Sunday, May 27, 2012
Saturday, May 26, 2012
Unaweza Ukaona Hizi Picha Ukafikiri Ni Magunia Ya Sukari,Mchele N.k
Wakazi wa manispaa ya Bukoba wakinunua kitoweo senene.
Haya magunia yamejaa senene.
Haya magunia yamejaa senene.
Nape Atinga Bukoba na Missenyi
Nape akizungumza na viongozi katika Ofisi ya CCM mkoa wa Kagera
Nape akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na baadhi ya ujumbe aliofuatana nao kwenye uwanja wa gofu
Vijana waliopo kati ya Baraza la Vijana, Missenyi, wakimsikiliza Nape
Nape akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na baadhi ya ujumbe aliofuatana nao kwenye uwanja wa gofu
Vijana waliopo kati ya Baraza la Vijana, Missenyi, wakimsikiliza Nape
Tuesday, May 22, 2012
Mikopo Inayololewa Nchini Ingelenga watu Kama Hawa
Wauzaji wa Senene katika soko la Bukoba wakiwa katika shughuli za kutafuta kipato
Lakini na akina mama katika eneo la Rulenge wilaya ni ngara wakiwa katika kazi ya kutafuta kipato
Wateja bado wananunua bidhaa katika wilaya ya Ngara
Lakini na akina mama katika eneo la Rulenge wilaya ni ngara wakiwa katika kazi ya kutafuta kipato
Wateja bado wananunua bidhaa katika wilaya ya Ngara
Wakuu Wa Wilaya Mkoani Kagera Kuyaweza Maagizo Ya Kanali Massawe?
Wakuu wa wilaya wapya wa mkoa wa Kagera wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Kagera mara baada ya kula kiapo wiki iliyopita.
Na Angela Sebastian
Bukoba
Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanal mstaafu Fabian
Massawe amewaagiza wakuu wa Wilaya wapya kuhakikisha wanasimamia mapato
na matumizi sambamba na miradi mbalimbali katika Halmashauri za Wilaya
zao ili kuondoa ubadhirifu wa fedha za umma ambao umekuwa ukifanywa na
baadhi ya watendajikatika Halmashauri hizo na Manispaa.
Alitoa
wito huo wiki iliyopita wakati akiwaapisha wakuu wapya wa Wilaya saba za mkoa huu
walioteuluiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete
hivi karibuni.
Kanal
Massawe alisema kuwa wakuu wa Wilaya wanakazi kubwa ya kusimamia mapato
na matumizi ya Serikali na kuthibiti suala la ubadhilifu wa fedha ya
umma ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya watenaji wa Halmashauri wasiokuwa wadilifu.
“Hii
nitimu ya ushindi aliyoiteua mh.Rais na kuwa na imani nayo kwahiyo
mnatakiwa kuonyesha imani hiyo kwa vitendo,kuweni na macho makali kama
ya mwewe anavyomnyemelea kifaranga na kumnasa kuhakikisha mnasimamia kwa karibu
miradi mbalimbali ya Halmashauri zenu na Manispaa ikiwa ni pamoja na
kusimamia mapato na matumizi na pale watakapobainika wafujaji wa pesa
wachukuliwe hatua na kufikishwa mahakamini wakati uchunguzi ukiendelea”alisema Massawe
“Hatuhitaji
kuwasubiri wageni waje kubaini matatizo tulionayo wakati sisi tupo
sitaki kuona mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali anakuja kugundua madudu
ya ubadhilifu wakati sisi tupo tunachelea madudu hayo nataka hiyo iwe
historia mkoani hapa, tufanye kazi kwa nguvu zote kwa usimamiazi wa
karibu wa miradi, tukague miradi mbaliambali ya maendeleo ikiwa ni
pamoja na barabara,vyumba vya madarasa na miradi mingine zinazojengwa
kwa pesa ya umma kwani asilimia kubwa hazijengwi kwa viwango
vinavyokusudiwa kwa kulingana na pesa iliyotolewa”aliongeza Masawe.
Alisema
kuwa Serikalia imekuwa ikitoa aasilimia 80 ya mapato yake katika
Halmashauri kwa ajili ya kuhudumia wananchi lakini wananchi hawafaidiki
na pesa hiyo bali wajanja hujichakachulia na kuwafanya wananchi kukosa
maendeleo na kuichukia Serikalia yao kwa sabaua ya wachache wasio na
maadili lazima tuwashughulikie kwa kasi kubwa .
Aliwataka
wakuu hao wa Wilaya kuhakikisha wanahamasisha viongozi wa ngazin za
chini yao kuanzia vitongoji na kata kuitisha vikao na mikutano ya
wananchi ili waweze kuibua miradi ya maendeleo wao wenyewe ili kuondoa
tatizo la kuwa miradi inayoletwa katika maeneo yao ni ya Serikali ambapo
wakipata elimu wataweza kuibua wenyewe na kuimiliki bila kusema si yetu
ni ya Serilakali ambapo alitoa mfano wa shulez akata ambazo hapo mwanzo
wananchi walisema ni mali ya Serikali lakini wameelimishwa na kutambua
kwamba ni mali yao na kuweza kuchangia bila tatizo.
Aidha
aliwasihi wakuu hao kupamba na suala la magendo ya kahawa mabalo
limeshamili katika mkoa huu kwani walanguzi hao hukosesha mapato
Serikali.
Aliwataka kuhimiza wananchi kutunza amani
ambayo ni tuni ya Taifa hili na kukemea vitendo vya kujichukulia sheria
mikononi ambavyo husababishwa imani za kishirikina ambayo ni kero na
changamoto kubwa inayo ukabili mkoa wa Kagera na viongozi wake.
Pia
amewataka kuhakikisha wanasimamia vyanzo vya maji na utunzaji wa
mazingira na kama mtu akibainika anaharibu mazingira kwa kuchoma moto au kujenga katika vyanzo vya maji na kufanya uharibifu wa aina yoyote katika sula la mazingira achukuliwe hatua ikiwa ni sambamba na kufikishwa mahakamani kwa sheria ya uharibifu wa mazingira.
Aliwataka
kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya zoezi la sense ya watu na makazi
ambalo itafanyika mwezi Agost mwaka huu ili Serikali iweze kupata
takwimu sahii ya watu inayowahudumia.
Akiongea kwa niaba ya wakuu hao wa Wilaya kanal mstaafu Suleman Njiku ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Misenyi alisema kuwa wameapa kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii na nguvu zao zote ili kuwaletea wananchii maendeleo ya kweli na si vinginevyo.
Wakuu
wa wilaya walioapishwa ni Costantine kanyasu (Ngara),Richard Mbeho
(Biharamulo),Dali Rwegasira (Karagwe),Zipora Pangani (Bukoba),Limbules
Kipuyo (Muleba),Kanal mstaafu Issa Njiku (Missenyi) na Luten kanali
mstaafu Benedict Kitenga (Wilaya mpya ya Kyerwa).
mwisho
Haya Bwana Kabwe Wasalime Majuu
Zitto Kabwe, Nimekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa zamani wa Marekani Nancy Pelosi na Mbunge Dennis Kucinich.
Afya Kwanza Urais Wakati Mwingine asema Mwandosya
Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya, jana aliapishwa Ikulu kushika wadhifa huo huku akikataa kuzungumzia mipango yake ya baadaye ya kisiasa. Profesa Mwandosya akijibu moja ya maswali ya waandishi wa habari baada ya kuapishwa, lililohusu iwapo bado ana nia ya kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, alisema hawezi kuzungumzia suala hilo mpaka hapo afya yake itakapotengemaa.
“Mbona mnapenda sana kuniuliza suala hili? Maana kila mwandishi akiniona anapenda kuuliza hili au leo mmeuliza kwa sababu mmeona nimekuja karibu na jengo hili? (Ikulu)…” alihoji huku akicheka na kuongeza: “Ngoja kwanza tuangalie afya…. Eeh! Afya kwanza halafu hayo mambo mengine yatafuata.” Profesa Mwandosya alihamishiwa Ofisi ya Rais kutoka Wizara ya Maji aliyokuwa akiiongoza awali, baada ya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Rais Jakaya Kikwete, Mei 4, mwaka huu.
Hata hivyo, waziri huyo ambaye aliomba kugombea urais kupitia CCM akipamba na Rais Kikwete mwaka 2005, hakuweza kuapishwa na mawaziri wenzake Mei 7, mwaka huu kwa kuwa ndiyo kwanza alikuwa amerejea kutoka India alikokuwa kwa muda mrefu akipatiwa matibabu kutokana na ugonjwa ambao hata hivyo, haujawahi kuwekwa hadharani.
Katika mchakato wa kinyang’anyiro hicho ndani ya CCM, Profesa Mwandosya alishika nafasi ya tatu, nyuma ya Rais Kikwete na Dk Salim Ahmed Salim. Jana, Profesa Mwandosya alizungumzia afya yake kwa kusema kuwa anaendelea vizuri... “Afya yangu ni kama mnavyoiona, naendelea vizuri tu, mwaka jana nilikuwa nikitembea kwa msaada wa magongo lakini leo nimeweza kutembea mwenyewe bila msaada wa magongo, kwa kweli naendelea vizuri,” alisema Waziri huyo.
Kuhusu wadhifa wake mpya alisema.... Soma zaidi; http://www.mwananchi.co.tz
Semina Elekezi Kwa Wakuu Wa Mikoa, Wilaya na Makatibu Tawala
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda wakiperuzi mada kwenye vitabu kwa umakini wakati wa mafunzo
Baadhi ya Wakuu wa Mikoa wakifuatilia mada katika mafunzo hayo Picha na Ikulu
Baadhi ya Wakuu wa Mikoa wakifuatilia mada katika mafunzo hayo Picha na Ikulu
Monday, May 21, 2012
Miaka 16 Tangu Kuzama kwa Mv Bukoba
Meli ya Mv Bukoba ikizama usiku wa kuamkia tarehe 21,May,1996
Mnara wa kumbukumbu ya abiria waliopoteza maisha uliopo eneo la Igoma Jijijini Mwanza.
Kwa Hisani ya Bukoba Pamoja Blogspot
Mnara wa kumbukumbu ya abiria waliopoteza maisha uliopo eneo la Igoma Jijijini Mwanza.
Kwa Hisani ya Bukoba Pamoja Blogspot
LEO
ikiwa ni kumbukumbu ya miaka kumi na sita tangu kuzama kwa meli ya Mv
Bukoba,baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Kagera wamehoji utekelezaji wa
ahadi ya Rais Kikwete ya ununuzi wa meli mpya.
Meli
ya Mv Bukoba ilizama May 21,1996 na kusababisha vifo vya zaidi ya watu
mia tisa,ambapo wakati wa kampeini za uchaguzi Mkuu mwaka 2010 Rais
Kikwete alihaidi ununuzi wa meli mpya kama mbadala wa meli iliyozama.
Wakihojiwa
kwa nyakati tofauti juu ya kumbukumbu ya tukio hilo baadhi ya wananchi
wamesema hawajaona juhudi zozote za utekelezaji wa ahadi hiyo na kuwa
tangu wakati huo usafiri wa majini umezorota.
Mmoja
wa wananchi hao Selestine Mwebesa mkazi wa kijiji cha Ruhunga wilaya ya
Bukoba alisema mbali na kupoteza ndugu mmoja katika ajali hiyo,hakuna
jitihada zozote zinazoonekana katika utekelezaji wa ahadi ya rais
Kikwete.
Alisema
utekelezaji wa ahadi hiyo haupashwi kuchelewa kwani kuzama kwa meli ya
Mv Bukoba iliongeza pengo la usafiri kati ya wananchi wa Mkoa wa Kagera
na Mkoa wa Mwanza.
Pia
mwananchi mwingine Pontian Kaiza mkazi wa Kijiji cha Kibeta nje kidogo
ya mji wa Bukoba alisema pamoja na ahadi ya meli mpya kuonekana imewekwa
kando,pia alidai kuna malalamiko mengi ya wananchi ambao hawakupata
kifuta machozi kama kilivyodaiwa kutolewa na serikali.
Alisema
mmoja wa jamaa zake aliyemtaja kwa jina la Joseph Peter ambaye
alimpoteza mke wake katika ajali hiyo ni miongoni mwa wananchi wengi
ambao hawakupata kifuta machozi kilichotolewa huku wengine wakilalamikia
kiwango kidogo walichopewa.
Mmoja
wa wananchi waliopona katika ajali hiyo David Mtensa mkazi wa mjini
Bukoba wakati wa kumbukumbu ya tukio hilo mwaka jana alinukuliwa
akiilalamikia Serikali juu ya kiwango kidogo cha fedha zilizotolewa kwa
waathirika wa ajali hiyo.
Alidai
kiasi cha shilingi laki moja kilichotolewa kwa abiria aliyenusurika na
laki tano waliopoteza ndugu hakikulingana na madhara waliyopata kwa
kuzingatia kuwa baadhi yao walikuwa wafanyabiashara waliolazimika kuanza
upya.
Miongoni
mwa ahadi nyingi alizozitoa Rais Jakaya Kikwete wakati akitafuta muhura
wa pili wa uongozi ni ununuzi wa meli mpya,ambapo mpaka sasa hakuna
jitihada za wazi zinazoonekana juu ya utekelezaji wa ahadi hiyo.
Watendaji Wa Kata Na Vijiji Walia Na Wanasiasa
Na Mwandishi Wetu
Bukoba
VIONGOZI ngazi ya juu na wakisiasa wametakiwa kutoa ushirikiano kwa watendaji wa vijiji na kata ili kufanikisha shughuli nyingi za maendeleo ya jamii kukamilika kwa wakati.
Ushauri huo,umetolewa na watendaji wa vijiji na kata ndani ya halmashauri ya wilaya ya Bukoba,waliokuwa wakihudhuria semina ya kikazi ili kuwawezesha kutambua na kufuata wajibu wao katika shughuli zao za kila siku iliyofanyika katika vituo viwili vya Maruku na Lyamahoro.
Watendaji hao walibainisha kuwa shughuli zao hasa za kuhimiza na kukusanya michango zinakuwa ngumu na kuonekana kuleta kero kwa jamii kutokana na baadhi ya viongozi wa kisiasa kuitisha mikutano yao na kuanza kupokea kero za wananchi kwa madai wao ni watetezi,hivyo na kusababisha zoezi la kuimiza maendeleo kwenda kwa kusuasua.
"Tatizo kuu la jamii yetu kutohudhuria mikutano ya hadhara ni kutokana na wanasiasa wetu,kufika katrika mikutano yao na kuomba kusikiliza kero za wananchi,na mwisho kuwataka wananchi kutokubali lolote linalohusu masuala ya maendeleo hasa kuchangia"alisema Abdallah Rwabigimbo,afisa mtendaji kata Katoma.
Alisema kuwa mara nyingi jamii inawaona watumishi hawa kama ni sehemu ya kuwanyanyasa,jambo ambalo si kweli na linawafanya kuishi kwa mashaka juu ya maisha yao ya kila siku,na kusababisha jamii kuacha kuhudhuria mikutano pale wanapoitisha juu ya kupewa taarifa juu ya mapato na matumizi.
Hata hivyo,wameomba serikali kuangalia ni jinsi gani itaweza kuwapatia motisha viongozi wao wa kuchaguliwa yaani wenyeviti wa vitongoji ili kuwezesha kazi zao kufanyanyika vizuri na kwa ushirikiano mwema.
"Serikali iangalie jinsi gani inaweza kuwapatia motisha wenyeviti wa vitongoji ili kuharakisha shughuli za maendeleo,kwani wakati mwingine shughuli zetu zinakwama kutokana na viongozi hawa kutokuwa na mwamko kutokana na majukumu yao"alisema William Buberwa,afisa mtendaji kata Buhendangabo.
Kwa upande wake mratibu wa semina hiyo Philimon Magesa,ambaye pia ni afisa utumishi wa halmashauri ya wilaya Bukoba,aliwaasa watendaji hao kufuata sheria zilizopo hasa wakati wa kufanya shughuli zao za ulinzi na amani katika maeneo yao huku wakifatilia sana kanuni za maadili ya kazi.
Magesa alisema kuwa lengo kuu la semina hiyo,kuwapatia mafunzo watendaji hawa kufuata taratibu mbalimbali zilizo ndani ya kazi zao za kila siku na mada kuu ikiwa ni kufuata misingi ya utawala bora.
Semina hiyo iliyoendeshwa na mwezeshaji Venance Shilingi,kutoka chuo kikuu cha Mzumbe iliwashirikisha jumla ya washiriki 120 wakiwa watendaji wa vijiji na kata ikiwa kata 29 na vijiji 94 vilivyo ndani ya halmashauri ya wilaya ya Bukoba.
MWISHO

Saturday, May 19, 2012
JK Still In US
President
Jakaya Kikwete talks during a symposium with a theme "Food Security
at the G-8: Changing the development landscape" at the Ronald Reagan
building and International Trade Centre in Washington DC. The session
outlined key components of the G8 deliverables for food and nutrition
security.
President Barak Obama of the United States of America introduces President Jakaya Kikwete as he acknowledges the presence of four African leaders present symposium themed "Food Security at the G-8: Changing the development landscape" at the Ronald Reagan building and International Trade Centre in Washington DC. The session outlined key components of the G8 deliverables for food and nutrition security. Others were HE Meles Zenawi, Prime Minister of Ethiopia, Prof. John Evans Atta Mills, President of Ghana and African Union Chairman and President of Benin, HE Dr Boni Yayi.
US Secretary of State Hon Hillary Clinton gestures after a group photo with African leaders and the USAID Administrator Dr Rajiv Shah (third right) prior to a reception to celebrate the new partnership to advance food security on the occasion of the G-8 summit at the D. Franklin room at the State Department in Washington DC.

Subscribe to:
Posts (Atom)