Wednesday, May 16, 2012
Jk Akimpa Nape Maelekezo
Mwenyekiti
wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimwagiza jambo, Katibu wa NEC, Itikadi
na Uenezi, Nape Nnauye wakati wa semina ya kuwajengea uelewa wa Utawala
bora, Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, iliyofanyika
jana May 15, 2012, kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma.
Semina hiyo iliandaliwa na Mpango wa Hiari wa Nchi za Umoja wa Afrika
kujipima kwa vigezo vya Utawala Bora-APRM. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM,
Wilson Mukama. (Picha na Bashir Nkoromo)
Saturday, May 12, 2012
Chuo Cha Mafunzo Ya Udereva Lake Zone Driving School Chanufaisha Wakazi Wa Mkoa Wa Kagera
Kaimu Kamanda Wa polisi mkoani Kagera Vitus Mlolere akifunga mafunza ya awali ya waendesha Pikipiki na Magari katika kata ya Kyebitembe na Karambi ambayo yalieneshwa na Chuo cha Lake Zone Driving School cha Mkoani Kagera.
Hapa anafunga mafunzo mengine katika kata ya Nshamba iliyoko wilayani Muleba Mkoani Kagera ambapo jumla ya wahitimu arobaini walipatiwa mafunzo hayo kutoka Lake zone
Mkurugenzi wa Chuo Cha Lake Zone Driving School Winstoni Kabantega akitoa ufafanuzi juu ya mafunzo waliyoyapata wahitimu wa kata za Kyebitembe na Karambi
Kabantega akitoa ufafanuzi tena katika kufunga mafunzo ya kata Nshamba wilayani Muleba
Hapa anafunga mafunzo mengine katika kata ya Nshamba iliyoko wilayani Muleba Mkoani Kagera ambapo jumla ya wahitimu arobaini walipatiwa mafunzo hayo kutoka Lake zone
Mkurugenzi wa Chuo Cha Lake Zone Driving School Winstoni Kabantega akitoa ufafanuzi juu ya mafunzo waliyoyapata wahitimu wa kata za Kyebitembe na Karambi
Kabantega akitoa ufafanuzi tena katika kufunga mafunzo ya kata Nshamba wilayani Muleba
Wahitimu wa mafunzo ya awali ya udereva wa kata ya Kyebitembe na Karambi wakisoma risara kwa mgeni rasimi hayupo pichani mafunzo hayo yalitolewa na Chuo cha udereva cha Lake Zone Driving School
Wahitimu wa mafuzo ya awali ya udereva kutoka kata ya Nshamba wakisoma risara
Moja wa askari wa Kikosi cha usalama barabarani mkoani Kagera PC Joseph akiwaapisha wahitimu wa mafunzo ya awali ya udereva yaliyofungwa katika wilaya ya Muleba Mkoani Kagera
Wahitimu wa mafuzo ya awali ya udereva kutoka kata ya Nshamba wakisoma risara
Moja wa askari wa Kikosi cha usalama barabarani mkoani Kagera PC Joseph akiwaapisha wahitimu wa mafunzo ya awali ya udereva yaliyofungwa katika wilaya ya Muleba Mkoani Kagera
Wednesday, May 9, 2012
Wakuu Wa Wilaya Watangazwa
Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya Wapya
NA.
|
KITUO CHA KAZI
| |
| 1. | Novatus Makunga | Hai |
| 2. | Mboni M. Mgaza | Mkinga |
| 3. | Hanifa M. Selungu | Sikonge |
| 4. | Christine S. Mndeme | Hanang |
| 5. | Shaibu I. Ndemanga | Mwanga |
| 6. | Chrispin T. Meela | Rungwe |
| 7. | Dr. Nasoro Ali Hamidi | Lindi |
| 8. | Farida S. Mgomi | Masasi |
| 9. | Jeremba D. Munasa | Arumeru |
| 10. | Majid Hemed Mwanga | Lushoto |
| 11 | Mrisho Gambo | Korogwe |
| 12. | Elias C. J. Tarimo | Kilosa |
| 13. | Alfred E. Msovella | Kiteto |
| 14. | Dkt. Leticia M. Warioba | Iringa |
| 15. | Dkt. Michael Yunia Kadeghe | Mbozi |
| 16. | Mrs. Karen Yunus | Sengerema |
| 17. | Hassan E. Masala | Kilombero |
| 18. | Bituni A. Msangi | Nzega |
| 19. | Ephraem Mfingi Mmbaga | Liwale |
| 20. | Antony J. Mtaka | Mvomero |
| 21. | Herman Clement Kapufi | Same |
| 22. | Magareth Esther Malenga | Kyela |
| 23. | Chande Bakari Nalicho | Tunduru |
| 24. | Fatuma H. Toufiq | Manyoni |
| 25. | Seleman Liwowa | Kilindi |
| 26. | Josephine R. Matiro | Makete |
| 27. | Gerald J. Guninita | Kilolo |
| 28. | Senyi S. Ngaga | Mbinga |
| 29. | Mary Tesha | Ukerewe |
| 30. | Rodrick Mpogolo | Chato |
| 31. | Christopher Magala | Newala |
| 32. | Paza T. Mwamlima | Mpanda |
| 33. | Richard Mbeho | Biharamulo |
| 34. | Jacqueline Liana | Magu |
| 35. | Joshua Mirumbe | Bunda |
| 36. | Constantine J. Kanyasu | Ngara |
| 37. | Yahya E. Nawanda | Iramba |
| 38. | Ulega H. Abadallah | Kilwa |
| 39. | Paul Mzindakaya | Busega (mpya) |
| 40. | Festo Kiswaga | Nanyumbu |
| 41. | Wilman Kapenjama Ndile | Mtwara |
| 42. | Joseph Joseph Mkirikiti | Songea |
| 43. | Ponsiano Nyami | Tandahimba |
| 44. | Elibariki Immanuel Kingu | Kisarawe |
| 45. | Suleiman O. Kumchaya | Tabora |
| 46. | Dkt. Charles O. F. Mlingwa | Siha |
| 47. | Manju Msambya | Ikungi (mpya) |
| 48. | Omar S. Kwaangw’ | Kondoa |
| 49. | Venance M. Mwamoto | Kibondo |
| 50. | Benson Mpesya | Kahama |
| 51. | Daudi Felix Ntibenda | Karatu |
| 52. | Ramadhani A. Maneno | Kigoma |
| 53. | Sauda S. Mtondoo | Rufiji |
| 54. | Gulamhusein Kifu | Mbarali |
| 55. | Esterina Kilasi | Wanging’ombe (mpya) |
| 56. | Subira Mgalu | Muheza |
| 57. | Martha Umbula | Kongwa |
| 58. | Rosemary Kirigini | Meatu |
| 59. | Agness Hokororo | Ruangwa |
| 60. | Regina Chonjo | Nachingwea |
| 61. | Ahmed R. Kipozi | Bagamoyo |
| 62. | Wilson Elisha Nkhambaku | Kishapu |
| 63. | Amani K. Mwenegoha | Bukombe |
| 64. | Hafsa M. Mtasiwa | Pangani |
| 65. | Rosemary Staki Senyamule | Ileje |
| 66. | Selemani Mzee Selemani | Kwimba |
| 67. | Lt. Col. Ngemela E. Lubinga | Mlele (mpya) |
| 68. | Iddi Kimanta | Nkasi |
| 69. | Muhingo Rweyemamu | Handeni |
| 70. | Lucy Mayenga | Uyui |
MAJINA 63 WAKUU WA WILAYA WA ZAMANI NA
VITUO VYAO VYA KAZI
| NA. | JINA | KITUO CHA KAZI |
| 1. | James K. O. Millya | Longido |
| 2. | Mathew S. Sedoyeka | Sumbawanga |
| 3. | Fatuma L. Kimario | Igunga |
| 4. | Capt. (Mst.) James C. Yamungu | Serengeti |
| 5. | Lt. (Mst.) Abdallah A. Kihato | Maswa |
| 6. | Sarah Dumba | Njombe |
| 7. | Jowika W. Kasunga | Monduli |
| 8. | Elizabeth C. Mkwasa | Bahi |
| 9. | Col. Issa E. Njiku | Misenyi |
| 10. | John B. Henjewele | Tarime |
| 11. | Elias W. Lali | Ngorongoro |
| 12. | Raymond H. Mushi | Ilala |
| 13. | Francis Miti | Ulanga |
| 14. | Evarista N. Kalalu | Mufindi |
| 15. | Mariam S. Lugaila | Misungwi |
| 16. | Anna J. Magowa | Urambo |
| 17. | Anatory K. Choya | Mbulu |
| 18. | Fatma Salum Ally | Chamwino |
| 19. | Deodatus L. Kinawiro | Chunya |
| 20. | Ibrahim W. Marwa | Nyang’hwale (mpya) |
| 21. | Dkt. Norman A. Sigalla | Mbeya |
| 22. | Moshi M. Chang’a | Mkalama (mpya) |
| 23. | Jordan M. Rugimbana | Kinondoni |
| 24. | Georgina E. Bundala | Itilima (mpya) |
| 25. | Halima M. Kihemba | Kibaha |
| 26. | Manzie O. Mangochie | Geita |
| 27. | Abdula S. Lutavi | Namtumbo |
| 28. | Zipporah L. Pangani | Bukoba |
| 29. | Dkt. Ibrahim H. Msengi | Moshi |
| 30. | Col. Cosmas Kayombo | Kakonko (mpya) |
| 31. | Lembris M. Kipuyo | Muleba |
| 32. | Elinasi A. Pallangyo | Rombo |
| 33. | Queen M. Mlozi | Singida |
| 34. | Juma S. Madaha | Ludewa |
| 35. | Angelina Mabula | Butiama (mpya) |
| 36. | Hadija H. Nyembo | Uvinza (mpya) |
| 37. | Ernest N. Kahindi | Nyasa (mpya) |
| 38. | Peter T. Kiroya | Simanjiro |
| 39. | John V. K. Mongella | Arusha |
| 40. | Baraka M. Konisaga | Nyamagana |
| 41. | Husna Mwilima | Mbogwe (mpya) |
| 42. | Sophia E. Mjema | Temeke |
| 43. | Francis Isaac | Chemba (mpya) |
| 44. | Abihudi M. Saideya | Momba (mpya) |
| 45. | Khalid J. Mandia | Babati |
| 46. | Anna Rose Nyamubi | Shinyanga |
| 47. | Dani B. Makanga | Kasulu |
| 48. | Amina J. Masenza | Ilemela |
| 49. | Mercy E. Silla | Mkuranga |
| 50. | Christopher R. Kangoye | Mpwapwa |
| 51. | Lt. Edward O. Lenga | Kalambo (mpya) |
| 52. | Halima O. Dendego | Tanga |
| 53. | Lephy B. Gembe | Dodoma |
| 54. | Saidi A. Amanzi | Morogoro |
| 55. | Jackson W. Msome | Musoma |
| 56. | Elias C. B. Goroi | Rorya |
| 57. | Lt. Col. Benedict Kitenga | Kyerwa (mpya) |
| 58. | Erasto Sima | Bariadi |
| 59. | Nurdin H. Babu | Mafia |
| 60. | Khanifa M. Karamagi | Gairo (mpya) |
| 61. | Gishuli M. Charles | Buhigwe (mpya) |
| 62. | Saveli M. Maketta | Kaliua (mpya) |
| 63. | Darry Rwegasira | Karagwe |
OFISI YA WAZIRI MKUU,
DAR ES SALAAM.
9 MEI 2012
VITUO VYAO VYA KAZI
Uvccm Kagera Inapokosa Imani Na watendaji Wake
Kagera
KAMATI
ya utekelezaji ya Jumuiya ya Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapindizi
(CCM) MKoa wa Kagera (UVCCM) imemkataa katibu wa UVCCM wa Wilaya ya
Karagwe kutokana na tuhuma za kushindwa kuwajibika kikamilifu katika
shughuli za chama.
Kauli
hiyo ilitolewa jana na mwenyekiti wa UVCCM Mkoa huo Deusidedith Katwale
wakati akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za CCM mkoani humo.
Katwale
alisema katika kikao cha kamati ya utekelezaji ya UVCCM mkoa kimeridhia
kumkataa Lufunjo Nkinda ambaye ni katibu wa UVCCM Wilaya ya Karagwe
kutokana na kushindwa kwake kuwajibika na kukiuka maadili ya Chama chao.
Alizitaja
baadhi ya tuhuma zinazomkabili katibu huyo kuwa ni pamona na ulevi wa
kupindukia,uharibifu wa mali za umma,kuomba michango bila mpangilio na
kushindwa kuwaheshimu viongozi na mamlaka zilizo juu yake kichama ambapo
pia aliongeza kuwa amekuwa akijipa vyeo ambavyo havipo katika chama cha
CCM.
“Ukweli
anamatatizo makubwa kichama, anajiita katibu wa CCM wa Wilaya idara ya
Vijana nafasi ambayo haipo kwenye chama wengine anawambia kuwa yeye ni
usalama wa Taifa wa CCM jambo ambalo linatutia doa kama chama ”Alisema
Katwale.
Alisema
kuwa kwa mujibu wa taratibu za Chama na Uvccm katibu huyo ameisha
kanywa mara tatu na kushindwa kujirekebisha ambapo mara ya nne
aliandikiwa barua na Katibu wa Wilaya kwa ajili ya kumkanya na matokeo
yake alimjibu katibu huyo wa Wilaya Anatory Nshange kwa barua ya matusi
akimtukana jambo ambalo ni kinyume na taratibu za chama na katiba yake.
Alisema
kuwa Kamati hiyo ya UVCCM mkoa inawaomba Uvccm makao makuu watumie
taratibu za uajiri wamchukue mtu wao na kumpeleka wanakotaka.
Kwa
upande wake katibu huyo anayetuhumiwa Lufunjo alipohojiwa na waandishi
wa habari juu ya tuhuma hizo zinazomkabili alisema kuwa hakuna barua
yoyote ambayo aliwahi kutumiwa inayomtuhumu juu ya jambo la aina yoyote
na kwamba hajawahi kuitwa kwenye kikao chochote kwa mijubu wa taratibu
za jumuiya.
“Tuhuma
hizo si za kweli mimi nimefanya kazi za kiutendaji katika kata zote
arobaini za Wilaya ya Karagwe,kukataliwa na kuondolewa kwangu ni majungu
ya baadhi ya wanachama wasiokitakia chama mema.
Wakati
huo huo kamati hiyo imempongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kwa
usikivu wake na kuteua baraza jipya la mawaziri ambalo wamedai kuwa
wanaimani nalo na wameridhika nalo hususani alivyozingatia kuwaingiza
vijana katika baraza hilo .
mwisho
Manispaa Ya Bukoba Wathamini Walipa Kodi wenu
Barabra hii iko mtaa wa Kashenye kata ya Kashai Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera imekatika na hivyo kusababisha usumbufu
kwa watumiaji barabara hiyo, mtaa wa Kashenye ni moja ya mitaa iliyoko katika manispaa ya
Bukoba ambayo imesahaulika mtaa huu ni moja ya mitaa yenye miundo mbinu
hatarishi.
Tuesday, May 8, 2012
Wenye Hati chafu Wawajibishwe Naibu Waziri Wa Maji
Naibu
Waziri wa Maji, Bilithin Mahenge akifungua mkutano wa mkuu wa 13 wa
mwaka wa mamlaka hizo unaendelea kwenye hoteli ya Blue Pearl, Ubungo
Plaza
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
NAIBU Waziri wa Maji, Binilith Mahenge ameziagiza bodi za Mamlaka ya Maji safi na Majitaka mijini kuwachukulia watumishi wote hatua zinazostahili , ambao wamesababisha mamlaka zilizopata hati zenye mashaka katika Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Mamlaka hizo kwa mwaka fedha uliopita(2010/2011).
Kauli hiyo imetolewa leo(jana) na Naibu Waziri huyo wakati alipofungua mkutano mkuu wa 13 wa mamlaka hizo unaendelea kwenye hoteli ya Blue Pearl, Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. Mkutano huo wa siku mbili umehusisha watu 200 ambao ni wakurugenzi, watalaamu wa wizara hiyo, TAMISEMI, Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa EWURA, DAWASA na DAWASCO na wadau wengine.
Mada kuu ya mkutano huo ni “Kuzijengea Mamlaka Uwezo wa Rasilimali watu katika Kutoa Huduma Endelevu”
“ Ukaguzi wa
Hesabu za Mamlaka na ripoti zake ni kioo muhimu cha kupima uttendaji
kazi, usimamizi wa mapato na matumizi ya fedha za umma kwenye mamlaka…
Sikuridhika na kiwango cha kuongezeka mamlaka zilizopata hati zenye mashaka kutoka tatu mwaka 2009 /2010 hadi tano mwaka 2010/2011. Tegemeo langu mamlaka zote zipate hati safi ya ukaguzi wa hesabu.
Naibu Waziri Mahenge alizitaja
mamlaka hizo kuwa ni Mtwara, Musoma, Songea, DAWASA na DAWASCO, ambapo
alizitaka kuongeza nguvu katika usimamizi wa fedha katika mamlaka zao
kwa kuhakikisha hesabu za mamlaka hizo zinatayarishwa kwa usahihi unaokubalika n kuondoa kasoro zilizojitokeza.
Aidha Mahenge aliongeza kuwa kasi ndogo ya utekelezaji wa program ya miradi ya maji iliyopangwa
inachangiwa na uhaba wa fedha kwa kiasi kikukubwa na upungufu wa
wataalamu wanaoweza kusimamia kwa makini utekelezaji wake kuanzia ngazi
za mikoa , wialya, miji midogo na miradi ya kitaifa.
Aliyataja maeneo yenye upungufu kuwa ni usimamizi
fedha za miradi, ununuzi, utoaji taarifa za utekelezaji wa miradi,
ukusanyaji na utoji wa taarifa za miradi, uchambuaji na utunzaji
takwimu.
Alisema
hali hiyo inaonyesha umhimu wa kujenga uwezo kwa watendaji katika
ngazi zote ili mapungufu yaliyopo yasiendelee kuonekana, hivyo
alizitaka bodi hizo kuwa na mipango ya mafunzo inayotekelezeka na
kulenga mapungufu hayo.
Mahenge alisema changamoto nyingine katika
utkelezaji wa program ya maendele ya sekta ya maji ni kuchelewa kwa
fedha za maendeleo kutoka wadau wa maendeleo, hali ambyo imesababisha wakandarasi kupunguza kasi ya ujenzi na kutoza riba, ikiwemo kuchelewa kukamilika kwa ujenzi.
Alisema
uchelewaji wa malipo unatokana na hasa na uchelewashaji wa taarifa za
utekelezaji kutokakwa watekelezaji wa ngazi zote. Hivyo hadi kufikia
Aprili mwaka huu jumla ya sh. bilioni 32.7 hajijalipwa kati ya hizo
fedha za wakandarasi ni sh. bilioni 30.1 na wahandisi washauri ni sh.
bilioni 2.6.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mhadisi Christopher Sayi alisema katika
jiji la Dares Salaam na maeneo yanayohudumiwa na DAWASCO, kiwango cha
utaoji wa huduma ya majisafi kimeshuka na kufikia asilimi 51kipindi cha
mwezi Juni,2011 kutoka asilimia 55 ya Juni 2010.
Alisema upungufu huo umetokana na kupungua kwa uzalishajimaji uliosababishwa na mgao wa umeme na ongezeko la maeneo ya utoaji huduma kwa kupanuka kwa jiji.
Na Magreth Kinabo MAELEZO
Taarifa Ya Jana Kutoka CCM
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Hivi
karibuni chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kilielezea kile
ilichoeleza kuwa ni kutishwa na wimbi la mauaji yanayotishia amani ya
nchi kikidai kuwa jumla ya wanachama wake 15 wameuawa katika wilaya ya
Igunga peke yake.
Madai
hayo ya CHADEMA, pamoja na wanachama wengine na mashabiki wao,
yalitolewa na Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, ambaye alidai
kuwa mauaji hayo yana mkono wa serikali ya CCM, ambayo kwa madai yao
imeona wazi kuwa upepo wa kisiasa umekiendea vibaya na sasa kinataka
kujiimarisha katika utawala kwa kuua watu wanaoipinga.
Akifungua
kikao cha Baraza Kuu la chama hicho jijini Dar es Salaam Aprili 29
mwaku huu mwenyekiti huyo alifafanua kuwa mbali na kuuawa kwa watu
wanne kwa pamoja na juzi kifo cha mwenyekiti wao wa tawi huko Arumeru
mkoani Arusha, jumla ya wanachama wake 15 wameuawa katika wilaya ya
Igunga peke yake tangu kumalizika kwa uchaguzi mdogo wa jimbo hilo
mwaka jana.
Mbowe
katika maelezo yake alijaribu katika maeneo kadhaa kuihusisha CCM na
au serikali yake katika matukio kadhaa yaliyowakabili baadhi ya
wanachama na viongozi wa Chadema katika maeneo mbalimbali nchini
likiwemo lile la Mbunge Highness Kiwia ambaye Suala lake bado Lipo
mikononi mwa vyombo Vya dola likishughulikiwa.
Katika
sehemu kubwa ya maelezo ya Ndg. Mbowe amejitahidi kuonesha kuwa mauaji
yote yaliyoikabili na yatakayokuwa yakiikabili Chadema kupitia wafuasi
wake yanafanyika kisiasa, Jambo ambalo ni la uzushi, kwani Halina
ushahidi wa kisheria hata kimazingira, wa Moja kwa Moja unaoondosha
ujinai au makosa hayo, na kuwa ni makosa yanayolenga muktadha wa
kisiasa.
Huku
akitaka kuuaminisha umma kuwa huo ndio ukweli, Ndg. Mbowe amesisitiza
kuwa hilo lime kuwa likitekelezwa na CCM kwa lengo la kuwatisha
wananchi kujiunga na chama hicho hoja ambayo haina msingi wowote wa
kiutafiti.
Hivyo
CCM kwa kutambua kuwa Suala la mauaji linabeba Kosa la jinai, na kwa
kuwa Ndg. Mbowe ameshutumu Moja kwa Moja CCM na serikali yake
kuihusisha na mauaji hayo, ni vema sasa nasi tukatoa msimamo wetu dhidi
ya tuhuma, hiyo.
Kwanza,
si busara hata kidogo kuihusisha CCM katika matukio hayo, kwani
uchunguzi unaofanywa na vyombo vya dola umeshindwa mpaka sasa kuhusisha
matukio hayo na siasa, badala ya kuyahusisha na makosa ya jinai ambayo
hufanywa na watu kwa malengo tofauti na yale ambayo Ndg. Mbowe anataka
kuwaaminisha watu.
Pili,
CCM haijawai, haiwezi, na haitakuja fanya jambo lolote lenye lengo la
kuvuruga Amani na Usalama wenye utulivu ndani ya taifa letu, hivyo
uzushi na usingiziaji uliofanywa na Mtu Kama Ndg. Mbowe, si vema
kuuacha kimya, badala yake nimetumia wasaa Huu muhimu Kujibu, na kutoa
ufafanuzi ili Kuupa umma wa watanzania habari sahihi.
Ni
aibu kwa Chama kama Chadema kujitahidi kwa nguvu zote kujaribu kuficha
ukweli wa mauaji yanayotoa roho za watanzania wenzetu kwa kuyapa sura
ya kisiasa. Hizi ni juhudi za makusudi za kutaka kuficha ukweli wa
kinachotokea.
Ni
aibu kwa chama kama Chadema kujaribu kutumia mauaji mabaya kama haya
kutafuta mtaji wa kisiasa. Huku ni kuonyesha jinsi gani wamefilisika
kisiasa mpaka wanafikia mahali pa kuamini kuwa wanaweza kutumia
chochote kama mtaji wa kisiasa, vikiwemo vifo vya watanzania wenzetu.
Huku si kufilisika tu ila kwakweli ni unyama unaotakiwa kulaaniwa na
kila muungwana.
Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM
Waandishi Wa habari Kagera Wafundwa na Mkuu Wa mkoa
Bukoba
Kanal
mstaafu Fabiani Massawe ni mkuu wa mkoa wa kagera amewashauri
wanachama na waandishi wote mkoani humu kuandika habari za uchunguzi
wakifuata misingi,maadili na kanuni za uandishi wa habari ili kufanya
kazi yao kuwa nyepesi na isiyokuwa na migongano isiyokuwa ya lazima.
Massawe
aliwashauri waandishi kuandika habari za uhakika kwa kutumia vyanzo
sahihi kabla ya kuandika habari na kutoandika habari zinazopendelea
upande mmoja na zenye maslahi binafsi ili kuepuka kusababisha
migawanyiko ndani ya jamii inayoweza kusababisha uvunjifu wa amani ambapo alitoa mfano wa vita vya Kimbali vilivyosababishwa na uchochezi wa baadhi ya vyombo vya habari huko nchini Rwanda.
Aliwataka
waandishi kuacha tabia ya kuomba mishiko au bahasha ndipo waandike
habari kwa madai kuwa tabia hiyo ni kujidhalilisha na kuonekana
waandishi ni watu wa kulalamika kila wakati kuwa hawana kitu jambo
ambalo ameziomba klabu na waajiri wa vyombo mbalimbali kulifanyia kazi
kwani ni kero inayowafanya watoa habari kujenga uadui na waandishi kwa
madai kuwa wamekuwa wakitishia kuwa wakinyimwa mishiko hawaandiki habari
ya aina yoyote.
Pia
amewashauri waajiri wa vyombo mbalimbali vya habari hususani radio za
kijamii zipatazo tano za mkoa wa Kagera kutafuta utaratibu wa kuwaondoa
waandishi makanjanja ambao wamekuwa wakiajiriwa kwani wanalipwa ujira
mdogo huku waandishi wenye ujuzi na kazi hizo wakikosa nafasi jambo
ambalo amedai kuwa matokeo yake wamekuwa wakitumia radio hizo kujadili
maisha ya watu na kuongea mambao yasiyofaa katika jamii huku wengine
wakitangaza habari za mapenzi tu wakati kuna habari zinazogusa jamii
mfano wahamiaji haramu na rushwa hazipati nafasi jambo ambalo amedai
kuwa ni kuidhalilisha taaluma hiyo muhimu.
Kanal
Massawe alikuwa mgeni rasmi katika sherehe za kuadhimisha sikuukuu hiyo
ya uhuru wa vyombo vya habari ambapo kwa mkoa wa Kagera ilifanyika
katika ukumbi wa Coffee Tree in ndani ya Manispaa ya Bukoba na
kudhaminiwa na muungano wa vilabu vya waandishin wa habari
nchi (UTPC)na kuudhuliwa na viongozi mbalimbali wa mkoa huo ikiwa ni
pamoja na Mwenyekiti wa bodi ya kahawa nchini Pius Ngeze,Kamanda wa
Takukuru mkoa Domina Mkama,Kaimu kamanda wa polisi mkoa Vitus
Mlorele,mkuu wa Wilaya ya Bukoba Samweli Kamote na viongozi wa vyama vya
siasa mkoa na Wilaya.
Aidha mkuu
huyo wa mkoa aliiahidi kuwachangia kiasi cha shilingi milioni moja kama
mchango wa kununulia kiwanja cha kujenga ofisi ya klabu hiyo ili waweze
kuondokana na usumbufu wanaoupata wa kupanga kwenye
majumba ya watu ambapoa wamekuwa wakiwasumbua mara kwa mara pasipokuwa
na sababu za msing .
Katika
hatua nyingine klabu ya Waandishi wa habari mkoani Kagera (KPC) imetoa
msaada mbalimbali katika wodi za wagonjwa katika hospitalia ya mkoa wa
Kagera.
Tukio hilo lililifanyika May 5 katika hospitali hiyo kwa kukabidhi misaada mbalimbali katika wodi za watoto hospitalini hapo.
Mwenyekiti
wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani Kagera John Rwekanika alisema
kuwa wanachama wa KPC wapatao 34 wamelazimika kutoa misaada hiyo
katika tamasha lao lakuadhimisha uhuru wa vyombo vya habari duniani
iliyoadhimishwa mei 5 badala ya mei 3 mwaka huu inayoadhimishwa kila mwaka kutokana na wanachama na wanachama wengi kukabiliwa na majukumu mwengi katika tarehe rasmi inayoadhimishwa ulimwenguni.
Alisema
kuwa misaada iliyotolewa ni pamoja na sabuni,sukari na biskuiti vyote
vyenye thamani ya shilingi laki 2 ambapo vyote viligawiwa katika wodi za
watoto ambazo alizitaja kuwa ni namba saba yenye wodi mbi A na B
tofauti na kuwa jumla ya watoto 55 waliolazwa katika hospitalia hiyo
wamepokea misaada.
Alisema
kuwa waandishi wa habari ni sawa na taasisi au jumuiya yoyote ya kirai
inyopaswa kushirikiana na raia katika shughuli zote za kijamii kuwa
kutokana na chama chao kuwa na ushirikiano wa dhati wameonelea kutumia
fursa hiyo kuungana na wagonjwa,wazazi na wauguzi wa hospitali hiyo.
Kwa
upande wake kaimu mganga mfawidhi wa hospitalia hiyo Dk.Leonce Mboyerwa
alisema kuwa kitendo kilichofanya na waandishi wahabari hao wa Klabu
hiyo ni cha kizalendo na kuwa kimeonyesha ni kiasi gani waandishi
walivyo na mchango mkubwa katika jamii.
Mboyerwa
aliongeza kuwa waandishi wa habari wanafanya kazi katika mazingira
magumu lakini wameweza kuonyesha moyo wao wa upendo katika maadhimisho
yao ya uhuru wa vyombo vya habari kwa kuungana na jamii inayowategemea
kuwa hata taasisi nyingine za Kiserikali na zisizo za Kiserikali
wanapswa kuiga mfano uliotolewa na wanachama na uongozi wa KPC.
Aidha
mmoja wa wazazi katika Wodi ya watoto namba saba A Joyce Rweyemamu
alisema waandishi wa habari wameonyesha kitendo cha utu na kuwa
wameionyesha jamii kuwa wao ni kioo cha jamii.
Alisema
kuwa pamoja na misaada walioipokea kutoka kwaandishi hao kuwa wawapo
katika hospitali hiyo wanakabiliwa na changamoto ya kukosekana kwa
madawa na kuwa mgonjwa aliyelazwa analazimika kujinunulia madawa ambapo
wagonjwa wengine wanakuwa hawa uwezo wa kujinunulia madawa kuwa jambo
hilo linadhiri afya na kusababisha vifo vya mara kwa wagonjwa.
Naye
mku wa idara ya watoto hospitalia ya mkoa wa Kagera Gerad Kabyemera
alikiri kuwepo kwa hari hiyo ya upungufu wa madawa na kuwa tatizo hilo
halisababishwi na uongozi wa hospitali balia linasababishwa na stoo kuu
ya madawa makao mkauu ya afya Dar Es Salaam.
Kabyemera
alisema kuwa uongozi wa hospitali unaomba wastani wa asilimia 100 ya
madawa kutoka makao makuu lakini wanatumiwa wastani wa asilimia 40 ya
madawa walioomba ambayo hayawezi kutosheleza mahitaji ya wagonjwa
kulingana na idadi ya wagonjwa wanaolazwa katika hospitali hiyo.
mwisho
Monday, May 7, 2012
Mkapa Amuunguza Rais Kikwete
| ||
|
Rais Jakaya kikwete Awaapisha Mawaziri Jana
Dk. Harrison Mwakyembe akila kiapo kuwa waziri wa Uchukuzi mbele ya Rais Jakaya Kikwete kwenye viwanja vya Iku asubuhi hii.
Shamsi Vuai Nahodha akila kiapo kuwa waziri wa Ulinzi mbele ya Rais Jakaya Kikwete.
Dk Husein Mwinyi akila kiapo kuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii mbele ya Rais Jakaya Kikwete
Mh. Mathias Chikawe waziri wa Sheria na Katiba.
Shamsi Vuai Nahodha akila kiapo kuwa waziri wa Ulinzi mbele ya Rais Jakaya Kikwete.
Dk Husein Mwinyi akila kiapo kuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii mbele ya Rais Jakaya Kikwete
Mh. Mathias Chikawe waziri wa Sheria na Katiba.
SIKU YA VYOMBO VYA HABARI KAGERA
Anaitwa Bi Renatha Kipaka akitoa msaada kwa mmoja wa wagonjwa katika Hospitari ya watoto katika Hospitari ya mkoa wa Kagera,Waandishi wa habari walitembelea hospitari hiyo na kutoa misaada mbalimbali.
Baada ya hapo iliandaliwa pati hapani mkuu wa mkoa wa Kagera kanali msataafu Fabiani Masawe akihutubia wageni waalikwa wakiwemo waandishi wa habari
Majembe wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Kagera huku wakila mvinyo
Baadhi ya wageni walipata fursa ya kuongea machache juu ya Madia Day
Baada ya hapo iliandaliwa pati hapani mkuu wa mkoa wa Kagera kanali msataafu Fabiani Masawe akihutubia wageni waalikwa wakiwemo waandishi wa habari
Majembe wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Kagera huku wakila mvinyo
Baadhi ya wageni walipata fursa ya kuongea machache juu ya Madia Day
Subscribe to:
Posts (Atom)


























