Saturday, April 21, 2012

Friday, April 20, 2012

Ngeleja Nakusikiliza Ndugu Mwakilishi UN


Waziri wa Nishati na Madini Mh. William Ngeleja (kulia) amekutana na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania Bw. Alberic Kacou ofisini kwake jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya kuelekea Dodoma ambapo vikao vya Bunge vinaendelea.

Mh. Ngeleja amekutana na Mwakilishi huyo baada ya kuwasili kutoka katika mkutano wa kimataifa ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa unaohusu Nishati uliofanyika nchini Ubelgiji. 

Mh. Ngeleja aliiwakilisha Tanzania katika sekta ya Nishati ambapo Umoja wa Mataifa unategemea Nishati kuwafikia watu wote ifikapo Mwaka 2030.

Mh. Ngeleja amesema kuwa pamoja na changamoto zilizopo haswa upatikanaji wa fedha, Serikali ya Tanzania imedhamiria kusambaza nishati nchini Tanzania (yenye watu zaidi ya milioni 45) kutoka asilimia 18.5 hadi asilimia 30 ifikapo mwaka 2015.

Naye Mwakilishi wa Umoja wa Matifa amemshukuru Waziri kwa jitihada zake kupitia wizara hiyo na akasisitiza kuwa Nishati kwa kila mtu ni haki ya msingi hivyo uharakishwaji wa mpango huo wa nishati kwa wote upewe umakini mkubwa.

Pia ameahidi kufikisha maombi ya Waziri wa Nishati ikiwa ni pamoja na kuondolewa vikwazo vya upataji wa fedha kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki Moon.

Kusoma zaidi: http://tz.one.un.org

Imetolewa na Ofisi ya Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa – Afisa Mawasiliano.

Viongozi Wa Dini Wafanya Semina Ya Sensa

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhani Khijjah akizungumza na viongozi  mbalimbali wa dini kuelezea umuhimu na ushiriki wao katika kufanikisha sensa ya watu na makazi itakayofanyika kitaifa mwezi Agosti mwaka huu  wakati wa mkutano wa viongozi wa dini unaoendelea  jijini Dar es salaam.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhani Khijjah (kushoto) akiandika maswali yaliyoulizwa na viongozi wa dini kuhusu namna serikali ilivyojipanga kukamilisha sensa ya watu na makazi  itakayofanyika mwezi Agosti 2012. Wengine ni mkurugenzi mkuu wa ofisi ya taifa ya takwimu Dkt. Albina Chuwa (katikati) na kamishna wa sensa Bi. Hajjat Amina Mrisho.

Baadhi ya viongozi wa dini wanaoendelea na mkutano wao jijini Dar es salaam wakipitia vitabu na vipeperushi  vyenye jumbe mbalimbali  kuhusu zoezi la sensa ya watu na makazi litakalofanyika nchi nzima mwezi  Agosti mwaka huu  baada ya wataalam kutoka  Ofisi ya Taifa ya Takwimu kutoa semina fupi kuhusu ushiriki wa viongozi hao katika kufanikisha sensa hiyo 
 
Na Aron Msigwa MAELEZO

Usalama Barabarani

Moja ya Arama za Barabarani ambazo ni muhimu kuzijua

Na Antidius Kalunde
Bukoba
 
WAMILIKI wa vyuo vya ufundishaji wa madereva wametakiwa kuacha kutanguliza maslahi yao binafsi kwa kutanguliza suala la biashara huku wakiwa hawatoi elimu bora kwa madeleva wanaowafundisha jambo ambalo linaendelea kusababisha ajali nyingi hapa nchini kutokana na vyuo kutokuwana sifa bora.
 
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa kamati ya usalama Barabarani mkoani Kagera Winstoni Kabantega wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya baadhi ya vyuo vinavyotoa elimu kwa madeleva kutokuwa na sifa za ufundishaji.
 
Alisema kuwa kwa hivi sasa vyuo vingi vinatoa madereva ambao hawana sifa za kutosha kutokana na wamiliki kutanguliza pesa bila kujali matatizo yanayoweza kutokeza badae mara baada ya madeleva hao kumaliza masomo.
 
Aidha ameiomba serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani ya nchi chini ya jeshi la polisi kuhakikisha inapitia kila chuo na kuangalia kama kina sifa za kutosha katika ufundishaji kwani bila kufanya hivyo tatizo la madereva wazembe haliwezi kumalizika huku wananchi wakiendelea kupoteza maisha ya vilema visivyotarajia.
 
Katika hatua nyingine Kabantega amezungumzia suala la kuhepuka ajali ni lakila Mtanzania kwani wananchi inawabidi kushirikiana na jeshi la polisi kuhakikisha taarifa za wamiliki wa vyuo visivyokuwa na sifa ya kutosha katika kuzalisha madeleva vinafungwa.
 
Akielezea wiki ya nenda kwa usalama barabarani ambayo kitaifa ilifanyika mkoani kagera kuanzia tarehe 3 october hadi tarehe 8 mwaka jana, alisema kuwa wananchi wa mkoa wamejifunza mengi kutokana na maadhimisho hayo na kujua sheria jambo ambalo litaendelea kuounguza ajali kwa mkoa huo.
 
Aliongeza kuwa katika takwimu  za hivi karibuni zimeonyesha kuwa mkoa wa Kagera ni mmoja ya mikoa minne ambayo imepunguza tatizo la ajali za barabarani kutokana na elimu inayotolewa na kikosi cha usalama barabarani cha polisi kwa kushirikiana na vyuo vya madeleva ambavyo vina sifa ya kutosha.
 
Katika hatua nyingine Kabantega alilitaka jeshi la Polisi kupitia kikosi cha usalama barabarani kufuata sheria sahihi kuliko kuendelea kuendekeza vitendo vya rushwa ambavyo vikiendelea udhibiti wa madeleva wazembe utakuwa mgumu.
 
MWISHO

Habari Leo Na Nipashe Za Leo Ni Balaa


Rais Kikwete Amaliza Ziara Brazil


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na viongozi wa  chama cha wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa wa nchi ya Brazil alipokutana nao katika siku ya mwisho ya  ziara yake ya kikazi jijini Sao Paulo, katika siku yake ya mwisho ya ziara yake ya Brazil April 19, 2012. Wa pili kulia ni Makamu wa Rais wa chama hicho Bw Joao Guilherme Sabino Ometto na kushoto ni Mkurugenzi wa chama hicho Thomaz Zanotto na kulia ni Waziri wa kazi na Uwezeshaji Wanachi Kiuchumi na Ushirika wa Zanzibar Mh Haroun Ali Suleiman.





Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na wajumbe wa chama cha wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa wa nchi ya Brazil alipokutana nao katika siku ya mwisho ya  ziara yake ya kikazi jijini Sao Paulo April 19, 2012.PICHA NA IKULU

Thursday, April 19, 2012

Wabunge Ambao Wanaanza Inawabidi kuwasikiliza Wakubwa

Waziri Mkuu Mizengo Pinda Akizungumza na mbunge Mpya wa Jimbo La Arumeru Mashariki Joshua Nassari(CHADEMA) kabla ya kuanza Kikao cha Bunge Leo Mjini Dodoma hapa kama walivyokutwa na Mpiga picha wetu katika viwanja vya Bunge

Wednesday, April 18, 2012

Hii Ya Zambi Imenitisha Nilipokutana na Mwananchi

We litafute alafu utajua ni kwanini Zambi anasema CCM inaweza Kung'oka 2015 katika Uchaguzi Mkuu

Mkutano Wa Viongozi wa Waislamu Na Wakristo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa dini alipowasili kwenye Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam,kwa ajili ya kufungua Kongamano la Dini la Waislam na Wakristo, lililoanza jana Aprili 18, 2012
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua rasmi Kongamano la Dini la Waislam na Wakristo lililoanza jana Aprili 18, kwenye Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Kaka Mjengwa Hata mimi Nimeipenda Hii Sheria

Sheria ya Uasalama barabarani hairuhusu pipiki za abilia kupakia watu watatu kwa upande wa raia ila Polisi Ruksa kupakiwa wawili akiwemo dreva wao. MTUNGA SHERIA NDIE..................................
PICHA KWA HISANI YA MJENGWA

Msitu Mnene Lakini Ni Hifadhi Ya Taifa Je Tunailinda?

Hapa ni Msitu wa pori la Kikulula Ranchi lililoko Katika wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera na ni moja ya eneo ambalo linatumika kulishia mifugo aina mbalimbali zikiwemo N'GOMBE aina ya Kongwa BEEF Lakini kama kawaida ya Mtu mzima kutembelea maeneo kama haya.

Hili Nalo Ni Daraja Wananchi Wanalitumia Kupita

Moja ya Daraja ambalo linaonekana halifai kwa matumizi ya wananchi hasa kupita na kuvuka kwani halina usalama wowote ule na halieleweki,hapa ni wilayani Karagwe mkoani Kagera katika kata ya Kihanga barabara ya kuelekea Kikulula ranchi.

MADIWANI MULEBA WAPITISHA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2012/13

Na Antidius Kalunde
Muleba

MADIWANI wa halmashauri ya wilaya ya Muleba mkoa wa Kagera Wamepitisha bajeti  ya mwaka 2012/13, ambapo zaidi ya shilingi Bilioni 41.1 zinatarajia kukusanywa kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo ruzuku ya serikali.

Bajeti hiyo iliyowasilishwa na mwenyekiti wa halmashauri hiyo ,  George Katomero iliridhiwa na baraza baada ya kujadiliwa kwa siku mbili April 14/15 na hivyo kutoa nafasi kwa wajumbe wa baraza hilo kuifanyia marekebisho katika masuala kadhaa, ikiwemo matumizi ya mapato yanayotokana na nyanzo vya ndani.

Awali akiwasilisha makadirio ya bajeti hiyo Bw. Katomero alisema kati ya fedha hizo zinazotarajiwa kukusanywa huo, zaidi ya bilioni 3.2 zinatokana na vyanzo vya ndani, huku nyingine zikitarajiwa kupatikana kupitia ruzuku ya serikali kuu na wahisani.

Hata hivyo madiwani hao wamekubaliana kwamba kiasi cha shilingi bilioni moja zitumike katika miradi ya maendeleo badala ya milioni 527.1 zilizotengwa awali kwa miradi lengo likiwa kuboresha maisha wa wakazi wa wilaya hiyo.

Mmoja wa madiwani hao, Justus Magongo wa kata ya Muhutwe alisema hakuna sababu ya halmashauri kutegemea kwa kiasi kikubwa fedha za ruzuku zinazotewa na serikali kuu kwa madai kuwa sio za uhakika katika upatikanaji wake, na kuwa wakati mwingine uletwa kwa kuchelewa.

Aidha madiwani hao waliitaka halmashauri kuongeza nguvu katika ukusanyaji wa mapato ili kufikia lengo hasa kutokana na bajeti ya mwaka huu kuwa na ongezeko la takribani shilingi bilioni 15 kutoka  shilingi 26,236,096,906 kwa mwaka 2011/12 hadi kufikia shilingi 41,118,283,893 mwaka 2012/13.




Mwisho

WANA JANGWANI WENZANGU



Kwanza nawapa pole wana Yanga wenzangu kwa kushindwa kufanya vizuri katika mechi za misho wa ligi kuu Tanzania Bala lakini siku za hivi karibuni katika kanda ya ziwa mmepoteza michezo yote miwili mechi ya kwanza timu ya toto African ya Mwanza aliwachapa kwa magolo 3 kwa 2 na siku ya jana timu ya Kagera sugar ya mjini Bukoba iliwapiga goli Moja kwa bila pamoja na kuonyesha mpira mzuri lakini matokeo yakawa vile

Cha msingi ni kuweka jitihada zaidi na kujiandaa upya katika michuano ijayo imekuwa ni mara ya Kwanza kwa timu yetu hii nzuri kufanya vibaya katika kipindi cha mwisho wa ligi kuu ya Tanzania bala.

Msikate tamaa bado wapenzi wenu tuko pamoja haya ni matoeke katika michezo wala hakuna haja ya kuwa na hasira ya aina yoyote ile bado twawapenda wana jangwani

By Kalunde