilo wakati likiwa katika harakati za kutekeleza uharifu kwenye mgodi wa Tulawaka huku likiwa na wenzake waliofanikiwa kukimbia lilishtukia mtego ulikuwa umewekwa na jeshi la polisi hivyo likalazimika kuanza kumimina risasi ovyo.


Kamanda huo alisema jeshi la polisi baada ya kuona hivyo lilijibu mapigo yaliyofanikisha kuuawa kwa jambazi huyo huku majambazi wenzake wakikimbilia kusikojilikana, alisema katika tukio hilo jeshi hilo lilifanikiwa kupata silaha mbalimbali, risasi na mabomu ya kutupa kwa mkono.


Alizitaka silaha ambazo jeshi la polsi lilifanikiwa kuzikamata katika tukio hilo kuwa ni pamoja na bunduki moja ya AK 47, Bunduki 2 aina ya SMG, risasi 246, magazini 7 na mabomu 3 ya kurusha kwa mkono.


Kalangi alisema jambazi liliouwawa na askari hao mwili wake umehifadhiwa kwenye hospitali teule ya wilaya ya Biharamulo, alisema jeshi hilo liko katika msako mkali wa kuwanasa majambazi yaliyokimbia wakati wa tukio hilo.


Alipongeza askari walioshiriki katika operationi hiyo maalumu, pia aliwashukuru wananchi waliotoa taarifa za siri zilizilisaidia jeshi la polisi kuyanasa majambazi hayo, aliwaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili liweze kutimiza adhima yake ya kuthibiti uharifu mkoani Kagera.

Bungeni Jana: Wabunge Wateule Wa Jk Walivyokula Kiapo


 Mbunge wa Kuteuliwa James Fancis Mbatia akiapa Bungeni Mjini Dodoma Juni 12, 2012.
Spika wa Bunge Anne Makinda akimkabidhi kanuni za Bunge Mbunge wa Kuteluliwa James Mbatia baada ya kumwapisha, Bungeni Mjini Dodoma, Juni 12,2012.
 Mbunge wa Kuteuliwa, Sospeter  Mwijarubi Muhongo akiapa, Bungeni Mjini Dodoma, Juni 12, 2012.
Mbunge wa Kuteuliwa Janet Zebedayo Mbene akiapa, Bungeni Mjini Dodoma  Juni 12, 2012.
 Mbunge wa Kuteuliwa Saada  Mkuya Salum akiapa Bungeni Mjini Dodoma Juni 12, 2012.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akizungumza na Mbunge wa Namtumbo Vita Kawawa (kushoto) na Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu  Nchemba kwenye viwanja vya Bunge Mjini  Dodoma  Juni 12, 2012.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba na Mbunge wa Viti Maalum  Rose Kamili Sukum kwenye viwanja vya bunge Mjini Dodoma, Juni 12,2012.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Namtumbo, Vita Kawawa (kushoto) , Mbunge wa Viti Maalum  Leticia Nyerere (kuli) na Mbunge wa Iramba Magharibi,  Mwigulu Nchemba kwenye viwanja vya Bunge  Mjini Dodoma Juni 12,2012.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum, Felister Bura, kwenye jengo la Utawala la Bunge Mjini Dodoma  Juni 12, 2012.
Waziri Mkuu, Mizengo pinda  akizungumza na  Mbunge wa Viti Maalum  Pauline Gekul na watoto wake Irene (kushoto)  na Inocentia kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 12,2012.Picha na Ofisi  ya Waziri Mkuu
 

Magazeti Magazeti



































Monday, June 11, 2012

Polisi Kagera Yauwa Jambazi Na Kukamata Buduki Tatu Na Mabomu

Na Mwandishi Wetu
Kagera

JESHI la polisi Mkoani Kagera limefanikiwa kumuua jamabazi katika majibizano ya risasi na kufanikiwa kukamata  bunduki tatu risasi 246,mabomu ya kurushwa kwa mkono matatu na sare pea mbili ambazo zionafanana na kabisa na za jeshi la wananchi wa Tanzania.

Akiongea na wandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa polisi Mkoani humo Philp Kalangi amesema tukio hilo lilitokea tarehe
9 Juni majira ya saa 10 alfajiri katikaeneo la Mavota-Tulawaka Wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera Mtu anayesadikiwa kuwa ni jambazi ambaye hafahamiki jina wala makazi yake aliuawa baada ya kupigwa risasi na askari polisi katika shambulizi.

Kamanda Kalangi, alisema tukio hilo lilitokea baada ya msiri kufichua mpango uliokuwa umepangwa na majambazi ambayo yalikuwa na lengo la kwenda kuvamia Mgodi wa Barrick Tulawaka ulioko Biharamulo Mkoani humo,jeshi la polisi baada ya kupata taarifa  hizo mkuu wa upelelezi mkoa wa Kagera SSP,Peter Matage aliandaa mtego kupitia njia ambayo ja,bazi hilo lingetumia.

Alisema kutokana na taarifa za msiri jambazo huyo ndiye alikuwa kiongozi na alibeba silaha  zote mwenyewe  na tayari alikuwa amewatanguliza wenzake mbele ambao wangekutana eneo la tukio.

Kamanda alisema katika shambulizi hilo la kushitukiza na kurushiano risasi kati ya jambazi huyo na askari na hatimaye kuuawa kwa jambazi hilo  na kukutwa na bunduki tatu ambazo mbili ni AK  47 ,SMG moja,riasi 246,mabomu ya kurushwa kwa mkono matatu,sare za jeshi la wananchi pea mbili na buti pea moja na makoti mawili ya mvua ambayo yalikuwa yamefungiwa bunduki mbili,na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali teule ya Biharamulo.


Kamanda Kalangi alisema  katika tukio jingine jeshi hilo  linawashikiliwa watuhumiwa wanne aliokuwa wamepanga njama za kutaka kumuua ( ALBINO )aishie Wilayani Missenyi Mkoani humo.

Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Gaston Galela( 50 ),ambaye ni Mnyarwanda,alikamatwa akiwa Bwanga mkoani Geita kwa mganga wa kienyeji, Njenwa Charles ( 30 )msukuma  na mkazi wa Mutukula Byamungu Felician (  53 )mkazi wa Mutukula na  Masanja Mabula ( 40 )mkazi wa Mutukula.

Alisema wamefanikiwa kuwatia mikoni watuhumiwa hao kufuatia taarifa iliyotolewa kwa jeshi hilo kupitia kwa mpelelezi wa makosa ya jinai mkoani humo Petera Matage aliyeanda mgego wa kuwanasa na kufanikiwa.

Wakati huohuo jeshi hilo Mkoani Kagera wamefanikiwa kumkamata Chamilion Kamugisha miaka ( 20 )mkazi wa Hamgembe Manispaa ya Bukoba Mkoani humo Juni 5 majira ya saa 10.00 asubuhi eneo la Mutukula Wilaya Ya Missenyi akiwa na noti bandia  US Dollar 1000,wakati akiwa katika harakati za kubadilisha katika fedha za kitanzania.

Kamanda huyo wa polisi Mkoani hapa ambaye ndiyo mara yake ya kwanza kufanya kazi mkaoni Kagera amewataka wanachiwa mkoa huo kuwa na usgirikiano na jeshi la polis sambamba na kuachana na mila potofu huku akisema mali azipatikani kwa imani za ushirikina ni juhudi na maarifa.

MWISHO

Tatizo La Moto Katika Shule Ya Sekondari Rugambwa Lisipuuzwe


Mkuu wa upelelezi wa aamkoa wa Kagera Peter Matagi, akiwaelezea wanafunzi wa shule ya sekondari ya Rugambwa hatua za awali uchunguzi wa chanzo cha moto uliotokea shuleni hapo, aliwaambia wanafunzi kuwa chanzo cha moto huo hakikutokana na hitilafu ya umeme.

Posted on: 11 Jun 2012



Mkuu wa wilaya ya Bukoba akiwaeleza wanafunzi wa shule ya sekondari ya Rugabwa hatua ambazo serikali itaendelea kuzichukua kuthibiti majanga ya moto ambayo hutokea mara kwa mara katika shule hiyo.

Posted on: 11 Jun 2012



Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Rugambwa wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Bukoba Bi Pangani.

Posted on: 11 Jun 2012



Mabaki ya vifaa vya wanafunzi vilivyoteketea kwa moto vikiwa ndani ya bweni lililoungua.

Posted on: 11 Jun 2012



Jengo la bweni la usambara ambalo sehemu yake iliungua kwa moto na kuteketeza mali za wanafunzi.
 
Picha na Audax Mutiganzi

Maisha Yanaendelea

Biashara Ya Mapera...






  Mojawapo ya soko la kuuzia bidhaa ndogondogo katika kijiji cha Mkima kilichopo Sumbawanga. picha Meshack Maganga wa Mjengwablog