Monday, June 11, 2012

Kongamano UDSM


Mwanataalum mkongwe, Profesa Goran Hyden akijibu hoja na maswali mbalimbali yalitolewa na wahadhiri na wanataalum mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania juzi mjini Dar es salaam wakati wa kongamano la siku moja la wanataalum liloandaliwa maalum na Chuo Kikuu cha Dar es salaam la kutambua mchango wake kitaalum.


Katibu Mkuu zamani wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Juma Mwapachu akichangia mada juzi mjini Dar es saam wakati wa kongamano la siku moja la wanataalum liloandaliwa maalum na Chuo Kikuu cha Dar es salaam la kutambua mchango wa Profesa  Goran Hyden alioutoa ndani na nje Tanzania.Kulia ni Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es  salaam Profesa Rwekaza Mukanda.

Profesa Bernadeta Killian wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam akitoa mada juzi mjini Dar es salaam kuhusu kitabu cha Profesa Goran Hyden cha Beyond Ujamaa in Tanzania wakati wa kongamano la siku moja la wanataalum liloandaliwa maalum na Chuo Kikuu cha Dar es salaam la kutambua mchango wake kitaalum.

Mwanataalum mkonge Profesa Goran Hyden (kushoto) akibadilishana mawazo na Balozi wa Zambia nchini Judith Kangoma (kulia) juzi mjini Dar es salaam wakati wa kongamano la siku moja la wanataalum liloandaliwa maalum na Chuo Kikuu cha Dar es salaam la kutambua mchango wake kitaalum wa Profesa alioutoa ndani na nje Tanzania.



Waziri Mkuu Mstaafu wa Uganda Profesa Apolo Nsibambi(kulia) akichangia mada juzi mjini Dar es saam wakati wa kongamano la siku moja la wanataalum liloandaliwa maalum na Chuo Kikuu cha Dar es salaam la kutambua mchango wa Profesa  Goran Hyden alioutoa ndani na nje Tanzania. Wengine ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma George Yambesi(katikati) na Profesa Goran Hyden(kushoto)
Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO- Dar e salaam.

Makamu Wa Rais Dk Bilal Afungua Maonyesho Ya Kwanza Ya Tanzania Homes Expro



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu ujenzi wa Nyumba za Shirika la nyumba la Taifa, NHC, kutoka kwa Ofisa Masoko wa Shirika hilo, Mariam Ndabagenda, wakati Makamu alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho ya kwanza ya Tanzania Homes Expro, yaliyofanyika leo Juni 10 katika Viwanja vya Mlimani City Mwenge jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Mauzo wa Shirika hilo, William Genya (wa pili kulia) ni Ofisa Mauzo mwandamizi wa Shirika hilo, Emmanuel Lymo. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu utengenezaji wa Viage vya ujenzi wa Nyumba kutoka kwa Ofisa Masoko wa Kampuni ya Insignia Ltd, Obed Machoka, wakati Makamu alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho ya kwanza ya Tanzania Homes Expro, yaliyofanyika leo Juni 10 katika Viwanja vya Mlimani City Mwenge jijini Dar es Salaam.Picha na Muhidin Sufiani-OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akisiliza maelezo kuhusu ujenzi wa Nyumba 220 zinazojengwa eneo la Jangwani Beach, jijini Dar es Salaam, zinazotarajia kutumia jumla ya Sh. Milioni 208, kutoka kwa Ofisa Mtendaji wa Kampuni ya Global Land Solutions Ltd, Murtaza Adamjee, wakati Makamu alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho ya kwanza ya Tanzania Homes Expro, yaliyofanyika leo Juni 10 katika Viwanja vya Mlimani City Mwenge jijini Dar es Salaam.Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akisiliza maelezo kuhusu matumizi ya Nyaya za Africab kutoka kwa Ofisa Masoko na Mauzo wa Kampuni hiyo, Khuzema Janowalla, wakati Makamu alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho ya kwanza ya Tanzania Homes Expro, yaliyofanyika leo Juni 10 katika Viwanja vya Mlimani City Mwenge jijini Dar es Salaam.Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Magazeti Nagazeti




















Friday, June 1, 2012

PINDA KATIKA KIKAO CHA SADC

Pinda Amwakilisha Jk Kikao Wa SADC

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikaribishwa kwa gwaride baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Luanda, Angola May 31, 2012 kumwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika Kikao cha Wakuu wa Nchi za Jumuiya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, SADC. Anaongozwa na Waziri wa  Nishati na Maji wa Angola  Joao Baptista Borges. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikaribishwa kwa gwaride baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Luanda, Angola May 31, 2012 kumwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika Kikao cha Wakuu wa Nchi za Jumuiya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, SADC. Anaongozwa na Waziri wa  Nishati na Maji wa Angola  Joao Baptista Borges. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza  na Waziri wa Nishati na Maji wa Angola, Joao  Baptista Borges baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Luanda nchini Angola May  31, 2012 ambako atamwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika kikao cha  Wakuu wa Nchi za  Jumuiya  ya Maendeleo  ya Kusini mwa Afrika SADC Juni 1, 2012. (Picha na Ofisi  ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe baada ya kuwasili Luanda Angola May 31, 20121 ambako atamwakilisha Rais Jakaya Kikwenye katika Kikao cha Wakuu wa Nchi  za Jumuiya ya Maendeleo ya Afrika SADC Juni 1, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengio Pinda akisalimiana na Rais wa Angola Jose Edwardo dos  Santos katika kikao cha Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleoo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC kilichofanyika  Juni 1, 2012 Mjini Luanda Angola . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Kanoni Ni Balaa Pamoja na jua Kuwaka





Ni jana majira ya saa nane mchana wakati ambapo juu lilikuwa kali sana kutokana na hali ya hewa ilivyoshinda jana ni vigumu kwa mtu amabaye alikuwa mbali na tukio kuamini hili ila ni kwamba kuanzia mda wa saan nane mpaka jioni wafanyabiashara waliopo maeneo ya mto kanoni walipatwa na mafuliko ya ghafura mara baada ya mto kanoni kuanza kumwaga maji yake nje ya mto huo.
Nikiongea na baadhi ya wafanyabihashara haowlisema tumeanza kuona maji yakiongezeka katika vibanda vyetu na baadae yakazidi kuwa mengi mpaka sasa tumefunga.
Vingozi wa manispaa ya mji wa Bukoba wana kila sababu ya kuwatafutia eneo la kufanyia bihashara tofauti na maeneo hayo ili kunusulu maisha na bihashara yao.