Saturday, October 27, 2012

UCHAFUNZI WA MAZINGIRA ZIWA VICTORIA UNATISHA



Wanyama aina ya Punda wakiwa wamebeba mchanga uliokuwa unachimbwa katika ufukwe wa ziwa victoria kwenye mwalo wa Igombe jijini mwanza shughuli nyingi za kibinadamu zinazofanyika katika mwalo huo zinachangia uharibifu wa mazingira


wanahabari kutoka mikoa mbalimbali ya tanzania bara na visiwani wakishuhudia uharibifu wa mazingira baada ya mafunzo ya siku nne mkoani Mwanza

Mwezeshaji wa mafunzo hayo ya uandishi wa habari za mazingira Bw. Deo Mfugale akiwaongoza wanahabari wakati wa ziara ya mafunzo mwalo wa Ibombe ikiwa ni hatua ya mwisho ya mafunzo hayo.

MNYAUKO BACTERIA WATISHIA USALAMA WA NDIZI KAGERA

UGONJWA unaoshambulia migomba wa mnyauko bacteria umeanza kuathiri upatikanaji wa ndizi kwenye maeneo mbalimbali yaliyoko mkoani Kagera.

Ugonjwa huo unasambaa kwa kasi hasa kwenye maeneo ya wilaya za Muleba na Karagwe ambayo uzalisha  ndizi nyingi mkoani Kagera na maeneo mengine ya wilaya za Bukoba na Misenyi.

Hali ya ugonjwa huo unaoshambulia migomba wa mnyauko bacteria imechangbia kupunguza uzalishaji wa ndizi mkoani Kagera jambo ambalo limechangia kupanda kwa bei ya ndizi zinapopelekwa kwenye masoko.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kwamba kwenye soko kuu la Bukoba ndizi kubwa inauzwa kwa wastani wa kati shilingi 15,000 hadi 20,000 ambapo miaka iliyopita ndizi kubwa zilikuwa zinauzwa kwa wastani wa kati ya shilingi 6,000 hadi 8,000.

Kupanda kwa bei ya ndizi iliyochangiwa na ugonjwa wa mnyauko bacteria wa migomba kumewalazimisha baadhi ya wakazi wa mkoa wa Kagera ambao hutegemea ndizi kama chakula chao kikuu kubadilika ambapo sasa wanalazimika kula ugali na wali.

Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Kagera wamelazimika kubadili fikira zao za kudhani kuwa ndizi ndicho chakula kikuu baada ya kushindwa kumudu gharama za kununua ndizi kwenye masoko ambazo bei yake ni kubwa.

Baadhi ya wakulima bora wa migomba mkoani Kagera ambao mashamba yao yameathirika kutokana na ugonjwa wa mnyauko bacteria wa mogomba ni pamoja kamishina mstaafu wa jeshi la polisi Alfred Tibaigana.

Kamishina Tibaigana shamba lake liko katika kijiji cha Buganguzi wilayani Muleba limeathirika sana, Mkulima huyu kabla ya ugonjwa huu alikuwa na uwezo wa kuzalisha wastani tani 40 za ndizi kwa wiki ambapo sasa anazalisha wastani wa tani zisizozidi 10 kwa wiki.

Aidha, baadhi ya wakulima mkoani Kagera wameitahadharisha serikali kuchukua hatua za haraka za kuthibiti ugonjwa huu unaosambaa kwa kasi ili zao la ndizi mkoani Kagera lisibaki kwenye vitabu vya historia.

JK Katika Kikao Cha Kazi



 Wajumbe wakichangia katika kikao cha kazi (retreat) cha siku tatu cha Mawaziri, Naibu Mawaziri na maofisa waandamizi wa serikali wanaokutana kujadili mikakati endelevu na utekelezaji wa sasa na wa baadaye katika Ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha kazi (retreat) cha siku tatu cha Mawaziri, Naibu Mawaziri na maofisa waandamizi wa serikali wanaokutana kujadili mikakati endelevu na utekelezaji wa sasa na wa baadaye katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma. Pamoja naye meza kuu ni Makamu wa Rais Dk. Mohamed Ghalib Bilali (kulia) na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.



 Rais Jakaya Mrisho kikwete na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda wakipitia Waraka wa Utumishi Namba 5 wa mwaka 2009 kuhusu matumizi bora na salama ya vifaa na mifumo ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEKNOHAMA) serikalini wakati wa kikao cha kazi (retreat) cha siku tatu cha Mawaziri, Naibu Mawaziri na maofisa waandamizi wa serikali  kujadili mikakati endelevu na utekelezaji wa sasa na wa baadaye katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma.



PICHA NA IKULU

Magazeti Magazeti



















Monday, October 22, 2012


RAIS KIKWETE AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA KENYA LEO IKULU DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa  Jakaya Mrisho Kikwete ametaka wananchi wa Kenya wapewe nafasi ya kuamua ni viongozi gani wanawataka katika Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Machi mwakani.
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa wananchi wa Kenya wanayo haki ya msingi kabisa kuamua hatma ya taifa lao katika Uchaguzi Mkuu huo.
Mheshimiwa Rais aliyasema hayo leo Oktoba 21, 2012 alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa wabunge wa vyama mbalimbali vya siasa vya nchini Kenya uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam.
Ujumbe huo uliongozwa na Naibu Waziri Mkuu wa Kenya na Waziri wa Fedha Mhe. Uhuru Kenyatta ambaye pia ni Mwenyekiti wa  chama cha TNA na Waziri wa Sheria wa Kenya Mhe Eugene Wamalwa wa chama cha New Ford Kenya. Wote wawili ni wagombea wa nafasi ya Urais katika uchaguzi ujao.
Wengine katika msafara huo walikuwa ni Naibu Waziri wa Afya na mbunge wa Mombasa Mhe. Kambi Kazungu, Mbunge wa kuteuliwa wa chama cha TNA  Bi Rachel Shebesh, na Mbunge wa Kajiado kwa tiketi ya TNA Moses ole Sakuda na mbunge wa zamani Mhe Abdullahi Alli.
Rais Kikwete aliwapongeza kwa kuamua kufanya kazi kwa pamoja licha ya kuwa watakuwa  washindani katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu huo.
Mheshimiwa Rais ameitakia heri nchi ya Kenya katika uchaguzi huo ujao, na kusisitiza kwamba nchi hiyo ya jirani ina umuhimu katika mustakabali wa kiuchumi kwa nchi  za Afrika Mashariki.
Rais Kikwete wakati huo akiwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) alikuwa miongoni mwa viongozi walioshughulika sana kutafuta ufumbuzi wa ghasia na vurugu zilizozuka kufuatia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2007 nchini Kenya.
Rais Kikwete alikaa siku tatu nchini Kenya akitafuta usuluhishi wa vurugu hiyo ya kisiasa nchini humo, ambayo katika mazungumzo yake leo ameyataja kama ajali iliyolipata Taifa la Kenya, na ambayo majirani wake hawaitarajii kutokea katika uchaguzi ujao.
Imetolewa na:
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS
DAR ES SALAAM,


  IJUWE BARUA KUTOKA KANDA YA ZIWA-Kipindi Kipya cha Television Channel ten! Kila jumapili Saa 12;00 jioni

Ndugu  unaombwa kutazama kipindi kipya cha Television kiitwacho "Barua kutoka kanda ya Ziwa" kila siku ya Jumapili saa 12:00 Jioni channel ten .Kipindi hiki  kimeishanza kurushwa
Kipindi hiki ni cha dk 30, ni kipindi cha kwenye field siyo studio na kwa asilimia kubwa mfumo wake ni wa uibuaji wa masuala yaliyojificha katika jamii hasa maeneo ya pembezoni hasa vijijini (Ni cha uchunguzi).Mtayarishaji mkuu wa kipindi hiki ni mimi mwenyewe .
Husikose kutazama kila jumapili saa 12:00 jioni. Ambao hawakuweza kutazama kipindi kilichopita mnaweza kukitazama online hapa chini. 
 

Email ya kipindi ni baruatv@hotmail.com
Mungu awabariki sana
Wasalaam,
Mathias Byabato
0754 527358
Host-Barua Kutoka Kanda ya Ziwa

MPANGO WA JESHI LA POLISI LA KUWAPIMA WANANCHI KWA HIARI WACHANGAMKIWA





Mganga mkuu wa jeshi la polisi mkoani Kagera Dr. Husein Gamu, ambaye amehamasisha mpango mzima  wa kuwapima vipimo vya UKIMWI kwa  hiari  zoezi hilo lilifanyika eneo la standi kuu ya mabasi iliyoko katika manispaa ya Bukoba na kuhudhuriwa na watu wengi hususani vijana.

Wanaharakati Wapewa Mafunzo Ya Kujilinda


Francis Godwin (kushoto) akipokea cheti maalum baada ya  kuhitimu mafunzo ya ulinzi kwa wanaharakati wa haki za binadamu yaliyotolewa na Kituo cha Haki za Binadamu Tanzania (THRD) jijini Dar es Salaam jana. Anayekabidhi  cheti ni mgeni rasmi katika hafla hiyo Mwanaharakati Dk. Azaveli Lwaitama. Katika mafunzo hayo jumla ya  wanahabari watatu ndio walionufaika na mafunzo. Mbali ya Godwin wengine ni Saed Kubenea na Keneth Simbaya.



Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UPTC) Kenneth Simbaya akikabidhiwa cheti chake.




Mwenyekiti wa Bodi ya THRD, Bi Matrida Kabisama akikabidhiwa cheti chake na Lwaitama.
Mdau Benny alikuwa miongoni mwa washiriki.


Saida Amour kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akipokea cheti.




Neema Ole Ndemno kutoka Arusha akipokea cheti.
 Francis Godwin (mwenye suti mbele) akiwa na  wanaharakati wengine wa haki za binadamu baada ya  kumaliza mafunzo ya ulinzi kwa watetezi wa haki za binadamu jana.

JK Akutana Na Ujumbe Wa Kenya


Rais JAkaya Mrisho Kikwete akipeana mkono na Naibu Waziri Mkuu wa Kenya na Waziri wa Fedha Mhe. Uhuru Kenyatta ambaye pia ni Mwenyekiti wa  chama cha TNA. Kushoto kwa Rais ni Waziri wa Sheria wa Kenya Mhe Eugene Wamalwa wa chama cha New Ford Kenya. 
Wengine ni Naibu Waziri wa Afya na mbunge wa Mombasa Mhe. Kambi Kazungu (kulia), Mbunge wa kuteuliwa wa chama cha TNA  Bi Rachel Shebesh, na Mbunge wa Kajiado kwa tiketi ya TNA Moses ole Sakuda (kushoto) na mbunge wa zamani Mhe Abdullahi Alli alipokutana na ujumbe huo Ikulu jijini Dar es salaam Jumapili Oktoba 21, 2012
  Rais JAkaya Mrisho Kikwete akipeana mkono na  Waziri wa Sheria wa Kenya Mhe Eugene Wamalwa wa chama cha New Ford Kenya. Kulia kwake  Naibu Waziri Mkuu wa Kenya na Waziri wa Fedha Mhe. Uhuru Kenyatta ambaye pia ni Mwenyekiti wa  chama cha TNA. Kushoto kwa Rais ni  
Wengine ni Naibu Waziri wa Afya na mbunge wa Mombasa Mhe. Kambi Kazungu (kulia), Mbunge wa kuteuliwa wa chama cha TNA  Bi Rachel Shebesh, na Mbunge wa Kajiado kwa tiketi ya TNA Moses ole Sakuda (kushoto) na mbunge wa zamani Mhe Abdullahi Alli alipokutana na ujumbe huo Ikulu jijini Dar es salaam Jumapili Oktoba 21, 2012

Rais JAkaya Mrisho Kikwete akizungumza na Naibu Waziri Mkuu wa Kenya na Waziri wa Fedha Mhe. Uhuru Kenyatta ambaye pia ni Mwenyekiti wa  chama cha TNA, Waziri wa Sheria wa Kenya Mhe Eugene Wamalwa wa chama cha New Ford Kenya, Naibu Waziri wa Afya na mbunge wa Mombasa Mhe. Kambi Kazungu (kulia), Mbunge wa kuteuliwa wa chama cha TNA  Bi Rachel Shebesh, na Mbunge wa Kajiado kwa tiketi ya TNA Moses ole Sakuda (kushoto) na mbunge wa zamani Mhe Abdullahi Alli alipokutana na ujumbe huo Ikulu jijini Dar es salaam Jumapili Oktoba 21, 2012

PICHA NA IKULU

Magazeti Magazeti