Tuesday, June 25, 2013

Maisha Yana............

0 b49e9
Mwakaganga Village, Mbarali, Mbeya.

Mzee Mandela bado yuko hali mahututi

mandela 655d6


RAIS mstaafu wa Mandela Nelson Mandela, bado yuko hali mahututi ingawa madaktari wanadhibiti hali yake baada ya afya yake kuzorota mwishoni mwa wiki.
Taarifa kutoka ikulu ya rais zinasema kuwa Mandela angali yuko chini ya uchunguzi wa madaktari ambao wameweza kuidhibiti hali yake.
 Anaugua maradhi ya mapafu na amelazwa hospitalini kwa zaidi ya wiki mbili sasa.
Mapema leo familia yake ilimtembelea hospitalini, mzee Mandela ambaye anasifika kwa vita alivyopigana dhidi ya utawala wa wazungu nchini Afrika Kusini.
Amekuwa akiugua ugonjwa wa mapafu mara kwa mara na hii ni mara ya tatu kwa Mandela kulazwa hospitalini mwaka huu.
Rafiki na jamaa wameendelea kukusanyika katika hospitali alikolazwa Mandela mjini Pretoria kumtakia afya njema mzee Mandela.
Mmoja wa waliomtembelea Mandela , mfanyabiashara Calvin Hugo, aliawachilia huru njiwa weupe, kama heshima yake kwa Mandela anaeyendelea kuugua hospitalini.
Alisema kitendo chake kilikuwa ishara ya, hatua ya Mandela kuikwamua nchi ya Afrika Kusini kutoka kwa mkoloni.
Baadhi ya jamaa zake wamekusanyika nyumbani kijijini eneo la Qunu, kujadili kile wanachosema ni habari muhimu sana. Chanzo: bbcswahili

DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO


untitled2 61c7e
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia washiriki wa kutano, wakati akifungua rasmi Mkutano wa 24 wa mwaka wa nguvu za Atomiki Tanzania, wa Utafiti na Mfunzo ya ukuaji wa Teknolojia ya Sayansi ya Nyuklia, ulioanza leo Juni 25, 2013 katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha

untitled3 dfcdd
Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo

Monday, June 24, 2013

MAANDALIZI YA SABASABA MKOANI KAGERA KATIKA VIWANJA VYA CCM MJINI BUKOBA.



JESHI LA POLISI MKOANI RUVUMA LAKAMATA MENO 18 YA TEMBO.

Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma  Deusdedit Nsimeki akipanga maneno ya tembo kulingana na uneno /uzito kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Mwandishi wa habari wa katika Gazeti la Mtanzania Hamoni Mtega akiwa amenyanyua jino la tembo

————————————————– 


JESHI  la Polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kukamata meno ya Tembo  18 yenye uzito wa kilo 84 yenye  thamani ya Tsh216,000,000/ambapo meno hayo 18 ni sawa na dola 15 elfu za kimarekani pia ni sawa na Tembo tisa waliouwawa .

  Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake leo Kamanda wa polisi mkoani Ruvuma  Deusdedit Nsimeki amesema kuwa tukio hilo la kukamata meno hayo lilitokea Juni 20 Mwaka huu majira ya saa 3.00 usiku  katika kijiji cha Majala kata ya Nandembo iliyopo wilaya  ya Tunduru mkoani Ruvuma .

   Kamanda Nsimeki amesema kuwa  tukio hilo la kukamatwa kwa meno hayo ya tembo lilitokea  baada ya askari polisi wa wilaya hiyo kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema ndipo wao waliweka mtego wa kuwanasa watuhumiwa hao lakini bahati mbaya watuhumiwa hao walikurupuka na kuacha mizigo ya meno hayo iliyokuwa imefungwa kwenye mifuko tofauti tofauti.

    Alisema kuwa watuhumiwa waliokurupuka walikuwa wanne huku kila mmoja na baiskeli ambazo walikuwa wamebebea meno hayo na kwa upande wa watuhumiwa wa meno ya tembo kukurupuka bila kutiwa mbaroni na jeshi hilo limekuwa ni tukio la pili la kwanza  lilitokea katika  kijiji  cha Hanga wilayani Namtumbo na la pili ndiyo hilo la wilaya ya Tunduru zote za mkoani Ruvuma .

Aidha kamanda alisema kuwa jeshi la polisi linajitahidi kuwasaka watu ambao wamejificha na wanajihusha na matukio hayo ya ujangili kwa wanyama  na hasa tembo.

Pia ametoa wito kwa wananchi uendelea kushirikiana jeshi la polisi mkoani Ruvuma kwa kutoa taarifa za siri zitakazowezesha kukamatwa kwa wahusika wa vitendo vya uhalifu wa aina yoyote kwa sababu suala la ulinzi ni kila mmoja hivyo kunasoaswa kuwepo kwa ushirikiano wa karibu baina ya polisi na wananchi.
Picha na habari kwa hisani ya Demashonews.blogspot.com

SHEREHE ZA KUAPISHWA SKAUTI MKUU WA CHAMA CHA SKAUTI TANZANIA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM JUNI 23, 2013

 Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania mteule Mhe. Mwantumu Mahiza akisubiri kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijiandaa kuvishwa skafu na skauti kabla ya kumuapisha Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza akisubiri kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akivishwa skafu na skauti kabla ya kumuapisha Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza akisubiri kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 201

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi baada ya kumuapisha Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza baada ya kumuapisha Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi vitendea kazi Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza baada ya kumuapisha  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza baada ya kumuapisha  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha na  Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza baada ya kumuapisha  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim, Jaji Kiongozi Fakih Jundu na Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza baada ya kumuapisha  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha na  Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza pamoja na viongozi wa maskatu na skauti  baada ya kumuapisha  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha na  Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza na familia yake baada ya kumuapisha  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha na  Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza pamoja na waheshimiwa wabunge ambao ni maskauti  baada ya kumuapisha  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na skauti Ismail Aden Rageh na wabunge maskauti  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha na  Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza pamoja na wanachama wa UWT wilaya ya Ilala  baada ya kumuapisha  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha na  Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza na viongozi wa skauti nchini baada ya kumuapisha  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na skauti Livingstone Lusinde ambaye pia ni Mbunge wa Mtera  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013

MMILIKI WA AC MILAN ATUPWA JELA MIAKA SABA KWA KUKUTWA NA HATIA YA KUFANYA NGONO NA KIBINTI CHA MOROCCO

Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
MMILIKI wa AC Milan, Silvio Berlusconi amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela na kufungiwa maisha kufanya kazi katika ofisi za umma baada ya kukutwa na hatia ya kumlipa binti mdogo afanye naye ngono katika moja ya pati zake za ‘bunga bunga’.
Waziri huyo Mkuu wa zamani wa Italia, Berlusconi, mwenye umri wa miaka 76, alimlipa binti mdogo wa Morocco, Karima El Mahroug, anayekwenda kwa jina la utani, Ruby, kwa ajili ya ngono na baadaye akajaribu kumbambikizia kesi ya wizi kwa kuwapigia simu Polisi na binti huyo akakamatwa. Berlusconi na mwanamke huyo wamekanusha kufanya ngono.
Mwendesha mashitaka alipendekeza afungwe miaka sita kwa kuzini ni binti mdogo na matumizi ya nguvu, lakini majaji watatu wa kike katika Mahakama ya Jijini Milan jana walitaka afungwe muda mrefu zaidi, miaka saba. 
Verdict: Italy's former Prime Minister Silvio Berlusconi, pictured last year, was found guilty today of paying Moroccan Karima El Mahroug, nicknamed Ruby the Heart-stealer, for sex at a 'bunga bunga' party
Verdict: Italy's former Prime Minister Silvio Berlusconi, pictured last year, was found guilty today of paying Moroccan Karima El Mahroug, nicknamed Ruby the Heart-stealer, for sex at a 'bunga bunga' party
Mfungwa: Mmiliki wa AC Milan, Silvio Berlusconi (juu) amekutwa na hatia ya kumlipa binti mdogo wa Morocco, Karima El Mahroug wafanye naye ngono
San Siro: Berlusconi is the owner of AC Milan, pictured here with former maanger Carlo Ancelotti in 2007
San Siro: Berlusconi ni mmiliki wa AC Milan, hapa akiwa katika picha ya pamoja na kocha wa zamani wa klabu hiyo, Carlo Ancelotti mwaka 2007

Berlusconi pia amefungiwa maisha kufanya kazi katika ofisi za umma baada ya Waziri huyo Mkuu wa zamani kukutwa na hatia leo. 
Lakini mfungwa huyo anaweza kukata rufaa mara mbili kabla hajamaliza kifungo chake, ambayo inaweza kuchukua miezi au miaka.
Maana yake hatatumikia kifungo chake hadi ashindwe rufaa zake. 
Klabu yake ya AC Milan – ambayo amekuwa Rais wake kwa vipindi vitatu tofauti tangu mwaka 1987 – inayoundwa na nyota kadhaa akiwemo Mario Balotelli – ilimaliza katika nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu ya Italia, Serie A msimu uliopita ikizidiwa pointi 15 nyuma ya wapinzani, Juventus.
Sentenced: President of the court Giulia Turri (centre) read out the damning verdict
Kifungo: Rais wa Mahakama, Giulia Turri (katikati) akisoma hukumu

Baada ya hukumu, Mwanasheria wa Berlusconi, Niccolo Ghedini, mara moja alitangaza kukata rufaa akisema hukumu hiyo ni kama ilivyotarajiwa, haikutenda haki.
“Hii ni kinyume cha uhalisia,” Ghedini aliwaambia Waandishi wa Habari nje ya Mahakama. “Nimetulia kwa sababu nimekuwa nikisema kwa miaka mitatu kwamba kesi haiwezi kuendeshwa hapa,” alisema Ghedini. 
Alias: Karima el-Mahroug is better known as 'Ruby the Heartbreaker'
Kimwana:
Alisema pati hiyo ya chakula cha usiku ilikuwa kwa ajili ya watu maaum; Mwendesha mashitaka amesema walifanya ngono na mwanamke huyo aliyelipwa kuhudhuria.
Hata kama Berlusconi alikuwa anamjua mwanamke huyo katikati ya kesi hiyo, Karima el-Mahroug, anafahamika vyema kwa jina lake la utani, Ruby the Heart Breaker, ametoa ushahidi.
Alikuwa ana umri wa miaka 17 wakati huo anadaiwa kufanya kitendo hicho, lakini sasa amefikisha miaka 24. wakati umri wa kufanya ngono Italia ni miaka 14, na ni kinyume cha sheria kumlipa binti aliye chini ya umri wa miaka 18 kwa ajili ya ngono.
El-Mahroug aliitwa kwa utetezi, lakini akashindwa kutokea kwa sababu kadhaa,kuchelewesha hukumu. Timu ya Berlusconi mara moja ikamengua katika orodha ya mashahidi.
Statement: Silvio Berlusconi's lawyer Niccolo Ghedini speaks to reporters outside the courthouse in Milan, Italy, today after judges found him guilty of having sex with a minor
Maelezo: Mwanasheria wa Silvio Berlusconi, Niccolo Ghedini akizungumza na Waandishi wa Habari nje ya Mahakama jana Jijini Milan, Italia.

BAYERN MUNICH WAMTAMBULISHA RASMI PEP KATIKA MKUTANO MZITO ALLIANZ ARENA…JUPP HEYNCCKES SAFARI YAIVA!!

Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Mabingwa wa mataji matatu, Bayern Munich wamemtambulisha kocha wao mpya, Pep Guardiola leo katika Mkutano na Waandishi wa Habari, The Bavarians wakijiandaa kuendelea kutamba katika soka ya nyumbani na Ulaya.
Kocha huyo wa zamani wa Barcelona amesema yuko tayari kukabiliana na changamoto za kufundisha timu iliyofanya vizuri msimu uliopita chini ya Jupp Heynckes, ikishinda mataji ya Ligi Kuu ya nyumbani na makombe mawili, pamoja na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
“Lazima nikubali mlinganisho,” alisema Guardiola, akiwa katika vazi nadhifu la suti ya vipande vitatu ya rangi ya kijivu akizungumza Kijerumani kwenye Mkutano uliofanyika ukumbi wa mikutano wa klabu, Allianz Arena.
“Lazima niwe tayari kuishi na hiyo. Nipo chini ya shinikizo, wazi, lakini nafahamu hili na nakubali changamoto hii bila woga na ndiyo maana mimi ni kocha,”alisema.
Guardiola, ambaye aliyeshinda mataji 14 katika miaka minne ya kuwa na Barcelona, usajili wake ni mkubwa Bayern na hasa ikizingatiwa anahamia timu iliyofanya vyema. Alitumia mwaka wake mzima baada ya kuacha kazi Hispania mwaka 2012, kwa kupumzika New York, Marekani.
“Kitu nachofikiria kwa sasa ni zawadi, baraka kuwa hapa na Bayern,”alisema kocha huyo Mspanyola, aliyesaini Mkataba wa miaka mitatu.
Pressure? Pep Guardiola has just taken over at European champions Bayern Munich
Shinikizo? Pep Guardiola anakuwa kocha wa mabingwa wapya wa Ulaya, Bayern Munich
Confident: And he needs to be - Guardiola has big shoes to fill
Kujiamini: Guardiola akizungumza leo
Grand gathering: Many were present to witness Guardiola's unveiling as Bayern boss
Waliohudhuria mkutano huo wa kutambulishwa Guardiola bosi mpya BayernFabulous four: Guardiola was joined by Matthias Sammer, Karl-Heinz Rummenigge and Uli Hoeness

Wanne mashuhuri: Guardiola aliungana na Matthias Sammer, Karl-Heinz Rummenigge na Uli Hoeness
Aisema sababu ya kwanza iliyomfanya akubali ofa ya kuifundisha Bayern ni wachezaji wa klabu hiyo na historia yake.
Welcome, Pep! The manager already looks comfortable in his surroundingsKaribu, Pep! Kocha tayari anajisikia nyumbani katikati ya watu
Big reputation: Guardiola's success at Barcelona means many have high hopes for him in Germany Kiroho safi? Guardiola akiwa na kocha anayeondolewa Bayern, Jupp Heynckes.

Maisha Yana........................

MAHELA ba515

Marekani yatoa onyo kali kwa msafara wa Rais Obama Dar

obama1 51ff9
Rais wa Marekani, Barack Obama
LICHA ya ujumbe wa Rais wa Marekani, Barrack Obama kutarajiwa kufikia katika hoteli kubwa zenye hadhi wakati kiongozi huyo atakapowasili nchini Julai Mosi mwaka huu, Ikulu ya Marekani imetoa tahadhari ya vyakula ambavyo hawatakiwi kuvigusa wakiwa nchini ikiwa ni pamoja na kutumia maji ya bomba.
Mbali na tahadhari hiyo, ziara hiyo ya Obama itakuwa na ulinzi mkubwa ambao pengine haujawahi kutokea katika historia ya viongozi wa nje wanaotembelea Tanzania kwani utahusisha idadi kubwa ya magari, ndege za kijeshi na meli kubwa ya kivita ambazo zitakuwa zikifanya doria karibu na pwani ya Tanzania.
Tahadhari za matumizi ya chakula, maji na nyinginezo zimetolewa katika nchi zote tatu za Afrika ambazo Obama atatembelea, kila moja kwa jinsi Wamarekani hao wanavyoitathmini.
Rais Obama atatembelea nchi za Tanzania, Senegal na Afrika Kusini.
Ulinzi

Vyombo vya usalama vya Marekani vimejipanga kuhakikisha ziara ya kiongozi huyo haivurugwi kwa namna yoyote ile. Tayari ndege za jeshi zilizobeba magari ya akiba 56, yakiwemo 14 aina ya ‘Cadillac One’ maalumu kwa ajili ya kiongozi huyo, yamewasili katika nchi hizo tatu za Afrika atakazotembelea.

Kwa mujibu wa gazeti la Washington Post la Marekani, ndege hizo pia zimebeba malori matatu ambayo yamesheheni karatasi maalumu za kuzuia risasi kupenya kwenye vioo, zitakazobandikwa kwenye madirisha ya hoteli ambazo Rais Obama na ujumbe wake watafikia.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, mamia ya mashushushu wa Marekani tayari wako katika nchi hizo. Meli maalumu za kubeba ndege za kivita, maarufu kwa jina la ‘amphibious ship,’ ikiwa na hospitali maalumu na yenye vifaa vyote itaweka nanga baharini, jirani na nchi atakayokuwa Rais Obama, tayari kukabiliana na dharura yoyote itakayotokea. Gazeti hilo liliandika kuwa ndege za kivita za Marekani zitakuwa zikipeana zamu kufanya doria kwa saa 24, katika anga la nchi ambayo Rais Obama atakuwepo, iwapo ndege za ‘adui’ zitakaribia eneo linaloitwa ‘anga ya rais.’ Kwa mujibu wa gazeti hilo, ziara ya Rais Obama aliyoifanya hivi karibuni katika nchi za Ujerumani na Ireland Kaskazini, japo kulikuwa nagharama kwa walinzi, lakini safari za nchi za Afrika zimeelezwa kuwa na gharama kubwa zaidi.
Tahadhari

Kwa mujibu wa taarifa ya maelekezo ya Ikulu ya Marekani, ambayo Mwananchi imepata nakala yake, watu watakaokuwa kwenye msafara wa Obama wametakiwa kutotumia kachumbari. Pia imewataka kutumia maji ya chupa zaidi.

“Kutokana na mfumo wa maji uliopo, tunashauri watu wetu kutumia maji ya chupa zaidi kwa kunywa na hata kwa kupiga mswaki,” ilisema taarifa hiyo.

Kwa kuelewa fika tatizo la ugonjwa wa malaria nchini, ujumbe wa Obama umeshauriwa kutumia dawa ya mbu ya kupaka na kupuliza inayoitwa Deet.

Deet ni dawa maarufu huko Marekani na ikiwa katika aina tofauti ikiwamo ya kupaka na kupuliza na imekuwa ikitumiwa na jeshi la Marekani kwenye vita mbalimbali tangu miaka ya 1940 kabla ya kuanza kutumiwa na raia mwaka 1957.
ATM nazo noma
Pia watu watakaokuwa kwenye msafara wa Rais Obama wametakiwa kuhakikisha wanatumia mashine za kutolea fedha (ATM) zilizoko karibu na hoteli watakazofikia.
“Kuna tatizo la uhalifu kwa hiyo siyo vizuri kutumia ATM ambazo ziko katika sehemu zisizo salama. Pia katika kipindi watakachokuwa Tanzania watu wanapaswa kutumia teksi ambazo zimeidhinishwa na hoteli.
“Pia siyo vizuri kuacha kompyuta ya fedha kwenye vyumba mtakavyolala. Pia kina mama wanapaswa kuchukua tahadhari ya mabegi yao watakapokuwa wanapita mitaani,” ilitahadharisha taarifa hiyo. Chanzo: mwananchi.co.tz

Magazeti


DSC 0022 bef87
DSC 0023 19ea4
DSC 0024 7e9a0
DSC 0025 ebea1
DSC 0026 37964
DSC 0027 611a2
soma mengine zaidi....

DSC 0028 b5df8
DSC 0029 11337
DSC 0030 eb20b
DSC 0031 b0364
DSC 0032 9a38c
DSC 0033 6d8da
DSC 0034 5866c
DSC 0035 c9db0
DSC 0037 80c42