Monday, April 15, 2013

Mengi atoa Sh100m Harambee ya kuchangia Chuo kikuu cha kiislamu cha Al-haramain

bak1 8a98d
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dkt Reginald Mengi ambaye alichangia shilingi milioni 100 kwa ajili ya kusaidia upanuzi na maendeleo ya Chuo Cha Kiislamu cha Al-Haramain kwenye hafla ya harambee iliyofanyika Jumamosi usiku katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.

bak2 13b81
Mufti wa Tanzania Sheikh Issa bin Shaaban Simba akimshukuru Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dkt Reginald Mengi ambaye alichangia shilingi milioni 100 kwa ajili ya kusaidia upanuzi na maendeleo ya Chuo Cha Kiislamu cha Al-Haramain kwenye hafla ya harambee iliyofanyika Jumamosi usiku katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam

bak3 e9dbb
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Mufti wa Tanzania Sheikh Issa bin Shaaban Simba, KATIBU Mkuu wa Baraza la Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Sheikh Suleman Lolila (wa pili kulia), Kadhi Mkuu Sheikh Abdallah Mnyasi (kulia) na Shehe wa Mkoa wa Dar es salaam Alhaj Alhad (kushoto) wakiomba dua baada ya harambee kusaidia upanuzi na maendeleo ya Chuo Cha Kiislamu cha Al-Haramain kwenye hafla iliyofanyika Jumamosi usiku katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam

bak4 0aef7
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dkt Reginald Mengi ambaye alichangia shilingi milioni 100 na Mwenykiti wa NCCR-Mageuzi Mhe James Mbatia aliyechangia shilingi milioni mbili kwa ajili ya kusaidia upanuzi na maendeleo ya Chuo Cha Kiislamu cha Al-Haramain kwenye harambee iliyofanyika Jumamosi usiku katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam

bak6 1cde7
Rais Kikwete akihutubia kwenye harambee ya kuchangia upanuzi wa ujenzi Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al- Haramain (Chanzo: Ikulu).

CHADEMA Yafichua Njama Za Vigogo

“Wenzangu wengine katika kesi hii ni Prof. Abdallah Safari, Tundu Lissu, Edson Mbogoro, Peter Kibatara na Nyaronyo Kicheere. Huko mbele tutaongeza mawakili wengine, akiwamo mmoja anayewekwa na familia ya Lwakatare.

Ifuatayo ni taarifa kamili ya Marando ambaye pia ni mwanasheria maarufu nchini na mmoja wa wakongwe wastaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa:

“Leo tumewaita hapa ili kuwaomba mtufikishie ujumbe kwa Watanzania, kwamba nikiwa mwanasheria na mtu ambaye nimepata ujuzi wa kazi za ushushushu, nimefanya uchunguzi matukio haya ya utekaji na utesaji na kugundua mambo mengi mno.

Uchunguzi huu nimeufanya kabla na baada ya kukamatwa kwa Mkurugenzi wetu wa Ulinzi na Usalama, Wilifred Muganyizi Lwakatare, ambaye hivi sasa anashtakiwa mahakamani kwa tuhuma za kupanga ugaidi.

Nimefanya hivyo kwa kuangalia maslahi mapana ya taifa langu na chama changu. Katika uchunguzi wangu huo, nimegundua mambo mengi ikiwamo kuwapo kwa genge la watu ndani ya serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanaopanga mipango hii ya kishetani na kisha kuwasingizia watu wengine.

Angalieni mfano huu: Unaoitwa na polisi na Mwigulu Nchemba “mkanda wa Lwakatare” unadaiwa uliwasilishwa Jeshi la Polisi Desemba mwaka jana.

Lakini jeshi hilo halikumkamata yeyote wala kumhoji, hadi pale Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda alipovamiwa na kuumizwa.

Aidha, Nchemba amedai kumiliki video ile Desemba mwaka jana, lakini rekodi hiyo iliwekwa kwenye mitandao ya kijamii (YouTube na Jamii Forum) baada ya kutekwa kwa Kibanda. Hapa mtu makini anaweza kujiuliza, hiki kimelenga nini?

Kwamba genge hili la kina Nchemba na wenzake, walipanga kumteka Kibanda, wakatimiza lengo lao hilo, baadaye wakaingia kwenye plan B ya kutaka kuihusisha CHADEMA.

Wakamtumia Ludovick Joseph Rwezahula ambaye ni mshtakiwa wa pili katika kesi ya Lwakatare, kufanikisha mkakati wao huu wa kishetani.

Huu ni mchezo mchafu na wa hatari mno ambao kwa vyovyote vile, haupaswi kuvumiliwa.

Kuanzia sasa nimeamua kwa dhati kabisa kukomesha mchezo huu ambao unahatarisha uhai wa taifa letu.

Mnaweza kujiuliza kwanini CHADEMA kimechukua uamuzi huu wa kuweka kundi kubwa la wanasheria katika kesi hii ya Lwakatare. Jibu ni kwamba tumegundua kuwa kesi hii imefunguliwa kwa lengo maalumu la kuidhoofisha CHADEMA na kuinusuru CCM ambayo inakabiliwa na dhahama ya kushindwa katika uchaguzi mkuu ujao kutokana na kushamiri kwa makundi.

Hivyo wameamua kumfungulia kesi Lwakatare, kwa lengo la kutaka kuaminisha umma kuwa CHADEMA ni chama cha magaidi, kinapanga ugaidi na hivyo kichukiwe. Hilo ndilo lengo lao. Basi!

 Pili, nitakwenda mahakamani kuwasilisha ombi maalumu la kuomba amri ya mahakama kuagiza makampuni ya simu za mkononi kuwasilisha mahakamani statement za simu za watu kumi (10) ili kusaidia mahakama kutenda haki na jamii kujua ukweli wa mambo haya.

Watu ambao nitaomba mahakama itoe amri ya kuletwa taarifa zao za simu na meseji (sms) ni Naibu Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa nchini (TISS), Jack Zoka, anayetumia simu Na. 255756809535, Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu Lameck Nchemba, anayetumia simu tano zikiwamo 0754 008888, 0757 946223, 0714 008888 na 0787 513446 na Ludovick Joseph Rwezahula ambaye simu zake ni 0715 927100 na 0753 927100.

Mwingine ambaye mawasiliano yake yanahitajika, ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Emmanuel Nchimbi anayetumia simu Na. 0754 003388, Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Mwananchi, Dennis Msacky anayetumia simu mbili; 0655 331010 na 0764 331010 na Sinbad Mwagha, ambaye ni Ofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa, anayetumia simu 0754 006355.

Wengine ni Shaali Ali, Ofisa mwingine wa Usalama wa Taifa anayetumia simu Na. 0716990099, Saumu K. Malungu, mwenye kutumia simu 0719 541 434 na 0789 614 629, simu mbili zinazotumiwa na mtuhumiwa mkuu wa utekaji wa Dk. Steven Ulimboka, Ramadhani Abeid Ighondo ikiwamo 0713 760 473, simu za Ridhiwani Kikwete ambazo ni 0754 566299, 0784 566 299, simu ya Dk. Ulimboka ambayo ni 0713 731 610, pamoja na simu zote tatu za Wilfred Lwakatare, ambazo ni 0786 774697, 0713 237869 na 0758 417169.

Mtu mwingine muhimu nitakayeomba mahakama itoe amri ya kutolewa kwa taarifa zake, ni mwandishi wa habari na mpigapicha wa magazeti ya serikali, Muhidini Issa Michuzi.

Mwandani huyu wa Ikulu, ndiye aliyeandika ujumbe kwa njia ya barua pepe kuipongeza ofisi binafsi ya rais (OBR) na usalama wa taifa kwa kupata video ya Lwakatare.

Pongezi za Michuzi kwa TISS ndizo zinanisukuma kuiomba mahakama kuagiza kupatikana taarifa zake. Michuzi anaipongeza TISS kwa kuibua njama za wahalifu, lakini mimi ninajua TISS ikipata njama za aina hiyo haraka inapeleka ushahidi polisi, lakini huu wa Lwakatare ulipelekwa Youtube, badala ya kwenye vyombo vya sheria.

Maneno ya Michuzi kwamba ni TISS imeibua hiyo video yanathibitisha ushiriki wa TISS kwenye mchezo huo mchafu, na kwamba CHADEMA kinajua kuwa Michuzi alishirikiana na watu wa usalama wa taifa katika kazi hiyo chafu.

Software za video (editing) walizotumia zilitoka kwake. Fedha ya kuandaa hiyo video zilitoka Usalama na Ikulu. Tunajua kuwa wale vijana wa Ada Estate na yule jamaa aliyempelekea kigogo wa Jamii Forum, walilalamika sana kwa mmoja wa wamiliki wa JF.

CHADEMA kinajua kuwa mmoja wa watuhumiwa hawa, Mwigulu Nchemba anafanya mipango na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Vodacom ili kumsaidia kufuta taarifa zake.

Nachukua nafasi hii kuionya kampuni hiyo kuacha kucheza mchezo huo kwa kuwa ni kinyume na sheria za Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA).

Tunahitaji mawasiliano haya kwa kuwa simu za Mwigulu zinaonesha mtuhumiwa huyo akifanya mawasiliano mfululizo na Ludovick, yakiwamo yale ya tarehe 4 Machi 2013. Hii ilikuwa siku moja kabla ya Kibanda kutekwa.

Hawa niliowataja ni watu muhimu sana katika upangaji wa mkakati wa utengenezaji wa video ya Lwakatare na vitendo vya kihalifu vya utekwaji wa Kibanda na tukio la kutekwa na kisha kutupwa msutuni kwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka.

Kwa mfano, simu ya Mwigulu Nchemba namba 0714 008888, 0756 008888 na 0757 946223, zimefanya mawasiliano mara kadhaa na Ludovick Joseph, Saumu K. Malungu, Jack Zoka, Ali Shaali na Ramadhani Ighondo.

Mawasiliano hayo yalifanyika katika kipindi ambacho mgomo wa madaktari ulishamiri; baadaye yakarudi tena kati ya 26 Desemba mwaka jana na 15 Machi mwaka huu.

Miongoni mwa mawasiliano ambayo tunaona yanahusika na ujambazi huu, ni yale ya 28 Desemba, siku ambayo mkanda wa Lwakatare umerekodiwa.

Tarehe 4 hadi 6 Machi 2013, siku moja kabla ya Kibanda kutekwa na yale ya usiku wa manane (saa 8:17) wa 13 Machi 2013, ambako mchana uliofuata Lwakatare alikamatwa.

Huyu Mwagha ndiye aliyekuwa anatumika kuwasiliana na Saumu Malungu ambaye tulimtaja kuwa ndiye aliyekuwa amepewa kazi na Mwigulu na Usalama wa Taifa, kurubuni vijana wetu kwa fedha ili kutoa ushahidi wa uongo juu ya video ya Lwakatare.

Vilevile, mawasiliano ya Mwigulu na Mwagha katika kipindi hicho nayo tunayahitaji. Kwa sababu huyu Mwagha anayetumia simu 0754006355, mbali na kuwasiliana na Mwigulu, ndiye aliyekuwa anawasiliana na mmoja wa waliomteka Ulimboka; na ndiye aliyewasiliana na Saumu kati ya tarehe 20 Januari na Machi 6 mwaka huu.

Ludovick alifanya mawasiliano ya mwisho na Joyce Augustine, ambaye anatumia simu Na. 0717 559210, mawasiliano ambayo yalifanyika saa 5:13 usiku.

Hiyo ndiyo ilikuwa simu yake ya mwisho usiku huo; katika siku hiyo Ludovick aliwasilisna na Joyce mara tisa kuanzia saa 12: 54 asubuhi.

Kwa mujibu wa taarifa za kwenye mtandao wa Jamii Forum, ambako video ya Lwakatare ilitumwa, Ludovick alikamatwa Machi 15 mwaka huu.

Hata hivyo, rekodi katika simu yake Na. 0715 927100 inaonyesha tarehe 17 Machi, Ludovick alifanya mawasiliano na Joyce Augustine. Mawasiliano hayo yalifanyika saa 8:09 usiku, wakati inadaiwa na polisi alishakamatwa.

Naye mhariri wa Mwananchi, Msacky ambaye anatajwa kutaka kutekwa na Ludovick na Lwakatare, amekuwa na mawasiliano kadhaa na Ludovick – mtu anayepanga kumteka.

Ludovick na Msacky walifanya mawasiliano mfululizo kati 27 Desema 2012, siku moja kabla ya video ya Lwakatare haijarekodiwa na tarehe 7 Machi siku moja baada ya Kibanda kutekwa.

Msacky alitumia simu zake hizo mbili (0764 331010 na 0655 331010) kuwasiliana na Ludovick, huku Ludovick akitumia 0753927100.

Mawasiliano ya 31 Desemba yalifanyika Ludovick akiwa Tegeta, jijini Dar es Salaam. Mawakala hawa wawili wa Usalama wa Taifa (Ludovick na Msacky) walikutana 31 Desemba 2012, katika hoteli ya Tamal, Mwenge jijini Dar es Salaam.

Baada ya kupitia taarifa hizi za mawasiliano ya simu za Mwigulu Nchemba, Ludovick Joseph, Ramadhani Ighondo na Saumu Malungu tumegundua yafuatayo:

Kwamba, Ramadhani Ighondo amefanya mawasiliano mara nyingi na Mwigulu, Mwagha na Zoka; naye Mwagha amefanya mawasiliano na Mwigulu na Saumu; naye Saumu amefanya mawasiliano na Mwagha, Mwigulu na Shaali Ali, ambaye ni ofisa Usalama wa Taifa.

Tumegundua vilevile, kuwapo mawasiliano kadhaa kati ya Ludovick na Msacky; Ludovick na Mwigulu; Msacky na Nchimbi; Msacky na Mwagha, Saumu na Mwagha na Ramadhani Ighondo Abeid, anayetuhumiwa kumteka Dk. Ulimboka na Mwagha na Mwigulu.

Tumegundua pia kuwapo mawasiliano kati ya Ulimboka na Ramadhani; Zoka na Ighondo na Ridhiwani na Ighondo. Mawasiliano haya yalifanywa mfululizo usiku wa Juni 2012 siku ambayo Dk. Ulimboka alitekwa.

Tumepata kufahamu pia kwamba baadhi ya watu waliotajwa na gazeti la MwanaHALISI kuwa waliwasiliana na Ighondo usiku wa Juni 26, mwaka 2012, wamefanya mawasiliano pia na Mwigulu, Mwagha na Shaali Ali.

Mwagha ni ofisa Usalama wa Taifa anayefanya kazi makao makuu ya idara hiyo. Ndiye yule anayetumika kuendesha michezo ya kuhonga wanasiasa wa CCM na upinzani.

Ni Mwagha anayepanga wabunge na kuwapanga waongee nini kwa maslahi ya CCM. Ushenzi wote anaoongea Mwigulu bungeni hupewa na Mwagha kwa maelekezo ya Jack Zoka.

Naye Shaali ndiye aliyekutana na ofisa wetu wa usalama, Ahmed Sabula na mwenzake, Machi 29 mwaka huu katika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam. Katika mkutano huo kati ya Sabula, kijana wetu wa usalama na ofisa usalama wa serikali, Shaali alitaka Sabula akubali kutumika kwa kutoa taarifa za vikao vya chama, kuwasilisha kwake nyaraka za Kamati Kuu na kueleza mipango ya chama katika kesi ya Lwakatare.

Kwenye mpango huu, ofisa huyo wa Usalama wa Taifa ambaye ninamfahamu vizuri, alimuahidi Sabula kiasi cha sh milioni 30 na kwamba fedha hizo angelipwa wiki iliyopita. Aliahidiwa pia kwamba kila nyaraka atakayopeleka atalipwa ujira.

Aidha, Sabula aliahidiwa kulipwa sh 500,000 kila mwezi; ofisa wetu huyu ameripoti tukio hilo kwa viongozi wake wa chama. Yule mwenzake aliandaliwa kuwa shahidi wa kesi ya Lwakatare; aliambiwa akikubali dili hiyo atalipwa kila mwezi sh 500,000 lakini akaombwa kuwa mvumilivu kwa kuwa atalazimika kupotea kwa miezi kama mitano hadi sita.

Kitendo cha Mwigulu kuwasiliana  na Ramadhani Ighondo, Mwigulu kuwasiliana na Ludovick, Saumu kuwasiliana na Mwigulu, Ighondo kuwasiliana na Ulimboka, Zoka kuwasiliana na Ighondo, tena katika muda ule ule ambao Ighondo amewasiliana na Ulimboka na Saumu kuwasiliana na Mwagha, ni uthibitisho tosha kwamba Usalama wa Taifa wako nyuma ya mipango hii michafu ya kupanga utekaji na kisha kutaka kukichafua CHADEMA.

Aidha, kitendo cha Ludovick kuwasiliana na Msacky; Ighondo kuwasiliana na Mwagha, Ridhiwani Kikwete kuwasiliana na Ighondo, tena kila baada ya Ighondo kuwasiliana na Ulimboka na Jack Zoka, ni uthibitisho mwingine kuwa genge hili la wahalifu linashirikiana na baadhi ya watu kutaka kuangamiza taifa.

Ni uthibitisho tosha kwamba hawa ndiyo wanaowahonga wanachama wa CHADEMA na watu wengine ili watoe ushahidi feki dhidi ya Lwakatare, na kwamba ni Usalama wa Taifa walioandaa ile video uchwara inayopigiwa chapuo na Mwigulu.

Chama Cha Mapinduzi kinajua kwa hali ya sasa hakiwezi kushinda uchaguzi wa mwaka 2015 huku CHADEMA ikiwa katika hali nzuri ya kisiasa tunayoiona sasa.

Wanajua kabisa CCM imegawanyika, kundi lolote litakalopita ndani ya CCM, litahujumu kundi jingine. Ni kama ilivyotokea uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki.

Ndiyo maana wanapanga kila mbinu kutaka kuiangamiza CHADEMA. Nasi tunasema katu hatutakubali kuona CHADEMA kinakufa. Tutapambana usiku na mchana. Jua na mvua hadi tushinde hila hizi.

Tunawaambia wanachama wetu na wale wanaotuunga mkono, CHADEMA ni chama kikubwa. Kina mtandao kila mahali, kuanzia Ikulu hadi polisi; na hivyo hakitakufa au kuzorota kwa mambo ya kupikwa.

Ni imani yangu kwamba amri ya mahakama itawafichua wote hawa na kuirudisha Tanzania katika amani yake. Ni lazima tufikie mahala watu hawa wafahamike mbele ya umma, tunataka wafahamu kuwa maisha ya mwanadamu yana thamani kuliko siasa chafu na ufisadi wanaouendeleza,” alihitimisha Marando.
Chanzo:http://freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=47920
Yawahusisha na matukio ya Ulimboka, Kibanda, Lwakatare

na Josephat Isango
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetaja majina ya baadhi ya watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikidai kuwa ndio wanaopanga mipango ya kishetani na kisha kuwasingizia watu wengine.
Hatua hiyo inakuja huku Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa chama hicho, Wilfred Lwakatare pamoja na Ludovick Joseph wakikabiliwa na kesi ya ugadi, wakidaiwa kupanga mikakati ya kuteka na kudhuru watu.
Sakata hilo limeibua gumzo hadi bungeni baada ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba kudai kuwa ndiye alipeleka video ya Lwakatare polisi na kukituhumu chama hicho akidai ni cha kigaidi.
Hata hivyo, CHADEMA kupitia kwa viongozi wake wakuu, wamekuwa wakidai kuwa video hiyo imetengenezwa na CCM kwa kushirikiana na vyombo vya dola ili kukidhohofisha chama hicho, na hivyo kuahidi kufichua mpango huo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Makao Makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam, Mjumbe wa Baraza Kuu wa CHADEMA, Mabere Marandu alisema kutokana na njama hizo kuanzia leo ataongoza jopo la mawakili sita wa chama kumtetea Lwakatare.

Saturday, April 13, 2013

Maisha Yanaendelea

1 bbee6
Kigwe Village, Morogoro.

  JK :AFUNGA SEMINA YA UTEKELEZAJI WA MFUMO MPYA WA UTENDAJI SERIKALINI

jk6 a8617
Rais Jakaya Kikwete akifunga semina kwa mawaziri na makatibu wakuu  walioketi na kupanga mikakati ya utekelezaji wa mfumo mpya wa kusimamia utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya maendeleo katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma. Mfumo huo unaanza kutekelezwa  kwa kutumia uzoefu wa Performance Management and Delivery Unit (PEMANDU) ya Malaysia. Mfumo huu utajumuisha uanzishwaji wa taasisi ya President’s Delivery Bureau (PDB) ambayo itafanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Katika mfumo huu, uchambuzi wa kina wa kimaabara (labs) utafanyika ili kuandaa programu za utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Awamu ya kwanza ya labs ilizinduliwa rasmi na Rais Kikwete  tarehe 22 Februari, 2013 na kukamilika Aprili, 2013. Maeneo ya awamu ya kwanza ya labs yanahusisha elimu, kilimo, nishati, mapato, maji na miundombinu ya uchukuzi. 

pe2 10d31
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali na Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue wakiwa na mawaziri na makatibu wakuu wakimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Performance Management and Delivery Unit (PEMANDU) ya Malaysia Dkt Idris Jala wakti wa kuujadili  mfumo mpya wa kusimamia utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya maendeleo uliokabidhiwa kwa wizara hizo sita katika   semina elekezi  kwa mawaziri na makatibu wakuu iliyofanyika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma. Mfumo huo unaanza kutekelezwa  kwa kutumia uzoefu wa PEMANDU, ambapo utajumuisha uanzishwaji wa taasisi ya President’s Delivery Bureau (PDB) ambayo itafanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Katika mfumo huu, uchambuzi wa kina wa kimaabara (labs) utafanyika ili kuandaa programu za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

pe3 b6ce3
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilali na Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue wakiweka saini kama wadhamini wa waraka wa  kujifunga katika utekelezaji wa mfumo mpya wa kusimamia utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya maendeleo uliokabidhiwa kwa wizara hizo sita katika   semina elekezi  kwa mawaziri na makatibu wakuu iliyofanyika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma. Mfumo huo unaanza kutekelezwa  kwa kutumia uzoefu wa Performance Management and Delivery Unit (PEMANDU) ya Malaysia. Mfumo huu utajumuisha uanzishwaji wa taasisi ya President’s Delivery Bureau (PDB) ambayo itafanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Katika mfumo huu, uchambuzi wa kina wa kimaabara (labs) utafanyika ili kuandaa programu za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

pe5 34774
Rais Jakaya Kikwete akiongea wakati wa semina kwa mawaziri na makatibu wakuu  kujadili mikakati ya utekelezaji wa mfumo mpya wa kusimamia utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya maendeleo katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma. Mfumo huo unaanza kutekelezwa  kwa kutumia uzoefu wa Performance Management and Delivery Unit (PEMANDU) ya Malaysia. Mfumo huu utajumuisha uanzishwaji wa taasisi ya President’s Delivery Bureau (PDB) ambayo itafanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Katika mfumo huu, uchambuzi wa kina wa kimaabara (labs) utafanyika ili kuandaa programu za utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Awamu ya kwanza ya labs ilizinduliwa rasmi na Rais Kikwete  tarehe 22 Februari, 2013 na kukamilika Aprili, 2013. Maeneo ya awamu ya kwanza ya labs yanahusisha elimu, kilimo, nishati, mapato, maji na miundombinu ya uchukuzi (Picha zote na Muhidin Michuzi).

Ugaidi Walivuruga Bunge

bunge 77749
Dodoma. Spika wa Bunge, Anne Makinda jana ni kama aliruhusu mvutano wa wazi baina ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wale wa Chadema ambao kila upande uliutuhumu upande mwingine kwa kuhusika kwa viendo vya ugaidi.
Licha ya kutozungumzia suala hilo moja kwa moja, lakini msingi wa tuhuma hizo ni kesi iliyofunguliwa mahakamani dhidi ya Mkurugenzi wa Usalama wa Chadema, Willifred Lwakatare ambaye anakabiliwa na makosa yanayomtuhumu kwa ugaidi.

Katika mazingira hayo ni dhahiri wabunge waliingilia uhuru wa mahakama kwani kesi husika iko mahakamani na Spika Makinda katika moja ya miongozo yake jana alisema: “Itabidi Kamati ya Kanuni ikutane kwa kuwa mambo yanayozungumzwa yako mahakamani, hivyo ni muhimu mahakama ikaheshimiwa.”
Kifungu cha 114 (1) cha Sheria ya Kanuni za adhabu (Penal Code), kinatoa adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja jela kwa mtu yeyote ambaye kwa namna yoyote anatoa matamshi yenye mwelekeo wa kushawishi uamuzi wa mahakama kwa suala lolote ambalo liko mahakamani likisubiri uamuzi.
Matamshi hayo ni yale yenye mwelekeo wa kupindisha mwenendo wa kesi husika au yenye mwelekeo wa kutaka uamuzi upendelee upande fulani au matamshi yenye lengo la kudhalilisha au kushusha hadhi ya mamlaka ya mtu ambaye kesi yake iko mbele ya mahakama.
Mjadala kuhusu ugaidi ulianza kuchipua juzi wakati Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alipowasilisha maoni ya kambi yake kuhusu hotuba ya Waziri Mkuu kwa kusema: “Umeibuka uchochezi mpya wa kisiasa wenye ubia kati ya chama tawala na vyombo vya dola na kinachoitwa ugaidi.”
Mbowe alisema kambi yake inashangazwa na uhodari wa Serikali katika kuchukua hatua kwa suala la mtu aliyebambikiwa kesi ya ugaidi kwa ushahidi wa kughushi kuwa yeye ndiye gaidi.
“Kambi yetu inasikitika sana kuona wale wote waliokuwa wakiwasiliana na hao wanaoitwa magaidi ambao pia ni viongozi wa CCM na washirika wao hawajachukuliwa hatua yoyote,” alisema Mbowe na kuongeza:
“Tunaulaani mkakati huu wenye nia ovu ya kufifisha demokrasia hapa nchini...mpango huu haramu hautafanikiwa ... na hili nalo likiachiwa likakomaa litaliingiza Taifa letu katika hatari nyingine ya machafuko.”
Jana suala hilo lilichukua sura ya kisiasa zaidi pale wabunge wawili; Mwigulu Nchemba wa Iramba Magharibi (CCM) na Tundu Lissu wa Mbunge wa Singida Mashariki walipochangia hotuba hiyo na kuzama katika eneo la ugaidi, hali iliyosababisha mvutano mkali bungeni.
Kauli ya Nchemba
Nchemba ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Tanzania Bara) aliishambulia hotuba ya Mbowe akieleza kuwa hakuna haja ya kuhangaika na suala la ugaidi kwa kuwa Chadema ndiyo wanahusika nalo kwa kupanga kumdhuru mwandishi wa habari.
soma zaidi http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1747134/-/129yj3y/-/index.html#disqus_thread

Friday, April 12, 2013

Maisha Yana................................

DSCF9477 86da1
Mwambao Wa Ziwa Nyasa

Dk. F. Mghanga AKUMBUKA ILIVYOKUWA TANZIA YA EDWARD MORINGE SOKOINE

sokoinebc1 48899
Edward Moringe Sokoine (1938 - 1984)
Ni miaka ishirini na tisa iliyopita. Siku ya Alhamisi, majira ya jioni kama saa kumi na moja. Anga la jiji la Dar es Salaam lilikuwa jeusi likihanikizwa na mawingu madogo madogo yaliyojikusanya kuashiria kamvua kalikokuwa kametawala siku hiyo. Hizi ni nyakati za masika katika sehemu kubwa ya nchi.Ndo kwanza nimerudi toka shule, tayari nimeshajipakia ugali wangu wa njano (Yanga) na maharage ya Iringa.
Nipo mtaani nikicheza na wenzangu chandimu. Hatuna viatu, tupo pekupeku lakini hatujali kitu. Maisha yalikuwa mazuri bila kujua adha na masumbufu ambayo wazazi walikuwa wanayapitia ili kutufanya watoto wao tuweze kwenda chooni.Nikiangalia pembeni, akina mama walikuwa wamekaa wakisukana na wengine walikuwa kwenye vibustani vyao wakipalilia matuta ya viazi vitamu. Hakika hatukujua lililokuwa limetokea masaa machache yaliyopita hapa nchini kwetu.Lakini ghafla redio zikaanza kupiga wimbo wa taifa.

Si aghalabu kusikia wimbo wa taifa mida kama ile tena kipindi kile kisichokuwa na sikukuu wala mgeni yeyote wa kitaifa. Haiyumkiniki kuna jambo kuu limetkea. Katika utoto wangu, ghafla nikaacha kucheza, akina mama waliokuwa wakisogoa nao wakapigwa na ubaridi wa ghafla. Katika mshawasha wangu wa kitoto nikaijongelea redio kutaka kujua kilichojiri jioni hiyo ya Alhamisi nyeusi.
Dakika kadhaa zilipita kabla ya wimbo wa taifa kuisha.Sauti iliyojaa huzuni ikasikika. Hata katika utoto wangu, naweza kusema kwa hakika kuwa sauti ile ilikuwa katika huzuni na majonzi na ilionesha ni ya mtu aliyekuwa katika kilio muda si mrefu uliopita. Naam, ilikuwa ni sauti ya hayati baba wa Taifa. Nayakumbuka maneno yake mpaka sasa. Hivi ndivyo alivyosema:"Ndugu wananchi, leo mnamo majira ya saba mchana, ndugu yetu, mwenzetu, Waziri Mkuu na Makamu wa Pili wa Rais, Edward Moringe Sokoine amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea huko Morogoro wakati akilejea Dar es Salaam kutoka Dodoma kwenye mkutano wa Bunge"Naam, hiyo ndiyo sababu ya kupigwa kwa wimbo wa Taifa jioni ile. Utando mweusi ukatanda.
Simanzi ikatawala. Vilio vikasikika, furaha ikatoweka. Giza la mawingu meusi likaongezea upotevu wa furaha. Nikausikia ukelele mkuu kutoka kwa mama mmoja aliyekuwa ameshika jembe akipalilia bustani yake "Mama wee mkombozi wetu amekufa, nani atatutetea sisi wanyonge?" Hakika ndivyo aliomboleza mama yule.Huzuni kuu ikaniingia ghafla. Nikajiwazia "Sokoine kafa? Hapana, amekufa?" Nafsi ilikataa kuamini, akili ya utoto ikaniambia haiwezekani. Ghafla machozi yakaanza kunitiririka. Naam nililia. Nilimlilia mzalendo wa kweli. Wazazi walilia, wananchi walilia, hata Nyerere alilia tena hadharani, hakulia kiunafiki alilia kweli.Watanzania wapenda haki tulilia, tulimlilia mpenda haki mwenzetu.
Sokoine mzalendo wa kweli. Mwana wa Kitanzania asilia, mtetezi wa kweli wa wanyonge, mchapakazi, mpigania mema ya nchi.Naam, yawezekana kwa wengine ameshafutika lakini kwa wapenda haki, Sokoine atabaki kuwa kioo chetu daima. Huyu ndiye mtu aliyekuwa na sifa nilizozitaja wakati ule kwenye ile ndoto yangu ya "Namuona mtu huyu". Yawezekana alikuwa na kasoro zake kama mwanadamu na hata kiutendaji lakini daima nia yake njema kwa watu wake iliyafunika makosa yake hayo. Alipendwa na wanyonge na kuchukiwa na wezi, wabadhiifu wa mali ya umma na wahujumu uchumi (leo tunawaita mafisadi). Huyu ndiye aina ya mtu tuliyemuhitaji Tanzania ya leo.
Nimemkumbuka Sokoine, mtanzania mzalendo mwana mpenda nchi aliyenifanya nihisi msiba wake kuwa unanihusu kwa ukaribu mno. Naam, wajamaa kama kina Subi lazima watamkumbuka mtu huyu na kumuomboleza daima.Mungu alipenda kumchukua ingawa tuliona amemchukua mapema mno.Pumzika kwa aman

JK azindua mradi wa miundombinu ya umeme dodoma

mcc7 411fd

Rais Jakaya Kikwete akibofya kitufe huku akishuhudiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC), Daniel Johannes na  Balozi wa Marekani nchini Alfonso Lendhardt wakishuhudia uzinduzi huo wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya kusambaza umeme mkoani Dodoma katika kijiji cha Mkoka, wilaya ya Kongwa, Dodoma

mcc6 d0448
Rais Jakaya Kikwete akifunua pazia huku Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC), Daniel Johannes na Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lendhardt wakimpongeza kwa uzinduzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya kusambaza umeme mkoani Dodoma chini ya ufadhili ya serikali ya Marekani kupitia MCC katika kijiji cha Mkoka, wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma
                                                                 
mcc9 94ae3
Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC), Daniel Johannes katika picha ya pamoja na viongozi na wadau mbalimbali katika sherehe ya uzinduzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya kusambaza umeme mkoani Dodoma chini ya ufadhili ya serikali ya Marekani Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali na Afisa Mtendaji Mkuu wa kupitia MCC katika kijiji cha Mkoka, wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma (Picha zote na Muhidin Muchuzi)

Magazeti magazeti

DSC 0080 b4ef5

DSC 0081 a6250
DSC 0082 d1df0
DSC 0083 8e6de
DSC 0084 3c7f0
DSC 0085 eff95
DSC 0086 fb7b5

DSC 0088 5a643
DSC 0089 a687d
DSC 0090 8c8e5
DSC 0091 c0bf6
DSC 0092 5e88e
DSC 0093 5aca6
DSC 0094 7ec12
DSC 0096 6b159
DSC 0097 f1d1b
DSC 0098 6390f

Kagera Press Club yafanya mkutano Mkuu Wa Mwaka 2013

Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Kagera(KPC) kimefanya Mkutano Mkuu wa mwaka,ambapo pamoja na mambo mengine kimejadili na kupitisha wanachama wapya.

Katika Mkutano huo uliofanyika ukumbi wa St Francis,mjini Bukoba pia wanachama walijadili taarifa mbali mbali zilizowasilishwa na uongozi na kufikia maazimio mbalimbali.

Miongoni mwa maazimio ya Mkutano huo,ni kuendeleleza umoja kwa ajili ya ustawi wa chama,huku waandishi wa habari wakikumbushwa kufanya kazi zao kwa maadili na weredi.

Pia Mkutano huo ulimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe,pamoja na wadau wengine wa Kagera Press Club ambao kwa nyakati tofauti wameunga mkono juhudi za Umoja huo ili kufikia malengo yake.

Baadhi ya waandishi wa habari katika matukio mbalimbali ndani na nje ya ukumbi,Baadhi wakikagua vifaa vya kisasa vya kazi na wengine wakitoa michango yao.

Katibu wa chama cha waandishi wa habari mkoa Ndg Phinias Bashaya na Mwenyekiti John Rwekanika
 Method Kalikila wa Gazeti la Rumuli na Livinus Feruzi wa Gazeti la Majira wakifuatilia mjadala
Ayoub Mpanja(Radio Free Africa)Ashura Jumapili-Tanzania Daima
Mathias Byabato-Channel Ten
Antidius Kalunde Mkuu Wa Bukoba Jamii Akijaribu Mambo
Ashura Jumapili-Tanzania Daima
Mdau Arodia Domonick,Radio Karagwe akimpa mtoto haki yake
Winrida Saimon Mwandishi wa Gazeti la Ijawebonele linalomilikiwa na ELCT/Dayosisi ya Kaskazini Magharibi
Meddy Mulisa-Mhariri Radio Kasbante na mwandishi wa Daily News akinukuu mambo muhimu wakati wa mkutano.
Anaonekana Jonas Mchunguzi-Mwandishi na mtaalamu wa kupiga picha  za habari na matukio akikagua kamera ya kisasa.
 Prudence Kibuka-Nipashe  akiendeleza majadiliano na wenzake wakati wa mapumziko.
 Picha kwa Hisani ya Phinias Bashaya

Waganga Wa Tiba asilia Watakiwa Kutowalaza Wagonjwa Majumbani Mwao

Bukoba.
 
WAGANGA na wakunga wa tiba asilia katika wilaya ya Bukoba mkoani Kagera wametakiwa kutolaza wagonjwa wanaowahudumia majumbani mwao, ili kuepuka kupata kesi za mauaji pindi mtu atakapokufa kwa bahati mbaya wakati akipatiwa huduma.
 
Kauli hiyo ilitolewa juzi katika uwanja wa Uhuru na mkuu wa wilaya ya Bukoba,  Bi Zipporah Pangani wakati akiwakabidhi vyeti vya serikali waganga 13 ambavyo vinawaruhusu kufanya kazi ya kutoa tiba kwa jamii kisheria.
 
Bi  Pangani alisema kuwa waganga wa tiba asilia na wakunga wanaofanya hivyo wanakiuka sheria na taratibu za nchi, na kuwa kama kuna mganga anataka kutoa huduma hiyo lazima ajenge kituo chenye hadhi hiyo ambacho pia lazima kipate kibali kutoka serikalini cha kulaza wagonjwa.
 
Aidha aliwataka waganga hao kuwashauri wananchi kupata vipimo sahihi vya kitaalam kuhusu magonjwa yanayowasumbua ili kumwezesha mganga kutoa tiba ya ugonjwa anaoufahamu badala ya kutibu kwa kubahatisha.
 
“Mtu anaweza kuwa anaumwa typhoid (homa ya matumbo) unamg’ang’ania wakati ungeweza kushirikiana na daktari wa hospitali akapata vipimo sahihi na hatimaye mkashirikiana kumtibu maana wote nia yenu ni moja ya kutoa tiba kwa wananchi” alisema Bi Pangani.
 
Alisema kuwa vyeti walivyopatiwa ni vya muda na kuwa baada ya hapo mganga ambaye atafanya kazi bila kusababisha matatizo katika utendaji wake ndiye atapewa cheti cha kudumu na wizara yenye dhamana.
 
Akizungumza katika mkutano huo mfupi wa kukabidhiwa vyeti hivyo, mwenyekiti wa chama cha waganga na wakunga wa tiba asilia (STAMATA) katika manispaa ya Bukoba,  Bw. Habibu Mahyoro alisema watu wanaoishi kwa kutegemea viungo vya binadamu sio waganga bali ni matapeli na ni wachawi.
 
Bw. Mahyoro aliiomba serikali kuwawezesha kupata vitendea kazi ikiwamo vyombo vya usafiri ambavyo vitatumika kutoa elimu kwa jamii kwa lengo la kupunguza matukio ya wanaojihusisha na matendo maovu ikiwamo mauaji ya albino na vikongwe.
 
Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo STAMATA mkoa wa Kagera ilianzishwa mwaka 2011 ikiwa na wanachama 47, ambapo sasa ina wanachama 89 kutoka katika wilaya za Missenyi, Bukoba na Karagwe  na wanachama 13 miongoni mwao ndio wamepatiwa vyeti.
 
Mwisho.