Wednesday, February 27, 2013

RAIS KIKWETE ATEMBELEA JKT

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na uongozi wa juu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) jijini Dar es salaam alipotembelea leo February 27, 2013. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange pia walihudhuria.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa juu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) jijini Dar es salaam alipotembelea leo February 27, 2013. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange pia wapo.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya saa toka kwa  Mkuu  wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael Muhuga huku  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange wakishuhudia. Saa hiyo imeandaliwa na makamanda wa JKT kumpongeza Rais Kikwete kwa kurejesha mafunzo ya jeshi la ulinzi kwa mujibu wa sheria kuanzia mwaka huu.

UZINDUZI WA MPANGO GSI

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikata utepe kuashiria uzinduzi  wa Mpango  Mkakati  wa Miaka Mitano  wa Taasisi  ya  GSI Tanzania  kwenye ukumbi wa hoteli ya Blue Pearl  jijini Dar es salaam Februari 27, 2013. Wapili kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dr.Abdallha Kigoda. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Joyce Mapunjo.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama mikoba katika maonyesho yaliyoambatana na Uzinduzi wa  Mpandgo Mkakati wa Miaka  Mitano wa Taasisi  ya GSI Tanzania kwenye ukumbi wa Hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es slaam Februari  27, 2013. Kushoto ni Waziri wa Viwanda,Biashara na Masoko, Abdallah Kigoda na kulia ni  Katibu  Mkuu wa Wizara hiyo, Joyce Mapunjo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Tuesday, February 26, 2013

MANDHALI YA CHAMA CHA MSINGI MWEYANJALE KINACHOUNDA KCU 1990 LTD

 Jengo la chama cha msingi cha Mweyanjale kinachojihusisha na kilimo cha kahawa hai 'organic coffee' kinachounda chama cha ushirika Kagera (KCU 1990 LTD).
 Mwenyekiti wa chama hicho, Leopord Mtalemwa akiwa nje ya jengo la chama hicho.
 Maeneo yanayozunguka chama hicho.
Mtalemwa akiongea na waandishi wa habari.

Monday, February 25, 2013

NDANI YA MANISPAA YA BUKOBA KWAWAKA MOTO

MANISPAA ya Bukoba hapakaliki, hii inafuatia hatua ya madiwani wa manispaa hiyo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kususia kikao chama hicho ambacho hufanyika kabla ya kikao cha baraza la madiwani.


Baadhi ya madiwani wa CCM wamesusia kikao hicho baada ya watu wasiofahamika kusambaza waraka unaowakashfu.


Waraka huo unawakashfu madiwani kumi ambao ni pamoja na madiwani wa CCM 8 na wa vyama vya vya upinzani vinavyowaunga mkono 2.


Mwandishi wa waraka huo anatoa kashfa nzito kwa madiwani waliosaini waraka wa kutaka Mstahiki Meya wa manispaa ya Bukoba Anatory Amani apigiwe kura za kutokuwa na imani naye kufuatia tuhuma mbalimbali zinazomkabili.


Baadhi ya madiwani waliiongea walidai mgogoro ulioko kati ya Meya huyo na madiwani kuwa umeishaigawa CCM, kwa anyakati tofauti walisema kuwa hawana imani na meya huyo na ndio maana wanataka kumng'oa.


Walisema kuwa hata kama nyaraka zikisambazwa na kuwakasfu kamwe hawatarudi nyuma, "tunajua waraka huu aliyeuandaa hivyo hatuna wasiwasi nao, moto wetu uko palepale wa kumuondoa Amani madarakani" walisema bila kutaka majina yao yatakjwe.

Walisema kuwa hawataki kuongozwa na kiongozi yoyote mwenye huruka ya ufisadi ambaye anabuni miradi mingi kwa maslahi yake binafsi," Kiongozi yoyote atakayekuwa na mlengo wa kutaka kuifilisi manispaa tutakula naye sahani moja" walimaliza.


Manispaa ya Bukoba sasa kumewaka moto, pande zote zinazopingana kila mmoja anijiona ni mbabe, pande zinazopingana moja unaundwa na kundi la waziri wa maliasili na utalii, Balozi Khamis Kagasheki na upande nyingine inaongozwa ana Meya wa manispaa ya Bukoba Anatory Amani.

Kambi ya Kagasheki inamtaka Meya wa manispaa ya Bukoba Amani anga'atuke na kambi ya Amani inapinga mapendekezo hayo.



WAZIRI PINDA AKUTANA NA BALOZI WA CANADA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akisalimiana na Balozi wa Canada nchini, Mhe.Alexandre Leveque kabla ya mazungumzo yao, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Februari 25, 2013. (Picha na Ofisi a Waziri Mkuu)

VIONGOZI WASAINI MPANGO WA AMANI WA UMOJA WA MATAIFA

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maal: umu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 24, 2013
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe Ban Ki-moon akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maal: umu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 24, 2013

Monday, February 18, 2013

WAJERUMANI WATOA MSAADA WA VITABU VINAVYOELEZEA HISTORIA YA TANZANIA

 Mfano wa nyumba ya msonge iliyokutwa kwenye jengo la mambo ya kale inayomilikiwa na kampuni ya utalii ya Kiroyera.
 Meneja uendeshaji wa kampuni ya utalii ya Kiroyera, William Rutta akiangalia vitabu vilivyotolewa na Mrs.Edith Gottschling raia wa Ujerumani ambaye mme wake marehemu Klaus alikuwa mwenyekiti wa kwanza wa urafiki kati ya nchi ya Ujerumani na Tanzania.
 Yusto Mchuruza aliyekabidhi vitabu vilivyotolewa nba mjerumani akitoa ufafanuzi wa vitabu hivyo.
 Mambo ndania ya jumba linalohifadhi mambo ya kale.
 Yusto Mchuruza akimkabidhi vitabu William Rutta.

Saturday, February 16, 2013

SOMO LA DINI NA MAADILI KUFUNDISHWA RASMI SHULENI NA VYUONI TANZANIA NZIMA



MIKOA ya Kagera na Kigoma imezindua rasmi mihtasari  ya  somo la Dini na Maadili litakalofundishwa kuanzia shule za awali, msingi sekondari hadi vyuo vikuu.

Mihtasari hiyo imezinduliwa  rasmi na UMAKA (Umoja wa Madhehebu Kagera) wakishirikiana na serikali baada ya mihtasari hiyo kupitishwa rasmi na Kamishina wa Elimu ili isambazwe katika shule zote tayari kwa kutumika kufundishia wanafunzi katika ngazi mbalimbali.

Somo la Dini na Maadili limerasimishwa rasmi kufundishwa shuleni na vyuoni baada ya UMAKA kuona umuhimu wa kuwa na mihtasari ambayo ni rasmi na inayotambuliwa na serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ili itumike kufundishia watoto pia na kutahiniwa kama masomo mengine.

Umoja wa Madhehebu Kagera  (UMAKA) ulianzisha mchakato wa kuandaa mihtasari ya somo la Dini na  Maadili  wakishirikiana na serikali ili somo hilo liwe na mihtasari inayofanana katika kufundishia wanafunzi kuliko hapo awali ambapo somo hilo halikuwa na mihtasari ya kufundishia.

Kupitia somo la Dini na Maadili, wanafunzi  watafunzwa maadili mema ya kupendana na kuwapenda watanzania wenzao, kujenga jamii yenye kuwajibika na kumcha Mwenyezi Mungu bila kujali tofauti za ki-imani kwao, pia kulelewa na kukua katika malezi ya kufuata sheria na utawala bora.

Serikali katika kuboresha utumiaji wa Mihtasri mipya ya somo la Dini na Maadili imeagiza somo hilo likaguliwe na wakaguzi wa serikali pamoja na walimu wakuu wa shule kama masomo mengine na kutahiniwa katika ngazi zote hadi ile ya taifa.

Pia katika kuona umuhimu wa somo la Dini na Maadili kufundishwa shuleni, serikali imeamua mihtasari ya somo hilo itumike Tanzania nzima badala ya Mikoa ya Kagera na Kigoma walioshirikiana na serikali kuandaa mihtasari hiyo  ili wanafunzi wote wa Tanzania wafunzwe dini na maadili ya kitanzania.

UMAKA ilianzishwa miaka ya 1980 ikiwa na lengo la kushirikiana na Serikali na kushauri masuala mbalimbali yahusuyo maadili, amani, usalama na maendeleo ya jamii ya watanzania. UMAKA inajumuisha  Balaza la Maaskofu Tanzania (TEC),  Balaza la Waislam Tanzania (BAKWATA), na Baraza la Wakristo Tanzania (CCT).

MKUTANO WA UZUNDUZI WA SOMO LA DINI NA MAADILI KAGERA

 Baba Askofu Nestory Timanywa Jimbo Katoliki La Bukoba  Ambaye Amestaafu hivi Karibuni Akitoa Mada ya Historia ya Maadili Tanzania Ambapo Alisistiza sana Uwajibikaji wa Wazazi, Walezi na Viongozi Mbalimbali Kuwajibika Kuwalea Watoto katika Maadili Mazuri.
 Wajumbe wa Kikao cha Uzinduzi wa Mihtasari ya  Somo la Dini na Maadili Wakisiliza kwa Makini na Utulivu.
Hawa ni Viongozi wa Dini Mkoani Kagera Waliohudhuria Uzinduzi Mihtasari ya Somo la Dini na Maadili,Katikati Kutoka Kulia Ni Askofu Elisa Buberwa KKKT, Askofu Nestory Timanywa Jimbo Katoliki la Bukoba, Askofu Severine Niwemugizi Jimbo Katoliki la Rulenge, Nyuma Kabisa ni Masista na Mapadre Kutoka Kigoma, na Mstari wa Kwanza ni Viongozi wa BAKWATA Mkao wa Kagera.

mama kikwete aendelea na ziara lindi

IMG_8445
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasalimia watoto na wananchi wa kata ya Msinjahili waliohudhuria mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Kitumbikwela kilichoko katika wilaya ya Lindi Mjini tarehe 17.2.2013


IMG_8485Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wa Kata ya Msinjahili wakishangilia wakati wa mkutano wa hadhara ulihutubiwa na Mjumbe wa NEC wa wilaya ya Lindi Mjini Mama Salma Kikwete katika kijiji cha Kitumbikwela tarehe 17.2.2013.
IMG_8499Wanachama wapya wa Chama Cha Mapinduzi na jumuia zake wakila kiapo mara baada ya kukabidhiwa kadi na Mjumbe wa NEC wa Lindi Mjini Mama Salma Kikwete katika kijiji cha Kitumbikwela tarehe 17.2.2013.
IMG_8525
Mjumbe wa NEC wa Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wananchi wa kata ya  Msinjahili kwenye kijiji cha Kitumbikwela tarehe 17.2,2013.
 PICHA NA JOHN LUKUWI

Monday, November 5, 2012

MASSAWE AZINDUA MNARA WA VODACOM KISIWA CHA GOZIBA


Wakazi wa Kisiwa cha Goziba Kilichoko Wilayani Muleba wamekombolewa na kampuni ya mawasIliano ya Vodacom Tanzania baada ya kampuni hiyo kuzindua mnara wake wa mawasiliano katika kisiwa hicho ambapo wananchi sasa wanaweza kuwasiliana popote Tanzania na duniani kwa kutumia mtandao wa mawasiliano wa Vodacom.

Mnara wa Vodacom Kisiwani Goziba ulizinduliwa jana tarehe 30/10/2012 na Mhe. Kanali Mstaafu Fabian I. Massawe aliyembatana na Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhe. Lembrisi Kipuyo. Pia Katika uzinduzi huo Kampuni ya Vodacom iliwakilishwa na Salum Mwalimu ambaye ni Meneja Mahusiano ya nje wa Kampuni hiyo.

Katika Uzinduzi huo Meneja Mahusiano ya nje wa Vodacom Salum Mwalimu aliwaomba wananchi wa kisiwa cha Goziba kuulinda na kuutunza mnara huo kwani alisema kuwa mnara huo umejengwa kwa gharama kubwa, ni zaidi ya mara mbili ya gharama ya kujenga mnara mmoja katika eneo la nchi kavu. Pia aliwahakikishia wananchi wa Goziba kuwa huduma nyingine mbalimbali kama M- Pesa zitapelekwa kwao.

Wananchi wa Kisiwa cha Goziba ambao ni 6000 pamoja na kuchangia asilimia 25 ya pato la wilaya ya Muleba, walisema kuwa kabla ya mnara huo hawakuwa na aina yoyote ya mtandao wa simu, pia bado wanakabiliwa na changamoto katika huduma za kijamii kama shule, Zahanati, na maji safi na slaama. Vilevile usafiri wa kuaminika na kukumbwa na ujambazi wa mara kwa mara na kunyanganywa mali zao.

Wananchi hao waliishukuru Kampuni ya Vodacom Tanzania kwa kuwakumbuka kupitia mbunge wao Charles Mwijage wa Jimbo la Muleba Kasikazini kuwawekea mnara huo ambao utawatatulia baadhi ya kero zao kama kero ya ulinzi kwani itakuwa rahisi kutoa taarifa za uharifu kwa haraka sana pale unapotokea.

Mkuu wa Mkoa alisistiza sana wananchi hao kuutumia mtandao huo kwa manufaa yao na taifa lakini siyo kutumia simu zao kwa mambo ya uhasherati kwani UKWIMWI bado unatisha sehemu za visiwani. Aliwasistiza wananchi hao kuwa waaminifu walioko kwenye ndoa, kutumia kinga na vijana kusubiri muda wao wa kuoa ndiyo waoane. Pia Mhe. Massawe alitumia muda huo kuwagawia kinga (kondomu) wananchi hao na kuwashauri kuzitumia ili kupanga uzazi na kujikinga na virusi vya UKWIMWI.

Vodacom Tanzania tayari pia imetoa Tshs. 4,200,000/= kwa ajili ya ujenzi wa zahanati, pia Mkuu wa Mkoa naye alitoa Tshs 500,000/= ili kuendeleza jengo la zahati ya Goziba ambalo limefikia hatua ya Msingi. Changamoto ni vifaa vyote vya ujenzi kupatika na nje ya kisiwa hicho hata matofari ya kujengea yafyatuliwa Mwanza na kuletwa kisiwani humo isipokuwa mawe tu.

Mnara wa Vodacom siyo tu ni faida ya wakazi wa Goziba na visiwa vya jirani isipokuwa imekuwa mkombozi kwa Manahodha wa mitumbwi iliyokuwa inapotea mara kwa mara na kujikuta sehemu nyingine kwasababu ya kisiwa hicho kutoonekana kwa mbali. Mnara huo umekuwa ndiyo dira ya nahodha wanaokwenda huko kwasasa.

Wilaya ya Muleba inavyo visiwa 36 na 24 tu ndivyo vinakaliwa na wananchi. Pia serikali ianaendelea na juhudi za kuhakikisha huduma za kijamii zinapatikana katika kisiwa hicho ambapo inatarajia katika miaka miwili ijayo itakuwa tayari imeanzisha kituo cha Polisi kisiwani humo.

Imeandikwa na : Sylvester Raphael
Afisa Habari Mkoa
KAGERA @2012

 
MASSAWE AFANYA MAAJABU ATEMBELEA KISIWA CHA GOZIBA

Mandhari ya kisiwa cha Goziba.

Salum Mwalim Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom Akiongea na Wananchi wa Kisiwa cha Goziba.

Mkuu wa Mkoa kanali mstaafu Fabian Massawe, Katibu wa CCM, Kagera na Salum Mwalim Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom na RPC Kagera Philipo Karangi Wakiwasili Kisiwani Goziba, Massawe ni mkuu wa mkoa wa kwanza mkoani Kagera kutembelea kisiwa hicho tangu nchi ipate uhuru.

Saturday, November 3, 2012

Mamlaka Ya Mapato Kagera Yazindua Wiki Ya Mlipa Kodi

Baadhi ya maoofisa wa mamlaka ya mapato mkoani Kagera wakisikiliza hotuba ya ufunguzi iliyokuwa inatolewa  na mkuu wa wilaya ya Bukoba Bi Ziporah Pangani.

Mmoja wa maofisa wa TRA

Mkuu wa wilaya ya Bukoba Bi Ziporah Rion Pangani akitoa hotuba ya ufunguzi wa wiki ya mlipa kodi ulifanyika kwenye ukumbi wa chama cha msalaba mwekundu.

Mameneja wa TRA, kulia ni Bw. Mgimba na kushoto ni Magere.

KIKAO CHA MTANDAO UNAOYAUNGANISHA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KAGERA

 Dr George Buberwa akiongea wakati wa kikao cha mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali Kagera KANGONET  kilichofanyika kwenye ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Kagera.
 Wajumbe halali wa KANGONET.
 Wajumbe wengine.

 Bw. Kiiza alikuwa mmoja wa walioudhuria kikao cha KANGONET, wajumbe wa mtandao huo walikuwa wakulalamikia uongozi ulioko madaraka ambao ni pamoja na Katibu Christan Byamungu na mwenyekiti Yusto Mchuruza, walisema viongozi hao hawana imani nao.
 Kimani na Michael.

Afisa maendeleo ya jamii mkoani Kagera Charles Mwafimbo ndiye aliyeongoza kikao hicho.

JK: Azindua Taasisi Sayansi Na Teknolojia Ya Chuo Kikuu Cha Nelson Mandela Arusha

Rais Jakaya Kikwete, akikata utepe kuweka jiwe la Msingi ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo cha Kikuu cha Nelson Mandera, jijini Arusha, Novemba 02, 2012. Kushoto kwake ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. DMohammed Gharib Bilal. Kushoto ni Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Burton Mwamila
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandera, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo cha Kikuu cha Nelson Mandera, jijini Arusha , Novemba 02, 2012. Kulia ni Rais Jakaya Kikwete, aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo

 Rais Jakaya Kikwete, akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo cha Kikuu cha Nelson Mandera, jijini Arusha, Novemba 02, 2012. Kulia kwake ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. DMohammed Gharib Bilal. Kulia ni Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Burton Mwamila.
 Rais Jakaya Kikwete, akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Makamu wake na Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandera, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Burton Mwamila, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo cha Kikuu cha Nelson Mandera, jijini Arusha
                       
                                     Picha na OMR

Magazeti

Wabunge Vinara Wa Rushwa Hatarini




 BUNGE limeandaa kanuni za maadili ili kuwadhibiti wabunge ambao wanatumia mianya ya kanuni zilizopo kufanya makosa mbalimbali ikiwamo kujihusisha na vitendo vya rushwa. 

Habari zilizopatikana mjini Dodoma na kuthibitishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Shughuli za Bunge, John Joel zinaeleza kuwa hatua hiyo ya Bunge inatokana na kuongezeka kwa wabunge kutuhumiwa kwa makosa mbalimbali wanayoyafanya wakiwa nje na ndani ya Bunge. 

Joel alisema masharti hayo mpaka sasa yapo katika hatua ya kuchapwa na kwamba muda siyo mrefu maadili hayo ya kanuni yatatoka. “Tupo katika hatua ya kuichapa code of conduct (Kanuni za maadili) hiyo na kwamba muda si mrefu itatoka na kuanza kutumika.”

 Alisema wamegundua kuwa baadhi ya wabunge wanatumia kanuni za Bunge zilizopo kuzikwepa na kufanya mambo yasiyofaa ambayo yanashusha hadhi ya Bunge, hivyo masharti hayo mapya yatawabana zaidi.

 Kauli hiyo ya Joel inakuja siku mbili baada ya kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa madai ya kutoa rushwa kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa Jumuiya ya Wazazi uliomalizika jana mjini hapa. Zungu ambaye pia ni Mbunge wa Ilala, alikamatwa na makada wengine wa chama hicho saa 4:30 usiku katika kituo cha mafuta akidaiwa kujaribu kutoa rushwa ya Sh100,000 kwa wajumbe wa mkutano huo wa wazazi. Hata hivyo, Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Dodoma, Eunice Mmari juzi alikaririwa akisema vijana wake walimtia nguvuni Zungu katika Hoteli ya Golden Crown akiwa na wapambe wake wakiendelea kugawa fedha kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa wazazi.

 Mbunge mwingine ambaye ana kesi mahakamani kwa tuhuma za kujihusisha na rushwa ni Omar Badwel wa Bahi. Badwel anatuhumiwa kuomba rushwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga mkoani Pwani, Zipora Liana.

 Hatima ya Zungu, Badwel Kuhusu kukamatwa kwa Zungu, Mkurugenzi huyo wa Idara ya Shughuli za Bunge, alisema kuwa Bunge halitamchukulia hatua yoyote na badala yake linaviachia vyombo vya dola vifanye kazi yake. 

Joel alisema suala la Zungu bado ni tuhuma hivyo, ataendelea kuwa Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Ilala hadi hapo kama itathibitika kuwa ametenda kosa mahakamani. Alisema suala lake ni sawa na la Mbunge Badwel ambaye ana kesi mahakamani ya kutuhumiwa kujihusisha na rushwa, lakini bado anaendelea kuwa mbunge.

 Hatua hii ya Bunge pia inakuja wakati bado ripoti ya Kamati ya Bunge iliyoundwa kuchunguza tuhuma za wabunge kujihusisha na rushwa wakati wa Bunge la Bajeti mwaka huu, ikisubiriwa kusomwa bungeni. Agosti 2, mwaka huu Spika Makinda aliunda kamati ndogo ya kuchunguza tuhuma za rushwa zilizokuwa zikiwakabili baadhi ya wabunge ambao walidaiwa kwamba walihongwa ili kuikwamisha Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini.

 Kuundwa kwa kamati hiyo, kulitanguliwa na tukio la kuvunjwa kwa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini Julai 28, mwaka huu pia kutokana na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo, kujihusisha na rushwa na wengine kutumia nafasi zao kujinufaisha kwa kufanya biashara na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ambalo lipo chini ya kamati hiyo.

 Mabilioni ya Uswisi Katika hatua nyingine, Serikali imeanza kufanya uchunguzi wa kina ili kujua ukweli na kuwachukulia hatua watu wote walioficha mabilioni ya fedha nchini Uswisi. Waziri Mkuu alisema bungeni jana kuwa, mara baada ya uchunguzi huo kukamilika Serikali itatoa taarifa kuhusu uchunguzi huo. Pinda alikuwa akijibu swali aliloulizwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe wakati wa kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu jana asubuhi. 

“Jambo hili kwa uzito wake, tumeanza kulifanyia uchunguzi ili kujua ukweli wake na hatua stahiki za kuchukua, tukimaliza tutatoa kauli kama ilivyo kawaida yetu, “ alisema. 

Mbowe katika swali lake alitaka kujua Serikali imechukua hatua gani kuhusu taarifa za kuwapo kwa mabilioni ya fedha katika akaunti za benki mbalimbali nchini Uswisi ambazo zimewekwa na baadhi ya vigogo serikalini na viongozi wastaafu.

 Katika Bunge la Bajeti lililopita, Kambi ya Upinzani ililiibua suala hilo wakati wa hotuba yao ya Bajeti wakieleza kuwa kuna jumla ya Sh360 bilioni zilizofichwa na baadhi ya Watanzania katika benki mbalimbali nchini Uswisi. 

Taarifa kutoka Benki Kuu ya Uswisi inaonyesha kuwa baadhi ya fedha hizo zimewekwa katika akaunti za vigogo hao na kampuni za mafuta na gesi zilizopo nchini. Jumanne wiki hii, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika alipokuwa akichangia azimio la kuridhia marekebisho ya pili ya Mkataba wa Ushirikiano kati ya Jumuiya ya Nchi za Ulaya na Nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (ACP), alisema Serikali iutumie ushirikiano huo kurejeshwa mabilioni yaliyofichwa nchini Uswisi. 

Naye Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe akihutubia mkutano wa hadhara Rombo, mkoani Kilimanjaro Oktoba 26 mwaka huu, alimlipua Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru), Dk Edward Hoseah, akidai kuwa bosi huyo ameandika barua Uswisi, akieleza kwamba Tanzania haina masilahi na mabilioni ya fedha yaliyofichwa katika benki za nchini hiyo. Hata hivyo, Dk Hoseah alikanusha akisema kuwa tuhuma hizo hazina ukweli wowote.

                                              Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz/habari

Thursday, November 1, 2012

Bukoba Na Senene Tena

 Baadhi ya wakazi wa mji wa Bukoba wakichangamkia senene.
 Wanafunzi hawakubaki nyuma, huyu ni mmoja wa wanafunzi waliochangamkia senene wajianza kuonekana mkoani Kagera.
 Kitoweo hicho kikiwa sokoni.
 Senene wakirandaranda juu ya magunia.

Wafanyabiashara ya senene wakifanya vitu vyao.