Monday, May 27, 2013

  JK AKUTANA NA MARAIS WASTAAFU.


h 86c68
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizingumza na Marais Wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Mzee Benjamin Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu na Katibu Mkuu wa Umoja wa Afrika Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim kuhusiana na sherehe za miaka 50 ya AU alipokutana nao jijini Addis Ababa, Ethiopia,

TASWIRA MBALIMBALI ZA MAKAO MAKUU YA UMOJA WA AFRIKA


un1 a1931
un2 5dfba
un3 b7b18

Jk KATIKA MKUTANO WA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA AU JIJINI ADDIS ABABA


jk1 6222c
: Muono wa jicho la samaki katika Mkutano wa Sherehe za miaka 50 ya AU katika makao makuu ya umoja huo jijini Addis Ababa  Mei 25, 2013
jk3 93d98
Viongoi AU wakiwakumbuka waliotangulia mbele ya haki.

jk4 3f79a
Rais Jakaya Mrisho Kikwete Mkutano wa Sherehe za miaka 50 ya AU katika makao makuu ya umoja huo jijini Addis Ababa

KILIMO NGUZO MUHIMU KWA MAISHA YA WAAFRIKA-TANZANIA

untitled 90742
Injinia Mbogo Futakamba, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Usalama wa Chakula na UShirika akizungumza wakati wa Kikao cha Tatu cha Kazi kilichokuwa kikijadili kuhusu maeneo mapya takayoweza kuingizwa katika Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu ( SDGs). Naibu Katibu Mkuu aliongoza ujumbe wa Tanzania katika Kikao hicho kilichomalizika mwishoni mwa wiki hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York.Tanzania ni kati ya Nchi 30 zilizochaguliwa kushiriki majadiliano hayo. Maeneo ambayo yalijadiliwa katika Kikao hicho ni ; upatikanaji wa chakula na lishe bora, kilimo endelevu, mmomonyoko wa udongo, ukame na kuongezeka kwa jangwa, upatikanaji wa maji na ushughulikiaji wa maji taka.

Na Mwandishi Maalum
Tanzania imeikumbusha Jumuiya ya Kimataifa kwamba Kilimo bado kinaendelea na kitaendelea kuwa tegemeo la maisha ya waafrika wengi. Na kwa umuhimu huo, Kilimo kinatakiwa kupewa kipaumbele cha pekee wakati wa majadiliano kuhusu maeneo mapya yanayotarajiwa kuwa sehemu ya Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu ( SDGs).
Hayo yameelezwa na Injinia Mbogo Futakamba, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Usalama wa Chakula na Ushirika wakati alipoongoa Ujumbe wa Tanzania katika Kikao cha Tatu cha Kikundi kazi kilichokuwa kikijadili kuhusu SDGs kilichomalizika mwishoni mwa wiki hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
"Tunapoendelea na majadiliano haya kuhusu malengo mapya ya maendeleo endelevu, lazima tukumbuke kwamba Kilimo ni sehemu ya maisha ya waafrika wengi. Uchumi imara na endelevu, maendeleo endelevu na uondoaji wa umaskini utawezekana tu ikiwa kilimo kitaendelea kupewa kipaumbele ikiwa ni pamoja na kuongeza uwekezaji na upatikanaji wa miuondo mbinu ya kisasa ya kuboresha kilimo" akasema Naibu Katibu Mkuu.
Ni kwa sababu hiyo, akasema Tanzania imeridhika kwa kuona kwamba maeneo ya kilimo, usalama wa chakula na lishe bora, mmomonyoko wa udongo, ukame na kuongezeka kwa jangwa, upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji taka yalikuwa yamepewa kipaumbele cha kujadiliwa katika Kikao hicho cha Tatu.
Naibu Katibu Mkuu, akasema maeneo hayo na mengine yanayohusiana na hayo, yanapashwa kutoa malengo ya wazi kwaajili kufunguza fursa kubwa za kilimo kwa Afrika.
" Ili Afrika iwe na fursa kubwa ya kunufaika na kilimo tunahitaji ongekezo katika upatikanaji wa misaada ya mikopo, fursa na haki sawa kwenye masoko ya kimataifa na biashara, kuboresha uzalishaki kwa ekari, uwekezaji katika miundo mbinu ya kilimo ikiwa ni pamoja na mifumo ya umwagiliaji, utafiti, usindikaji viwandaji ili kupunguza upotevu baada ya mavumo".
Akasisitiza kwamba, majadiliano kuhusu maeneo hayo yamefanyika wakati muafaka na hasa ikizingatiwa kuwa asilimia 75 ya watanzania wanaishi maeneo ya vijijini na kutegemea kilimo kwa maisha yao.
Kwa mujibu wa Naibu Katibua Mkuu, Hata taarifa ya Banki Maendeleo ya Afrika kuhusu mkatakati wa sekta ya kilimo kwa mwaka 2010-2014 imeeleza wazi kwamba kilimo kinasaidia maisha ya asilimia 80 ya idadi ya watu katika Afrika na kinatoa ajira kwa karibu asilimia 60 ya watu katika maeneo mbalimbali ya kiuchumi.
Akizungumzia kuhusu suala la ardhi, Injinia Futakamba, alieleza kwamba ni jambo lililowazi kwamba idadi ya watu Afrika inaongezeka, hali inayochangia kuongezeka kwa mahitaji ya ardhi nzuri kwaajili ya kilimo, ufugaji, uvuvi na hata ufugaji wa nyuki.
kuhusu lishe, Naibu Katibu Mkuu, alieleza kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imelipa suala la lishe kipaumbele katika ajenda zake za maendeleo, hususani katika maeneo ya kilimo na afya kwa ujumla.
Akabainisha kwamba mkazo kuhusu lishe bora umelekezwa kwa watoto wakimo watoto wachanga na wenye umri wa kwenda shule, wanawake wajawazito na wanaonyonyesha. Na kwamba juhudi hizo zinatekelezwa kwa pamoja kati ya Wizara za Kilimo, Afya, Elimu na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
Itakumbukwa kwamba Tanzania ni kati ya nchi 30 ambazo zimechaguliwa kuongoza majadiliano hayo kuhusu maeneo mapya yanayopashwa kuwa sehemu ya malengo mapya ya maendeleo endelevu. Vikao Kazi hivi vinafanyika nchini ya Uenyeviti Wenza wa Wawakilishi wa Kudumu wa Kenya na Hungary, Mabalozi Macharia Kamau na Csaba Korosi.
Kikao cha nne cha kazi kinatarajiwa kufanyika kati ya tarehe 17-19 mwezi wa Sita mwaka huu ,ambapo itatarajiwa maeneo ya upatikanaji wa ajira bora na salama kwa wote, ulinzi wa jamii, vijana, elimu na utamaduni, afya na idadi ya watu yatajadiliwa
Kikao cha kwanza kabisa kilifanyika mwezi wa March huku Kikao cha pili kilifanyika mwezi Aprili ambapo maeneo kuhusu utawala bora, usawa wa kijinsia na uwezeshwaji wa wanawake na haki za binadamu na suala la kuondoa umaskini na maendeleo endelevu yalijadiliwa.

Maisha Yanaendelea

d2 ff669
Iringa, asubuhi hii. Hali ni shwari.

Saturday, May 25, 2013

Friday, May 24, 2013

AU washerehekea miaka 50

au 7161d
WAGENI mashuhuri na marais wa Afrika wameanza kuwasili mjini Addis Ababa Ethiopia kwa sherehe za kuadhimisha miaka hamsini tangu kuanzishwa kwa Muungano wa Afrika.
Muungano wa Afrika wakati huo ukijulikana kama OAU,uligeuza jina na kujulikana kama AU mnamo mwaka.
Leo Jumamosi kutakuwa na sherehe za kilele kuadhimisha miaka hamsini ya AU na Zitahudhuriwa na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na marais wengine wa Afrika.

Kauli mbiu ya sherehe za leo ni mjadala mkuu kuhusu ushirikiano wa nchi za Afrika na kuimarishwa kwa muungano huo.
Mwenyekiti wa tume ya muungano huo, Dr Nkosazana Dlamini Zuma, anaseme kuwa hii itakuwa fursa kwa AU kujadili kuhusu uwezo wa bara hili na ambacho kinaweza kufikiwa katika miaka hamsini ijayo.
Sherehe za AU zinakuja wakati swali kuu kwa AU ni kesi zinazowakabili washukiwa wakuu wa ghasia za baada ya uchaguzi wa Kenya mwaka 2007/08 Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto pamoja na mtangazaji wa redio Joshua Arap inaendelea katika mahakama ya kimataifa ya ICC.
Duru zinasema kuwa huenda mawaziri wa mambo ya kigeni wa nchi za Afrika wamekubaliana kuhusu azimio linalotaka kesi ya washukiwa hao kurejeshwa Kenya ambako inaweza kusikilizwa na hatua kuchukuliwa dhidi ya watakaopatwa na makosa.
Shereha hizi pia zinakuja wakati bara la Afrika linashuhudia migogoro nchini Mali, DRCongo huku Misri ikiwa bado haijatengamaa baada ya kufanyika mapinduzi ya kiraia yaliyomng'oa mamlakani aliyekuwa rais Hosni Mubarak.
Lakini mwenyekiti wa AU ana matumaini kuwa Afrika iko kwenye mkondo mzuri wa kimaendeleo.
Katika hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 21 wa AU, Dlamini Zuma alisema kuwa Afrika imekuwa kiuchumi katika muongo mmoja uliopita, imeshuhudia maendeleo ya kiuchumi , ustawi wa kikanda , uimarishwaji wa miundo mbinu na ushirikiano wa kikanda.
Sherehe hizi ambazo zitafuatwa na mkutano wa siku mbili wa marais wa AU, zitatoa fursa kwa wananchi wa bara la Afrika kuangazia ufanisi wa Muungano huo. Chanzo: bbcswahili

Magazeti

  • 00 a0713
    0 e8e9f
    1 a84dc
    2 2b2ca
    3 c9f38

    4 33040
    5 61155
    6 97c91
    7 e5600
    8 ce8d6
    9 21251
    11 8414c
    12 a72f7
    13 932e1

    ashikiliwa na polisi kwa kutorosha kobe

    Published in Jamii
    koeb b4087
    Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma David Misime akionyesha waandishi wa habari wanyama aina ya kobe zaidiya 70 waliofungwa kwenye mifuko ya Salfet waliokuwa wamekutwa kwa Moses Nyawaje 42 akiwa anataka kuwasafirisha kinyume cha sheria.

    TAARIFA YA JESHI LA POLISI

    10 51695
    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
    WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
    JESHI LA POLISI TANZANIA
    Anuani ya Simu “MKUUPOLISI”                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                     Ofisi ya  Inspekta  Jenerali wa Polisi,
    Simu : (022) 2110734                                                                                    Makao Makuu ya Polisi,
    Fax Na. (022) 2135556                                                                                                           S.L.P. 9141,
    Unapojibu tafadhali taja:                                                                        DAR ES SALAAM.
    24 MAY 2013
     
    TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
    Jeshi la Polisi Nchini linamshikilia mtu mmoja ambaye jina lake linahifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi kwa tuhuma za kueneza ujumbe wa uchochezi na chuki kwa wananchi na viongozi wa serikali kwa njia ya simu ya mkononi akituma SMS kwa lengo la kuchochea fujo, vurugu na kutoa matusi kwa viongozi hao.

    Mtu huyo amekuwa akifanikisha kazi hiyo kwa kutumia Chips (sim card) 13 za simu za mkononi ambazo amekamatwa nazo. Jeshi la Polisi linaendelea kumhoji mtu huyo na ushahidi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.
    Aidha, Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi wenye taarifa zingine za wahahlifu kama hao kujitokeza na kutoa taarifa hizo polisi ili wahalifu hao waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua stahiki, wakiwemo watu wanaowashawishi wenzao kwa njia ya fedha, kuwashauri ama kuwasaidia kwa namna yeyote ile katika kufanikisha uhalifu huo na kusababisha uvunjifu wa amani hapa nchini.
    Jeshi la polisi halitasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakayebainika kuvunja sheria za nchi.
    Imetolewa na:-
    Advera Senso-SSP
    Msemaji wa Jeshi la Polisi

    Thursday, May 23, 2013

    JK awahimiza Watanzania kulinda amani ya nchi

     Rais Jakaya Kikwete amewataka Watanzania kulinda na kudumisha amani ya nchi kwa kujiepusha na vikundi vya watu wanaochochea vurugu.

    Hayo aliyasema jana alipokuwa akizungumza na wakazi wa Kata ya Migoli, Tarafa ya Isimani wakati wa kuweka jiwe la msingi kwenye Barabara ya Iringa - Dodoma ambapo alisema matukio ya hivi karibuni yanahatarisha amani ya nchi.
    “Ndugu zangu kabla sijafikia tamati ningependa nizungumzie hili, nawaomba mdumishe amani na upendo. Taifa hili limedumu katika amani kwa muda mrefu, matukio ya hivi karibuni hayafurahishi…Wapo watu wanalala usiku na mchana wanapanga njama za kuvuruga amani ya nchi yetu, watu hawa wasipewe nafasi, wasisikilizwe kwani hawana nia njema na taifa letu,” alisema Kikwete.
    Kikwete alisema Watanzania wakikataa kuwasikiliza, kuwafuata na kutenda wanavyotaka Tanzania itabaki kuwa nchi ya amani na mipango yao haitafanikiwa.
    Kauli ya Kikwete imekuja huku kukiwa na matukio ya vurugu za kidini na matukio ya maandamano ya uharibifu wa mali yanayofanywa na baadhi ya makundi ya kidini nchini.
    Akizungumzia uzinduzi wa ujenzi wa barabara hiyo ambao ni sehemu ya Barabara Kuu ya Kaskazini inayounganisha Iringa-Dodoma kwa kiwango cha lami, Kikwete alisema barabara ni ufunguo wa uchumi katika taifa lolote duniani.
    “Wapo watu wanaohoji ni kwa nini tunatumia fedha nyingi kuwekeza kwenye ujenzi wa barabara, tungeweza kutumia fedha nyingi kwenye maeneo mengine, lakini pamoja na kwamba tumechelewa kuwekeza kwenye barabara bado kama nchi tuna nafasi ya kuunganisha nchi kwa barabara na kasi ya uchumi itakua,” alisema Kikwete.
    Kikwete alifafanua kuwa kwa sasa Serikali yake imeweka kipaumbele katika ujenzi wa barabara na kuongeza kuwa ndiyo sababu barabara nyingi zinazounganisha miji mikubwa na zile za kawaida zimejengwa na nyingine zinaendelea kujengwa kwa kasi.
    Alisema kutokana na hatua hiyo Serikali yake imeimarisha mfuko wa barabara ambapo wakati anaingia madarakani ulikuwa na kiasi cha Sh55 bilioni, lakini kwa kipindi cha miaka saba imefikia Sh430 bilioni na sasa mfuko huo unatarajiwa kutengewa Sh504 bilioni katika bajeti ya mwaka 2013/14.
    Kikwete aliwataka wakazi wa Iringa na maeneo yote zinakojengwa barabara kushiriki, kuzitunza kwa kulinda miundombinu yake na kushukuru nchi wahisani kwa ujenzi wa miundombinu nchini.
    Kuhusu umuhimu wa matumizi ya barabara alisema zitasaidia wakazi wa maeneo jirani kukuza uchumi na kuwataka kutumia fursa hiyo kufanya kazi za uzalishaji kwa bidiii ili waweze kunufaika na matunda ya barabara hizo.
    Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli alisema Serikali itahakikisha makandarasi wote wanaoendelea na ujenzi wa barabara nchini wanakamilisha kazi zao kwa wakati na wanajenga kwa kiwango kinachotakiwa.

    Maisha Yanaendelea


    Madhara ya ulabu

    mlev 9fcf6

    KAULI YA SERIKALI VURUGU ZA MTWARA


    NCHIMBI-2 4c2a6

    Na Lydia Churi.
    SERIKALI YAAPA KUWASAKA WAASISI WA VURUGU MTWARA
    Serikali imelaani vikali vurugu zilizotokea Mtwara na imeapa kuwasaka waasisi wa vurugu hizo ndani na nje ya Mtwara.

    Akitoa kauli ya Serikali Bungeni kuhusu vurugu zilizotokea Mtwara jana, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Emmanuel Nchimbi ameliambia Bunge kuwa wote waliohusika kupanga, kushawishi, kuandaa na kutekeleza vurugu hizo hawataukwepa mkono wa sheria.

    Katika kauli hiyo ya Serikali Waziri Nchimbi amesisitiza kuwa watanzania wanalo Taifa moja ambalo maliasili zake ni za watanzania wote hivyo tabia iliyoanza kujengeka ya kila eneo kutaka inufaike peke yake na mali za eneo husika italigawa taifa vipande vipande.

    Alisema baadhi ya taasisi za kiraia na vyama vya siasa kwa maslahi binafsi yasiyo na upeo mpana, vinaweza kudhani kuwa kuunga mkono madai ya namna hii ni kujiimarisha na kukubalika kwao kwa jamii lakini badala yake wataipasua nchi na kusababisha vifo vya maelfu ya watu pamoja na kulijaza taifa vilema na majeruhi.

    "Wasaliti wa taifa hili wanafahamu maendeleo makubwa yatakayopatikana Mtwara na nchi nzima kutokana na rasilimali gesi, hivyo wanatumia vibaya ufahamu wetu mdogo kuhusu gesi na kuchochea upinzani dhidi ya mradi huu unaotarajiwa kuwakomboa watanzania" Alisema Waziri.
    Alisema vita inayofahamika kama vita kuu ya Afrika katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo iliyopiganwa kati ya 1998-2003 msingi wake ulikuwa ni kupigia rasilimali, vita hii ilisababisha vifo vya watu milioni 5.4, magonjwa na njaa na kuhoji kuwa huko ndiko tunakotaka kulipeleka taifa letu.
    Alisisitiza watanzania wanatakiwa kujua kuwa wanayo dhamana ya kuendeleza umoja amani na kuchangia maendeleo ya nchi na tofauti zinazojitokeza lazima ziendelee kuzungumzwa kwa uwazi, kuheshimiana na kuzingatia sheria na taratibu za nchi yetu.
    Alisema raia mmoja, Karim Shaibu alifariki katika vurugu hizo na wakati huohuo askari wanne wa Jeshi la wananchi wa Tanzania walifariki baada gari lao waliokuwa wakisafiria kutoka Nachingwea kwenda Mtwara kupata ajali katika eneo la Kilimani Hewa. Askari wengine 20 walijeruhiwa katika ajali hiyo.

    Waziri Nchimbi aliyataja madhara mengine yaliyotokana na vurugu hizo kuwa ni kuchomwa moto kwa Ofisi za Mahakama ya Mwanzo ya Mitengo, Ofisi ya CCM kata ya Chikongola, nyumba binafsi ya Mwandishi wa Habari wa TBC na ya Afisa Mtendaji kata ya Magomeni. Aidha katika vurugu hizo, nyumba za askari polisi wanne pamoja ofisi ya kata ya Chilongola zilivunjwa na kuibiwa vitu mbalimbali.

    Jana majira ya saa 4 asubuhi kulitokea vurugu kubwa katika Manispaa ya Mtwara na viunga vyake zilizosababishwa na madai ya baadhi ya wananchi wa Mtwara kupinga usafirishwaji wa rasilimali gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam. Makundi ya vijana waliokuwa maeneo ya Sokoni, Magomeni na Mkanaredi walipanga mawe makubwa, magogo na kuchoma moto matairi barabarani hali iliyoendelea kusambaa maeneo mengine.

    Magazeti


    DSC 0086 40c77
    DSC 0087 9656e
    DSC 0088 b82f0
    DSC 0089 657b7
    DSC 0090 80a25

    DSC 0091 7c7c9
    DSC 0092 2e719
    DSC 0093 84c75
    DSC 0094 b032c
    DSC 0095 2a886
    DSC 0096 88bb3
    DSC 0097 0ea78
    DSC 0098 b2cbc
    DSC 0099 e6b46
    DSC 0100 88fc9

    Serikali Kuendelea Na Mpango Wa Kujenga Bomba La Gesi

    bungeni b5e17

    Na Lydia Churi, MAELEZO-DODOMA
    Serikali itaendelea na mpango wake wa kusafirisha gesi asilia kutoka mkoani Mtwara, Lindi hadi Dar es Salaam. Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo ameliambia bunge jana mjini Dodoma alipokuwa akiwasilisha bajeti ya wizara yake ya mwaka wa fedha 2013/2014.

    Alisema mradi wa kusafirisha gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es salaam utahusisha  ujenzi wa bomba  lenye urefu wa kilometa 532 ambapo bomba hilo litakuwa na uwezo wa kusafirirsha futi za ujazo za gesi asilia milioni 784 kwa siku.
    Alisema mradi huo utaigharimu Serikali shilingi bilioni 1,960 ambapo kazi za usanifu wa mradi na ulipaji wa fidia kwa wananchi wapatao 3,092 waliopisha maeneo ya mradi zimekamilika. Hatua za awali za ujenzi wa mitambo ya kusafisha gesi asilia zimeanza.
    Waziri Muhongo alisema kutokana na mradi wa gesi asilia wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara watapata manufaa mbalimbali yatokanayo na mradi huo ikiwa ni pamoja na tozo ya asilimia 0.3 ya mauzo ya gesi asilia, huduma za jamii kama vile zahanati, shule, umeme, maji  na mafunzo katika vyuo vya ufundi (VETA) na sekondari.
    Wakati huo huo, Serikali imefanikiwa kukamata madini yenye thamani ya shilingi bilioni 13.12 kati ya mwezi Oktoba 2012 na April 2013 yaliyokuwa yakisafirishwa nje ya nchi kinyume na sheria.
    Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo ameliambia bunge leo mjini Dodoma kuwa wahusika wameshachukuliwa hatua za kisheria kwa mujibu wa sheria ya Madini ya mwaka 2010.
    Alisema katika kuimarisha usimamizi wa biashara ya madini nchini, Serikali kupitia wakala wa madini (TMAA) imeanzisha madawati maalum ya kukagua madini yanayosafirishwa nje ya nchi kupitia viwanja vya ndege vya kimataifa vya Dar es salaam, Kilimanjaro na Mwanza.
     Wizara ya Nishati na Madini imeomba kuidhinishiwa na Bunge zaidi ya shilingi trilioni moja ambapo asilimia 90 ya fedha hizo ni kwa ajili ya maendeleo na asilimia 10 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida. Aidha Fedha za ndani ni asilimia 56.27 na za nje ni asilimia 43.73.

    JK AWEKA JIWE LA MSINGI BARABARA YA IRINGA - DODOMA




    jk3 0c5da
    JK akiweka jiwe la msingi Barabara ya Iringa –Dodoma .
    jk4 142b5
    Rais Jakaya Mrisho kikwete akiongea na wananchi wa Iringa
    jk5 eb45f
    Baadhi ya wananchi walio hudhulia

    jk f4cf9

    JK akipanda mti baada ya kuweka jiwe la msingi
    Picha na Said Ng'amilo (mjengwablog)