Thursday, January 16, 2014

Picha Mbalilmbali Za Kikao Cha Ushauri Wa Mkoa Wa Kagera (RCC) Mijni bukoba


 Mkuu wa Mkoa Wa Kagera Kanali Mstaafu Fabiani Massawe(katikati) ambayei ni mwenyekiti wa kikao hichoakisikiliza wajumbe mbalimbali wakitoa hoja zao.







Wajumbe mbalimbali wakifuatilia kikao hicho

Wednesday, January 8, 2014

Maisha Yanaendelea

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI CHARLES TIZEBA AKAGUA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE WA BUKOBA

 Naibu waziri wa uchukuzi akiteta jambo na mkuu wa mkoa wa Kagera, Charles Tizeba alipokuwa mkoani Kagera kukagua ujenzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba.


Utafikiri Kuna Ugomvi Kumbe Mchezo Wa Kuvuta Kamba

Mkapa atetea masilahi ya walimu nchini

mkapa 36710
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ameitaka Serikali kuboresha masilahi ya walimu ili waweze kutekeleza vyema majukumu ya kazi za kuwaandaa vijana kukabiliana na changamoto za utandawazi. (HM)
Amesema kuwa pamoja na kazi ngumu wanayofanya walimu, lakini bado suala la masilahi kwao ni kikwazo kunahitaji kuangaliwa kwa karibu, kwani kazi wanayofanya ni ngumu na inahitaji kujitolea na wito zaidi .
Kauli hiyo ameitoa wakati akifungua Chuo cha Ualimu cha Benjamin Mkapa kilichopo Mchangamdogo Wilaya ya Wete, ikiwa katika shamrashamra za kutimiza miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Ameeleza kusikitishwa na Serikali kushindwa kuangalia vyema suala la masilahi ya walimu na kuongeza kuwa Serikali imekuwa ikifanya mazungumzo zaidi na taasisi ambazo zimekuwa zikifanya au kutishia kufanya migomo na kuwaaongza maslahi yao .
"Serikali imekuwa ikifanya mazungumzo ya mara kwa mara na taasisi ambazo zimekuwa zikitishia ama kufanya mgomo, lakini walimu ambao wanafanya kazi ya wito zaidi masilahi yao yako chini," alifahamisha Mkapa.
"Najua mtajiuliza kwanini sikuyafanya hayo wakati wa utawala wangu, lakini nawaombeni mjifunze kutokana na makosa yangu ili tuweze kufika tulikokusudia," alieleza Mkapa
Aidha amesema kuwa kada ya ualimu ndiyo tegemeo na chimbuko la maendeleo katika taifa lolote duniani kutokana na kwamba wataalamu wote wanapita kwa mwalimu na kwamba huwezi kuzungumzia maendeleo bila ya kuigusa kada ya ualimu .
"Kwa kuzingatia umuhimu wa walimu, kuna kila sababu ya Serikali kuwajali walimu hasa katika kuwatimizia masilahi yao," alisema Mkapa. "Hata mataifa yaliyoendela kiviwanda kwanza yaliboresha sekta ya walimu kwa kuimarisha maslahi yao, hivyo na sisi tuige kwa wenzetu waliopiga hatua kimaendeleo," alieleza Mkapa .
Ameitaka jamii kuwaheshimu walimu pamoja na kuwapa ushirikiano mzuri kutokana na kwamba wao ndiyo walezi wa watoto.
"Walimu ni watu muhimu katika jamii, lazima tuwape ushirikiano ili waweze kufanya vizuri kazi zao za kuelimisha jamii," alisema Mkapa. Chanzo: mwananchi

Maliasili watimua watumishi 21

nyalandu b7c56
Wizara ya Maliasili na Utalii, imewasimamisha kazi watumishi wake 21 kwa tuhuma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusaidia ujangili wa nyara za Serikali. (HM)
Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya Polisi mkoani Singida, kumkamata ofisa wanyamapori katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida, kwa tuhuma za kupatikana na silaha mbili na nyara za Serikali, kinyume cha sheria.
Akitangaza hatua hiyo jana jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, alisema Serikali inasikitishwa na vitendo viovu vinavyofanywa na watumishi wake na haitavivumilia. "Tumesikitishwa na kitendo cha ofisa wanyamapori wilayani Singida kukamatwa na bunduki mbili na ndege aina ya Heroe 12 nyumbani kwake, hatua tuliyochukua ni kumsimamisha kazi na kufikishwa mahakamani," alisema na kuongeza:
"Wizara baada ya kufanya uchunguzi, imegundua kuwa kuna watumishi wanaoshirikiana na mtandao wa ujangili, hivyo imewasimamisha kazi watumishi 21 wa Idara ya Wanyamapori na tutachukua hatua zaidi."
Alisema kati ya watumishi hao, 11 wanatoka katika Kikosi cha Kuzuia Ujangili mkoani Arusha, wanne wanatoka Mkoa wa Rukwa katika Pori la Akiba la Lwafu, mmoja Kikosi cha Bunda, watatu Pori la Akiba la Maswa, mmoja Selous, na mwingine mapori ya Lupika, Lumesule na Lusangu.
Akifafanua kuhusu uhaba wa watumishi katika Idara ya Wanyamapori, Nyalandu alisema kwa zaidi ya miaka 10 wizara hiyo haikuwa ikiajiri watumishi hali inayosababisha kukosa watumishi wenye ujuzi.
"Tunajipanga kuajiri watumishi wengine wenye ujuzi na kuangalia maendeleo ya teknolojia hasa kwa kujifunza kwa wenzetu Afrika Kusini," alisema.
Kuhusu Operesheni Tokomeza Ujangili, alisema Serikali imeunda tume ya kimahakama itakayowahoji askari waliohusika na kurudisha taarifa. Hata hivyo alisema wako mbioni kuendelea nayo.
"Rais Jakaya Kikwete ameunda tume ya kimahakama na itatoa taarifa, ila sisi hatutalala, tutahakikisha kuwa tunapambana na ujangili ili kulinda nyara za Taifa," alisema Nyalandu.
Amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa wizara yake kwa kutoa taarifa zitakazowezesha kuwakamata wahalifu.
"Jitihada hizi siyo zetu wenyewe, tunashirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama. Tunawaomba wananchi washirikiane kulinda na kutoa taariza zitakazowezesha kukamatwa kwa wahalifu. Tunawaomba watumishi wetu wafanye kazi kwa moyo na uaminifu," alisema Nyalandu.
Mamlaka ya wanyamapori
Akiwa katika pori la akiba la Selous hivi karibuni, Nyalandu alieleza mkakati wa Serikali wa kuanzisha mamlaka ya wanyamapori ili kuwapa mamlaka watendaji wa sekta hiyo katika kutunza maliasili. Chanzo: Mwananchi

Chadema kumpinga Zitto Mahakama ya Rufani

zittokabwe1 e192c
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kiko katika harakati za kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, uliompa ushindi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zitto Kabwe. (HM)
Zitto ambaye pia ni Mbuinge wa Kigoma Kaskazini, juzi aliibuka mshindi katika maombi yake ya kuizuia Kamati Kuu (CC) ya chama hicho kumjadili na au kuchukua uamuzi wowote kuhusu uanachama wake, hadi kesi ya msingi kuhusu suala hilo itakapokuwa imesikilizwa.
Kadhalika, chama hicho kupitia kwa Mkurugenzi wake wa Mawasiliano na Uenezi, John Mnyika kimesema kinaendelea na utekelezaji wa uamuzi wa Kamati Kuu wa kutompa Zitto ushirikiano wa aina yoyote.
Wakili wa Chadema, Peter Kibatala, alisema jana kuwa japo wanauheshimu uamuzi wa Mahakama, hawajaridhika nao na kwamba wanakusudia kwenda Mahakama ya Rufani kuupinga.
"Ingawa uamuzi huu ni Interlocutory (uamuzi usiomaliza kesi), lakini sisi hatukuridhika nao. Hatukuridhika na uamuzi wa kutupilia pingamizi letu la awali, hati ya kiapo na hata amri yenyewe ya zuio la muda," alisema Wakili Kibatala na kuongeza:
"Kuna namna nyingi za kufanya kupinga uamuzi huo, kama vile kukata rufaa, kuomba marejeo au namna nyinginezo. Kwa hiyo kwa sasa tunaangalia namna bora ya kwenda Mahakama ya Rufani bila kuathiri matakwa ya kisheria."
Wakili Kibatala ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), alisema kuna haja ya kuiomba Mahakama ya Rufani kuuchunguza uamuzi huo kwa kuwa una athari si kwa Chadema tu, bali hata vyama vingine dhidi ya wanachama wake.
Kauli ya Mnyika
Mnyika kwa upande wake alisema kutompa ushirikiano Zitto ni uamuzi wa Kamati Kuu ambao ulitokana na hatua yake ya kwenda mahakamani kwa masuala ya chama, kinyume cha matakwa ya Katiba ya Chadema na Kanuni zake.
Mnyika alikuwa akirejea taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, baada ya kikao hicho akiwataka viongozi wa ngazi zote za chama hicho, wanachama, mashabiki na wapenzi wake, kutoshiriki wala kusaidia kwa namna yoyote mikutano yote ya nje, ndani au shughuli nyingine yoyote ya kisiasa itakayofanywa na Zitto na mawakala wake.
Ushindi wa Zitto
Katika maombi hayo namba 1 ya 2014, Zitto kupitia kwa Wakili Albert Msando, Zitto aliiomba Mahakama itoe zuio hilo la muda kwa CC ya Chadema, hadi kesi yake ya msingi namba 1 ya 2014 aliyoifungua mahakamani hapo itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
Awali, mawakili wa Chadema, Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu na Kibatala walipinga maombi hayo wakidai kuwa hayajakidhi matakwa ya kupewa zuio la muda.
Katika uamuzi wake juzi, Jaji John Utamwa alikubaliana na hoja za Wakili Msando kuwa maombi hayo yametimiza matakwa yote ya kupewa zuio hilo.
Maombi hayo ya Zitto yaliyotolewa uamuzi juzi yalitokana na kesi ya msingi aliyofungua mahakamani hapo Januari 2, 2014, dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema na Katibu Mkuu wa Chadema.
Katika kesi hiyo anaiomba mahakama ikizuie chama hicho, wakala wake na vyombo vyake vya uamuzi kumchukulia hatua zozote au kumjadili kuhusiana na uanachama wake, hadi hapo rufaa anayokusudia kuikata Baraza Kuu la chama hicho kupinga kuvuliwa nyadhifa, itakaposikilizwa.
Pia aliiomba Mahakama Kuu imwamuru Katibu Mkuu wa Chadema ampatie mwenendo na taarifa za CC za kumvua nyadhifa zake zote alizokuwa nazo ndani ya chama na iwazuie walalamikiwa kumwingilia katika utekelezaji wa majukumu yake kama Mbunge wa Kigoma Kaskazini. Kesi hiyo ya msingi imepangwa kutajwa mahakamani hapo Februari 13, mwaka huu. Chanzo: Mwananchi

Rasmu Ya Katiba Mpya Kwa Rais


Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Rasimu ya pili ya Katiba Mpya kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba wakati wa hafla ya kukabidhiwa rasimu hiyo iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.Rais Kikwete aliitaka Tume hiyo ya Katiba kuhakikisha kuwa Rasimu hiyo inawekwa kwenye mitandao yote ya kijamii ili wananchi waweze kuisoma na kuielewa na kuweza kutoa maoni yao kwa urahisi kupitia mitandaoni.
Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akipokea Rasimu ya pili ya Katiba Mpya kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba wakati wa hafla ya kukabidhiwa rasimu hiyo iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rasimu hiyo kwa Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Gharib Bilal mara tu baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rasimu hiyo kwa Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rasimu hiyo kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,Maalim Seif Shareef Hamad.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rasimu hiyo kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rasimu hiyo Rais Mstaafu wa awamu ya Pili,Mzee Ali Hasaan Mwinyi.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rasimu hiyo kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mzee Cleopa Msuya.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar,Mh. Pandu akipokea Rasimu hiyo.
Spika wa Bunge.
Jaji Mkuu.
Jaji Mkuu wa Zanzibar.
Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue.
Mwenyekiti wa Tume ya Katiba,Jaji Joseph Sinde Warioba akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya kukabidhi kwa Rais,Rasimu ya Pili ya Katiba iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee,jijini Dar es Salaam.Jaji Warioba alisema kuwa kulingana na idadi ya kura zilizopatikana kutoka kwa wananchi kuhusu uundwaji wa Serikali tatu, alisema kuwa idadi kubwa zaidi ni ya watu waliohitaji Serikali tatu kuliko walioipinga, hivyo Serikali tatu haipingiki ambapo kwa sasa itabaki ni kazi ya maamuzi ya Bunge la Katiba linalotarajia kuundwa mapema mwezi Januari mwakani.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mhe. Joseph S. Warioba mara baaada ya kuwasili katika viwanja vya Karimjee Hall kupokea Rasimu ya Pili ya Katiba. Kulia ni Mhe. Assaa Rashid, Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, 
 Rais Kikwete akisalimiana na Mhe Assaa Rashid, Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, 
 Rais Kikwete akisalimiana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu huku Jaji Mkuu wa Tanzania Bara Mhe Mohamed Chande Othman, Spika wa Bunge la Muungano Mhe Anne Makinda na Spika wa Zanzibar Mhe Pandu Ameir Kificho wakisubiri zamu zao
 Rais Kikwete akimuamkia  na Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi
 Rais Kikwete akimuamkia Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Cleopa David Msuya
 Meza kuu
 Sehemu ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba
 Jukwaa kuu la pili
 Sehemu ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba
 Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim akiwa na wajumbe wenzie wa Tume na maofisa wa serikali
 Dkt Asha Rose Migiro, Mama Amne Salim na Mama Warioba
 Sehemu ya wananchi walioshuhudia tukio hilo la kihistoria
 Wananchi wakiwa katika hafla hiyo
 Wananchi wakifuatilia hafla hiyo
 Watangazaji wa TBC wakiwa kazini kurusha live tukio hilo
 Baadhi ya wazee mashuhuri katika hafla hiyo. 
 Wadau mbalimbali
 Wadau katika hafla hiyo
 Sehemu ya viongozi wa vyama vya siasa
 Wadau wa habari 
 Wanasheria nguli, Mzee Mark Bomani na Profesa Issa Shivji wakiwa miongoni mwa wadau
 Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mhe Alfani Mpango akijumuika na wadau
 Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa na mabalozi
 Wadau na maafisa wa serikali
 Maafisa wa ofisi wa Masajili wa vyama
 Wadau
 Wadau na maafisa mbalimbali
 Makatibu wakuu
 Mawasiri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
 Mawaziri wa Bara na Zanzibar
 Mawaziri, wabunge na maafisa wa serikali
 Sehemu ya mawaziri wa bara na wa Zanzibar
 Msajili wa vyama vya siasa Jaji Mutungi (wa tatu kushoto) akiwa ameketi na wabunge na viongozi wa vyama mbalimbali 
 Sehemu ya waliohudhuria hafla hiyo
 Meza kuu ikimsikilia Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mhe. Joseph S. Warioba 
 Rais Kikwete akimkabidhi Sir George Kahama nakala ya Rasimu ya Pili ya Katiba
 Rais Kikwete akiwakabidhi Mzee Hassan Nassoro Moyo na Jenerali Sarakikya nakala ya Rasimu ya Pili ya Katiba
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein akisoma hotuba yake
 Rais Kikwete akihutubia
 Wabunge na wadau wengine wakifurahia hotuba ya Rais Kikwete
 Rais Kikwete, Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali wakiwapongeza wajumbe wa Tume kwa kazi nzuri
 Picha ya pamoja ya viongozi wakuu na wajumbe wa Tume
 Picha ya pamoja ya viongozi wakuu, wajumbe wa tume 
 Viongozi wakuu, viongozi wa vyama vya siasa na wajumbe wa Tume
 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akisalimiana na Mhe Tundu Lissu
 Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba 
 Rais Kikwete akiongea na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi na Mbunge wa Kuteuliwa Mhe James Mbatia
Nikiripoti kutoka hapa katika viwanja vya Karimjee ni mimi…. wa Mlimani TV
PICHA NA IKULU
SOMA RASIMU HIYO HAPO CHINI