Monday, May 20, 2013


MOTO WATEKETEZA DUKA USWAHILINI BUKOBA USIKU WA JANA NA KUSABABISHA HASARA KUBWA

 Ni mabaki ya vitu vilivyoteketea kwa moto baada ya duka la mfanyabiashara aliejulikana kwa jina la baba sima kuungua maeneo ya uswahilini karibu na maua gest

 duka lililoungua moto lipo uswahilini barabara ya maua gest,inasemekana machinga wengi wa mtaa huo walikuwa wakiweka mizigo yao katika duka hilo wakifunga shughuli zao muda wa jioni
 chanzo cha moto hakijafahamika, ila kwa habari zisizo rasmi inasemekana na tatizo la umeme



 baadhi ya vitu vilivyookolewa kutaka katika duka  la baba sima

 ilimradi kilikusanywa kila kilichoonekana hakijaungua

 baba sima mwenye duka (kushoto) akifarijiwa
 wayuka baba sima ebintu mbiigwa orwo omoyo gwaunga( ONGERA BABA SIMA VITU UTATAFUTA BORA UZIMA ni maneno ya mama akimfariji


tunakupa pole sana baba sima

Friday, 17 May 2013

MSAFARA WA MAGARI UNAOPITA MIKOA MBALIMBALI KUTOA ELIMU KUHUSU FISTULA WAZINDULIWA BUKOBA

Balozi wa vodacom Mwana FA akimsikiriza mgeni rasmi mkuu wa wilaya bukoba mama zippola pangani muda mfupi kabla ya kumpa funguo za gari ndogo tax itakayo zunguka maeneo yote yaliyopangwa kutoa elimu kuhusa fistula inatibika.


 umati wa watu ukisikiliza elimu kuhusu fistula, ugonjwa unaowapata akina mama wakati wa kujifungua


 Ni shirika lisilo la serikali ambalo linawataalamu wakiwemo madakitari, kampuni ya vodacom imewakabidhi kiasi cha shilingi bilioni nane kusaidia kutibu wakina mama wenye fistula shirika hili hutoa huduma za matibabu bure zikiwemo na gharama usafiri,chakula na malazi,baada ya wataalamu kubaini tatizo lafistula
 katibu tawala wa mkoa wa kagera(kushoto) akikaribishwa eneo la tukio soko kuu bukoba

 meneja mahusiano ya nje vodacom salumu mwalimu akitoa maelezo kwa nini vodacom imeamua kusaidia akina mama katika janga hili la fistula,kikubwa alisema vodacom kile inachokipata inajari sana huduma za jamii,na aliwataka wamama wanapopata vistura wasikate tamaa ya maisha vodacom kazi ni kwako
 Balozi wa vodacom mwana FA akisikiliza kwa makini

 Bi naima ishengoma mkazi wa katoro bukoba vijijini akitoa ushuhuda ,baada ya kupata  fistula mwanaume alimkimbia,lakini kupitia redio karagwe alipata habari na alipelekwa CCBRT na sasa amepona,aliwasisitiza wamama ambao fistula wasikate tamaa unatibika, tena huduma bure
 shuhuda sofia ibrahimu wa kyerwa karagwe,pamoja na ushuhuda mwingi aliotoa alimshukuru mume wake amidu winstoni kwa kumvumilia kipindi chote cha ugonjwa bila kumnyanyapaa,kumtenga,na kumuhudumia mpaka sasa kapona
 katibu tawala mkoa wa kagera akimkaribisha mgeni rasmi azungumze

 mgeni rasmi mkuu wa wilaya bukoba akitoa neno kwenye uzinduzi wa msafara kupita mikoa mbalimbali kutoa elimu kuhusu fistula inatibika
 piga hiyo namba ni bure eleza tatizo lako la fistula utasaidiwa
 ni gari maalumu linotumika katika msafara
 Balozi wa vodacom mwana FA kwa heshima ya wakazi wa bukoba alimwaga mistari


 Dj slay kwa siku hiyo alikuwa mc wa shughuli nzima,hapo yupo na balozi wa vodacom mwana FA

 Ulifika wakati wa mgeni rasmi kukabidhi ufunguo kuashiria uzinduzi wa msafara

 mmiliki wa jamcobk.blogspot.com akiwa na balozi wa vodacom mwana FA


MENEJA MAHUSIANO YA NJE VODACOM AKIONGEA NA VYOMBO VYA HABARI KABLA YA MSAFARA KUONDOKA KUPITIA ,CHATO,GEITA, MWANZA , SHINYANGA,SINGIDA,MOROGORO NA ATIMAE TAREHE 23-5-2013 MSAFARA UTAPOKELEWA NA MH RAIS JAKAYA KIKWETE,PONGEZI VODACOM NA CCBRT KWA KUONYESHA UZALENDO KWA AKINA MAMA

Wednesday, May 1, 2013

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JAKAYA KIKWETE AKIWA MBEYA

8E9U1585Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mtoto mdogo muda mfupi baada ya Kuwasili katika uwanja wa ndege wa Songwe mjini Mbeya jana.(picha na Freddy Maro)

RAIS JAKAYA KIKWETE ZIARANI MKOANI MBEYA KUONGOZA MEI MOSI

8E9U1593Maelfu ya Wakazi wa Mji wa Mbeya wakisalimiana kwa Shauku na Rais Dkt.Jakaya  Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Songwe mjini Mbeya tayari kuongoza sherehe za Mei mosi zinazofanyika mkoani huko kesho(picha na Freddy Maro)

DEREVA WA “BODA BODA” AKAMATWA NA SHORTGUN, RISASI SITA

GEDSC DIGITAL CAMERAPichani juu ni bunduki aina ya Shortgun Mossberg ikiwa na risasi sita ambayo ilikutwa kwenye begi la dereva huyo wa Boda boda aliyekamatwa na polisi tarehe 28.04.2013 (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
 Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
 
Jeshi la Polisi Mkoani hapa limemkamata mtu mmoja aitwaye Ally Rashid Salimu (23) Mwendesha pikipiki za abiria maarufu kwa jina la “Boda Boda” mkazi wa kata ya Sombetini jijini hapa akiwa na bunduki aina ya shortgun Mossberg yenye namba T292166 ikiwa na risasi sita.
 Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo saa 5:30 asubuhi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Liberatus Sabas alisema kwamba, tukio hilo lilitokea juzi tarehe 28.04.2013 muda wa saa 3:00 asubuhi katika maeneo ya Shamsi yaliyopo jijini hapa.
 Alisema siku ya tukio dereva huyo wa pikipiki akiwa katika eneo hilo alikuwa anaendesha pikipiki aina ya Skymark yenye namba za usajili T. 615 BZL huku akiwa amebeba begi lilionekana kutuna sana, ndipo askari waliokuwa doria katika eneo hilo walimtilia shaka na kisha kumfuatilia na kufanikiwa kumsimamisha.
 “Mara baada ya kumsimamisha askari hao walipekua begi hilo na kukuta silaha hiyo ikiwa na risasi sita na kisha kumfikisha mtuhumiwa huyo katika kituo kikuu cha polisi cha hapa Arusha mjini”. Alifafanua Kamanda Sabas.
Kamanda Sabas alisema upelelezi juu ya tukio hilo bado unaendelea na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani pindi utakapokamilika.
 Tukio hilo la ukamataji wa bunduki hiyo limekuja wiki tatu tu baada ya jeshi hilo kukamata bastola moja pamoja na risasi 41 kutoka kwa watuhumiwa waliokuwa wanahusishwa na matukio ya kumjeruhi Sister Mary Shobana na kisha kumnyang’anya fedha taslimu Tsh 30,000,000/= (Milioni thelathini) eneo la Notre Dame Njiro lililopo jijini hapa, fedha ambazo alitoka kuchukua benki ya Exim tawi la Shoprite.

Magazeti

9 b9e7b
10 186a7
11 1ec7b
12 c6c99

13 042fd
4 25ba4

5 37f7b8 78c2014 b3080

Monday, April 29, 2013

Maisha Yanaendelea

03 9ea2a
Mafundi ujenzi wakiendelea na kazi, Hii ni Barabara ya Morogoro eneo la magomeni Jijini Dar es salaam.

DKT. BILAL AKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE, UJUMBE MAALUM WA SYRIA


03 41812
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria, Hussam A'ala, wakati akimkaribisha ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam
04 0a173
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria, Hussam A'ala, na ujumbe wake wakati alipofika Ofisini kwa Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo
05 450ef
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria, Hussam A'ala, baada ya mazungumzo

Godbless lema aachiwa huru kwa dhamana



lema ec6a0

Mbunge Arusha, Godbless Lema
Mahakama kuu ya Arusha mapema leo asubuhi imemuachia huru kwa dhamana mbunge  wa Arusha mjini,kwa mashariti ya kuwa na mdhamini mmoja mwenye kitambulisho, na asaini hati ya dhamana yenye thamani ya shilingi milioni moja.

Watu 30 wavamia, kuvunja nyumba

1 7d1c6
Zaidi ya watu 30 usiku wa kuamkia jana walivamia na kuivunja nyumba ya Yasinta Malisa, iliyopo Kunduchi Ununio ,kando ya Bahari ya Hindi, huku wakimtishia kwa bastola mlinzi wa nyumba hiyo.
Kutokana tukio hilo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, amemtaka mmiliki wa nyumba hiyo kuwasilisha vielelezo vya umiliki wa eneo hilo polisi.

Hatua hiyo inalenga katika kuwawezesha polisi kuvipitia na kumpa ushauri wa ama kwenda mahakamani au kumkamata anayeshukiwa kubomoa nyumba hiyo.
"Wanatakiwa kuwasilisha vilelezo vya umiliki wa eneo hilo, lakini pia inaonyesha kuwa kuna mgogoro katika eneo husika. Vielelezo ndivyo vitaonyesha kila kitu na tutajua wapi kuna tatizo," alisema Kenyela.
Mmoja wa walinzi wa nyumba hiyo, Saitoti Nang'oro na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Ununio, Iddi Musa, walisema watu hao walivamia mtaa huo saa 9 usiku wakiwa na marungu, mapanga na bastola.
Akizungumzia na gazeti hili, Yasinta alisema baada ya kufiwa na mume wake mwaka jana, aliamua kuendeleza ujenzi wa nyumba hiyo, lakini siku tatu baada ya kuanza kazi, watu hao walivamia na kuivunja nyumba yake.
"Hili eneo tulilinunua kutoka kwa wazawa wa hapa Ununio na nina vilelezo halali, ila nashangaa kitendo kilichofanyika tena kimefanyika usiku, sasa kama wanamiliki eneo kihahali kwa nini waje usiku, mbona hakuna hata vilelelezo vyao katika ofisi za Serikali ya mtaa," alihoji.
Alisema alinunua eneo hilo miaka 20 iliyopita, huku akisisitiza kuwa eneo hilo halijapimwa na Serikali na wamiliki wake wanauza maeneo yao kama mashamba. Akisimulia alivyonusurika kuuawa Nang'oro alisema akiwa lindoni, aliona kundi la watu likija na wakati akijiandaa kuwahoji walimkamata na kumfunga kamba.
"Mmoja ndio alinishika na kunifunga kamba, wengine walikuwa wakibomoa nyumba kwa kutumia vyuma vikubwa. Yule aliyekuwa amenishika alikuwa pia ameshikilia bastola na aliniambia kuwa nisipokuwa mtulivu au nikikimbia atanipiga risasi," alisema Nang'oro.
Kwa upande wake, Musa alisema tangu achaguliwa kushika nafasi hiyo, vielelezo vilivyopo katika ofisi yake vinaonyesha kuwa mwenye eneo hilo ni Yasinta na siyo mtu mwingine.HCANZO MWANANCHI

Maisha Yana.................

1 2cb96
 Mbarali, Mbeya