Monday, April 22, 2013

Huu ndio mzimu unaoimaliza CCM

 

k1Na: John Bukuku, Morogoro

HAKIKA kwa muda mrefu Chama Cha Mapinduzi(CCM), kimekuwa kikijaribu kujiweka katika mazingira mazuri zaidi kisiasa. Hata hivyo licha ya kufanikiwa kwa kiwango fulani lakini bado kuna maeneo ambayo yamekuwa kikwazo cha CCM kushindwa kutimiza lengo lake. Ni wazi mzimu ambao unaimaliza CCM hivi sasa ni
hili la baadhi ya watendaji wa Serikali kwa ngazi mbalimbali kuonekana kikwazo cha utekelezwaji wa Ilani ya chama hicho ambayo inataka maisha bora kwa wananchi wake.
Utafunwaji wa fedha za umma umekuwa mkubwa katika nchi hii hali inayofanya katika halmashauri mbalimbali Tanzania kujikuta ikishindwa kufanikisha maendeleo.Kisa kuna kundi la watu ambalo lipo ndani ya Serikali kwa ajili ya kukwamisha juhudi za CCM katika kufikisha maendeleo kwa watu.
Moja ya malalamiko ya Wana-CCM katika maeneo mbalimbali ya nchini ni hili la ubadhirifu wa fedha ambazo zinatolewa na Serikal Kuu na kwenda kwenye halmashauri kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa Ilani ya CCM ambayo ndio imeunda Serikali.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Abdulrahaman kuanzia Aprili 14 hadi Aprili 21(Jumapili) , alikuwa akifanya ziara katika Mkoa wa Morogororo ambapo amezunguka katika wilaya zote za mkoa huo.
Moja ya kero kubwa aliyokutana nayo ni hii ya fedha za umma kuliwa na baadhi ya wajanja wachache ambao hawaitakii mema CCM kwa kuwa chanzo cha kukwamisha maendeleo.
Kinana anaonesha wazi kutofurahishwa na hali hiyo ambayo inafanywa na watendaji wasiokuwa waamini ambao wao wanachojua ni kufanya ubadhirifu wa fedha za umma ambapo katika hilo anatoa agizo kwa viongozi wa CCM kuwa makini nao na kufuatilia karibu.
Kwa lugha harisi Kinana anataka Wana-CCM kwa ngazi mbalimbali kuibana Serikali pale ambapo watendaji wao wanaonekana kufanya mambo kinyume na Ilani ya uchaguzi inayozungumzia maendeleo ya watu.
Akiwa katika wilaya ya Mvomero wakati wa ziara yake,Kinana anakutana na malalamiko makubwa ya wana-CCM wakiwamo madiwani wa Halmashauri ya wilaya hiyo ambao wamechoshwa na ubadhirifu wa fedha uliofanywa na moja ya watendaji wa halmashauri.
Wanachama hao wanakwenda mbali zaidi na kuamua kumueleza Kinana kuwa kwa hali iliyofikia na namna ambavyo mtendaji huyo analindwa licha ya kula fedha za umma huenda analindwa na watu waliowaita ‘Wakubwa’.
Kutokana na hali hiyo Kinana anaamua kutoa agizo la kuhakikisha wabadhirifu wa fedha za umma wakiwemo waliohusika kutafuna fedha za Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero zaidi ya sh.bilioni moja wanachukuliwa hatua.
“Hatutakubali kuona baadhi ya watendaji wanashindwa kutekeleza majukumu yao.Kazi yao imebaki kukwamisha utekelezaji wa ilani ya chama changu.
Hatuwezi kukaa kimya, tutaibana Serikali na pale ambapo tutaona ufumbuzi wake unahitaji mjadala wa kina tutakwenda kuzungumza haya kwenye Kamati Kuu ya CCM ili kupata ufumbuzi wake,”anasema.
Mbali ya Kinana kutofurahishwa na watendaji wa Serikali ambao wanakwamisha maendeleo ya wananchi kwa kula fedha, anatumia nafasi hiyo kuwageukia viongozi wa CCM ambao nao wanashindwa kusimamia majukumu yao.
Anasema katika maeneo ambayo amepita katika ziara yake yapo mambo mengi yanayolalamikiwa lakini la viongozi wa CCM kutowajibika ipasavyo nalo ni tatizo lingine kwa chama na lazima hatua madhubuti zichukuliwe kurudisha heshima ya chama .
Kwa mazingira hayo ili CCM kupambana na mzimu huo unaokwamisha kasi ya maendeleo ni wakati muafaka kwa Wana-CCM kutofumbia macho madhambi yanayofanywa na baadhi ya watendaji wa Serikali.
Ni jambo baya sana wakati CCM inataka kutatua kero za wananchi lakini kuna kundi ambalo lipo kwa ajili ya kukwamisha kasi hiyo ya kimaendeleo.Inasikitisha na kama Mtanzania nina haki ya kutoa maoni yangu kwa mustakabali wa taifa langu.

JK AKAGUA UJENZI WA NYUMBA ZA WAALIMU MBOGA SEKONDARI

  • 8E9U7250
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ujenzi wa nyumba za waalimu katika shule ya Sekondari ya Mboga, iliyopo kata ya Msoga wilayani Bagamoyo jana(Jumapili). 8E9U7357
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimwelekeza  jambo Diwani wa Kata ya Msoga Bwana Mohamed Mzimba wakati Rais alipotembelea shule ya Sekondari ya Mboga,kata ya Msoga wilayani Bagamoyo. picha na Fredy Maro
8E9U7421
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mboga kata ya Msoga leo wakati Rais alipotembelea shule hiyo leo kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba za waalimu shuleni hapo.(picha na Freddy Maro)

Saturday, April 20, 2013

Maisha Mazuri Kama Haya

Maisha Ya................................

IMAG0136 874ec
Picha na Iddy Allute akiwa mwisho wa Reli Kigoma

Magazeti

1 eeb14

2 eaea4
3.1 5d302
3 84368
4.1 2324d
4 c2af0
5 8fdbf
6.0 33e4d
6.01 a148d
6.1 3aaae
7 87be6
9 1c657
 

RAIS KIKWETE AKUTANA NA RAIS WA SHIRIKISHO LA WAFANYABIASHARA NA WENYE VIWANDA LA UTURUKI (TUSKON) NA UJUMBE WAKE LEO

 

tu1
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Rais wa Shirikisho la Wafanyabiashara na wenye viwanda la Uturuki (TUSKON) Bw. Rizanur Meral na ujumbe wake  leo April 19, 2013 Ikulu jijini Dar es salaam
tu2

KATIBU MKUU KIONGOZI, BALOZI OMBENI SEFUE AKUTANA NA BALOZI WA UINGEREZA NCHINI

  • omb2
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika mazungumzo na balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe Diana Melrose aliyemtembelea leo April 19, 2013 ofisini kwake Ikulu jijini Dar es salaam. mazungumzo hayo yalihusu maswala mbalimbali ya ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.
omb4
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akisalimiana na Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Uingereza (DFID) nchini Bw. Elliot Marshall aliyeongozana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe Diana Melrose (katikati) aliyemtembelea leo April 19, 2013 ofisini kwake Ikulu jijini Dar es salaam. mazungumzo hayo yalihusu maswala mbalimbali ya ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.
                                                      PICHA NA IKULU

Thursday, April 18, 2013

Nyongeza ya mishahara 30,000/-
•  Kima cha chini sasa 200,000/-

Na Martin Malera, Dodoma
 
WAKATI Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani, amekataa kutaja nyongeza ya mishahara ya kima cha chini kwa madai kuwa ni siri, imebainika kuwa mishahara hiyo imeongezeka kwa sh 30,000 tu.

Nyongeza hiyo inafanya kima cha chini cha mishahara ya watumishi wa umma, kufikia sh 200,000 kutoka sh 170,000 za mwaka wa fedha uliopita 2012/2013.

Baadhi ya wabunge walio kwenye Kamati ya Kudumu ya Katiba, Sheria na Utawala iliyokuwa ikijadili kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, waliliambia gazeti hili kuwa kima cha chini cha mshahara kimeongezeka kwa sh 30,000.

Hata hivyo, wakati akifanya majumuisho ya wizara yake jana, Waziri Kombani licha ya baadhi ya wabunge kumtaka atangaze kiwango kilichoongozeka, alisema kuwa hawezi kufanya hivyo kwani mshahara wa mtu ni siri.

“Kuhusu masilahi ya watumishi wa umma. “Hapa msinilazimishe kima cha chini, hapana. Hata sisi wabunge tunapoona kwenye magazeti yakitangaza mishahara yetu, hatufurahi kwa sababu mshahara ni siri yako,” alisema Kombani.

Waziri alirejea kauli yake juzi wakati akiwasilisha mwelekeo wa bajeti ya wizara yake kwamba kwa mwaka wa fedha 2013/2014 serikali imetenga sh trilioni 4.7.

Kiasi hicho ni kwa ajili ya nyongeza ya mishahara na kugharamia mishahara kwa watumishi wa Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na Wakala wa Taasisi za Serikali.

Kwa mujibu wa Waziri Kombani, kiasi hiki cha sh trilioni 4.7, pia kitatumika kugharamia ajira mpya 61,915, upandishwaji vyeo na nyongeza za kawaida za mishahara za mwaka, pamoja na nyongeza za mishahara kuanzia Juni 2013.

Mwaka wa fedha uliopita 2011/12, serikali ilitenga sh trilioni 3.7 ambapo mshahara wa kima cha chini uliongezeka kwa sh 20,000 na kufanya kima cha chini kupanda kutoka sh 150,000 hadi sh 170,000.

Hata hivyo Waziri Kombani aliwataka watumishi kuwajibika kwani wapo wanaolalamikia kutaka nyongeza ya mishahara, lakini hawataki kuwajibika.
Waziri Kombani alisema serikali imeandaa operesheni maalumu ya kufanya uhakiki wa vyeti vya watumishi wote nchini ili kubaini walioingia kazini kwa kutumia vyeti vya kughushi.

Alisema wapo baadhi ya waliotumia vyeti vya marehemu na wengine ndugu zao ambao pia wameajiriwa katika majina mawili ya watu wanaofanana.

Wakati serikali ikiongeza mishahara kwa kiwango kidogo, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), limekuwa likipendekeza kima cha chini kiwe sh 300,000 na katika mwaka huu wa fedha, imependekeza kima cha chini kiwe sh 400,000 ili kukabiliana na gharama za maisha zilizoongezeka mara dufu. 





AJALI YA GARI LILILOBEBA BIA MJINI BUKOBA KATA YA RWAMISHENYE




CCM yatikisa Gairo, Morogoro

1. KINANA AKIHUTUBIA GAIRO JIONI HII 71472
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana  akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara jioni hii kwenye uwanja wa shule ya msingi Gairo B, Gairo, mkoani Morogoro.

2.NAPE AKIHUTUBIA e7530
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye  akihutubia mkutano wa hadhara wa CCM kwenye  uwanja a shule ya Msingi Gairo B, mjini Gairo mkoani Morogoro jioni hii. Chanzo: Bashir Nkoromo

.wanajumuiya MUCE wapatiwa mafunzo ya jinsi ya kuzima moto

069 e0b4c
Insp. Kennedy Komba  Mkuu wa kituo cha zimamoto Iringa akitoa mafunzo ya uzimaji moto wa awali kwa wanafunzi  na wafanyakazi mbalimbali katika chuo kikuu cha mkwawa

083 61fab
Mmoja wa askari wa jeshila zimamoto mkoani iringa akielekeza namna ya kuzima moto kwa kutumia Kifaa cha kuzimia moto (fire extinguisher) Chuoni mkwawa.


100 b1b37
Zurufa Adamu  muhudumu  katika ofisi za Chuo  kikuu cha Mkwawa akifanya majaribio ya uzimaji moto katika kuhitimisha mafunzo ya siku tatu waliopatiwa.

108 ee58d
Insp. komba akielekeza namna ya kuzima moto sehemu ya wazi na mbinu zake.

109 25930
Zoezi la uzimaji moto likiendelea. Chanzo: Said Ng'amilo.

Mamlaka Ya Mawasiliano Na Makampuni Ya Simu Yatoa Tamko

2 9f498
Mkurugenzi wa Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof JOHN NKOMA  mapema leo asubuhi akitoa tamko juu ya usajili wa namba za simu za mkononi.


3 013c6
Mkurugenzi wa Vodacom RENE MEZA akisisitiza umuhumu wa kusajili namba za simu za mkononi.

4 2b0b3
Mkurugenzi wa Airtel SUNIL CALASO akifafanua jambo kwenye mkutano na waandishi wa habari juu ya tamko la usajili wa namba za simu za mkononi.
5 507cd
Mkurugenzi wa Zantel PRATAP GHOSE akizungumzia juu ya tamko la pamoja kuhusu usajili wa simu za mkononi.
Mapema leo asubuhi mkurugenzi wa  mamlaka ya mawasiliano nchini ametoa tamko la pamoja lililo azimiwa kwa kushirikiana na makampuni ya simu kwamba watumiaji wote wa simu za mkononi ambao hawaja sajili namba zao wafanye hivyo mara moja,kwani utaratibu unao fuata hivi sasa ni kufunga namba zote ambazo hazija sajiliwa,
Akifafanua zaidi amesema kwamba ni kosa la jinai kutumia namba ya simu isiyo sajiliwa na adhabu yake ni faini ya shilingi laki tano au kifungo cha miezi mitatu jela.
Mwisho amewataka  wananchi kuhakiki usajili wao kwa kupiga namba nyota 106 alama ya reli kutoka  katika simu zao za mkononi kwa mtandao wowote.
mtumiaji utapata ujumbe wa taarifa zako za usajili,na kama taarifa si sahihi tafadhali wasiliana na kampuni husuka haraka sana.

Maisha Yanaendelea

bora safari bab8d
Hii ni zaidi ya mshikaki, mbuzi watano na binadam wawili

Magazeti




  • 1 d1fb6


    2 3307b
    3 3cf41
    4 b36d8
    5 cd427
    6 e7756
    7 2ab60
    8 d74fe
    9 d2ab2
    10 f6226
    11 23e63
    12 4b97e

    14 327a5
    15 1029e
    16 a3d46

    18 a2f4e