Tuesday, October 9, 2012

Matukio Mbalimbali

 Dr Diodorus Kamala balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji akiwa katika picha ya pamoja na Watanzania na Watanzania waliomkaribisha nchini humo.
 Mke wa Balozi Kamala kulia akiwa na baadhi ya Watanzania waliomkaribisha nchini Ubelgiji.
Watoto wa Balozi Kamala waliovaa nguo za zambarau walikuwa miongoni mwa walioudhuria sherehe ya kumkaribisha na Dr. Kamala nchini Ubelgiji  iliyoandaliwa na Watanzania waishio nchini humo.

UONGOZI WA YANGA WAKANUSHA HABARI ZA UZUSHI

 Mchezaji wa yanga Osca Joshua akiwa ndani ya chumba chake.
 Wachezaji wa timu ya YangaOmega na Frank wakiwa wamejipumzisha ndani ya vyumba vyao.
 Meneja wa hoteli ya Smart ambayo wachezaji wa timu ya yanga walikuwa wamefikia.



Na Mwandishi wetu maalumu
VIONGOZI, wachezaji wa timu ya Yanga African na uongozi wa hoteli ya Smart ambayo hiyo ilikuwa imefikia ilipokuwa mkoani Kagera kucheza ligi kuu ya vodacom na timu ya Kagera sugar wamepinga vikali  taarifa zilizochapishwa kwenye moja ya  chombo vya habari.
Kwa nyakati tofauti wakati wakiongea na vyombo mbalimbali vya habari vilivyoko mkoani Kager wamesema sio kweli kwamb wachezaji wa timu hiyo uongozi uliwalaza mzungu wa  nne yaani chumba kimoja kwa wachezaji wa nne.
Walisema taarifa hizo sio sahihi kuwa zinalenga kuugawa uongozi wa timu hiyo na washabiki wake pamoja na wanachama, kiongozi  wa msafara wa timu hiyo Tito Osollo aliwaambia waandishi wa habari kuwa chumba kimoja kilikuwa kinatumiwa na wachezaji wawili tu.
“Walioandika habari hizi wanatumiwa haiwezekani mwandishi akaandika habari kuwa sababu za timu ya Yanga kufungwa na Timu ya Kagera Sugar kwamba zimechangiwa na wachezaji wane kulala chumba kimoja” alisema.
“Mwandishi aliyeandika habari hizi hafai kabisa ni mwongo na ninawaomba wanachama na mapenzi ya timu ya Yanga kumpuuza , hayuko makini na kazi yake hivyo anafanya kazi kwa matakwa ya wanaomtumia” alisema Osollo kwa hasira.
Alisema Club ya yanga kamwe haitawavumulia waandishi wanaotaka kuchonganisha wachezaji, wapenzi, wanachama na viongozi wa timu hiyo, “ Tumefungwa, unaposhindana tegemea mambo mengi kushinda, kushindwa na kutoka sare” alimaliza.
Kutokana sakata hilo meneja  wa hoteli ya Smart ameahidi kumfikisha mwandishi wa habari aliyeandika habari za upotoshaji kuwa wachezaji wa nne wa timu ya Yanga walikuwa wanalala ndani ya chumba kimoja.
“Nimeishawasiliana na mwanasheria wetu tunaandaa hati ya madai, mwandishi huyu nitamdai fidia ya shilingi bilioni 2 , ameidhalilisha hoteli yangu, sasa namshughulikia ipasavyo, nitamshtaki kama yeye sio chombo, chomo hakikumtuma aandike habari za uongo” alisema kwa msisitizo.
Nao wachezaji wa yanga walioongea kwa nyakati tofauti walikanusha taarifa hizo kwa kusema kuwa uongozi wa klabu ya Yanga haukuwalaza wachezaji wane kwenye chumba kimoja.

PROFESA LIPUMBA AWASILI KAGERA

Msafara ulienda kumpokea mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba.
Profesa Lipumba akiwa kwenye gari la wazi akiwapungia wananchi mara baada ya kuwasili mkoani Kagera ambapo atafanya mkutano wa hadhara katika kata ya Bakoba.

Monday, October 8, 2012

ZIARA YA MKUU WA MKOA KAGERA WILAYANI MULEBA

 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Massawe Akiwa Katika Picha ya Pamoja na Uongozi wa Shule ya Sekondari ya Katoke Lweru.
Mkuu wa Mkoa Akiongea na Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza Katika Shule ya Sekondari Katoke Lweru.

PINDA AKIWEKA SHADA LA MAUA KWENYE KABULI LA KARDINARI RUGAMBWA

VIJANA WAMUENZI PROTACE ISHENGOMA

jumuia ya umoja wa vijana ya CCM ikipatia hati maalumu kamanda wa UVCCM wa wilaya ya Misenyi, Protace Ishengoma

UCHAGUZI WA JUMUIA YA VIJANA CCM MKOANI KAGERA

 Vijana wakishangilia kabla ya uchaguzi
 Mmoja wa wagombea wa nafasi ya uenyekiti wa VCCM mkoani Kagera.
 Mjumbe wa NEC wa wilaya ya Karagwe Amri Karim alikuwa miongoni mwa walioudhuria mkutano wa uchaguzi wa UVCCM wa mkoa wa Kagera.

Makada wa CCM mkoani Kagera.

Sunday, October 7, 2012

MANDHARI YA MKOA WA KAGERA

 sehemu ya mji wa Bukoba.
 Mitaa ya mji wa Bukoba.
 Sehemu ya mto Kagera.
 Mto Ruvuvu ulioko wilayani Ngara.
Uwanja wa ndege wa Bukoba.

UGONJWA WA MNYAUKO WAENDELEA KUHATARISHA USALAMA WA NDIZI KAGERA

UGONJWA unaoshambulia migomba wa mnyauko bacteria umeanza kuathiri upatikanaji wa ndizi kwenye maeneo mbalimbali yaliyoko mkoani Kagera.

Ugonjwa huo unasambaa kwa kasi hasa kwenye maeneo ya wilaya za Muleba na Karagwe ambayo uzalisha  ndizi nyingi mkoani Kagera na maeneo mengine ya wilaya za Bukoba na Misenyi.

Hali ya ugonjwa huo unaoshambulia migomba wa mnyauko bacteria imechangbia kupunguza uzalishaji wa ndizi mkoani Kagera jambo ambalo limechangia kupanda kwa bei ya ndizi zinapopelekwa kwenye masoko.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kwamba kwenye soko kuu la Bukoba ndizi kubwa inauzwa kwa wastani wa kati shilingi 15,000 hadi 20,000 ambapo miaka iliyopita ndizi kubwa zilikuwa zinauzwa kwa wastani wa kati ya shilingi 6,000 hadi 8,000.

Kupanda kwa bei ya ndizi iliyochangiwa na ugonjwa wa mnyauko bacteria wa migomba kumewalazimisha baadhi ya wakazi wa mkoa wa Kagera ambao hutegemea ndizi kama chakula chao kikuu kubadilika ambapo sasa wanalazimika kula ugali na wali.

Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Kagera wamelazimika kubadili fikira zao za kudhani kuwa ndizi ndicho chakula kikuu baada ya kushindwa kumudu gharama za kununua ndizi kwenye masoko ambazo bei yake ni kubwa.

Baadhi ya wakulima bora wa migomba mkoani Kagera ambao mashamba yao yameathirika kutokana na ugonjwa wa mnyauko bacteria wa mogomba ni pamoja kamishina mstaafu wa jeshi la polisi Alfred Tibaigana.

Kamishina Tibaigana shamba lake liko katika kijiji cha Buganguzi wilayani Muleba limeathirika sana, Mkulima huyu kabla ya ugonjwa huu alikuwa na uwezo wa kuzalisha wastani tani 40 za ndizi kwa wiki ambapo sasa anazalisha wastani wa tani zisizozidi 10 kwa wiki.

Aidha, baadhi ya wakulima mkoani Kagera wameitahadharisha serikali kuchukua hatua za haraka za kuthibiti ugonjwa huu unaosambaa kwa kasi ili zao la ndizi mkoani Kagera lisibaki kwenye vitabu vya historia.

Saturday, October 6, 2012

WAZIRI MKUU PINDA AWASILI KAGERA

 Waziri mkuu Mizengo Pinda  akisalimiana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya usalama ya mkoa wa Kagera mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba kuhudhuria uzinduzi wa kanisa kuu la jimbo katoriki la Bukoba.
 Mkuu wa mkoa wa Kagera kanali mstaafu Fabian Massawe akimpokea Pinda.
Massawe akiongea jambo na waziri wa mali asili na utalii Balozi Khamis sued Kagasheki wakati wakisubili ujio wa waziri mkuu, Pinda kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba, kushoto ni katibu tawala wa mkoa wa Kagera Nassor Mnambila na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Kagera.

RAIS KIKWETE AFUNGUA MKUTANO WA DIASPORA JIJINI EDMONTON, CANADA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na ujumbe wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) katika ukumbi wa mikutano wa Fantasy Land jijini Edmonton, Canada, baada ya kufungua mkutano wa Watanzania waishio nchini humo (Tanzania Diaspora Conference) Ijumaa Oktoba 5, 2012

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua vifaa vya kukamu asali baada ya kufungua maonyesyesho ya mazo ya asali kwenye uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dae sa salaam Oktoba 5, 2012 kulia kwake ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdallh Kigoda. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MATAGE MKUU WA UPELELEZI WA JESHI LA POLISI KAGERA AAGWA

Baadhi ya askari walioudhuria sherehe za kumuaga Peter Matage anayehamia makao makuu ya jeshi la polisi.
Viongozi walioudhuria sherehe ya kumuaga Matage.
 Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Philip Kalangi, akiwatambulisha viongozi wa serikali walioudhuria sherehe za kumuaga Matage.
 Baadhi ya maofisa wa jeshi la polisi.
 Baadhi ya askari wa kikosi cha usalama barabarani walioudhuria sherehe hiyo.
 Baadhi ya askari wakigonganisha glasi na viongozi waliodhuria sherehe hiyo.
 Matage (kushoto) anayehamia makao makuu ya jeshi la polisi akiwa kwenye picha mkuu mpya wa upelelezi wa mkoa wa Kagera aliyetokea Zanzibar.
 Mtaalamu China, alikuwa miongoni mwa walioudhuria sherehe ya kumuaga Matage.
Matage akiwa ameshika tuzo aliyoipokea toka kwa mwakilishi wa mkoa wa Kagera, Fikir Kisimba, ilitolewa na askari wa kikosi cha upelelezi.

Thursday, October 4, 2012

RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE KATIKA ZIARA RASMI OTTAW, CANADA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na  ujumbe wake katika mazungumzo na  Gavana Jenerali wa Canada Mhe. David Johnson na mkewe Mama Sharon Johnson na viongozi wa serikali ya nchi hiyo katika  jumba la Rideau jijini Ottawa, Canada, katika hatua yake ya kwanza ya  ziara rasmi ya siku mbili jijini humo Jumatano Oktoba 4, 2012

ZITTO KABWE ACHANGIA BIMA YA AFYA KWA MJANE WA MWANGOSI NA MWANAWE KUPITIA NSSF

KATIKA siku ya mwisho ya harambee ya kumchangia mjane wa marehemu Daud Mwangosi, Ndugu Zitto Kabwe amejitolea kumchangia mjane wa marehemu kwa kumlipia ada ya uanachama wa Mfuko wa Hifadhi ya Kijamii (NSSF) kwa kila mwezi na kwa miaka mitatu mfululizo.

" Nimeona nami niunge mkono harambee hii.Pamoja na michango ya fedha iliyotolewa kumsaidia mjane kuanzisha mradi wa kujikimu, mimi naona ni muhimu pia mjane akawa na hakika ya huduma ya afya yake na watoto wake wanne. Hivyo, mchango wangu utakuwa ni kwenye eneo hilo Bima ya Afya na kwa miaka mitatu." Anasema Zitto Kabwe alipoongea na Mjengwablog.com, mtandao wa Kijamii ulioratibu harambee ya mjane wa Daud Mwangosi.


Hii ni mara ya pili kwa Ndugu Zitto Kabwe kuchangia kwenye masuala ya kijamii kupitia mtandao wa kijamii wa Mjengwablog.com, mara ya kwanza ni alitoa mchango wake pale Mtandao wa Mjengwablog.com ulipoendesha harambee ya kuwachangia watoto wa Somalia waliokuwa katika hatari ya kufa kwa njaa.


Katika harambee iliyomalizika Jumapili ya Septemba 30 mwaka huu na iliyochukua kipindi cha mwezi mmoja,zaidi ya shilingi milioni tano na nusu zimekusanywa.


Mchango huo wa Ndugu Zitto Kabwe una maana mjane wa marehemu ataweza kuwa na hakika ya yeye na watoto wake wanne kupata huduma za afya bila kufikiria malipo kwa kipindi cha miaka mitatu. Baada ya hapo,michango ya mjane huyo ya kila mwezi kwa mfuko huo wa hifadhi ya kijamii ( NSSF) ambayo atakuwa akilipiwa na Ndugu Zitto Kabwe itakuwa ni malimbikizo ya akiba yake ambayo mjane atakuwa na uwezo wa kuichukua kama akipenda. Kwa sasa mjane wa Daud Mwangosi hayuko kwenye utaratibu wowote wa Bima ya Afya, kwake yeye na wanawe.


Harambee ya mjane wa Daud Mwangosi iliyoendeshwa kwa uwazi kwa njia ya MPESA, TigoPesa, Airtel Money, NMB Mobile na Western Union ilimwezesha mchangiaji kuliona jina lake na mchango wake kwenye orodha ya wachangiaji iliyokuwa ikiwekwa mtandaoni kila siku. Michango ilikuwa ni hiyari, hakuna aliyeombwa kutoa na utaratibu haukuruhusu ahadi za kuchangia, bali, mwenye nacho alitoa na hapo hapo kuorodheshwa kama mchangiaji. Utaratibu haukuruhusu pia michango iliyofungamana na siasa za vyama.


Hatua hiyo ya uwazi na kutanguliza ubinadamu na si itikadi kwenye uchangiaji imechangia kupelekea Watanzania wengi wa kada zote, kwa namna moja au nyingine kushiriki kwenye kuchangia. Kuna waliochangia shilingi elfu moja na kuna waliochangia mpaka shilingi milioni moja.


Ari hii ya Watanzania kujitolea kusaidiana kwenye hali kama iliyomkuta mjane wa Daud Mwangosi imedhihirisha umoja na upendo tulionao kama Watanzania, na pia imeonyesha jinsi tunavyoijali amani yetu na hivyo jamii, kupitia michango hii, imeonyesha pia kwa vitendo, dhamira ya kulaani kwao vitendo vya maovu na vinavyotokana na matumizi ya nguvu yasiyo ya lazima kama kile kilichomtokea mwandishi Daud Mwangosi.


Baadhi ya watu maarufu katika jamii waliojitokeza kwa hiyari yao kumchangia mjane wa Daud Mwangosi kupitia mtandao wa kijamii wa Mjengwablog.com ni pamoja na Shy- Rose Bhanji, Ananilea Nkya, John Bukuku ( Mmiliki wa Fullshangwe.blog) na Ndugu Mobhare Matinyi aliyepata kuwa mhariri wa gazeti la Majira.


Michango kwa mjane wa Daud Mwangosi itaingizwa kwenye akaunti ya mjane ya CRDB, Iringa leo alhamisi, Oktoba 4, 2012. Vielelezo vya kibenki vitawekwa kwenye mtandao wa Mjengwablog.com kwa kila mmoja kuona jumla iliyowasilishwa kwa mjane na orodha ya majina ya wachangiaji.

Wednesday, October 3, 2012

Halmashauri Nchini Zingatieni hili

Na Mwandishi
Bukoba
HALMASHAURI ya manispaa ya Bukoba kupitia idara ya elimu imetakiwa kuanzisha utaratibu wa kutumia walimu wa shule binafsi wakati wa kuandaa majibu ya mitihani ya majaribio ya wilaya (mock) kabla ya kuisahihisha ili kuondoa mkanganyiko wa majibu na kuleta tafsiri sahihi ya mitihani hiyo.
 
Wito huo umetolewa hivi karibuni mjini Bukoba na meneja wa shule za Kaizilege zinazofundisha kwa michepuo ya Kiingereza (KEMEBOS) Eulogius Katiti wakati wakizungumza na wazazi, walezi na wanafunzi katika  mahafali ya tatu ya wahitimu wa darasa la saba.
 
Alisema katika mitihani ya majarobio na kujipima uwezo (Mock ) baadhi ya maswali hususan ya kuchagua wakati mwingine yanaletwa na majibu yasiyo sahihi na hivyo kuleta shida na hata kupelekea wanafunzi kushindwa kutoa jibu sahihi licha ya kufahamu jibu lake.
Katiti alisema hali hiyo inapelekea mitihani hiyo kupewa tafsiri isiyo sahihi na kuongeza kuwa kwa kutambua madhara ya tatizo hilo tayari wamechukua uamuzi wa kuonana na afisa elimu wa manispaa hiyo ili kumweleza jinsi ya kuliondoa.
 
“Tatizo hili linaleta shida hata kwa wanafunzi kushindwa kutoa jibu lililosahihi kutokana na wakati mwingine maswali ya kuchagua kukosa jibu, tayari tumechukua hatua za kumuona afisa elimu ili waanzishe utaratibu wa kutumia walimu wa shule binafsi kuandaa majibu sahihi (marking guide) kabla ya zoezi la kusahihisha kuanza” alisema meneja huyo.
 
Aidha aliongeza kuwa halmashauri hiyo pia inatakiwa kutumia walimu hao hata wakati wa zoezi la utungaji wa mitihani ili kuepuka kuleta maswali yasiyokuwa na maana halisi inayokuwa imetarajiwa.


Awali Mwenyekiti wa kamati ya shule hizo  Abubakhari Kagasheki aliwataka wazazi na walezi kujenga tabia ya kutembelea wao shuleni ili kufuatilia maendeleo yao, ikiwemo kutoa ushauri kwa viongozi wa shule jinsi ya kuendelea kuboresha taaluma.
 
Mwisho

Anaitwa Said Bahanuzi



Bahanuzi akishangilia baada ya kufunga lla kusawazisha

Bahanuzi akipongezwa

Young Afican



11 wa Yanga walioanza

Bukoba Wiki Hii

 Madhari ya mji wa Bukoba na sehemu ya viunga vyake.
 Hatua za mwisho za ukarabati wa kanisa katoriki la jimbo la Bukoba ambalo mwili wa marehemu kardinari Laurean Rugambwa utazikwa milele.

Maisha Yanaendelea

Magazeti Magazeti













Wajumbe Wa Tume Ya Katiba Waanza Tathimini Ya Kazi Ya Ukusanyaji Wa Maoni



Mjumbe wa sekretarieti ya Tumeya Mabadiliko ya Katiba, Mohamed KhamisHamad (kulia) akitoa ufafanuzi kwa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba 


 Picha na :- Ismail Ngayonga, 

 Information officer, Constitutional Review Commission

JK Aongelea Vifo Vya Akina Mama UN

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani, wakati wa uzinduzi wa mpango wa pili wa  Ubunifu wa Uboreshaji wa  Huduma za  Afya ya Mama na Mtoto, katika maeneo ya vijijijni Nchini  Tanzania, mpango  huo  wa   miaka mitatu unafadhiliwa na wafadhili wawili, Meya ya Jiji la New York na  philanthropies Michael Bloomberg na Dr. Helle Agerup ambapo wamechangia dola za kimarekani milioni 15 kutoka kushoto ni Meya wa jiji la New York Michael Bloomberg, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, Rais Jakaya Mrisho Kikwete,  na Dr, Helle Agerup
  Meya Michael Bloomberg, Ban Ki Moon, Rais  Jakaya Kikwete na Dr. Hellen wakiangalia video fupi iliyokuwa ikionyesha kazi zilizofanywa za ukoaji wa  akina mama wajawazito kwa kuwapatia huduma ya upasuaji wa dharura, huduma ambayo imepatika kwa ufadhili wa  Meya na   Philanthropies Michael Bloomberg ambapo kwa kupitia ufadhili alioufanya kuanzia mwaka 2006 zaidi ya wataalam 106 wakiwamo wakunga na manesi wamepatiwa mafunzo ya upasuaji wa dharura, pia huduma za afya zimeboreshwa kwa kujenga au kuvifanyia ukarabati vituo vya afya na zahanati katika ngazi za vijiji katika  maeneo ya  mikoa ya Pwani, Morogoro na Kigoma. Ufadhili  na kazi kubwa iliyofanywa na  Bloomberg   pamoja na juhudi za   Rais Jakaya Kikwete zimemvutia Dr. Hellen naye kuwekeza nchini Tanzania.

 Rais  Jakaya Kikwete akisaini kitabu cha wageni anayetizama pembeni ni Katibu Mkuu  Ban Ki Moon

Rais  Jakaya Kikwete akiongoza ujumbe wa Tanzania katika  mazungumzo yake na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Ban Ki  Moon ambaye naye aliongoza ujumbe wake. Matukio hayo yote yamefanyika siku ya  Jumanne katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa,  Jijini New York, Marekani.

Bei Ya Petroli Yaporomoka Ghafla



 MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetoa bei kikomo mpya ambazo zitaanza kutumika leo nchini kote ikiwa imeshuka kwa Sh 306, kwa lita ya petroli, Sh 192 kwa lita moja ya dizeli huku mafuta ya taa bei ikibaki bila kubadilika. 

Taarifa iliyotolewa jana na Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Ewura, Titus Kaguo, ilisema bei za mafuta ya petroli kwa Dar es Salaam itakuwa Sh 1,994 kwa lita moja ikiwa imeshuka kutoka Sh2,300 ya bei ya Septemba. Alisema mafuta ya dizeli bei yake imeshuka hadi kufikia Sh1,950 kutoka Sh2,142, wakati mafuta ya taa yanabakia Sh1,993 kutokana na kutoingia meli yoyote ya mafuta hayo. 

Taarifa hiyo ilisema bei hizo, zitaendelea kuongezeka kutokana na gharama za usafirishaji kutoka Dar es Salaam kwenda mikoani, ingawa kwa ujumla katika kila eneo punguzo litakuwa ni Sh 306 na Sh 192 kwa petroli na dizeli kwa kila lita moja. “Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2008, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko na Ewura itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta,”alisema na kuongeza; “Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya uamuzi stahiki kuhusu ununuzi wa bidhaa za mafuta kulingana na bei anayoiona mteja inamfaa.” 

 Kaguo alisema kampuni za mafuta zipo huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani ilimradi bei hizo ziwe chini ya bei kikomo na kama mfanyabiashara atakiuka atapewa adhabu ya kulipa Sh3 milioni. Pia alivitaka vituo vyote vya mafuta kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana ili mteja afanye uchaguzi wa kununua mafuta akiwa anajua bei halisi ya mafuta katika kituo husika. “Wanunuzi wanashauriwa kuhakikisha kuwa wanapata stakabadhi ya malipo inayoonesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita kwani stakabadhi hiyo ya malipo itatumika kama kidhibiti cha ununuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya ama kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo; ama endapo utakuwa umeuziwa mafuta yenye kiwango cha ubora kisichofaa,” aliongeza Kaguo.

 Hivi karibuni Baraza la Ushindani wa Haki (FCC), lilitupilia mbali rufani ya kampuni 13 zinazojishughulisha na uuzaji wa mafuta, zilizokuwa zinapinga kanuni mpya ya kukokotoa bei za mafuta iliyobuniwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura). Katika hukumu hiyo iliyotolewa wiki iliyopita, Mwenyekiti wa baraza hilo, Razia Sheikh, alisema uamuzi wa kuitupa rufani hiyo ulitokana na warufani, kushindwa kuthibitisha madai yao kikamilifu. 

Alisema baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili, baraza liliridhika kuwa Ewura ilikuwa imefuata taratibu zote zilizowekwa kisheria, kabla ya kutangaza kanuni mpya za kukokotoa bei za mafuta nchini. Katika usikilizaji wa shauri hilo, Mwenyekiti Sheikh alisaidiwa na wajumbe wawili ambao ni Malima Bundala na Ali Juma.

 Kampuni zilizokata rufaa ya kupinga uamuzi wa Ewura ni pamoja na BP Tanzania Limited, Engen Petroleum Tanzania Limited, Camel Oil Tanzania Limited, Oilcom Tanzania Limited, Total Tanzania Limited, Gapco Tanzania Limited na Hass Petroleum Tanzania Limited. Nyingine ni Orxy Oil Company Limited, MSG International Tanzania Limites, GBP Tanzania Limited, Lake Oil Limited, Moil Tanzania Limited and Acer Petroleum Tanzania Limited. Pamoja na kutupilia mbali rufani hiyo, Sheikh pia aliziamuru kampuni hizo kulipa gharama za kesi. 

Kwa mujibu nyaraka za baraza hilo, gharama za mawakili wa Ewura peke yake ni zaidi ya Sh100 milioni. Pamoja na mambo mengine, kampuni hizo zililiomba baraza hilo kuifuta kanuni hiyo mpya kwa vigezo kuwa, Ewura haikufikiria mambo kadhaa kabla ya kuitangaza. 

                    Chanzo: Mwananchi