Showing posts with label jami. Show all posts
Showing posts with label jami. Show all posts

Wednesday, June 27, 2012

Katibu Wa Vijana CCM (uvccm) Singida ‘Omary Mtuwa’ Akanusha Kuhamia Chadema.




Katibu wa umoja wa vijana CCM (UVCCM) mkoa wa Singida,Omary Hassan Mtuwa akitoa taarifa yake kwa waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) ya kukanusha taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari kuwa amekihama Chama Cha Mapinduzi na kujiunga na CHADEMA.Picha na Nathaniel Limu.

Katibu wa umoja wa vijana CCM (UVCCM) mkoa wa Singida, Omary Hassan Mtuwa, amekanusha vikali taarifa iliyotolewa na vyombo vya habari, kwamba amekihama chama chake na kujiunga na chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Mtuwa alisema taarifa hizo ni za uwongo uliopea, uzushi na zinalenga kumgombanisha yeye na chama chake pia na viongozi kwa ujumla.

Akifafanua, Mtuwa alisema taarifa hizo zimechapishwa na gazeti moja la kiswahili la kila siku (juni 18) mwaka huu ukurasa wa mbele ulibeba kichwa cha habari kuwa CHADEMA yavuna viongozi wa CCM.

Katibu huyo,alisema taarifa zilizoandikwa kwenye gazeti hilo zilizohusisha cheo cha Katibu wa vijana wa CCM mkoa wa Singida na kwamba anasoma chuo kikuu cha Ruaha, ni za uwongo mtupu.

Mtuwa alisema taarifa hiyo imemkosesha amani na imewasikitisha mno kwa vile, wahusika hawakumtendea haki kwa kumuuliza juu ya madai ya kuhamia CHADEMA. Mwandishi wa habari hiyo, ameandika taarifa hiyo bila kupata maoni kutoka kwake.

“Kama kweli CHADEMA wamevuna viongozi kutoka CCM,hilo mimi silijui na wala silitambui.Lakini kwa upande wangu, wameogopa na wamewapotosha Watanzania kwa kusema katibu wa UVCCM mkoa wa Singida,kahamia CHADEMA”,alisema na kuongeza;

“Mimi Omary Hassan Mtuwa,bado ni mwanachama hai wa CCM na ni mwaminifu wa kiwango cha juu.Nitaendelea kukitumikia chama changu kwa nguvu zote bila kutetereka hadi tone la mwisho”.

Alisema amefedheshwa na kuonewa sana na taarifa hiyo, iliyosheheni uwongo mwingi na kusababisha usumbufu mkubwa kwa mwajiri wake, familia yake na jamii kwa ujumla.

“Kwa hiyo, naomba gazeti hilo lifute,liniombe radhi na kutangaza hatua hiyo kupitia ukurasa wa mbele kama ambavyo limefanya katika kunichafua.Tofauti na hivyo,nitalazimika kwenda mahakamani kudai haki yangu”,alisema Mtuwa. 

Chanzo: MOblog.  http://dewjiblog.com

Mahakama Yatoa Onyo Kwa Madaktari

Chanzo:  http://www.fullshangweblog.com

Vodacom Yahamasisha Wabunge Kutumia Malipo Ya Baada...!




Baadhi ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,wakifafanuliwa jambo na Meneja wa wateja wa Malipo ya baada wa Vodacom Tanzania Bi. Yvone Bayona,jinsi ya kujiunga na mpango wa malipo ya baada ya kampuni hiyo katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma. Vodacom inaendesha zoezi maalum la kuwahamasisha wabunge kujiunga na mpango wa mteja mmoja mmoja wa malipo ya baada katika juhudi za kujiimarisha kisoko.




Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Salvatory Machemli (Ukerewe - Chadema) na Danstan Mkapa (Nanyumbu - CCM) wakielezewa na Afisa wa Vodacom Tanzania Bi.Melinda Siarra,jinsi ya kujiunga na mpango wa malipo ya baada ya kampuni hiyo katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma. Vodacom inaendesha zoezi maalum la kuwahamasisha wabunge kujiunga na mpango wa mteja mmoja mmoja wa malipo ya baada katika juhudi za kujiimarisha kisoko.
 Kutoka Blog ya Michuzi: http://issamichuzi.blogspot.com

Misha Yanaedelea



Kibondo igoma Moja

                                 


                                  

Taarifa Kutoka Kampuni Ya Bia Tanzania (TBL)




            TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

                           Toleo la Leo 

MASHINDANO YA NGOMA ZA ASILI YA BALIMI EXTRA LAGER 2012 KUTIMUA VUMBI KUANZIA JUNI 30.

Dar Es Salaam, June 25th 2012:
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager, leo imezindua rasmi mashindano ya ngoma za asili ya Balimi Extra Lager kwa mwaka 2012. Mashindano haya ambayo yametokea kupendwa sana na wakazi wa kanda ya ziwa yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi katika mikoa mbali mbali ya kanda ya ziwa kuanzia Juni 30.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo Jijini Dar es Salaam, meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager Bi. Edith Bebwa alisema; Bia ya Balimi Extra Lager imekuwa ikiendesha mashindano haya maarufu kama “Mashindano ya Ngoma za Asili ya Balimi Extra Lager” kwa zaidi ya miaka saba sasa , na kwa kweli napenda kusema kuwa ni mashindano yaliyotokea kupendwa sana katika kanda yetu hii ya ziwa,
Lengo kuu la kudhamini mashindano haya ni kushirikiana na wakazi wa kanda ya ziwa katika kuenzi na kulinda tamaduni za kanda alisema Bi Edith .
Kwa mwaka huu wa 2012, mashindano yataanza rasmi tarehe 30 Juni katika ngazi za mikoa na kumalizika tarehe 21 Julai. Tutaanza na mkoa wa Mwanza ukifuatiwa na mikoa ya Mara, Kagera, Shinyanga na Tabora, katika mpangilio ufuatao.

Tarehe Mkoa Viwanja
30/06/2012 KAGERA
Kaitaba
07/07/2012 MWANZA Ccm Kirumba
14/07/2012
TABORA Chipukizi
21/07/2012
SHINYANGA Shycom
21/07/2012
MUSOMA Bwalo la Magereza
28/07/2012.
FINALS MWANZA Ccm Kirumba
Akielezea juu ya zawadi za mwaka huu, bi. Edith Bebwa alisema; kama ilivyo ada ya Bia ya Balimi, kila mwaka tumekuwa tukiongeza zawadi ili kuongeza chachu ya ushindani na kuleta tija kwa washindani. Kwa mwaka huu tumeongeza zawadi kwa takribani asilimia 20 ukilinganisha na mwaka jana. Hii yote inaonesha jinsi gani bia ya Balimi inatambua, inajali na kuthamini utamaduni wa kanda yetu. Zawadi kwa washindi ni kama ifuatavyo;
Ngazi ya mkoa Finali
Mshindi wa kwanza 600,000 1,100,000
Mshindi wa pili 500,000 850,000
Mshindi wa tatu 400,000 600,000
Mshindi wa nne 300,000 500,000
Mshindi wa tano hadi wa kumi kila kikundi 150,000 250,000
Pamoja na zawadi hizi nono, pia Balimi Extra Lager itaendelea kutoa huduma muhimu kwa vikundi shiriki kama vile chakula na malazi. Tunaamini kabisa mambo yote haya yataongeza hamasa na msisimko katika mshindano ya mwaka huu. Na kauli mbiu yetu kwa mwaka 2012 “Balimi Extra Lager, twajivunia utamaduni wetu”.

Akizungumzia maandalizi ya fainali hizo, Meneja Masoko wa Tbl Fimbo Buttalah alisema; Maandalizi yote kwa upande wetu sisi wadhamini yameshakamilika, hivyo niwaombe tu washiriki wote ambao nimepata taarifa kuwa wamekuwa mazoezini kwa muda sasa, waendelee na mazoezi ili kuonesha uwezo wa juu utakaoleta ushindani na kutoa burudani yenye kiwango cha juu.

Kwa niaba ya bia ya Balimi Extra Lager, tunapenda kuwakaribisha watu wote kuhudhuria mashindano haya ambayo tarehe na mahali yatakapofanyikia zitakuwa zikitangazwa redioni ili waweze kushuhudia burudani hii na kuuenzi utamaduni wetu. Pia wananchi wasisahau kuwa katika burudani hizi pia wataburudika na Bia yao waipendayo ya Balimi Extra lager baridi, na kushinda zawadi mbali mbali katika promosheni za Balimi zitakazoambatana na Mashindano haya ya Ngoma za asili ya Balimi Extra Lager.
Kwa Maelezo zaidi wasiliana na:
Edith Bebwa, Brand Manager, +255767266410, edith.bebwa@tz.sabmiller.com
Fimbo Butallah, Marketing Manager, +255767266567, fimbo.butallah@tz.sabmiller.com
Editha Mushi, Communications & Media Manager, +255767266420, editha.mushi@tz.sabmiller.com

Kuhusu TBL
Tanzania Breweries Limited (TBL) inatengeneza, kuuza na kusambaza bia, vinywaji vyenye ladha ya matunda vilivyo na kilevi na vinywaji visivyo na kilevi hapa Tanzania. TBL pia ndiyo kampuni mama ya Tanzania Distilleries Limited pamoja na kampuni shiriki ya Mountainside Farms Limited.

Bia zinazotengenezwa na kampuni ya TBL ni pamoja na Safari Lager, Kilimanjaro Premium Lager, Ndovu Special Malt, Castle Lager, Vinywaji vingine vinavyotengenezwa na kundi la makampuni ya TBL ni Konyagi Gin, Amarula Cream, Redd’s Premium Cold na Grand Malt.

Kundi la makampuni ya TBL limeorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam, limeajiri watu wapatao 1,300 na linawakilishwa nchi nzima na viwanda vinne vya bia, kiwanda kimoja cha kutoneshea, kimoja cha kutengenezea kimea pamoja na bohari nane za kusambazia bia.

Kuhusu SABMiller
SABMiller plc moja kati ya makampuni makubwa ya bia duniani ikiwa na mikataba ya kutengeneza na kusambaza bia kwenye nchi zaidi ya 60 katika mabara matano. Bia zake ni pamoja na zile za kimataifa kama Miller Genuine Draft, Peroni Nastro Azzurro na Pilsner Urquell vilevile na bia nyingine zinazoongoza kwenye masoko ya ndani ya nchi mbalimbali. Nje ya Marekani, SABMiller ni moja ya kati ya makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji vya Coca-Cola duniani. Hivi karibuni SABMiller plc ilinunua kampuni ya bia ya Foster’s pamoja na shughuli zake za uzalishaji nchini India.SABMiller imeorodheshwa kwenye masoko ya hisa ya London na Johannesburg.

Thursday, June 21, 2012

Bei Ya Kahawa Mkoani Kagera Yashuka

Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Kagera John Binushu anaye andika akijadiri jambo na Mrajisi wa Vyama Vya Ushirika Mkoani Kagera Rwenkiko Shorosi


 Na Mwandishi Wetu Bukoba
 
CHAMA kikuu cha ushirika mkoani Kagera(KCU 1990 LTD)kimefikia maamuzi ya kushusha bei ya Kahawa,kwa kile kilichodaiwa kusababishwa na kushuka kwa bei hiyo katika soko la Dunia.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa chama hicho John Binunshu,kushuka kwa bei hiyo ni kutokana na bei ya mnadani kuporomoka kwa siku za hivi karibuni hivyo kulazimu KCU kubadirisha bei ya manunuzi tofauti kama ilivyokuwa hapo awali.

Binunshu alisema kuwa hata hivyo pamoja na kushuka bei hiyo,wakulima wa Kahawa mkoani hapa wasiwe na wasiwasi juu ya taarifa hizi kwani wataendelea kupatiwa taarifa za bei kadili hali ya soko itakavyokuwa inabadirika.

Katika taarifa ya Meneja mkuu wa KCU Vedasto Ngaiza,na nakusambazwa kwa mameneja wote wa  vyama vyamsingi vipatavyo 129 ambavyo vinaendelea na ununuzi wa Kahawa kwa msimu huu ambao umefunguliwa rasmi mwezi Mei mwaka huu,bei ya kahawa imeteremka kutoka shilingi 1350/=hadi kufikia shilingi 1100/=kwa Kahawa aina ya robusta maganda,huku robusta safi itakuwa ikinunuliwa kwa shilingi 2,200/= kwa kilo.


Aidha,Ngaiza alibainisha kuwa Kahawa nyingine aina ya Arabika maganda imeshuka kutoka shilingi 1550/=na kufikia shilingi 1300/=huku safi ikinunuliwa shilingi 2600/=.

Hata hivyo,Ngaiza amesisitiza kuwa wakulima wa zao hili wanapaswa kupokea mabadiliko ya bei hiyo,ila endapo bei itaongezeka mnadani uongozi wa KCU hautachelewa kurekebisha bei hiyo kwa mkulima.

Awali mabadiriko ya bei hizi,yalionekana kuanza kuleta wasiwasi juu kwa wakulima huku baadhi yao wakihushutumu uongozi wa KCU umeamua kutelemsha bei mara baada ya kubaini kuwepo wingi za kahawa kwa wakulima.

MWISHO