Amesema
bila amani na muungano wa wananchi maendeleo hayawezi kupatikana katika
nchi ambpo aliwataka vijana kuwa mtari wa mbele kuwaelimisha wananchi
wa kawaida juu ya umuhimu wa kuenzi, kudumisha na kuimarisha muungano wa
zanzibar na Tanganyika kama njia pekee ya kuhakikisha nchi inakuwa na
amani siku zote.
“Vijana
tuna wajibu kubwa wa kuwaenzi waliotuletea muungano wetu wa sasa,
taaluma zetu ziwe dira ya jamii katika kuenzi, kudumisha na kuimarisha
muungano wetu kwani ndio njia pekee ya kusaidia kudumisha amani na
usalama wan chi yetu, tuepuke kujiingiza katika mkumbo wa wale wanaodai
nchi haitatawalika,” amesema
Hata
hivyo Sadifa amewataka vijana kutodanganyika na vyama vinavyoeneza
chuki na maandamano yasiyokuwa na msingi wowote huku akifafanua kuwa
kisheria kuandamana na haki ya msingi lakini ifuate sheria na
yassingilie haki za wengine.
“Chama
pekee katika nchi hii ni CCM, kuna vyama vingine vimeanzishwa ambavyo
mimi binafsi naviita ‘Saccos’, hauwezi ukajikopesha fedha kienyejienyeji
kama alivyofanya Dk. Slaa! Vijana tuwe makini na saccos hizi ambazo
ajenda zao ni kukopeshana na vurugu tu,” amesema Sadifa
Kwa
upande wake mwenyekiti wa shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu
wanachama wa CCM kilimanjaro, Wakati Mtulya akizungumzia changamoto
wanazokumbana nazo, alisema kumekuwa na urasimu ndani ya bodi ya mikopo
kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, ambapo mikopo imekuwa ikitolewa kwa watu
wasiostahili huku walengwa wakiendelea kutaabika.
Amesema
kuwa kumekuwa na mchezo ndani ya bodi hiyo, ambapo mikopo imekuwa
ikitolewa kwa watoto wa matajiri huku wastahili ‘watoto wa wakulima’
wakibaki kuzungushwa na kuwekewa masharti magumu ya kupata mikopo hiyo
jambo ambalo limekuwa likichangia kuwepo kwa vitendo vibaya miongoni mwa
wanafunzi hao.
“Mikopo
ni yetu, sio ruzuku, lazima tukopeshwe kwa wakati kwani lazima
tutairudisha lakini jambo la kusikitisha, bodi hii imekuwa ikitoa mikopo
kwa watoto wa masaki, huku sisi watoto wea mkulima tukiendelea
kuzungushwa na kuwekewa masharti magumu ili kupata mikopo hiyo, hili ni
tatizo,” amesema Mtulya (habari na TAIFA LETU.com).